Elections 2010 Dk Slaa on Clouds FM

Dr. Ka kwepa kuifagilia clouds baada ya kuulizwa ana mtazamo gani kuhusu clouds kua radio ya vijana inayojikita kwenye burudani zaidi? Badala yake kajibu kijumla swala michezo!
 
So far hadi sasa, Hando yuko SMART. Maswali mazuri, anawakilisha wasikilizaji
 
Clouds wamesoma alama za nyakati, wamegundua chadema ndiyo chama dola kuanzia wiki ijayo na clouds hupiga sana serikalini
 
Siamini watu wa Masaki kuuliza maswali.

Kuna mlevi mmoja anasema matatizo ya Tanzania ni ya Afrika nzima. Ni kama vile anataka Dr. aongelee jinsi ya kutatua matatizo ya Afrika nzima, badala ya kujikita Tanzania.
 
anazungumzia upungufu wa amani unaweza kusababishwa hata na ukosefu wa ajira na maisha magumu
 
Amani imetokana na mfumo mzuri wa elimu hahahhaha Mwalimu huyo!
 
Jamani nimeshindwa kueleza yooote anapiga mawe kishenzi hapa anaongelea mdororo wa uchumi haaaaaaa huyu jamaa anaakili sana!
 
Naona sera anazozinadi Dr Slaa ni za msingi na zina tija ndani yake hasa ukiangalia kwenye suala la elimu ambalo ndio jambo la msingi na pia afya kwa kweli mahojiano bila kusahau masuala ya muungano
 
anazungumzia ustawi wa uchumi wa ajirani zetu, wao wanafanikiwa sisi bado, ina maana kwetu kuna tatizo.
yy anachaguliwa kuwa rais wa taz na ndio atapigania maslahi yao
 
Ninahoji UMAKINI na UADILIFU wa Dr Slaa!!!
Na Kamarade wa Kamarade

Katika mazingira ya sasa ambapo dunia imelazimishwa kuamini kuwa kuna tofauti ndogo sana kati ya Uislamu na Ugaidi, ninaingiwa na wasiwasi sana na hatua ya Dr Slaa kumuita Kikwete ni gaidi na kuwa chama chake ni cha magaidi.

Wasiwasi wangu unatilia maanani pia kuwa uchaguzi wa wiki hii unaenda katika historia kuwa ni uchaguzi ulionyesha dalili zote za mgawanyiko wa ufuasi wa wagombea katika misingi ya udini zaidi ya misingi ya uchama kama ambavyo tulizoea hapo kabla.

Kauli mbiu ya mgombea wa CHADEMA mwaka huu, yaani Dr Wilboard Slaa ni UADILIFU, UMAKINI na UWAJIBIKAJI.

Kauli ya Dr Slaa ya leo Jumanne tarehe 26 Oktoba katika viwanja vya Temeke Mwembe Yanga, ambapo safari yake ya kugombea urais ilianza isivyo rasmi miaka mitatu iliyopita, pamoja na kauli nyingine alizotoa tangia kampeni hizi zianze, zinanifanya nijiulize maswali magumu ambayo wangi wetu tulishindwa kufanya hapo kabla kutokana na sababu mbalimbali.

Ni jana tu katika gazeti la Majira iliripotiwa kuwa Dr Slaa alidai kuwa yeye siye aliyeanzisha udini isipokuwa ni mgombea wa CCM Jakaya Kikwete. Amedai kuwa Kikwete amekuwa akitumia nafasi yake kupendelea Waislamu. Na pia amedai kuwa hata timu yake ya kampeni ya Kikwete ni ya waislamu watupu na pia mgombea mwenza wake naye pia ni Muislamu.

