Dk Slaa amtaka Jk ataje waliopewa Sh1.7 trilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk Slaa amtaka Jk ataje waliopewa Sh1.7 trilioni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Oct 4, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Dk Slaa amtaka Jk ataje waliopewa Sh1.7 trilioni

  By Beatus Kagashe, Iringa

  MGOMBEA wa urais wa Muungano kwa tiketi ya Chadema , Dk Willibrod Slaa mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete kuwaeleza Watanzania ni kampuni zipi zilipata Sh 1.3 trilioni ambazo alisema amezitenga kwa ajili ya kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi duniani.

  Katika mkutano mwingine uliofanyika Chimala wilayani Mbarali, Dk Slaa alimwomba mnadhimu mkuu wa Jeshi la Wananchi, Abdulrahman Shimbo kutoa ufafanuzi wa kashfa ambayo haijawahi kutolewa ufafanuzi hadi leo ya migodi ya Meremeta na Buhemba ambazo zinadaiwa kuchota kiasi cha Sh155 bilioni.

  Rais Kikwete alitangaza mpango wa kunusuru uchumi kwa kutenga kiasi hicho cha fedha kukabiliana na mtikisiko wa kiuchumi uliozikumba taasisi za kifedha barani Amerika na Ulaya, mtikisiko ambao ulitarajiwa kutetesha uchumi wa nchi nyingine duniani.

  Kikwete alitangaza mkakati huo kwenye ukumbi wa Kilimani mjini Dodoma Juni 10 mwaka jana, ambao ulihusisha kutumia Sh21.9 bilioni kufidia wanunuzi wa mazao baada ya bei kushuka bila ya kutarajia, kutoa mitaji ya uendeshaji ya riba nafuu kwa mabenki, kutoa mikopo ya thamani ya Sh20 bilioni kwa benki ya TIB, kutoa Sh20 bilioni kwa ajili ya mikopo ydenye riba nafuu kwa ajili ya ununuzi wa zana za kilimo.

  Mkakati mwingine ni kuongeza idadi ya wakulima watakaopata mbolea ya ruzuku na kiasi cha Sh90 bilioni kwa ajili ya mbolea hiyo na pia kuboresha Reli ya Kati kwa kutumia dola 43 milioni za Kimarekani.

  Dk Slaa, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema, anataka maelezo ya uchanganuzi wa matumizi hayo baada ya mwaka mzima wa utekelezaji wa mkakati huo uliowekwa kwenye bajetinya mwaka 2009/2010. Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Iringa, Dk Slaa alisema kuwa matumizi ya fedha hizo yanatia shaka kutokana na kutojulikana kwenye Bunge badala yake kutangazwa kwenye kikao cha CCM kilichoofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.

  "Nataka Kikwete atueleza ni makampuni gani yalipewa fedha hizo na yamezitumiaje," alisema Dk Slaa. “Hizi fedha ni za umma, lakini hakuna anayejua nani kanufaika nazo. Nitazishughulikia na kuhakikisha zinarudishwa kwenye matumizi ya umma.

  ” Alisema alifikia hatua ya kutaka maelezo hayo kwa kuwa dalili zinaonyesha kuwa matumizi ya fedha hizo ni ya shaka mno na kwamba hayana tofautiani na yale ya ukwapuaji wa Sh 133 bilioni uliofanywa kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (Epa) kati ya mwaka 2005/2006. Alidai kuwa pesa hizo zimewanufaisha baadhi ya mawaziri, wanafamilia na maswahiba wa Kikwete ambao wanaogopa kuwataja hadharani.

  “Hizo fedha hazikupita bungeni, zilisomwa mbele ya mkutano wa wanachama wa CCM pale Mlimani City, mbona kampuni hazijulikani hadi leo. Tunataka tuzijue ni zipi na fedha zimegawiwaje kwa kuwa ni kiini macho; ni kama Epa nyingine,” alisema Dk Slaa. “Kama ni uongo, akanushe kama mwanawe na maswahiba zake hawachezi na raslimali zetu. Na kwanini atangazie Mlimani City kwenye kikao cha CCM,” alihoji. Aliahidi pia akiingia madarakani mwaka ujao atakagua fedha za serikali ya Kikwete kwa kuwa fedha hizo ni za umma na zimewanufaisha watu wachache tu.

