Dk. Ulimboka: Niko fit! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Ulimboka: Niko fit!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Aug 13, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  VIDEO:
  Dr Ulimboka arejea nchini akitokea Afrika Kusini kwenye matibabu. - YouTube

  Dk. Steven Ulimboka amerejea leo nchini bna kutyoa shukrani za dhati kwa watanzania kwa dua na michango yao kuinusuru afya yake na kuahidi kuendeleza mapambano dhidi ya huduma bora za afya na maslahi kwa madaktari.


  Ulimboka amerejea nchini wakati jamii bado ikiwa katika kizungu mkuti cha nani hasa aliyemteka na kumpa mateso makali Dk. Steven Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini na kiu ya wananchi sasa ni kutaka kujua ukweli kupitia kwake.

  Daktari huyo ambaye amejizolea umaarufu nchini kwa harakati za kudai haki na maslahi ya madkatari na huduma bora Hospitalini amerejea leo jijini Dar es Salaam akitokea nchini Afrika kusini ambako alipelekwa na Madaktari wenzake tangu Juni 30 mwaka ambako alikuwa akitibiwa majeraha aliyoyapata baada ya kutekwa na kundi la watu wasiojulikana.

  Dk. Ulimboka alitekwa, kupigwa na kutelekezwa kwenye Msitu wa Pande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaa lilidai kuwa aliyemteka daktari huyo ni raia wa Kenya ambaye tayari wanamshikilia.

  Dk. Ulimboka amewasili leo majiya ya saa 8 alasiri katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na SA Airways na kulakiwa kwa shangwe, hoihoi nderemo na vifijo kutoka kwa ndfugu jamaa na marafiki sambamba na madaktari wenzake na wanaharakati.

  Hakika Mungu yupo! Na anatenda miujiza yake, Ulimboka inakumbukwa aliondoka nchini akiwa hajiwezi kutokana na hali yake kuwa mbaya na kubebwa katika machela lakini leo amerejea mzima wa afya na anatembea mwenyewe.

  Licha ya vurugu za hapa na pale ambazo zilikuwa zikisababishwa na ndugu na jamaa ambao walitaka wanahabari wasilidake tukio hilo la kihistoria mithili ya Mtanzania kutwaa medali ya Dhahabu Olympic 2012 huko London lakini paparaziu waliweza kunasa taswira kadhaa na kuongea nae.

  “Nimepona ndugu zangu….nawashukuru nyote mlioniombea, watanzania, madaktari, ndugu na jamaa zangu nashukuru pia kunisaidia kupata matibabu bora hadi leo hii narudi nyumbani, niko fiti nikitembea mwenyewe,” alisema Dk. Ulimboka.

  Miongoni mwa wana harakati ambao Father Kidevu Blog ilifanikiwa kuwaona uwanjani hapo ni pamoja na Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Usu Malya na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari wanawake(TAMWA), Ananileya Nkya.

  Wanaharakati hao walijipamba na mabango kadhaa yaliyo kuwa na jumbe za “Dk Ulimboka karibu nyumbani uliumizwa kikatili ukitetea afya bora kwa watanzania.” “Dk Ulimboka damu yako ilimwagika na kuamsha ari kwa wananchi kudai huduma bora za afya.” “Dk Ulimboka wewe ni mpigania haki na afya bora kwa wananchi wote Mungu na watanzania wote tuko nawe.

  Nae Katibu wa Jumuiya hiyo Dk. Edwin Chitage ameiambia father Kidevu Blog kuwa kurejea kwa Dk. Ulimboka akiwa mzima ni ishara ya huduma bora aliyoipata akiwa nje ya nchi.

  Usiku wa kuamkia Juni 27, 2012 watu wasiofahamika walimteka, kumpiga, kumng’oa kucha na meno kisha kumtelekeza kwenye msitu wa pande Dk. Ulimboka.

  Wakati amelazwa Hospitali ya taifa Muhimbili chumba cha wagonjwa mahututi Kitengo cha Mifupa (MOI) alikuwa akihudumiwa na jopo la madaktari saba akiwapo Profesa Joseph Kahamba.

  Licha ya jopo jilo la madaktari kumhudumia kwa ukaribu lakini walishindwa kupata baadhi ya vipimo ili kubaini iwapo damu yake ilikua na sumu ama la kwa kusababu baadhi ya dawa zilishindwa kufanyakazi ndfipo uamuzi wa haraka wa kumpeleka nje ya nchi ukafikiwa na wanachi kumchangia fedha kiasi cha shilingi milioni 40 za matibabu yake.

  Aidha Katibu wa Jumuia ya madaktari Dk. Chitage amewaahidi wanahabari kuitisha mkutano mapema ili kujuza umma wa watanzania na dunia kwa kina kuhusu kupona Dk. Ulimboka.
  Chanzo: Father Kidevu Blog
  Dk. Ulimboka atua Dar


  JUMATATU, AGOSTI 13, 2012 06:29 NA GABRIEL MUSHI

  *Asema afya yake imeimarika zaidi, anamshukuru Mungu
  *Apokelewa na mamia Uwanja wa Ndege, gari lake lasukumwa


  HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka amerejea nchini jana. Dk. Ulimboka, alipokelewa na watu wa aina mbalimbali waliokuwa wamefurika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
  Dk. Ulimboka, aliwasili uwanjani hapo, saa 7:55 mchana jana na ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini na kupokelewa na madaktari, waliokuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali, wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake, (TAMWA) Ananilea Nkya.

  Licha ya kuwapo na ulinzi kutoka kwa madaktari, kuliibuka vurugu za hapa na pale ambazo zilipelekea kuzuiwa kumsogelea.

  Akionekana mwenye furaha na kujiamini, Dk. Ulimboka, alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari, huku akibubujikwa na machozi ya furaha.

