Dk. Slaa atikisa

Dk. Slaa atikisa

Mtaandika sana mwaka huu! Chezea kubadili gia angani! Slaa yupo CHADEMA na ndio ashafika hapo! Mtasubiri saana mwaka huu
 
kama ni kweli basi hii habari mbaya sana kwa CHADEMA na hatma ya siasa za upinzani na mabadiliko ya kweli ndani ya nchi yetu. Watanzania inabidi wasubiri tena miaka mingine 20 kuiondoa CCM madarakani, kwani siuoni ushindi wa UKAWA mwezi October bila kuwapo kwa na DR. Slaa bega kwa bega.

Wengi wakataka tamaa na siasa za nchi yetu na wengi hawatajitokeza kupiga kura!! hii ni mbaya sana!!
 
Siku Dr akiamua kukanusha hadharani hakika CcM wengi watalazwa na kama si kufa kabisa !!?

ccm hawawez kuumia kwasababu Dr Slaa hana mchango wowote kwa ccm. Slaa akiwa chadema ccm ikulu lazma iende, hata asipokuwa chadema ccm lazma iende,.

Tofauti na nyie chadema ambao hamna wagombea mpaka msubir walioshindwa ccm ndio muwaite wakomboz wenu.

Sasa ili kuwathibitishia kuwa ccm n moto wa kuotea mbali pamoja na slaa wenu pamoja na lowasa wenu wote mtabwaga.
Tuonane oct
 
Yan unakuta mtu mzima kabisa eti anaamini fununu za magazeti . sijui wabongo huu ujinga tunautoaga wapi
 
WAKATI aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, akisisitiza kuwa uamuzi wake wa kustaafu siasa upo pale pale, kujiuzulu kwake ghafla kumezua gumzo nchi nzima na kuwafanya wananchi wengine kushindwa kuamini walichokisikia.

Uamuzi wa Dk. Slaa kuacha madaraka ndani ya Chadema na kupumzika siasa uliwekwa hadharani jana na gazeti hili ikiwa ni siku moja tu tangu viongozi wa chama hicho kumkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kisha jana kuchukua fomu za kugombea urais.

Wakati gumzo likiendelea kwenye mitandao ya kijamii, Dk. Slaa jana aliliambia gazeti hili akisisitiza msimamo aliouchukua Jumanne iliyopita, akisema: “Mimi ‘position’ yangu bado ni ile ile, sijabadilika.”

Chumba cha habari cha Raia Tanzania, gazeti linalochapishwa na Kampuni ya Raia Mwema, jana kuanzia saa 1.00 kilikuwa kikipokea simu nyingi na barua pepe kutoka kwa watu mbalimbali, wakitaka kupata uhakika zaidi wa habari hiyo, wengine wakithubutu kuomba mawasiliano ya moja kwa moja ya kiongozi huyo ili wampigie simu kumpongeza au kumsihi abadili mawazo.

“Nilikuwa ninapata shida sana nikijiuliza, baada ya uamuzi wa chama kumpokea Lowassa, Dk. Slaa angeficha wapi uso wake kwa jinsi alivyokuwa akimsakama kwa ufisadi?

“Uamuzi aliouchukua ni wa kiongozi anayejitambua. Haongozwi na maslahi binafsi, bali misingi anayoisimamia. Fikisheni pongezi zangu kwake,” alisema mwananchi mmoja kwa simu kutoka Mbeya akijitambulisha kwa jina la Mwakarobo.

Watu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blog kadhaa, walitumbukia kwenye mjadala mrefu kuhusu kujiuzulu kwa Dk. Slaa, hata makundi ya kijamii yasiyokuwa na kawaida ya kujadili siasa, jana walijadili tukio hilo wengi wao wakionyesha mshangao wao.

Katika mtandao wa ‘mabadiliko’, gazeti la Raia Tanzania lilibandikwa mtandaoni saa 1.33 asubuhi, tofauti na kawaida ya mtandao huo ambao magazeti yote ya siku huingizwa saa mbili asubuhi.

Kwa asubuhi ya jana, msimamizi wa mtandao huo (moderator), alilipandisha hewani Raia Tanzania peke yake huku akiwaalika wanajukwaa hilo kwa kusema: “Tuanzie hapa leo kujadili, maana nilisema hata Chadema utatokea mgawanyiko.”

Wito huo uliitikiwa na mchangiaji mmoja kwa ujumbe uliosomeka: “Moyo wangu unalia machozi ya damu!” huku mwingine akisema: “Nilitegemea wanachama wa kawaida wasielewe, siyo kiongozi au viongozi kwani wao walipata nafasi ya kusikia wenyewe kutoka kwa muhusika.”

Mchangiaji mwingine alisema: “Ngoma inogile, sasa fukuto linapamba moto na ataondoka na watu wake. Dk. Slaa alikuwa amejiandaa kuwa Rais sasa tena wanamwondoa, inakuwa ngumu kwake.”

Katika mtandao wa Jamii Forums, Raia Tanzania lilibandikwa saa 12.00 asubuhi na mjadala wenye ukinzani ukafuata uliowaga wananchi pande mbili; mmoja ukiunga mkono hatua ya Dk. Slaa kustaafu siasa na wa pili ukipinga hatua hiyo.
Jiji la Dar es Salaam katika sehemu zenye mikusanyiko ya watu (vijiweni) na kwenye vyombo vya usafiri, mjadala ulikuwa ni kujiuzulu kwa Dk. Slaa, maoni tofauti yakitolewa huku wengine wakibaki na mshangao.

