Dk. Slaa: Tutajibu mapigo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa: Tutajibu mapigo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kilimasera, Jan 17, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinaandaa mikanda ya video itakayoonyesha matukio yote yaliyotokea wakati wa vurugu zilizozaa maafa wakati wa maandamano ya wanachama wa chama hicho katika Jiji la Arusha mwanzoni mwa mwezi huu.

  Hatua hiyo ya Chadema kuandaa mikanda ya tukio hilo inakuja kama majibu ya kile kilichofanywa na Jeshi la Polisi ambalo kwa siku kadhaa wiki iliyopita lilisambaza katika vituo vya televisheni video za matukio ya Arusha ambazo zimezusha manung'uniko ya chini kwa chini kutoka kwa wananchi wa Arusha na ndani ya chama hicho cha upinzani.

  Katika kujibu mapigo ya polisi, chama hicho kimesema hakina la kuficha kama walivyofanya viongozi wa jeshi hilo, badala yake wataonyesha tukio zima kabla, wakati na baada ya mkutano wao uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Januari 5 mwaka huu.

  Mgogoro kati ya polisi na Chadema ulitokana na maelekezo tofauti ya kutofanya maandamano kwa mujibu wa amri ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) iliyotolewa saa chache kabla ya kuanza kwa maandamano hayo yaliyosababisha jeshi kutumia risasi za moto na mabomu kuwatawanya waandamanaji hao.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Willibrod Slaa alisema kwa sasa wanakamilisha mkanda huo ambapo utatolewa kwa waandishi wa habari na umma wakati wowote kuanzia leo.

  Dk. Slaa alisema ingawa Jeshi la Polisi limetoa mkanda wao bado wana nafasi ya kuufahamisha umma kwa kutoa mkanda ambao haujahaririwa ili umma ufahamu kilichotokea.

  "Kama lilivyofanya Jeshi la Polisi sisi hatutaki kuzungumzia lolote juu ya mkanda wao… ila tunategemea kuonyesha ‘documentary' ya tukio zima hatua kwa hatua bila kuhariri kisha hapo ndiyo tutatoa kauli yetu," alisema Dk. Slaa ambaye alionyesha dhahiri kukerwa na video za polisi ambazo zinalalamikiwa kwa ‘kuchakachuliwa'.

  Alisema kwa sasa timu nzima ya viongozi wa chama hicho iko mikoani na inatarajia kurudi ili kuhakikisha inatoa taarifa yenye uhakika ya vurugu za maandamano hayo yaliyosababisha watu watatu kupoteza maisha na wengine 29 wakijeruhiwa kwa risasi na mabomu.

  Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi lilivitangazia vyombo vya habari kuwa IGP Said Mwema angekuwa na mkutano na waandishi wa habari lakini waandishi walipofika ofisini kwake alijitokeza Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja ambaye alitoa tamko akiwatuhumu wafuasi na viongozi wa Chadema kwa vurugu zilizosababisha mauaji kwenye mji huo wa kitalii.

  Kamishna huyo aliwawekea waandishi wa habari mkanda wao wa video ambao haukuonyesha namna viongozi wakuu wa Chadema walivyokamatwa huku pia ukiwa hauna picha za matukio mengine ambayo yalionyeshwa katika vituo tofauti vya televisheni siku ya tukio na siku moja baadaye.

  Kamishna Chagonja alitumia maelezo ya mdomo, maandishi na picha za video kuwaeleza wanahabari kile alichokiita "taarifa ambazo wananchi hawajaambiwa kuhusu vurugu za Arusha zilizotokea Januari 5 mwaka huu" ambazo kimsingi zilibeba tuhuma dhidi ya viongozi wa Chadema kuwa chanzo cha vurugu.

  Hata hivyo, picha za video zilizoonyeshwa kwa wanahabari zilionekana dhahiri kupingana kwa kiasi kikubwa na maelezo na sababu zilizotolewa kama kigezo cha kuyasambaratisha maandamano hayo kwa silaha.

  Picha hizo zilionyesha kundi moja tu la viongozi na wafuasi wa Chadema lililoanza maandamano kwa amani kutoka eneo ilipo Hoteli ya Mount Meru likitumia njia moja kuelekea Sanawari Mataa na hakukuonekana makundi mengine yaliyokuwa yakitumia njia nyingine kuandamana ambayo yangeleta bugudha na kuwapa polisi shida ya kulinda kama alivyodai kamishna huyo.

  Aidha, picha hizo za video pia hazikuonyesha waandamanaji walioanza kufanya fujo au kuashiria kufanya fujo mpaka walipofika eneo la Sanawari Mataa ndipo Jeshi la Polisi lilipovuruga hali ya amani kwa kuanza kufyatua mabomu ya machozi.

