Dk. Slaa na Zitto kupanda jukwaa moja

Dk. Slaa na Zitto kupanda jukwaa moja

Wano uhuru wa kufanya hivyo hii ni demokrasia ila waepuke kukashifu wanasiasa wengine huo sio mtaji sahihi wa kisiasa
 
Si alisema ameamua kuachana na siasa?
Mbona kuna mmoja alisemaga KAMWE hawezi hama ccm, kama kuna asiyemtaka ccm ahame yeye
Alafu mwingine akasemaga, fulani akiteuliwa kuwa mgombea urais mimi namwaga manyanga uanachama sababu huyo jamaa ni FISADI, leo hawa wawili ni kama kulwa na doto, HAUSHANGAI HAWA, huyo wa kisema kaachana na siasa people do come out of retirement.
 
Tumia Basi Akili Zako Mkuu. Unajidhalilisha Sana Kudhani Magufuli Ataweza Kuibadilisha Tanzania Ambayo Chama Kile Kile Sera Zile Zile, Ambazo Zimeshindwa Kufanya Kitu kwa miaka 50?

Uwezi kusafiri Kwa usafiri wa Kiforokobe. Utegemee utafika Kwa wakati. ccm Imechoka Haifai ipumzike.

Kije Chama Chenye Mtazamo Mbadala, kwa Maendeleo ya Taifa, wale wote Wanaopingana na Mabadiliko basi Watu hao wameridhika na umaskini wa nchi hii chini ya chama cha mapinduzi.

Lowasa hanadi sera ya chadema, yeye ana mambo yake tu anayoyajua mwenyewe, elimu,elimu,elimu wimbo aliokuw anauimba akiwa ccm amehama nao to chadema.
 
Lowassa na Sumaye wana sifa zinazofanana na zile zile za watanzania wapenda mabadiliko, wanaoichukia CCM na kazi zake zote za kishetani! Huwezi kuwafananisha na hao Zitto na Dr.W.Slaa ambao wamejipambanua kama wapinga mabadiliko na Tanzania yote inawafahamu kama vibaraka wa CCM.

Slaa na zito wana sifa zinazofanana wanasema ukweli na wanapigana vita dhidi ya MAFISADI
 
Last edited by a moderator:
Wapiga madili wataifilisi ccm mwaka huu ili kuinusuru kufa,lakini wamesha chelewa.Wtz tumesha dhamiria kuing'oa ccm hata kwa kutokwa jasho.
 
Lowassa na Sumaye wana sifa zinazofanana na zile zile za watanzania wapenda mabadiliko, wanaoichukia CCM na kazi zake zote za kishetani! Huwezi kuwafananisha na hao Zitto na Dr.W.Slaa ambao wamejipambanua kama wapinga mabadiliko na Tanzania yote inawafahamu kama vibaraka wa CCM.

Nchi hii ina rundo kwa mazuzu, hivi kweli mtu mwenye akili zake anaweza kuamini kuwa Sumaye ni mpenda mabadiliko? Huyu aliyeitwa Zero! Muulizeni ataleta mabadiliko yapi ili na sisi wengine tushawishike. Sumaye ana rekodi ya kuwa Waziri Mkuu aliyekaa madarakani kuliko yeyote, lakini Hana chochote cha kuonyesha kuwa akijifanya. Leo hii eti anaitwa mpenda mabadiliko!
 
Last edited by a moderator:
Yuda na genge zima la wasaliti family, babu mihogo, ze pumba , LE boss lady, watakuletea kolabo Kali iitwayo "KARATA YA MWISHO "

Kolabo hii imaandaliwa na producer mahiri KITENGO PRODUCTIONs.chini ya maproducer Bakari, marope, lamek, Na kuwekodiwa katika studio za kisasa Masaki.
 
Kuna kitu ambacho mimi sielewi hivi kuna MTU mwenye akili timamu hadi Leo hajaamua wakumpigia KURA hadi asikilize Porojo.....km nihivyo basi tunasafari ndefu sana
 
Nchi hii ina rundo kwa mazuzu, hivi kweli mtu mwenye akili zake anaweza kuamini kuwa Sumaye ni mpenda mabadiliko? Huyu aliyeitwa Zero! Muulizeni ataleta mabadiliko yapi ili na sisi wengine tushawishike. Sumaye ana rekodi ya kuwa Waziri Mkuu aliyekaa madarakani kuliko yeyote, lakini Hana chochote cha kuonyesha kuwa akijifanya. Leo hii eti anaitwa mpenda mabadiliko!
Ni lazima uwe mpumbavu uliyevuka viwango KUMUAMINI Sumaye, niloshangaa sana aliposema CCM walituahidi maisha bora ila mpaka sasa hamna kitu, NILISHANGAA sana na nikawashusha kabisa viwango ukawa hii yote kwa kumuamini huyu muongo na kumuita eti mwana mabadiliko.
 
Nakushangaa sana jogoo dume kama unashindwa hata kujua kuwa mfumo wa chama cha ccm ndio ulioongoa na unaoongoza nchi na sio mtu. Umewahi kujiuliza kama ccm walikuwa wanajua kuwa lowasa ni mmiliki richmond kwanini hawakusema waje kusema leo? Guys you have to be serious kidogo aisee. Msitufanye watoto
 
Kwahiyo lowasa na sumaye walikuwa wanasubiri kupigwa chini ccm halafu ndio ghafla wapende madiliko!, hamna lolote ni uroho wa madaraka tu si lowasa wala sumaye mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko zaidi ya kuendeleza wizi waliouanzia ccm

Na CCM nao ni waroho wa madaraka mbona wanangangani miaka zaidi ya 50 hawataki kutoka.Wanatafuta usiku na mchana mabao ya mkono. Ila safari hii mjiandae kisaikolojia kukabidhi dola.
 
Nakushangaa sana jogoo dume kama unashindwa hata kujua kuwa mfumo wa chama cha ccm ndio ulioongoa na unaoongoza nchi na sio mtu. Umewahi kujiuliza kama ccm walikuwa wanajua kuwa lowasa ni mmiliki richmond kwanini hawakusema waje kusema leo? Guys you have to be serious kidogo aisee. Msitufanye watoto
Mimi hapa ni chadema ya Dr. Slaa, hivyo siukubali mfumo wa ccm, najua hilo, ila mtu anapokuwa waziri mkuu (wote wawili ni jumla ya miaka 13), walikuwa na nafasi kubwa sana ya kuleta mabadiliko, mikataba michafu chafu ya awamu ya tatu ilipitia kwa Sumaye, mingine kwa Lowassa, kama ni hayo mambo, wangegoma kuisaini kisha kung'atuka, ila waliisaini na wakakaa kimya, leo nao wanalalamika hasa Sumaye kuwa maisha bora hayapo, wakati ni upofu wake wa kusaini mikataba mibovu ndo unanyonya wananchi, HAWA WAWILI WASITHUBUTU KABISA, hasa huyo mouthpiece Sumaye kuongea suala la mfumo. Kama ukikubaliana nao mimi pia nitaona hauko sawa!
 
Back
Top Bottom