Dk. Slaa atikisa

Dk. Slaa atikisa

Kwa Makamanda wote nchini...

Taarifa za kusema Dr.Slaa na John Mnyika wanataka kuhama chama ni propaganda zinazotengenezwa na CCM ili kuwachanganya wanachama wa CHADEMA.

Siyo taarifa za kweli hata kidogo, ondoeni hofu, jipangeni vizuri na uchaguzi wa madiwani. Kuweni Imara na Imani kwa viongozi wenu wa juu.

Hawa watu wawili wako bize sana na kazi ngumu ya kuandaa mkutano wa Kamati Kuu, Baraza kuu na kisha Mkutano mkuu.

Huu ni mwaka wetu wa ushindi kwa ngazi zote 3. Miruzi ya CCM isituondoe kwenye marengo yetu mwanana. Wamechanganyikiwa, wanaweweseka mchana wa jua kali.

Tuma kwa Kamanda mwingine

Ahsante Kwa taarifa! uzush huu umepelekea usumbufu mkubwa sana kwa wanachama wetu! wa2 wamejawa na hofu kubwa sana dhd ya huo huzush
 
Haya magazeti huwa hata hayanunuliwi na habari zake ndiyo hizi
 
ccm hawawez kuumia kwasababu Dr Slaa hana mchango wowote kwa ccm. Slaa akiwa chadema ccm ikulu lazma iende, hata asipokuwa chadema ccm lazma iende,.

Tofauti na nyie chadema ambao hamna wagombea mpaka msubir walioshindwa ccm ndio muwaite wakomboz wenu.

Sasa ili kuwathibitishia kuwa ccm n moto wa kuotea mbali pamoja na slaa wenu pamoja na lowasa wenu wote mtabwaga.
Tuonane oct

Asante mkuu, tukutane october kumpeleka Dk. Magufuli ikulu.
 
Kama ni kweli Dr Slaa mdini anambagua Lowassa kwakuwa sio dhehebu lake.nenda Dr kapumzike kwa amani
 
Hayo ndio maneno ambayo ccm wanapenda sana umma uyasikilize. Kufeni peke yenu na kujanaa kuwa wapinzai, cdm wamesema bado ni wamoja. Zile sheria kandaminzi ambazo mlidhani zitawabana wapinzani sasa ztawabana nini mkiwa wapinzani.Mtajiju kweli ccm

Chadema hawataki kusikia Dr Slaa amejiuzulu,Chadema wamesahau kuwa binadamu kambwa kwa heshima yake,Dr slaa anaona bora alinde heshima yake,apumzike siasa badala ya kulinadi lile FISADI NAMBA MOJA HAPA NCHNI TANZNIA lililo hamia chadema
 
raia tanzania ni magazeti ya kuuzia maandazi.
ulitegemea gazeti la ccm liisifu chadema??never.

dr.slaa yuko palepale

Upo katika stage ya denial .. Subiri dawa ikuingia sawasawa ... Ndo utakubali lisemwalo lipo
 
Raha ya siku hizi ni kwamba media za habari ni nyingi, pili wananchi wanajua vyombo vya habari vipi vinatumiwa.

Ukitambua hili, huwezi kuwa na hofu kama mnayotaka kuaminisha watu!
 
Chadema hawataki kusikia Dr Slaa amejiuzulu,Chadema wamesahau kuwa binadamu kambwa kwa heshima yake,Dr slaa anaona bora alinde heshima yake,apumzike siasa badala ya kulinadi lile FISADI NAMBA MOJA HAPA NCHNI TANZNIA lililo hamia chadema

Ni wewe huyu huyu uliyekataa kuwa siyo fisadi, alipokuwa CCM!
 
Chadema hawataki kusikia Dr Slaa amejiuzulu,Chadema wamesahau kuwa binadamu kambwa kwa heshima yake,Dr slaa anaona bora alinde heshima yake,apumzike siasa badala ya kulinadi lile FISADI NAMBA MOJA HAPA NCHNI TANZNIA lililo hamia chadema
Jk ndiyo fisadi,kama sio ampeleke Lowasa mahakamani
 
Issue ya Lowassa kuhamiaCDM nayo ilianza kama tetesi huku tukihakikishiwa kuwa ni propaganda tu za magamba....! Any way time will tell let us wait.