  Kwa upande mwingine, sinema hiyo iliyorekodiwa na Jeshi la Polisi kuhusu matukio yaliyotokea Arusha haikuonyesha mazingira ya kujeruhiwa kwa Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba wa Dk. Slaa.  Dk. Slaa: Tutajibu mapigo
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sikio la kufa halisikii dawa!
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  huu mgogoro naona utachukua miaka mingi sana kwisha ni wa kihistoria
   
 4. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Imekula kwa polisi,niwajuavyo cdm hawana utani kwenye mambo ya msingi kama haya
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kumbe na wao walikua wananasa matukio sasa kesi hii naona inaelekea patamu sema inauma sababu imepoteza maisha ya wanaharakati
   
 6. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  tena hizo videos wazigawe bure kila mahali cause nadhani vyombo vya habari huenda visirushe....
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  vyombo vya habari vyote wanaweza kutorusha?hata IPP
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  mmh! Bure tena.
   
 9. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kugawa bure ni ngumu may be wazionyeshe bure hv kwanini vyama vya siasa visiwe na vituo vyao vya tv au redio
   
 10. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  siunajua kitu cha bure wananchi wamepigikiga ukiwaambia wanunue video ya mauaji ya Arusha hata kama pesa wanayo wataona bora wakanywe lager au wanunue Kanumba and Co.
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  na wanavyompenda kanumba kuliko siasa
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Pamoja na hiyo inayoandaliwa, kuna unedited copy iliyochukuliwa kwa njia ya satellite ndiyo itakayotoa picha kamili kwa wakati na sehemu mwafaka juu ya unyama wa jeshi la polisi dhidi ya raia.

  Wala tusijisumbue sana malumbano na kuficha taarifa kamili wakati technolojia ipo kwa ajili ya kututumikia juu ya mambo kama haya. Zomba, pole sana umejitahidi mno kuokoa sura hapa lakini jitihada zimechelelew kwa karne ya 21 hii.

  Kila kitu hadi sasa kiko kweupeeee!!!!
   
 13. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Usicheze na propaganda... unakumbuka marudio ya mahujiano ya mdahalo wa Dr. Slaa ITV ulivopigwa Tick Tack...., hakuna neutral media nchi hii ndugu yangu.... everyone is looking for Numero Uno
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  they feared serikali
   
 15. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Sio ngumu ndugu yangu kwanza wanaweza wakaupload Youtube na free online tubes zote...

  DVD ukinunua kwa jumla na Kuziburn Cost per unit haitazidi hata 500/= kama hawawezi hiyo kazi waniambie tawafanyia... au kama hawana pesa wauze shangingi moja la mbunge... watafanya hii kazi na chenji itabaki ya kuwapeleka watoto kumi shule.
   
 16. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  polisi ndio watajuta kuwafahamu wakombozi wa tanzania,nakala nyingine ipelekwe kwa Ocampo.....
   
 17. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Naomba cd zikitoka nifahamishwe ziko wapi nkanunue. Zitakuwa muhimu kwa maisha yangu Tanzania. Alaf polisi cjui wanadhani wako CCP moshi wanawafundisha form four failure/3f. Yani wanaonesha picha,ikifika mke wa dr.slaa anapigwa wanakata,wanachomekea pale Lema anafoka wanakata,wanaonesha Ndesamburo anatoa maneno makali kwa uchungu wanakata,wanaonesha vioo vya jengo la ccm lililoharibiwa wanakata hata bila kuonesha nani alikuwa anatupa mawe kwenye jengo. Iyo ni video camera gani inayochuja kuonesha mabaya ya upande mmoja! Dr.wa ukweli kazi uliyoinza ya kujenga Tanzania mpya ni kubwa,nakutakia kheri.
   
 18. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mwaga mboga namwaga ugali...hii speed hii siyo ya sikio la kufa. Ni speed ya kuvunjana mbavu. Hata Tunisia mambo hayakuanza siku moja. In our best ways and wisdom, tusijaribu kutafuta short cut kwenye mambo yanayotaka kutumia vichwa vyetu. Tutaiharibu hii Tanzania.
   
 19. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nahofia askari waliofyatua risasi na kuua hao waTz wenzao. Wakionekana maisha yao mkononi!
  Haya mi yangu maombi tu nchi ielekee kwenye maziwa na asali, regardless of how....that God knows!
   
 20. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo kinaandaa mikanda ya video kuonesha ukweli ya yaliyojiri Arusha siku ya maandamano 5/1/2011. Hii inaonekana kupinga ule mkanda wa video uliochakachuliwa uliooneshwa kwenye televisheni za TBC1,ITV na Channel 10.

  Kwa mujibu wa Dk. Slaa ni kuwa video hiyo itaoneshwa kama ilivyo na haitahaririwa ili watu wajionee ukweli na waone matukio yote maovu yaliyofanywa na jeshi la Polisi ambayo hayakuoneshwa katika video iliyoandaliwa na Idara ya Habari Maelezo. Tunaambiwa tukae mkao wa kula ili tuone na tupate taarifa kamili ya CHADEMA kuhusu maandamano hayo. Haya mwaka wa tabu kwa JK

  Dk. Slaa: Tutajibu mapigo

  • LENGO NI KUJIBU ‘UCHAKACHUAJI' WA POLISI

  na Betty Kangonga

  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinaandaa mikanda ya video itakayoonyesha matukio yote yaliyotokea wakati wa vurugu zilizozaa maafa wakati wa maandamano ya wanachama wa chama hicho katika Jiji la Arusha mwanzoni mwa mwezi huu.