  Kuhusu kashfa ya Meremeta na Buhemba, Dk Slaa alisema badala ya Shimbo kujitokeza hadharani kuzungumzia uchaguzi mkuu, ni vizuri angejitokeza mapema kuzungumzia kashfa ya wizi wa fedha hizo unaodaiwa kufanywa na mgodi huo wa jeshi.

  “Bilioni 155 zilipotea baada ya kuibwa katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba. Sasa kama Shimbo ni muadilifu, ajitokeze hadharani kuwaeleza Watanzania fedha hizo ziko wapi... wizi ni wizi tu hata kama umetokea jeshini,” alisema Dk Slaa. Dk Slaa, ambaye amekuwa akiulizia suala hilo mara kwa mara bungeni ambako alikuwa akiwakilisha Jimbo la Karatu, alisema Waziri Mkuu ameshindwa kuto jibu la maswali kuhusu mgodi huo, kitu ambacho kinaacha dukuduku kwa Watanzania.

  Dk Slaa pia aliongeza kuwa maduka ya jeshi nchini kote yameondolewa kodi, lakini bidhaa zinauzwa sawa na mitaani, kitu alichokielezea kuwa ni wizi mkubwa ndani ya jeshi hilo. Alisema pia atatumia siku 100 kushughulikia mgogoro wa bonde la Ihefu na Mbarali ikiwa atapewa ridhaa ya kuongoza nchi kwa kuwa hata baada ya maelekezo ya Kamati ya Bunge bado CCM imekuwa na kigugumizi kutekeleza.

  “Hakuna mkataba ambao hauvunjwi hasa pale ambapo haukushirikisha wanajamii wa pale, mabonde yetu ila wamepewa wawekezaji na sisi tunalia hatuna cha kufanya, siku 100 nikiwa madarakani nalimaliza hili,” alisema Dk Slaa akizungumzia kitendo cha serikali kuwahamisha wafugaji kwenye bonde la Ihefu, Mbarali Machi 2006 bila ya utaratibu wala mipango. Alisema serikali ya CCM imekosa ubunifu wa kuendesha nchi ndio maana watu wanaobuni vitu wanakamatwa na kukatishwa tamaa.

  Alitolea mfano wa kijana aliyebuni na kutengeneza gobore na wengine wanaorusha matangazo ndani ya kata zao kuwa wanakatishwa tamaa badala ya kupewa kipaumbele na kusaidiwa. “Huu ndio mwisho wa CCM, haina jipya la kuwaambia watu zaidi ya kukimbizana na wapika gongo, ubunifu Tanzania umekuwa ujambazi, huu ni mfumo mbovu na elimu duni,” alisema Dk Slaa.

  Lakini pia, Dk Slaa alisema Chadema ni chama kinachomtegemea Mungu na nguvu za umma katika kuliongoza taifa hili kwa amani na mshikamano. Alisema kwa nguvu ya umma, Chadema imekubali kubadilika na kwamba sasa hakuna atakayeogopa vitisho katika mabadiliko kwa kuipa Chadema ushindi wa kishindo na kuitosa CCM. Alisema Rais Kikwete aliwahi kuulizwa na Rais wa Marekani sababu za Tanzania kuwa maskini wakati ina raslimali nyingi akajibu kuwa hajui.

  “Kama hajui kwa nini nchi yake ni maskini, kwanini anaomba kura?” Mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema, Peter Msigwa alisema kwenye mkutano huo kuwa nyumba nyingi jimboni humo hazina hati na akaahidi kuwa iwapo atachaguliwa atapigana kufa na kupona kuhakikisha wananchi wake wanapata hati hizo.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nimeicheck hiii mkuu, kuna harufu nyingine ya EPA hapa. Ngoja tumsikie atakanusha vp safari hii!
   