Lakini mbali na kauli hizi, Dr Slaa amewahi kukaririwa huko Iringa akidai kuwa karibu nusu ya maafisa wa usalama wa taifa wanaripoti kwake. Tamko ambalo ukichukulia historia yake ya kufanya kazi katika ikulu yetu na dhana iliyojengeneka kuwa kashfa mbalimbali ambazo amekuwa akiibua amekuwa anazipata kutoka kwa watu wake katika Idara hiyo nyeti ya Usalama wa taifa letu, ni wazi halikupaswa kutolewa jukwaani kama alivyofanya Dr Slaa.

Hatari ya tamko hilo ni kuwa mara baada ya uchaguzi hali haitakuwa shwari huko katika vyombo vyetu nyeti. Ni wazi matamko kama haya yameshaleta mgawanyiko mkubwa na hali ya kutokuaminiana kati yao kwa kiasi kikubwa. Hali ambayo inaweza kuleta madhara makubwa kwa usalama wa taifa letu. Tumeyaona hayo huko Zanzibar, hatupaswi kuwa wahanga wa madhara ya hali hiyo na upande huu wa nchi yetu.

Siku hiyo alipotoa madai hayo pia alitoa madai kuwa lile tamko la kuwataka watanzania kuwa makini na watu wanaotishia kumwaga damu wakati wa uchaguzi lilikuwa ni tamko la Mnadhimu Mkuu wa Jeshi Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo yeye kama binafsi.

Aliendelea kudai kuwa alifanya Afande Shimbo alifanya hivyo ili kutetea maslahi yake binafasi. Dr Slaa alidai kuwa ana ushahidi kuwa Shimbo kama alivyomwita, amepewa kile alichoita dili la kifisadi la kuingiza matrekta madogomadogo nchini.

Kuanzia hili la kuwa tamko lile lilikuwa ni la Jeshi na sio la vyombo vya ulinzi na uslama ni wazi Dr Slaa ameonyesha dalili za kukosa umakini kama rais mtarajiwa. Nasema hivi kwa sababu najua kuwa kwa uzoefu wake wa masuala ya usalama na utawala katika nchi yetu, alijua wazi kuwa lile halikuwa ni tamko la jeshi bali ni tamko la Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa ambayo Dr Slaa anaijua na anajua utendaji wake na majukumu yake.

Lakini pia Dr Slaa kama rais mtarajiwa naamini anajua wazi kuwa Luteni Jenerali Shimbo katika taratibu za majeshi yetu ndiye alikuwa mkubwa kati ya wasemaji wa vyombo vingine vya ulinzi na usalama waliokuwepo naye siku ile. Hawa ni pamoja na Kamishina Venance Tosi wa Jeshi la Polisi na Afande Kivuyo ambaye ndiye msemaji wa masuala ya intelijensia ya jeshi la Polisi.

Ni wazi kiutaratibu ni Jenerali Shimbo ambaye kwa muda sasa ndiye amekuwa msemaji wa Jeshi la Ulinzi akiwa kama afisa wa ngazi ya juu miongoni mwa watatu hao ndiye alipaswa kulisoma tamko liloandaliwa na kupitishwa na wakuu wa majeshi yetu pamoja na wale wa vyombo vingine vya usalama na sio kuwa tamko lilikuwa ni tamko lake.

Lakini kitendo cha Dr Slaa kuanza kudai kuwa Jenerali Shimbo ana biashara ya kifisadi ya matrekta ilikuwa ni upotoshaji wa hali ya juu kwani ni wazi anajua kuwa katika jeshi letu kuna kitengo cha biashara kinajulikana kama SUMA JKT. Na kwa kushirikiana na Jeshi letu la Ulinzi ambao ndio waliwezeshwa na serikali kusimamia mradi wa matrekta hayo zaidi ya elfu moja, SUMA JKT ndiyo yenye utaalamu wa kutekeleza jukumu la kuyafikisha kwa walengwa na pia kuangalia uwezekano wa kujifundisha teknolojia yake ili hapo baadae jeshi letu kupitia kiwanda chake cha Nyumbu kuweza kuyatengeneza hapa hapa nchini.

