Maishamapya
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,279
- 375
Kimsingi itakuwa vigumu sana kwa Tv zetu kuonyesha video inayopingana na Taarifa ya Serikali, Labda wapeleke Tv za nje au za mashirika ya Dini
Kwa taarifa yao ni kuwa mkanda huo utagawiwa kwa umma pia. Hivyo hata TV zikibana watu watauona kwenye sebule za watu; vijiweni na hata kwenye baa. Kwa taarifa tu ni kuwa hakuna sumu mbaya inayoenea kwa haraka kama ile inayosambazwa kupitia mtandao huru (nguvu binafsi). Sote sasa tunajua kilichomtoa yule Rais wa Tunisia. ... Si kupitia vyombo vya habari vya umma ila mitandao. Taarifa zikafikia watu, waliposhtuka watu wako barabarani. Endapo TV zitagoma kuonyesha zitazidisha kiu ya watanzania kuusaka ukweli. Ukweli unatabia moja, huwa haufichwi mvunguni maana utatoka tu siku moja.
Aluta Continua CDM!