 3. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,679
  Likes Received: 21,937
  Trophy Points: 280
  Ndio maana wanahofia sana Dr Slaa kuingia madarakani kwani wataumbuka sana. Kwa vile wizi huu haukumfaa Mtanzania wa kawaida, sasa ndio wakati wao kuonyesha kuchukizwa kwao na ufujaji huo kwa kutumia silaha moja tuu,KURA. N kuhakikisha haiibiwa kwa gharama yeyote.
   
 4. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Sijui Hapa JK atajibu nini
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,234
  Trophy Points: 280
  Kwa upuuzi kama huu mbona uchaguzi hauji haraka tukamwondoa JK na mafisadi wake haraka:-   
 6. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakuu embu check hii link kufahamu kitu kinachozungumziwa na Dr. Slaa

  Bank of Tanzania Distributes Stimulus Package


  Bank of Tanzania Distributes Stimulus Package
  Friday, 18 December 2009 07:51

  In an effort to fill the country's recent revenue collection gaps, the Bank of Tanzania (BoT) has given the government nearly Tzs 600 billion from the stimulus package that was announced last year by President Jakaya Kikwete.

  According to Prof. Benno Ndulu, the governor of the BoT, this funding is part of the total Tzs 1.7 trillion stimulus package that was reserved in order to shield the country's economy from the effects of the global financial and economic crises.

  Money from the stimulus package that has been allocated to the government has reportedly been used to support the education, health and agriculture sectors.

  In addition, the stimulus plan is intended to be used as a means to directly compensate exporters for losses, to guarantee debt rescheduling, and to increase the loans that are provided to farmers in order for them to obtain seeds, fertilizer and tractors.

  Apart from the agriculture sector, other sectors that are critical to the country's economic stability are also scheduled to receive funds from the stimulus package; these sectors include investment, infrastructure and food security.

  Additionally, the government has also reportedly planned to grant guarantees to financial institutions in order to deal with various loans, amounting to Tzs 270 billion, that had been given to companies which they later failed to repay due to the economic crisis.

  The terms of the guarantee have been set to extend for 2 years, during which time, based on arrangements that have been made between the government and the financial institutions that have extended these unpaid loans, the firms will not be charged interest on their repayment for the duration of the guarantee.

  In a recent interview with The Citizen, Prof. Ndulu indicated that the shortfall in revenue collections has been caused, in part, by the recent global financial crisis, saying that the government had already borrowed Tzs 473 billion from the stimulus package and had also floated bonds that were worth Tzs 120 billion in an effort to further bridge the gap in the country's revenue collection.

  "One aim of the stimulus package was to cover gaps in revenue collection, and we set aside Tzs 825 billion for that purpose," he said in The Citizen report, "but only Sh600 billion has been solicited so far."

  According to Prof. Ndulu, recent reports, which indicated that approximately Tzs 400 billion of the money that was loaned to the government by the International Monetary Fund (IMF) had been given to local banks, were unfounded.

  Prof. Ndulu went on to explain that these funds were not meant to be distributed to local banks, but rather were to be used in order to stabilize the foreign exchange reserve.

  In addition, the BoT governor said that no entity, other than the government, had received money from the stimulus fund, but that arrangements had been made in order to guarantee that those who were promised assistance through the fund were given assistance through selected banks, which are scheduled to begin receiving money from the package within a few days.
   
 7. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #7
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kukanusha? Hawawezi. Kuthibitisha? Hawawezi zaidi.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Maeneo kama haya ndiyo huwa namzimia Dr. Slaa, it is very likely hizi hela zimeenda tena kwa wale wale mafisadi wetu na Dr ana faili zima.......... Sasa subiri utaona maelezo ya kujishikashika hapa na pale yatakapoanza kutolewa na akina Makamba, Kinana, Wassira na usijeshangaa Gavana wa benki kuu naye akajitosa kutoa maelezo. JK kama kawaida atakuwa mdogoooooo!!!!

  Huyu jamaa ndiyo maana anaogopa mdahalo!!!!!!
   