Ni wazi kuwa Dr Slaa hakuwa makini ama kwa kutofuatilia ukweli kuhusu madai kwamba kazi hiyo ni kwa manufaa ya Jenerali Shimbo, lakini pia haingii akilini kwa mtu yeyote mwenye chembe ya umakini kuanza kuanzisha uhasama na vyombo vya ulinzi na haswa jeshi letu akiwa safarini kuelekea Ikulu.

Kuhusiana na matamshi yake kuwa Jakaya Kikwete amekuwa akiwapendelea Waislamu, maneno ambayo pia yamekuwa yakiongelewa kichinichini katika vibaraza mbalimbali na hata katika nyumba za ibada, ni wazi Dr Slaa kama mgombea wa nafasi nyeti ya Urais hakupaswa hata kuthubutu kuyafikiria ukiachilia mbali kuyasema hadharani. Alichofanya Dr Slaa ni kuyafikisha manung'aniko hayo yasiyo na chembe ya ukweli katika majukwaa ya kisiasa.

Dr Slaa ametangaza rasmi kuwa mapambano ya chinichini kwa chini kati ya maslahi ya Watanzania wafuasi wa dini ya kiislamu kwa upande mmoja na Watanzania wafuasi wa dini ya Kikristo kwa upande mwengine ni mapambano ya kisasa na sio kijamii kama tulivyozoea hapo kabla.

Lakini pia kwa mujibu wa taarifa zilizokuwa zikizunguka katika radio mbao za jiji letu ni kuwa Dr Slaa kwa kutumia nafasi yake kama Katibu Mkuu wa chama chake, amewashauri na kukubaliwa na Meneja wa Kampeni wake Prof Baregu kuwaamuru wagombea wao kuwasiliana na Maaskofu wa Kanisa la Katoliki katika majimbo yao ili waweze kutumia "mtandao wa kanisa" kulinda kura zao dhidi ya "hujuma za CCM".

Ukichukulia hayo na hili la leo, ni wazi kuwa ama Dr Slaa ana mapungufu makubwa katika Umakini anaoupigia kauli mbiu ama basi zile dalili za kuwa anaweza kushinda na kuukwa urais siku chache zijazo zimemchanganya kiasi cha kumfanya kuwa tayari kufanya lolote lile ili kuhakikisha kuwa anapata kila kura anayoweza. Hata kama itabidi kuigawa nchi katika mapande mapande.

Zaidi ya matamshi hayo, Dr Slaa ambaye amekuwa akiahidi uendeshaji wa serikali makini pindi atakapochaguliwa, huko nyuma amekuwa akifanya makosa mbalimbali ambayo nayo pia yanaibua maswali na hoja kadhaa kuhusiana na umakini wake kama Rais Mtarajiwa.

Moja ya matendo hayo ni jinsi gani alivyolishughulikia suala la mahusiano yake na mwanamama mmoja ambaye yasemekana ni mke halali wa mtu mwengine. Kati ya mambo ambayo amekuwa akidai kama utetezi wake ni lile la kuwe eti hakujua kuwa mwanamama yule ni mke wa mtu na hivyo hana kosa kisheria wala kimaadili.

Kwa mtu yeyote anayethamini heshima ya Urais, changamoto na majukumu yake, ni wazi atajiuliza maswali mengi zaidi kutokana na utetezi kama huu.

Hivi kweli yawezekana kabisa mtu ambaye hata kabla hajatangazwa kuwa mgombea Urais kupitia chama chake ilikuwa ni siri ya wazi kuwa ndiye alikuwa na nafasi kubwa kama sio pekee ya kugombea urais wa nchi kujiingiza katika mahusiano na mwanamke na hata kufikia kuishi naye pamoja na watoto wa mwanamke huyo bila ya kuhoji hali halisi ya mahusiano ya mwanamke huyo na baba watoto wake. Hili linaleta maswali pia kuhusiana na uthabiti na umakini wa chama chake kwa ujumla.

