Dkt. Bashiru Ally pole lakini maneno huumba

Dkt. Bashiru Ally pole lakini maneno huumba

Kwahiyo kwenye Wizara ya Afya wameachwa wale Mawaziri wa Nyungu? Hii inaonyesha mama naye anaamini kuwa corona ilishajiondoa baada ya kusimangwa na maombi
Ila Mama ajichunge sana na yule Naibu,siyo mtu mzuri ana karama ya kuwaombea wakubwa wake dua mbaya na zinawapata kweli
 
Hebu tusubiri mpaka jumanne baada ya hii ''sabatical live'' kwisha.Kuna teuzi raia No.1 aliahidi zitaendelea!
 
Kinachonishangazi mbona watu wamefurahi sana.....kwani aliwakosea nini mpaka watu wafurahie kuporomoka kwake
Hiki hapa
JamiiForums1791349533.jpg
 
Atarudi kwenye ukatibu mkuu sisiemu lakini alipaswa awe demoted kabisa kabisa arudi udsm kumark course work za wanafunzi
Yaani kurudi UDSM ni demotion? No wonder watu wenye mtizamo huu kazi yao kila mara ni kufikiria vyeo ni sehemu ya kwenda kupiga badala ya kutumikia umma...Kwenda UDSM kwake ni promotion siyo demotion kwakua ataendelea na carrier yake...Alipoondolewa kabla ya kufikia nafasi ya juu kwenye taaluma hiyo kwa mwanazuoni ni sadaka kwa nchi yake...Itoshe kusema Dr. Bashiru ameisaidia nchi kwakukubali teuzi hizo na kwakua aliyeona anafaa aliondoka ni sahihi kabisa kama angerudi alikotoka, hata hivyo aliyepo ameona anamfaa bado kwenye bunge pengine kuisaidia nchi kwenye maamuzi...Tusiwe na macho hasi kwa kila jambo....Tabia ya kupenda vyeo bila tija ni hatari kwa taifa; Mh. Rais Samia ametuonya kuwa tunajenga nyumba moja kila nafasi ni muhimu katika kuijenga nyumba yetu Tanzania.
 
Hi vitu hufanya kazi nje ya uwezo na utashi wa kawaida wa binadamu....Na hii ndio maana tunaaswa sana tuwe na tafakuri kubwa tunapotamka mambo makubwa kwenye mazungumzo yetu

Bashiru msomi wa chuo kikuu cha Dsm wakati anateuliwa kushika wadhifa wa katibu mkuu wa CCM ... Kwa mdomo wake alitamka wazi kuwa nafasi hiyo ni kubwa sana kwake na hatarajii kushika nafasi nyingine kubwa na hata kama itatokea ATAIKATAA

Matendo ya Mungu si ya wanadamu.. Ikatokea nafasi ya katibu mkuu kiongozi ...nafasi kubwa zaidi kuliko ile ya ukatibu mkuu wa chama...!!!

Kwakuwa tumeumbwa kusahau na tumeumbiwa utashi wa kuwa dhaifu kuyakana maneno yetu hasa penye ulaji Bashiru alishindwa kutengua kauli yake ile.

Ni wazi kiroho kuwa kwakuwa alishakataa ile nafasi kubwa zaidi ya ukatibu mkuu basi kudra zimemfanya awe katibu mkuu kiongozi aliyehudumu muda mfupi zaidi.

Kama bado anajisikia kushika nafasi nyingine kubwa basi atengue kauli yake ile na mambo yatakuwa safi.

Midomo huumba... Tuwazayo na tutamkayo kwa asilimia 80 huwa...!!!! Tumakinike na kauli zetu.!

View attachment 1741824
Mungu hadhihakiwi.
 
Back
Top Bottom