Dk. Slaa atikisa

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
WAKATI aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, akisisitiza kuwa uamuzi wake wa kustaafu siasa upo pale pale, kujiuzulu kwake ghafla kumezua gumzo nchi nzima na kuwafanya wananchi wengine kushindwa kuamini walichokisikia.

Uamuzi wa Dk. Slaa kuacha madaraka ndani ya Chadema na kupumzika siasa uliwekwa hadharani jana na gazeti hili ikiwa ni siku moja tu tangu viongozi wa chama hicho kumkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kisha jana kuchukua fomu za kugombea urais.

Wakati gumzo likiendelea kwenye mitandao ya kijamii, Dk. Slaa jana aliliambia gazeti hili akisisitiza msimamo aliouchukua Jumanne iliyopita, akisema: "Mimi ‘position' yangu bado ni ile ile, sijabadilika."

Chumba cha habari cha Raia Tanzania, gazeti linalochapishwa na Kampuni ya Raia Mwema, jana kuanzia saa 1.00 kilikuwa kikipokea simu nyingi na barua pepe kutoka kwa watu mbalimbali, wakitaka kupata uhakika zaidi wa habari hiyo, wengine wakithubutu kuomba mawasiliano ya moja kwa moja ya kiongozi huyo ili wampigie simu kumpongeza au kumsihi abadili mawazo.

"Nilikuwa ninapata shida sana nikijiuliza, baada ya uamuzi wa chama kumpokea Lowassa, Dk. Slaa angeficha wapi uso wake kwa jinsi alivyokuwa akimsakama kwa ufisadi?

"Uamuzi aliouchukua ni wa kiongozi anayejitambua. Haongozwi na maslahi binafsi, bali misingi anayoisimamia. Fikisheni pongezi zangu kwake," alisema mwananchi mmoja kwa simu kutoka Mbeya akijitambulisha kwa jina la Mwakarobo.

Watu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blog kadhaa, walitumbukia kwenye mjadala mrefu kuhusu kujiuzulu kwa Dk. Slaa, hata makundi ya kijamii yasiyokuwa na kawaida ya kujadili siasa, jana walijadili tukio hilo wengi wao wakionyesha mshangao wao.

Katika mtandao wa ‘mabadiliko', gazeti la Raia Tanzania lilibandikwa mtandaoni saa 1.33 asubuhi, tofauti na kawaida ya mtandao huo ambao magazeti yote ya siku huingizwa saa mbili asubuhi.

Kwa asubuhi ya jana, msimamizi wa mtandao huo (moderator), alilipandisha hewani Raia Tanzania peke yake huku akiwaalika wanajukwaa hilo kwa kusema: "Tuanzie hapa leo kujadili, maana nilisema hata Chadema utatokea mgawanyiko."

Wito huo uliitikiwa na mchangiaji mmoja kwa ujumbe uliosomeka: "Moyo wangu unalia machozi ya damu!" huku mwingine akisema: "Nilitegemea wanachama wa kawaida wasielewe, siyo kiongozi au viongozi kwani wao walipata nafasi ya kusikia wenyewe kutoka kwa muhusika."

Mchangiaji mwingine alisema: "Ngoma inogile, sasa fukuto linapamba moto na ataondoka na watu wake. Dk. Slaa alikuwa amejiandaa kuwa Rais sasa tena wanamwondoa, inakuwa ngumu kwake."

Katika mtandao wa Jamii Forums, Raia Tanzania lilibandikwa saa 12.00 asubuhi na mjadala wenye ukinzani ukafuata uliowaga wananchi pande mbili; mmoja ukiunga mkono hatua ya Dk. Slaa kustaafu siasa na wa pili ukipinga hatua hiyo.

Jiji la Dar es Salaam katika sehemu zenye mikusanyiko ya watu (vijiweni) na kwenye vyombo vya usafiri, mjadala ulikuwa ni kujiuzulu kwa Dk. Slaa, maoni tofauti yakitolewa huku wengine wakibaki na mshangao.

Chanzo: Raia Tanzania
 
Namshauri arudi CCM maana huku tunatimua mafisadi kisayansi...anakatwa tu
 
Dr kavuta mshiko wake kakubali kubeba aiu

Pesa balaa, iliuza hadi Yesu
 
hata ya lowasa yalianza hivihivi...
Hahaaa,,, tusubir tuone..
Naona mliochumbiwa na lowasa mmeanza kutikisa vijambio
 
Mwaka huu CcM Kwenu ni sawa na ngombe aliepelekws machinjioni hamna jinsi lazima kuangalizwa
kibura tu hata mjifaraguwe namna gani
kazi imekwisha.
 
Hayo ndio maneno ambayo ccm wanapenda sana umma uyasikilize. Kufeni peke yenu na kujanaa kuwa wapinzai, cdm wamesema bado ni wamoja. Zile sheria kandaminzi ambazo mlidhani zitawabana wapinzani sasa ztawabana nini mkiwa wapinzani.Mtajiju kweli ccm
 
why ni gazeti moja tu linaripoti haya?

tena kwa habari za kuokoteza kwenye mabadiliko forum
 
Back
Top Bottom