Lakini je historia inatufundisha nini jinsi ya wale kina mama na kina baba ambao wanaonyesha dalili za kuwa watu wakubwa kidunia ambao hubambikiwa wenza ambao ama wana nia ya kuhakikisha wanafikia kiti cha enzi wakiwa nao ili kuhakikisha maslahi yao ama kikundi Fulani nyuma yake ama wale ambao hupenyezwa kwao pengine hata na vyombo vya dola ama makundi ambayo yana nia ya kukudhuru huko mbeleni, iwe kisiasa ama maisha.

Na kama ni kweli kuwa Dr Slaa amekuja kujua ukweli huo na hivyo kuthibitishia umma kuwa mwanamke huyo hakuwa mkweli kwake katika karibia mwaka na zaidi waliokuwa wakiishi pamoja, iweje aendelee kuwa na imani na mtu kama huyo na zaidi kupanda naye na kumuweka mbele katika majukwaa ya kisiasa.

Lakini hili pia linaleta maswali mengine. Suala la Uadilifu analolitumia kama kauli mbiu ama dira ya utawala wake kama akishinda.

Hivi katika dunia yetu hii ambayo wazee tumekuwa tukipigia makelele sana janga la kushuka kwa maadili kwa vijana wetu, ni mfano gani ambao Dr Slaa anauonyesha mbele ya vijana na watoto zetu. Ni maadili gani anayo halalisha kwa makeke kiasi hicho kama ambavyo wale anaowaita kuwa ni maifsadi wafanyavyo?

Lakini pia hili la Uadilifu linakwenda zaidi ya hapo.

Dr Slaa akiwa kama Katibu Mkuu wa CHADEMA na kwa mujibu wa katiba yao ndiye anayepaswa kuwa msimamizi mkuu wa masuala yote ya kifedha. Lakini pia ndiye anayepaswa kusimamia na kuripoti ipasavyo matumizi yote ya fedha yakiwemo yale ya ruzuku ambayo ni kodi yetu anayotuahidi kuwa anaenda kuiokoa mikononi mwa wale tuwaitao mafisadi.

Kwa mujibu wa Mkaguzi Mkuu wa mahesabu ya serikali hivi karibuni, alitaarifu kuwa tangia miaka miwili iliyopita baada ya sheria ya kumpa wajibu wa kukagua matumizi ya fedha za ruzuku ziendazo katika vyama vya siasa, ni CCM tu ndiyo waliowahi kuwasilisha mahesabu yao kwake. Akiwa na maana hakuna chama kingine chochote kikwemo CHADEMA ambacho kimetekeleza jukumu hilo la kiuadilifu. Hili linaleta swali kubwa kuhusu Uadilifu wa Dr Slaa na pia chama chake.

Lakini pia wakati wa mapambano makali kati ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA marehemu Chacha Wangwe, kulikuwa na taarifa ama tuhuma kuwa Dr Slaa aliamuru vijana wake akiwemo John Mnyika na mwengine aliyetajwa kama Mtemelwa, kukusanya risiti bandia ili ziweze kuwakilishwa kwa wafadhili wa chama hicho huko ughaibuni. Kwa mujibu wa madai hayo, mambo hayo yalifanyika mara baadaya Uchaguzi wa mwaka 2005. Hili nalo linaleta maswali magumu kuhusu uadilifu anaoahidi Dr Slaa na CHADEMA kama chama.

Zaidi ya hayo, kumekuwa na madai miongoni mwa viongozi wa CHADEMA kulumbana kutokana na Dr Slaa kama Katibu Mkuu na Mkuu wa Sekretariat ya chama hicho kushindwa kuwasilisha mahesabu ya mapato na matumizi ya chama hicho kwa miaka takribani mitano sasa katika Baraza Kuu la chama kama ambavyo katiba ya chama hicho inavyotaka.