Ni incomparable situation kabisa!!

Tetesi za Lowassa kuhama au kuachana na CCM zilianza mapema mara baada ya CC ya CCM kuja na "top five" ya akina Membe, January, Asha Rose, Magufuli na Amina Salumu kwenda Halmashauri kuu.

Watu wakawa na tumaini kuwa labda kikao hicho kingeweza kushinikiza ili maamuzi ya CC yatenguliwe na ushahidi ni matukio ya baadhi ya wajumbe wa HK kumwimbia mwenyekiti wao JK nyimbo za kumsanifu pamoja na wale wajumbe watatu wa CC kuonesha kutokukubaliana na utaratibu uliotumika kuwapata hao top five kwamba ulikiuka kanuni na misingi ya katiba ya chama chao!!

Hali ikawa tofauti, ikawa ileile, mchakato uliendelea pasipo jina la Edward Lowassa hadi wakapata "top three" lakini this this time wakidhani ni njia ya kumridhisha EL na wafuasi wake, Member akakatwa pia ktk steji ya kikao cha HK!

Kwa tuliofuatilia mchakato huo wa CCM wa kumpata mgombea Urais wao kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii na Television, tulimwona Edward Lowassa kwa mara ya kwanza tangu baada ya kwisha kwa zoezi la kusaka wadhamini akiwa mbele ktk session hatua ya mkutano mkuu amenuna na lugha ya mwili wake ikionesha wazi kuwa huyu yupo pale kimwili tu lakini akili yake iko mbaaaali, kwingine kabisa. Tena uwepo wake pale ni wazi ilikuwa ni kwa heshima ya watu Fulani tu!!

Tuliambiwa kuwa baada ya session ya kwanza (wakati wale top three wakiomba kuchaguliwa na kisha upigaji kura), jamaa hakurudi tena wala kusema lolote hadi mkutano mkuu unafungwa na ktk uzinduzi wa ilani yao ya uchaguzi!

Wenye akili tulijua CCM kuna mpasuko unainyemelea. Tulijua kuwa huyu bwana aidha atalisanua akiwa humohumo CCM au atahama chama.

Possibility kubwa ni kuwa watu tulikuwa tunafikiria atakwenda ACT ya ZZK kwa sbb tayari alishakaribishwa na uvumi uliokuwa unaenezwa mapema ni kuwa yeye ndiye mfadhili wa chama hicho. Hakuna aliyedhani (I stand to be corrected) kuwa atahama na kwenda CHADEMA.......hii ni wazi ilikuwa ni surprise!!

Kwa hiyo situation ya Dr Slaa na EL ni tofauti kabisa. Sawa na uniambie leo kuwa Abdulhaman Kinana ahame CCM aende chama kingine chochote sema hata CHADEMA kwa sbb zozote zile. Hili haliwezi kutokea ktk siasa za kiafrika na especially hizi za kwetu za kibongo!!
 
WAKATI aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, akisisitiza kuwa uamuzi wake wa kustaafu siasa upo pale pale, kujiuzulu kwake ghafla kumezua gumzo nchi nzima na kuwafanya wananchi wengine kushindwa kuamini walichokisikia.

Uamuzi wa Dk. Slaa kuacha madaraka ndani ya Chadema na kupumzika siasa uliwekwa hadharani jana na gazeti hili ikiwa ni siku moja tu tangu viongozi wa chama hicho kumkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kisha jana kuchukua fomu za kugombea urais.

Wakati gumzo likiendelea kwenye mitandao ya kijamii, Dk. Slaa jana aliliambia gazeti hili akisisitiza msimamo aliouchukua Jumanne iliyopita, akisema: “Mimi ‘position’ yangu bado ni ile ile, sijabadilika.”

Chumba cha habari cha Raia Tanzania, gazeti linalochapishwa na Kampuni ya Raia Mwema, jana kuanzia saa 1.00 kilikuwa kikipokea simu nyingi na barua pepe kutoka kwa watu mbalimbali, wakitaka kupata uhakika zaidi wa habari hiyo, wengine wakithubutu kuomba mawasiliano ya moja kwa moja ya kiongozi huyo ili wampigie simu kumpongeza au kumsihi abadili mawazo.

“Nilikuwa ninapata shida sana nikijiuliza, baada ya uamuzi wa chama kumpokea Lowassa, Dk. Slaa angeficha wapi uso wake kwa jinsi alivyokuwa akimsakama kwa ufisadi?

“Uamuzi aliouchukua ni wa kiongozi anayejitambua. Haongozwi na maslahi binafsi, bali misingi anayoisimamia. Fikisheni pongezi zangu kwake,” alisema mwananchi mmoja kwa simu kutoka Mbeya akijitambulisha kwa jina la Mwakarobo.

Watu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blog kadhaa, walitumbukia kwenye mjadala mrefu kuhusu kujiuzulu kwa Dk. Slaa, hata makundi ya kijamii yasiyokuwa na kawaida ya kujadili siasa, jana walijadili tukio hilo wengi wao wakionyesha mshangao wao.

Katika mtandao wa ‘mabadiliko’, gazeti la Raia Tanzania lilibandikwa mtandaoni saa 1.33 asubuhi, tofauti na kawaida ya mtandao huo ambao magazeti yote ya siku huingizwa saa mbili asubuhi.

Kwa asubuhi ya jana, msimamizi wa mtandao huo (moderator), alilipandisha hewani Raia Tanzania peke yake huku akiwaalika wanajukwaa hilo kwa kusema: “Tuanzie hapa leo kujadili, maana nilisema hata Chadema utatokea mgawanyiko.”

Wito huo uliitikiwa na mchangiaji mmoja kwa ujumbe uliosomeka: “Moyo wangu unalia machozi ya damu!” huku mwingine akisema: “Nilitegemea wanachama wa kawaida wasielewe, siyo kiongozi au viongozi kwani wao walipata nafasi ya kusikia wenyewe kutoka kwa muhusika.”

Mchangiaji mwingine alisema: “Ngoma inogile, sasa fukuto linapamba moto na ataondoka na watu wake. Dk. Slaa alikuwa amejiandaa kuwa Rais sasa tena wanamwondoa, inakuwa ngumu kwake.”

Katika mtandao wa Jamii Forums, Raia Tanzania lilibandikwa saa 12.00 asubuhi na mjadala wenye ukinzani ukafuata uliowaga wananchi pande mbili; mmoja ukiunga mkono hatua ya Dk. Slaa kustaafu siasa na wa pili ukipinga hatua hiyo.
Jiji la Dar es Salaam katika sehemu zenye mikusanyiko ya watu (vijiweni) na kwenye vyombo vya usafiri, mjadala ulikuwa ni kujiuzulu kwa Dk. Slaa, maoni tofauti yakitolewa huku wengine wakibaki na mshangao.

Chanzo: Raia Tanzania

Acha the propaganda mfu. CHADEMA ni mpango wa Mungu, LOWASSA ni tumaini jipya la watz na UKAWA ndio njia sahihi ya kutimiza adhma ya watz ya kutaka mabadiliko na SLAA ndiye kinara wa hili. Eti raia Tanzania sema Marehemu CCM
 
mwaka huu mtakuja na kila habari, ila ndo hivyo gia ilishabidilishiwa angani
 
ccm hawawez kuumia kwasababu dr slaa hana mchango wowote kwa ccm. Slaa akiwa chadema ccm ikulu lazma iende, hata asipokuwa chadema ccm lazma iende,.

Tofauti na nyie chadema ambao hamna wagombea mpaka msubir walioshindwa ccm ndio muwaite wakomboz wenu.

Sasa ili kuwathibitishia kuwa ccm n moto wa kuotea mbali pamoja na slaa wenu pamoja na lowasa wenu wote mtabwaga.
Tuonane oct

mdharau mwiba ...
 
Back
Top Bottom