  “Nashukuru, asanteni sana…nimefarijika na mapokezi yenu, kwanza namshukuru sana mwenyezi Mungu nimerejea salama, ni furaha ya kipekee, nawashukuru ndugu zangu na madaktari wenzangu.

  “Nimerejea salama… afya yangu imeimarika kabisa, namshukuru Mungu kwa hilo. Nakaribisha maswali,” alisema Dk. Ulimboka ambaye muda wote huo, alionekana akilengwa lengwa na machozi.

  Pamoja na Dk. Ulimboka kutoka nafasi kwa waandishi wa habari kuuliza maswali, baadhi ya madaktari na ndugu wa karibu walipinga utaratibu huo.

  Kitendo hicho, kilisababisha kelele nyingi kuibuka, huku wakimshangilia kwa furaha wakisema jembe!.. jembe, jembe limerudi.

  Wakati akielekea kwenye gari nako aliendelea kuimbiwa nyimbo za kishujaa, kama vile ‘vijana msilaleee laleee vijana msilalee, bado mapambano..’ huku wanaharakati nao wakishikilia mabango yaliyoandikwa ‘shujaa karibu nyumbani’, Dk. Ulimboka karibu nyumbani, umeumizwa ukitetea haki ya afya bora, kwa maendeleo ya wananchi.”


  Dk. Ulimboka aliondoka uwanjani hapo kwa kutumia gari aina ya Nissan Safari, lenye namba za usajili T 864 BAV.

  Wakati gari hilo, linaondoka uwanjani hapo, madaktari walilizuia na kuanza kulisukuma hadi geti kuu la kutoka chumba cha wageni maalum.


   
 2. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  sijakuelewa hapo kwenye aya ya tatu unaposema "BAADA YA KUTEKWA NA WATU WASIOJULIKANA"
  Ina maana wewe bado hujui waliomteka dr ulimboka? Tafuta toleo la mwisho la mwanahalisi lililofungiwa utamjua mtekaji.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  [​IMG]
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Tukio la kupigwa kwa dr Uli na kupona kwake ni MUUJIZA WA MUNGU USIO KIFANI,KWA KILA AAMINIYE UWEPO WA ALLAH
   
 5. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  No matter what they did, they didn't stop him.
  Lengo ilikua ni kumdhalilisha na kumvuja ujasiri
  But hawawezi kufanya hivo, maybe awaruhusu
  He says NO to intimidation, na hiyo ni aibu yao

  Hata ambao tulikua hatushobokei mgomo huu
  Sasa tunausnga mkono in the name of freedom!
  #GoUlimbokaGo!, #ALutaContinua!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,497
  Likes Received: 81,829
  Trophy Points: 280

  Wahusika waliomfanyia unyama walijua wameshammaliza, na hii ndio amri waliyopewa na wakubwa wao, lakini Mungu Mkubwa Dr bado anadunda sasa ngoja tuangalie jinsi watakavyoendelea na sinema yao ambayo Watanzania wengi tumeshaistukia hata bure hatuko tayari kuiangalia.
   
 7. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Wapigania haki duniani mara nyingi hawafaidi wao, bali hufaidi wengine. Nchi hii ina watu wachache sana, wanaoweza kuthubutu, nao ni kama Dr Ulimboka. MUNGU AKUREHEMU DR.
   
 8. M

  Mkekuu JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Karibu dk wa ukweli,si yule wa magogoni aliyetaka kukutoa uhai.
   
 9. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,060
  Likes Received: 1,099
  Trophy Points: 280
  All I can say is wow
   
 10. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Welcome back comrade!
  Tuko nyuma yako, pambana.
  Your blood will nourish the tree of freedom.
   
 11. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  is he a dead man walkin??!!
   
 12. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Our God is a loving God!
   
 13. S

  SHEMGUNGA JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 13, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  ulter continous!
   
 14. w

  wade kibadu Senior Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulimboka alifanya harakati kwa makusudi ya mungu na ameteseka mungu akimbembeleza mpaka today kaz kwao magamba.
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  In the morning when I wake up, I will sing my praise unto you my Lord
  I will shout I will dance to you, You have been my help forever ever
  Eeeh My God is good oh, Eeeh My God is good oh
  Eeeh My God is good oh, Eeeh My God is good oh
  Eeeh your God is good oh, Eeeh your God is good oh
  Eeeh your God is good oh, Eeeh your God is good oh
  Moto e moto, moto e moto e mama e
  Simbalelu twende kulumba lose bwana begu(?),zambe wa moyo
  Zambe wa moyo, zambe wa moyo …

  Karibu Dr Ulimboka
  Jua mwenyezi mungu ana mpango mkubwa na maisha yako....
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Watanzania bwana , tunafurahia kuona wengine wakipambana katika ujinga. Hivi suala la mgomo ni la kufurahia kweli, ili watu wa hali ya chini waendelee kudhurika au?
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Hakuna Mungu anayemwamuru mtu kugoma, acha kukufuru wewe, Shetani huyo alimtuma, ila Mungu kamponya ili arudi apime kama alichokuwa akiwafanyia wanyonge kinastahili kweli.
   
 18. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Najua anaongea tu lakini moyoni mwake hana hamu...
   
 19. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  mwambie aliyekutuma ailoweke akili yako kwenye jik ipate weupe wake wa asili! usitutafutie ban!
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kwa nini uwe nyuma yake , na usitangulie mbele yake? teh teh teh , acheni kumdanganya Ulimpoka asije akaingia Mkenge tena, kitendo alichokuwa akiwafanyia wagonjwa Mungu hakipendi, bali kinapendwa na wanaharakati, wanasiasa uchwara na watu wanaopenda kuona vurugu zikitokea nchini.
   
Loading...