 9. d

  david2010 JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu watanzania ni wakati wa kuangalia na kujua majira, hayo yote ambayo DR w.Slaa anawaambia ini Ukweli na isingekuwa ukweli EPA NA RICHMOND tusingejua, lakini ahukuriwe Mungu wa Eliya alimtuma Dr W.Slaa kugombea nafasi ya urais nilikuwa nasoma unabii uliotolewa na mtumishi wa Mungu kutoka Marekani 4.7.2008 ya kwqmbq kunqa vitu Mungu anaenda kufanya Tanzania kuna baadhi iliwahusu maaskofu na watumishi pia atenda kutupa rais ambaye ni mwanaye aliyemchagua ambaye ni mcha Mungu wa kweli,('' i am going to give you a new presedent whom is my choosen son'')i will destroy all idols and show wonders say the Lord of Host i will show the treasure which was hidden say the Lord of Host'' nimejaribu kunukuu hiyo sehemu chache lakini nitawapa website ili kila mtu aweze kuusoma na kuielewa hivyo jamani DR slaa hakuingia pabaya bali ni kusudio la Mungu yeye kuliongoza Taifa nilishangaa maana kitu ambacho watanzania wamekiomba ndio hicho Mungu aliwajibu hata kabla ya kuomba ameshasikia na kabla hatujanena atafanya. tahadhari MUngu anaenda kuwapiga wote wanotumia uchawi kwa ajili ya uchaguzi na amesema atavunjavunja miungu yao na yeye anaenda kushuka tanzania wote watakaofanya wizi wa kura na kutumia nguvu watamjua yeye ni Bwana wa Majeshi ameyesema hayo na yatatimia, pia nilikuwa na baadhi ya watu ambao wanaongozana sana na rais anayemaliza muda wake kikwete ambaye najua ni usalama wa taifa niliongeanaye baadhi ya vitu na alitamba kuwa sisim watashinda nikamwambia wakitumia haki hawatashinda lakini mwaka huu Mungu hataacha muibe kura tena neno linasema mwizi na aache wizi wake na amrejee bwana, alichoniambia hilo la kura ni kweli na wanaiba na pia CCM hawajali manufaa ya watu wengi maana wabunge waliowengi kama lowasa asingepitishwa hivyo inawakumbatia wenye nazo na kuwaacha wasio nacho , lakini nilichojifunza pia nawaomba watanzania tujitokeze kumpa dr w. slaa kura maana wakiwaona vijana wanajua hao ni wahuni na hawapigi kura ila ccm inawajali kwa kuwanunulia wamama kanga na kuwalaghai ndio mbinu wanazotumia ccm na nyingine nyingi ya kuwanunua watu wakapigie kura. aliniambai mh huyo. lazima tuwe macho pia chadema nendeni vijijini mwache kuzunguka mjini kwani watu wa mjini wanawajua hao mafisadi wa ccm hivyo msitumie nguvu nyingi kuwaelimisha watu huku mjini bali nguvu nyingi muelekeze huko vijijini kama loliondo ambako jk aiwauza wamasai kwa kuwakana si watanzania na wanazalilishwa na kubakwa na waarabu na maeneo mengine ambapo baadhi ya watu wanamjua Nyerere ndio bado rais na ndio siasa za ccm vijijini kuwa nyerere ndio aliowaletea uhuru na maendeleo hivyo chama hicho kinafuata njia ya nyerere wakati wameshaasi na kupotea. Mungu iBariki Tz na Rais mteule DR W Slaa.Na uaibishe CCM na wachawi wao na wanajimu kwa kuwa wameiuza nchi Takatifu kwa majambazi na Wachawi na Wanajimu ndio wanaowaongoza kwa kuwadanganya lakini USHUKURIWE WEWE ULIYE MTAKATIFU WA ISRAEL UNLIYESEMA DAMU YA WATU WASIO NA HATIA NIMWISHO.UNAENDA KULETA MABADILIKO YA KWELI,TAREHE 1 NOVEMBER ITAKUWA NEW DAY NEW PRESIDENT NEW PEOPLE OF TZ WITH ALL YOUR WISDOM ND BLESSING THEN IT WILL BE CALL BLESSED LAND OF TANZANIA AMEN.:A S 465:

   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  :a s 13:
   
 11. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wakuu wa mahesabu tupeni hapa mchanganuo wa matumizi ya hizi hela kama zingeelekezwa kwa elimu , matibabu , wakulima n.k ili wengi wapate mwanga ni nini maana ya Trillions anazozungunzia Doctor Slaa
   
 12. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu tuwekee website si unajua wengine ni akina Tomaso?