Mbaya zaidi hata sasa wakati kukiwa na sheria kali ya Matumizi ya Fedha katika Uchaguzi ambayo Dr Slaa alikuwa mmoja wa vinara wa kuipigia kelele kupelekwa bungeni na kupitishwa, yapo malalamiko kuwa kiasi kikubwa cha fedha ambazo wafadhili mbalimbali wa chama hicho wamekuwa wakizitoa kabla na baada ya kuanza kwa kampeni hazijawakilishwa kwa mhazini wa kamati ya kampeni anayetajwa kwa jina la Sussan.

Hii ni pamoja na zile shilingi milioni 100 ambazo miezi kadhaa iliyopita zilitolewa kwa mbwembwe na mfanyabiashara machachari Mzee Sabodo. Fedha ambazo inadaiwa kuwa tangia Mwenyekiti Mbowe apokee cheki yake, amekataa kuziwasilisha kwa mweka hazina wa kampeni wala Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho na kuamua kuenda nazo huko Uchina ambako yasemekeana alifanya manunuzi ya vifaa vya kampeni bila ya kuwahusisha wahusika. Na hadi sasa hakuna mahesabu aliyoripoti ama kukabidhi kwa chama.

Na hili sio mara ya kwanza kutokea na mbaya zaidi ni mambo ambayo yamezoeleka ndani ya CHADEMA yakiwa na baraka za Dr Slaa kama katibu mkuu na msimamizi mkuu wa fedha wa chama.

Kauli mbiu hii ya Uadilifu huu pia inatikiswa na madai ya kuwepo kwa jitihada za Mwenyekiti wa CHADEMA Bwana Mbowe, alikuwa akijaribu kulazimisha wale wanao daiwa ni watu wake kuwekwa katika nafasi za juu za wateule wa viti maalumu bungeni wa chama hicho tofauti na alama na vigezo vyao halisi. Taarifa hizo zilidai kuwa katika hili Dr Slaa aliungana mkono na Mwenyekiti wake na hivyo kuwalazimisha wazee wa chama hicho kuja juu na kumpinga Mwenyekiti wao hadharani kwa mara ya kwanza.

Hayo yamefanyika sasa baada ya miaka mitano ya chama hicho kutikiswa na madai kama hayo katika uteuzi wa wabunge wa viti maalumu waliokiwakilisha chama hicho miaka mitano iliyopita.

Mambo kama haya siyo tu yanahoji uthabiti wa hoja ya Uadilifu na Umakini ambayo Dr Slaa na CHADEMA wamekuwa wakiitumia kuikosoa CCM na kuwaahidi watanzania kuwa wataisimamia ipasavyo lakini pia linazua maswali dhidi ya umakini wa Dr Slaa kama kiongozi ambaye anaweza kupewa ridhaa ya watanzania kuliongoza taifa katika jitihada za kurudisha umakini, uadilifu na uwajibikaji.

Nimeamua kuhoji haya sasa kwa kuwa hapo mwanzo wengi tulidhani kuwa Dr Slaa hataweza kushinda na CHADEMA wataweza tu kuongeza viti bungeni, jambo ambalo wengi tungependa kuona likitokea.

Lakini ukweli ni kuwa hivi sasa kumejengeka hisia ya kuwa kuna uwezekano wa Dr Slaa kushinda uchaguzi na kuwa Rais wetu atakeyekabidhiwa mamlaka ya kuongoza taifa letu lakini zaidi vyombo vyetu vya dola. Jukumu ambalo hata kama tumezoea kuona likiwa mikononi mwa watu wenye UADILIFU wa kutia mashaka lakini kamwe hatujawahi kuona na hivyo kuzoea kukabidhiwa mtu aliyekosa UMAKINI.

Na hivyo ni wajibu wetu kuhoji ili hata kama tutakuwa tumechelewa kuepusha gharika la kuwa na Amiri Jeshi Mkuu mwenye UMAKINI unaotia shaka, basi angalao hoja hizi zikawepo katika makarabsha ya historia ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom