Dk Slaa asema Mufti hakufanya utafiti

Dr SLAA hakusema afanye uchunguzi alisema afanye utafiti. Sasa wewe Hemed Suya unajua tofauti ya uchunguzi na utafiti? ukujua tofauti yake siku nyingine hutouliza swali kama ulilouliza leo
 
Hivi karibuni mufti wa Waislamu wa Tanzania aliwatuhumu chadema kuwa maandamano wanayofanya yanatishia amani ya nchi. Kesho akaibuka katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Dr.Slaa na kumwambia mufti afanye uchunguzi kwanza kabla hajasema lolote. Hili lilipokelewa kwa shangwe na wafuasi wa cdm humu jf huku wakirusha makombora ya hapa na pale kwamba mufti hawezi wala hana hiyo elimu ya kufanya uchunguzi hivyo kibarua anachopewa na Dr. Ni kikubwa kuliko uwezo wake. Naomba kuuliza kati ya dr na mufti anayeweza kufanya uchunguzi vizuri ni nani? Kwa sababu hata Dr. Angekuwa ana uwezo wa kufanya uchunguzi asingeweza kuchukua mke wa mtu bila ya yeye kujua kuwa mchumba aliyenaye na anaemtangaza kuwa mchumba wake ni mke wa mtu. Naomba kuwasilisha.

Nakushauri yafuatayo na kama ni Mtanzania mzalendo na mwenye uelewa na weledi nadhani utafunga bongo lako..............................

  1. Achana na mambo ya udini na fikra finyu muda wote,usimtetee mufti hati kwasababu ni muislamu ukatumia nafasi hiyo kuwalinda watu wasio na fikra mbadala
  2. Kumbuka kuwa Mufti ni zao la CCM na Bakwata anayoiongoza ni kati ya jumuiya za CCM kama vile UVCCM nk..chukua hatua ufikirie kama muislamu utaikomboaje Bakwata kutoka kwenye makucha ya CCM
  3. Achana na mambo yasiyo na tija kwa Taifa na acha kuwa na masihara na mambo sensitive katika taifa letu...
Nitafute..........
 
Hivi karibuni mufti wa Waislamu wa Tanzania aliwatuhumu chadema kuwa maandamano wanayofanya yanatishia amani ya nchi. Kesho akaibuka katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Dr.Slaa na kumwambia mufti afanye uchunguzi kwanza kabla hajasema lolote. Hili lilipokelewa kwa shangwe na wafuasi wa cdm humu jf huku wakirusha makombora ya hapa na pale kwamba mufti hawezi wala hana hiyo elimu ya kufanya uchunguzi hivyo kibarua anachopewa na Dr. Ni kikubwa kuliko uwezo wake. Naomba kuuliza kati ya dr na mufti anayeweza kufanya uchunguzi vizuri ni nani? Kwa sababu hata Dr. Angekuwa ana uwezo wa kufanya uchunguzi asingeweza kuchukua mke wa mtu bila ya yeye kujua kuwa mchumba aliyenaye na anaemtangaza kuwa mchumba wake ni mke wa mtu. Naomba kuwasilisha.

Pole sana kinachokusumbua ni kuibua mada ambazo haziko objective. Madai ya Dr Slaa ni kuwa Mufti hakufanya uchunguzi na siyo hajui kufanya uchunguzi. Ungestick kwenye mada husika usingekuwa na haja kuweka hii post.

Lakini kwa kuwa umeamua nawe kuwa irrational kama hao wanaosema Mufti hawezi kufanya uchunguzi. Swali lako la nani zaidi kati ya Dr Slaa na Mufti linaleta mashaka juu ya uwezo wako wa kuchambua hoja. Kuhusu swali lako la nani zaidi nauliza ni ktk lipi? OK let's say Mufti ni zaidi. So what? Ni vizuri ufahamu kuwa uwezo binafsi wa mtu kufaya utafiti ni juu yake and is not of public interest.