Chanzo: Raia Tanzania

Mmmmh! Kifua kinaanza kujaa
 
Hili gazeti raia Tanzania sitalisoma kabisa maana kila kitakachokuwa kimeandikwa huko ni uongo
 
CCM na vyombo vyao vya Udaku wanawashwa makalioni sana!! endeleeni kujiliwaza Chadema/ukawa ndo mwamba wa siasa za Tanzania kwa sasa....hadi sasa tathmini inaonyesha kuwa Umaarufu wa Magufuli umeporomoka hadi kufikia asilimia 10 kutoka asilimia 60 za awali baada ya kuchaguliwa hii ni habari na dalili mbaya sana kwake.
 
Nipo pamoja na Dr.Slaa kwa maamuzi atakayoyachukua kulinda heshima yake .
 
Duh!! CCM mwaka huu mnakazi! Hizi propaganda za kitoto ndio zina zidi kuwa punguzia credibiliy.
 
.Slaa ni mtu mkubwa kwenye Taifa hili sio kwa CHADEMA tu. Kama Lowasa ilimchukua muda kuja kusema hadharani anasimamia nini mara baada ya kukatwa jina ndio hivyo hivyo kwa Dr.Slaa anahitaji muda wa kupumzisha kichwa ni breaking news kwake maana hadi mkutano wa Mwanza wa kuwapokea akina Bulaya na Lembeli Dr.Aliwekwa kwenye gari ya wazi kama ndiye mgombea urais vile huku akiwa na furaha na kucheza na Lissu alimtaja Kahama kama mgombea kwa hiyo inahitaji muda asipelekeshwe.
 
Kwa Makamanda wote nchini...

Taarifa za kusema Dr.Slaa na John Mnyika wanataka kuhama chama ni propaganda zinazotengenezwa na CCM ili kuwachanganya wanachama wa CHADEMA.

Siyo taarifa za kweli hata kidogo, ondoeni hofu, jipangeni vizuri na uchaguzi wa madiwani. Kuweni Imara na Imani kwa viongozi wenu wa juu.

Hawa watu wawili wako bize sana na kazi ngumu ya kuandaa mkutano wa Kamati Kuu, Baraza kuu na kisha Mkutano mkuu.

Huu ni mwaka wetu wa ushindi kwa ngazi zote 3. Miruzi ya CCM isituondoe kwenye marengo yetu mwanana. Wamechanganyikiwa, wanaweweseka mchana wa jua kali.

Tuma kwa Kamanda mwingine
 
Kwa Makamanda wote nchini...

Taarifa za kusema Dr.Slaa na John Mnyika wanataka kuhama chama ni propaganda zinazotengenezwa na CCM ili kuwachanganya wanachama wa CHADEMA.

Siyo taarifa za kweli hata kidogo, ondoeni hofu, jipangeni vizuri na uchaguzi wa madiwani. Kuweni Imara na Imani kwa viongozi wenu wa juu.

Hawa watu wawili wako bize sana na kazi ngumu ya kuandaa mkutano wa Kamati Kuu, Baraza kuu na kisha Mkutano mkuu.

Huu ni mwaka wetu wa ushindi kwa ngazi zote 3. Miruzi ya CCM isituondoe kwenye marengo yetu mwanana. Wamechanganyikiwa, wanaweweseka mchana wa jua kali.

Tuma kwa Kamanda mwingine

mbona waitasoma namba mwaka huu? WALIANZA kwa kumulizea Tundu Lissu ooo mbona hakuwepo kaja hadharani, wameahamia kwa Mnyika. Mnyika yuko busy kuliko mnavyofikiri ninyi na nguvu nyingi ya CHADEMA inategemea pia kwa KOMREDI MNYIKA mtasubri sana DOGO yuko poa
 
Dr slaa ni dume la siasa,amekuwa gumzo kuliko mgombea urais wa ccm magufuli,
Maccm wamebaki na hoja moja tu,eti dr slaa alimchafua lowasa,mbona awasemi dr slaa ndiye aliye ibua wizi wa epa,mbona awasemi dr slaa ndiye aliyeibua wizi richimond,wizi ambao ni kweli alimtuhumu lowasa lkn lowasa mwenyewe amekiri ni kweli kulikuwa na wizi katika rich mondo lkn yeye akuhusika,aliyehusika ni bosi wake,mbona maccm hawasemi haya?
 
Tulieni dawa iwaingie, jambo usilolijua ni kama usiku wa giza, sijui mtazificha wapi sura zenu mwaka huu.
 
Kwa Makamanda wote nchini...

Taarifa za kusema Dr.Slaa na John Mnyika wanataka kuhama chama ni propaganda zinazotengenezwa na CCM ili kuwachanganya wanachama wa CHADEMA.

Siyo taarifa za kweli hata kidogo, ondoeni hofu, jipangeni vizuri na uchaguzi wa madiwani. Kuweni Imara na Imani kwa viongozi wenu wa juu.

Hawa watu wawili wako bize sana na kazi ngumu ya kuandaa mkutano wa Kamati Kuu, Baraza kuu na kisha Mkutano mkuu.

Huu ni mwaka wetu wa ushindi kwa ngazi zote 3. Miruzi ya CCM isituondoe kwenye marengo yetu mwanana. Wamechanganyikiwa, wanaweweseka mchana wa jua kali.

Tuma kwa Kamanda mwingine

Issue ya Lowassa kuhamiaCDM nayo ilianza kama tetesi huku tukihakikishiwa kuwa ni propaganda tu za magamba....! Any way time will tell let us wait.
 
Back
Top Bottom