Nisichokubaliana na baadhi yenu humu ni hili la WATANZANIA kufa kwa malengo ya KISIASA kama ilivyotokea Arusha na kabla ya hapo Pemba. Hakuna kifo kinachokubalika lakini hili la vifo vya kisiasa halina TIJA wala maana yoyote kwa Mtanzania wa kawaida. Ni afadhali Mtanzania afe kwa kudai AJIRA, kulalamikia bei ya kilo ya unga, bei ya mkate, bei ya umeme, bei ya maji, karo kubwa za shule, huduma mbaya za elimu kwenye mashule ya UMMA na mambo yanayofanana na hayo.
Tusiendelee kuua watu wetu kwa malengo ya KISIASA ambayo hayawabadilishii lolote watu wetu. Wakati wa kampeni, Dr Slaa alisisitiza mara kwa mara juu ya kutomwaga damu ya Watanzania ili aende IKULU. Ni nini kinafanyika sasa?