Tukumbushane wanaJF kuwa hapa jamvini si mahala pa watu wa kushikiwa akili. Ibua hoja yako mahususi siyo fulani kasema hiki au huyu kasema kile.
 
mimi ningeshauri taasisi zote za kidini ziendelee kujikita zaidi kuanzisha shule, vyuo, vituo vya afya, zahanati na mahospitali ..... ! hii itawafanya wawe busy zaidi kuliko kukosa shughuli za kufanya
wataanzishaje shule , hospitali vyuo wakati serikali inao watu maalum inaowapa ruzuku mpaka bilioni mia sita wakati wenzao wakiambulia sifuri, yaani hakuna wa kuwawezesha hata kwa kidogo wanachoanzisha wenyewe au hulijui hilo baba? kisha nao wakitaka kujiunga na jumuiya zitakazowapa campani kama vile vatcan wenzao wanawambia watasilimisha nchi na nchi haina dini ila ya kwao na ndo serikali yao. fanya utafiti utajua kwa nini hawana shughuli za kufanya, ok by
 
Umoja wa kitaifa unatikiswa na wachumia tumbo; ebu kila mmoja wetu ktk nafasi yake atimize wajibu wake na akumbuke haki ni tunda la amani.
Kama tutaendelea kuruhusu nchi iibiwe kama ilivyo hivi sasa, na huduma za jamii zikaendelea kukaa tenge, haya mahubiri hayataingia ndani ya akili za watu siku moja na hiyo siku yaja; tena i-karibu kwani walopewa madaraka wameziba masikio na macho yao pia hayaoni. Wameamua kuwaacha maelfu ktk lindi la shida zao, wanaongea tu bila utekelezaji; wamejifanya miungu watu. Nenda Ocean road, ni less than a km toka ikulu, lakini huduma wanayopata wagonjwa waweza lia bila kupigwa.
Tanzania ni yetu sote ebu tuwaze mbali zaidi ya matumbo yetu ili tulijenge taifa letu kwa kizazi kijacho.
Naomba kuwakilisha
 
Nakuhurumia Dr. unapochezea sasa sipo,itakula kwako,waislamu tunatambua CDM ni chama cha kanisa,ushahidi soma waraka wa uchaguzi 2010 wa kanisa katoliki,muulize Mrema aliwafanya nini waislam na kilimpata nini, nadhani mmeiona action ya Kongamano la kiislam lililofanyika Arusha,inshort waislam sio wanafiki tupo open.Itakula kwako kama utafiti tunaanza na wewe.
 
WanaCamaraderie na wana Jamvi,
Hizi ndizo Issues.
i) Udini umetoka wapi katika hoja za Dr Slaa?
2) Yaani Chama kituhumiwe kuvunja Amani, mtu yeyote mwenye akili timamu ategemee Katibu Mkuu wa Chama hicho akae kimya tu. Cammon, wana jamvi let us be serious. Ni upuuzi wa aina hii kufumbia mambo ndio kulikotufikisha hapa tulipo kama Taifa.
3) Nimesema mara kadhaa, na ninmeirudia juzi Kigoma, palipo na ukweli na haki au misingi ya ukweli inapofumbiwa macho tutapiga kelele. Hakuna aliye juu ya sheria, haki, ukweli. Hata "Mungu angelikuwa anafanya makosa kama hayo tungelimkemea", kwa bahati nzuri hafanyi makosa. Hiyo ni kuonyesha kuwa hakuna chini ya mbingu ambaye hatakemewa au kusahihishwa kama kwa misingi ya kisheria, ukweli tunaamini amekosea. Ikumbukwe hakuna mwenye "monopoly ya ukweli". Truth is but and is indivisible, hivyo iwe kiongozi wa dini (yeyote), iwe kiongozi wa Serikali wa ngazi yeyote atakemewa au kukosolewa kwa kadiri ya uzito wa kosa au upotoshaji. Wana JF hao wanaojadili personalities badala ya issues mimi hawanisumbui kwa vile tunajua "simple minds discuss people and great minds discuss issues". Tatizo hapa ni issues zilizokuwa raised na kiongozi wa dini je zina ukweli au la, kama sivyo hatuwezi kukaa kimya wakati Taifa linapotoshwa,inaweza kuwa kwa kutokujua kiongozi huyo au kwa malengo yeryote aliyonayo.

Chadema sasa ni nafasi yetu kutwaa dola tuondoshe udini unaoshamiri
 
Kudadadeki,majini na nyota tena,ngoja ni kachekee pembeni nitarejea coz cna meno ya mapokezi.
 
Naona sasa jk ataamini maneno ya cdm kwamba kuna siku moja itafika nchi itashindwa kutawalika. Sasa tunayaona.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom