Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,505
- 51,106
Alianza na kauli, kwa kusema chama chenye dola kushindwa kutetea dola yake ni uzembe!. Alishangaa iweje uwe na dola kisha upoteze dola.
Naam!. Kwenye uchaguzi huu tumeona alichomaanisha!. Bila shaka sote tuliona nini maana ya kutumia dola kubaki na dola, Tulishuhudia Kura kwenye vikapu vya akina mama, nyingine kwenye mabegi. Wapo waliozishika hizo kura na kuzipekeka polisi, polisi wakawajibu kwa mkato tu "Hatushughulikii masuala ya uchaguzi".
Maelfu kwa maelfu ya Mawakala wa vyama shindani wakapigwa zengwe, wakazuiwa kuingia, na wale walioningia wakapigwa zengwe wasipate nakala za matokeo.
Kule Zanzibar watu wakaonekana wanaopiga kura kwa lumbesa, mtu mmoja kura lundo.
Falsafa ya Bashiru Ally Kakurwa mtoto wa Kiislamu huyo aliyepitia madrasa!
Lakini huyu ni mwalimu wa chuo kikuu, msomi mkubwa, kafundisha wanafunzi wengi tu nadharia za demokrasia, ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi ya nchi yao wenyewe. Kafundisha sana masuala ya class struggle, ni role model wa maelfu ya wanafunzi wake wa ndani ya darasa na nje ya darasa! Sijui ametuma ujumbe gani kwa watu ambao walikuwa inspired naye kabla ya kuingia kwenye siasa pale wanapoona amekuwa katibu mkuu wa chama ambacho leo kimenufaika kwa mchakato feki na haramu kabisa wa uchaguzi, uliogubikwa na wizi wa kura wa kutisha katika historia ya nchi hii toka uhuru!
Lakini cha kuchekesha zaidi, Sheikh Bashiru Ally Kakurwa eti ni mjamaa, mfuasi wa Nyerere. Eti naye alikuwa mdau mkubwa wa Kigoda cha mwalimu. Eti naye alikuwa akiimba kama kasuku kuhusu uadilifu na sense ya haki ya mwalimu Nyerere.
Haya hatukuhadithiwa, tumeona kwenye TV mihadhara ya kigoda cha Mwalimu, Tumemuona Bashiru Ally Channel ten akielezea falsafa za haki, uadilifu, demokrasia, uhuru, umoja, n. k lakini hatukujua kuwa miaka michache baadaye, Bashiru huyuhuyu atakuwa ni katibu mkuu wa chama kilichonufaika kwa kuhujumu wananchi kuwaweka madarakani watu wawatakao wao wenyewe kupitia sanduku la kura!
Nikiangalia miaka michache ijayo nini itakuwa Legacy ya Bashiru Ally kwenye utumishi wa CCM, Siioni zaidi ya kushiriki kuwanyima wananchi viongozi na wawakilishi wawatakao watokanao na ridhaa zao wenyewe!. Kiufupi naye ni mshiriki asiyeweza kujivua lawama kwa dhulma hii kubwa waliyotendewa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata kama ngazi ya urais wa Muungano mlikuwa mkiitaka kwa udi na uvumba lakini Bashiru, hivi kweli Hussein ni wa kumshinda Maalim Seif kwa zaidi ya 57%?
Bashiru hivi kweli Tulia ni wa kumshinda Sugu Mbeya?
Hivi kweli Zitto ni wa kushindwa na yule Jamaa pale Kigoma? na mifano ya ya namna hii ni mingi nchi nzima!
Msomi na Mjamaa Bashiru hongera sana kwa kushiriki ipasavyo kuithibiti demokrasia vilivyo!, Maana sasa demokrasia ni kama adui yenu mliyefanikiwa kumdhibiti asifurukute!, But ngoja nikwambie kitu kimoja mko myopic sana kwa hizi moves zenu, kwa sababu ili mfanikiwe katika lengo lenu hilo ovu itabidi muwe wanafiki zaidi, walaghai zaidi, waonevu zaidi, madhulumati zaidi, msiheshimu wananchi zaidi.
Mtafanya hivyo mpaka mtakapokutana na kigingi kutoka kule ambako hamkukudhania kabisa, kisha hapo common sense zitawarudia kuwa ni USELESS KUDHANI KIKUNDI KIDOGO KINA AKILI KULIKO UMMA, maana umma utasimama na nguvu yeyote itakayokema yaani itakayoweka kigingi cha kuzuia dhulma zenu, nguvu ya kuzuia uonevu wenu, nguvu ya kuzuia ulaghai wenu!. Nguvu hiyo Ama inaweza iwe ni nguvu yoyote ya ndani ya nchi au ya nje ya nchi au zote mbili kwa pamoja as long as wananchi wataona hii inasimama nao na inawatetea wataiunga mkono kwa maua, nderemo, vifijo, bashasha, kucheza, kusifu, n. k!.
Mwalimu Bashiru, Nikukumbushe tu kuwa mahali popote pale duniani uchaguzi hovyo na corrupt, huzaa serikali hovyo na corrupt na hutengeneza bunge hovyo na corrupt lisiloogopa wananchi bali wale waliowawezesha kuingia bungeni kwa njia corrupt!. Kamwe haiwezekani kupata maendeleo kwa bunge na serikali ya aina hiyo, maana hiyo si serikali na bunge la watu kwa ajili ya watu, bali ni kundi tu la watu wachche tu wenye "special interests" lenye kumiliki silaha na kwa silaha hizo huwatisha wananchi wasinyanyuke na kudai haki yao ya kuwa na viongozi watokanao na ridhaa yao, lakini ukweli ni kuwa serikali ya hivyo na bunge la hivyo havina legitimacy mbele ya watu hao!
Bashiru Umeshiriki dhambi ya kuwadhulumu haki wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, unajisikiaje, "umewaweza" wapinzani au "umeiweza" nchi?. Kwamba umeacha alama ya heshima au alama ya aibu?
Shame on you!