  Hatua hiyo ya Chadema kuandaa mikanda ya tukio hilo inakuja kama majibu ya kile kilichofanywa na Jeshi la Polisi ambalo kwa siku kadhaa wiki iliyopita lilisambaza katika vituo vya televisheni video za matukio ya Arusha ambazo zimezusha manung'uniko ya chini kwa chini kutoka kwa wananchi wa Arusha na ndani ya chama hicho cha upinzani.

  Katika kujibu mapigo ya polisi, chama hicho kimesema hakina la kuficha kama walivyofanya viongozi wa jeshi hilo, badala yake wataonyesha tukio zima kabla, wakati na baada ya mkutano wao uliofanyika kwenye viwanja vya NMC Januari 5 mwaka huu.

  Mgogoro kati ya polisi na Chadema ulitokana na maelekezo tofauti ya kutofanya maandamano kwa mujibu wa amri ya Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) iliyotolewa saa chache kabla ya kuanza kwa maandamano hayo yaliyosababisha jeshi kutumia risasi za moto na mabomu kuwatawanya waandamanaji hao.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Willibrod Slaa alisema kwa sasa wanakamilisha mkanda huo ambapo utatolewa kwa waandishi wa habari na umma wakati wowote kuanzia leo.

  Dk. Slaa alisema ingawa Jeshi la Polisi limetoa mkanda wao bado wana nafasi ya kuufahamisha umma kwa kutoa mkanda ambao haujahaririwa ili umma ufahamu kilichotokea.

  "Kama lilivyofanya Jeshi la Polisi sisi hatutaki kuzungumzia lolote juu ya mkanda wao… ila tunategemea kuonyesha ‘documentary' ya tukio zima hatua kwa hatua bila kuhariri kisha hapo ndiyo tutatoa kauli yetu," alisema Dk. Slaa ambaye alionyesha dhahiri kukerwa na video za polisi ambazo zinalalamikiwa kwa ‘kuchakachuliwa'.

  Alisema kwa sasa timu nzima ya viongozi wa chama hicho iko mikoani na inatarajia kurudi ili kuhakikisha inatoa taarifa yenye uhakika ya vurugu za maandamano hayo yaliyosababisha watu watatu kupoteza maisha na wengine 29 wakijeruhiwa kwa risasi na mabomu.

  Wiki iliyopita, Jeshi la Polisi lilivitangazia vyombo vya habari kuwa IGP Said Mwema angekuwa na mkutano na waandishi wa habari lakini waandishi walipofika ofisini kwake alijitokeza Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Paul Chagonja ambaye alitoa tamko akiwatuhumu wafuasi na viongozi wa Chadema kwa vurugu zilizosababisha mauaji kwenye mji huo wa kitalii.

  Kamishna huyo aliwawekea waandishi wa habari mkanda wao wa video ambao haukuonyesha namna viongozi wakuu wa Chadema walivyokamatwa huku pia ukiwa hauna picha za matukio mengine ambayo yalionyeshwa katika vituo tofauti vya televisheni siku ya tukio na siku moja baadaye.

  Kamishna Chagonja alitumia maelezo ya mdomo, maandishi na picha za video kuwaeleza wanahabari kile alichokiita "taarifa ambazo wananchi hawajaambiwa kuhusu vurugu za Arusha zilizotokea Januari 5 mwaka huu" ambazo kimsingi zilibeba tuhuma dhidi ya viongozi wa Chadema kuwa chanzo cha vurugu.

  Hata hivyo, picha za video zilizoonyeshwa kwa wanahabari zilionekana dhahiri kupingana kwa kiasi kikubwa na maelezo na sababu zilizotolewa kama kigezo cha kuyasambaratisha maandamano hayo kwa silaha.

  Picha hizo zilionyesha kundi moja tu la viongozi na wafuasi wa Chadema lililoanza maandamano kwa amani kutoka eneo ilipo Hoteli ya Mount Meru likitumia njia moja kuelekea Sanawari Mataa na hakukuonekana makundi mengine yaliyokuwa yakitumia njia nyingine kuandamana ambayo yangeleta bugudha na kuwapa polisi shida ya kulinda kama alivyodai kamishna huyo.

  Aidha, picha hizo za video pia hazikuonyesha waandamanaji walioanza kufanya fujo au kuashiria kufanya fujo mpaka walipofika eneo la Sanawari Mataa ndipo Jeshi la Polisi lilipovuruga hali ya amani kwa kuanza kufyatua mabomu ya machozi.

  Kwa upande mwingine, sinema hiyo iliyorekodiwa na Jeshi la Polisi kuhusu matukio yaliyotokea Arusha haikuonyesha mazingira ya kujeruhiwa kwa Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba wa Dk. Slaa.

Loading...