Nadhani imefika wakati kukaa na viongozi wa dini ya kiislam kuwasikiliza kwanini chadema imekuwa kero kwao? kwanini kila kukicha Chadema imekuwa ikisemwa vibaya na viongozi wa dini hiyo. inawezekana hamusikii kwa kuwa hayatolewi ktk vyombo vya habari visivyo vya dini. lkn kila kukicha tuhuma za waumini wa kiislam inashika kasi, kila pembe ya tz .
hii kama taachwa iendelee na kutokaa nao meza kuangalia sorce au kutumia vyombo vyao vya habari kuwasiliana nao itaathiri kwa kiasi kikubwa mustkabali wa chadema kisiasa. Inawezekana wanatumiwa kisiasa na wapinzani wa chadema, lkn ni wazi chadema kama chama kinachotaka kujaribu kujikosha ktk jamii ya kitanzania hakuna budi kutafuta njia mbadala ya kuondoa dhana hii. njia pekee ni kukaa na viongozi hao, kuwasikiliza malalamiko yao na pengine kaungalia nini source: au kutumia redio zao kuwaeleza uzuri wa chadema kwao na kuwaondoshea wasiwasi watz hao
Hakuna kitu bora zaidi ya mazungumzo na kila kona duniani leo pale pande mbili wanapokaa na kutatua tatizo lao kwa nia njema basi matokeo huwa mazuri!
Mfano Kenya ilipoingia ktk mgogoro mkubwa wa Kikabila na Kisiasa viongozi waliamua kukaa chini na kuzungumza iwe ni kwa nia njema ama ni kwa kulazimishwa na jumuia ya kimataifa lakini walikaa pamoja na kumaliza mgogoro ule!
Zanzibar walipokuwa na mgogoro wa Kisiasa ingawaje miaka ya nyuma walishakaa mara nyingi kuzungumza bila mafanikio lakini walipoamua kuutatua kwa nia njema tumeona mafanikio leo Wa ZAnzibar wote wamekuwa ndugu tena na kueka nyuma tofauti za Kisiasa! mifano iko mingi!
Hapa kwetu TZ tatizo kubwa lipo ni la UDINI ingawaje Dini zingine zinakanusha kuwa hakuna udini! Waislamu wamethibitisha kwa maandishi, kongomano, vitabu, Radio, Mikutano ya hadhara, Mihadhara na hata kumkabidhi nyaraka za siri kuhusu Udini aliyekuwa Rais wa Awamu ya Kwanza, Mkapa, Mwinyi na hata KIKWETE! lakini mpaka sasa hakuna hatua zilizochukuliwa!
Kinyume chake tumeona Serikali ya Awamu ya Kwanza kuchukua hatua za Makusudi kabisa kuwasaidia makabila ya Wabarbaig wapate elimu ili wanufaike na matunda ya Uhuru!
Waislamu ambao wanalalamika na kuthibitisha hakuna anaewasikiza na tumeshuhudia mara kadhaa Serikali ikiwajibu kwa Kuwakamata Viongozi wao na hata kutumia Polisi kutawanya Maandamano yao na hata kuwaua! rejea kitabu cha Profesa H.NJOZI
Pictures - Mwembechai Killings and The Political Future of Tanzania
Chadema kama wanania nzuri na Taifa hili na nia yao ni WA TZ wote wafaidike na matunda ya Uhuru bila kujali dini, rangi, kabila au ukanda hawana budi kuthibitisha hilo kwa vitendo na wala mazungumzo na Waislamu hayatazaa Matunda ikiwa nia ya CHADEMA sio nzuri!
nasema hivyo kwa sababu historia huwa inajirudia kwani Wakati TANGANYIKA inapata uhuru Wasomi wengi walikuwa Wakristo na Waislamu hawakwenda shule ambazo nyingi zilikuwa za Wakoloni ambao walikuwa MISSIONS!
Viongozi wa Kiislamu waliliona hilo na kumkabili Julius Nyerere ili Uhuru ukipatikana Waislamu nao wawezeshwe ili kupata fursa sawa! Nyerere alikubali hilo ktk meza ya Mazungumzo lakini alipokuwa Ikulu alifanya kinyume na makubaliano kwa kauli yake mwenyewe alisema haya:
"I have established in TANU a department of political education and I have put a Lutheran Minister in charge. He was not a great politician, but I selected him because of his balance, his gentleness and his strong solid faith..."
Gonga hapa kupata maelezo yote kuhusu Asili ya UDINI TZ!!!
ISLAM AND POLITICS IN TANZANIA
Mimi si msemaji wa Waislamu ila nadhani hawako Tayari kudanganywa kama Watoto wadogo! bila shaka wako tayari kuzungumza na chama chochote cha kisiasa lakini kwa masharti yafuatayo wengine wanaweza kuongeza:
1) Wanataka haki na usawa ktk nyanja zote za Maendeleo ya Kisiasa, Kijamii nk.!
2) Waislamu hawataki upendeleo bali usawa!
3) Waislamu wanataka Katiba mpya itakayowashirikisha moja kwa moja!
Kama CHADEMA wako tayari kukaa meza moja na viongozi wa Waislamu basi ni hatua moja kubwa kwani Waislamu ni sehemu ya Wapiga kura waliowengi kama walivyo Wakristo lakini ushauri wangu kwa Waislamu ni kuwa ikiwa CDM watakubali kukaa meza moja na Waislamu basi kuwe na mkataba maalum ambao ni matakwa ya Waislamu na ikiwa CDM watafanikiwa kuongoza TZ basi mkataba huo ni lazima utekelezwe!
Hata huko Amerika kawaida Vyama vya Kisiasa huzungumza na makundi tofauti tofauti kama vile Wayahudi na kura zao huamua nani awe Rais!
"Tanzania haina DINI" kauli hii imepitwa na wakati na sasa umefika wakati wa kuweka kila kitu ktk meza ya mazungumzo vinginevyo.......