   
 13. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mhh!!! Tuwasubiri mavuvuzela wa CCM!!
   
 14. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  Nairejesha Ripoti ya MMMJ

  [​IMG]
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
 16. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2010
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Unafikiri hiyo mipicha na mibango iliyojaa barabarani na kuchafua sana miji yetu imetoka wapi? na fedhaza kuwalipa watu ili wahudhurie mikutano ya jk na kukodi mabasina malori zinatoka wapi? can't this be the stimulus package?
   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Safari ni safari imebidi nisome japo kwa kurashia hiyo Confidential uliyopost nawashauri na wenzangu msione uvivu kuifungua na kuisoma unaweza kutamani kuvunja hata monitor ya computer kwa hasira naomba kwa ufupi pitia haya mahitimisho ya mwanakijiji ili ukifungua post nzima utapata hamuasa ya kusooma;
  Endeleeeeeea!!!!!!!


  Yafuatayo basi, tunaamini ni mahitimisho kadhaa ambayo mtu yeyote makini anaweza kuyafikia akichunguza na kufuatilia ushahidi na madai tuliyoyatoa hadharani. Si lazima tukubaliane juu ya mahitimisho haya na watu mbalimbali wanaweza kufikia mahitimisho tofauti. Hata hivyo, haya ni ya muhimu na kutusukuma kutafakari ni hatua gani kama taifa tuzichukue ili kulifunga na kulimaliza suala hili la Meremeta ambayo kwa hakika ni "aibu" ya taifa letu.
  1. Kwa watu wengi wakiwemo wabunge na watendaji wengi wamekuwa wakichanganya mambo mawili ambayo yote yakichunguzwa vizuri yataonesha jinsi gani taifa limezugwa likazugika. Utata wote wa kampuni ya Meremeta ni lazima utatuliwe kwani bila ya kufanya hivyo tutaendelea kuthibitisha kuwa utajiri wetu umekuwa ukitumika kuchochea migogoro katika eneo la maziwa makuu na kwa namna fulani kuthibitisha jinsi gani utajiri huo unaporwa na makampuni ya kigeni yakiwa na baraka zote za watawala wetu.
  2. Kiasi cha dhahabu kilichokuwa kinapatikana kati ya 1997-2000 ni kikubwa sana hasa ukiangalia takwimu zinazoonesha kiasi kilichosafirishwa nje, hata hivyo kiasi rasmi kilichorekodiwa ni kiduchu mno. Je dhahabu yote ile iliweza vipi kusafirishwa na ilichukuliwa na nani na kwa namna gani? Tunaamini Meremeta na watu waliokuwa nyuma yake wanahusika kwa kiasi kikubwa na uporaji huu wa madini yetu.
  3. Meremeta iliundwa kwa ajili ya kikundi cha watu wachache kuweza kujipatia fedha nje ya Bajeti ya Tanzania kuweza kufadhili manunuzi ya silaha na usafirishaji wa silaha haramu kuelekea kwenye maeneo ya migogoro ya maziwa makuu75. Hilo ndilo lengo la kwanza la Meremeta ambalo linafichwa na kutajwa kuwa ni la "usalama wa taifa". Ununuzi wa dhahabu kutoka kwa wauzaji wadogo wadogo uliofanywa na Meremeta haukufanywa kwenye eneo la Buhemba tu bali hadi huko Kigoma ambako madini toka Congo yalikuwa yakiletwa na kuuzwa kwa madalali wa Meremeta. Ni kwa kiasi gani madini toka Congo yalipatikana kwa damu na kununuliwa na kampuni ya "serikali" linabakia kuwa miongoni mwa maswali muhimu.
  4. Utajiri wetu wa maliasili ndio kiini cha kundi la watu wachache (wananchi wenzetu na wageni) kuamua kujitajirisha na kufanya kufukuru. Uwepo wa dhahabu na urahisi wa upatikanaji wake umewavutia watu wa kila aina. Bahati mbaya sana uwepo wa machafuko kati ya majirani zetu nako kumevutia watu wengine waovu ambao wametumia nafasi hiyo ya mateso ya binadamu wenzao ili kujitajirisha.
  Tunaweza kuona bila ya msaada mkubwa jinsi gani utajiri wa madini ni sehemu kubwa ya mgogoro wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Congo na jinsi gani utajiri huo umekuwa pia ni sababu ya machafuko huko Angola, Siera Leone na Liberia.
  Kama Watanzania na kama Waafrika wakati umefika wa kudai utajiri wetu utumike kwa ajili yetu na kuzuia utajiri wetu kuwa laana juu yetu kama ilivyo katika baadhi ya nchi ambazo zina utajiri wa kila aina lakini zimeishia kuwa na umaskini wa kutupwa.

  Kuna ushahidi mkubwa wa jinsi gani vyombo vyetu vya sheria na usalama vimezembea kwenye usukani kiasi cha kuwezesha na wakati mwingine kushiriki moja kwa moja katika uporoji wa raslimali zetu bila ya kujali nani anaathirika. Kitendo cha vyombo vyetu kuruhusu ndege za kina Bout na Dr. Kambale kutua kwenye viwanja vyetu ni kitendo cha aibu.

  Tunashangazwa na jinsi gani uongozi wa juu wa taifa letu umekuwa kama mbuni ukijificha kichwa chake mchangani wakati mwili wake wote unaonekana. Kwa kiasi kikubwa umefanikiwa katika kuzuia habari za Tanzania kuhusika katika usafirishaji wa silaha haramu kutoka katika vyombo vya habari vya kimataifa lakini umeshindwa kuzuia uporaji wa urithi wetu kwenda ng'ambo.
  Hata hivyo ukimya huu sasa hauwezekani tena kwani hii ni aibu yetu sote kama Watanzania. Ni aibu ambayo tunayo budi kuiita kwa jina lake, na kujaribu kwa uwezo wetu wote kuondokana nayo.

  Kuna mtandao mzito sana wa ufisadi ambao umewezesha mambo mengi kufanyika. Mtandao huo tunaamini umejikita katika nafasi mbalimbali serikalini na umetanda hadi nje ya nchi na hivyo kuwezesha mambo mengi kufanyika pasipo kujali matokeo yoyote (with impunity).
  Mtandao huu ni mtandao ambao umewezesha mambo mengi kufanikiwa kuanzia uundwaji wa Meremeta, kashfa katika sekta ya Nishati, kashfa za madini, kashfa za wizi wa fedha kutoka Benki Kuu n.k Ni mtandao ambao tunaamini kabisa licha kuendeleza kuchota utajiri wetu kwa kiasi kikubwa unaendeleza dhana ya kuwa Watanzania ni maskini.

  Bado kuna mambo mengi ambayo tunahitaji kuyajua na hasa nafasi ya watumishi mbalimbali wa serikali katika suala zima la Meremeta na usafirishaji wa silaha haramu. Kwani tunabakiwa na mshangao mkubwa jinsi gani watu hawa wote wanathubutu kufanya wanayofanya huku wakifumbiwamacho na wengine wakiendelea na nafasi zao hadi sasa na huku wengine wakizawadiwa nafasi na vyeo vikubwa zaidi.

  Kama dhahabu na madini mengine yameweza kutuletea matatizo na kututengenezea uongozi uliopo sasa, itakuwaje siku ambapo mafuta yataanza kububujika kutoka katika visima vyetu? Tusipoamua kutengeneza sasa mifumo na miundo ambayo itahakikisha kuwa kundi lile lile la waporojai wa dhahabu, almasi na tanzanite yetu halijikiti katika kupora mafuta yetu basi tujue kuwa yale tunayoyaona kwenye vyombo vya habari huko Nigeria, Sudan na Guinea yatatokea hata kwetu.

  Tunashuhudia malumbano ya mafuta bidhaa ambayo haijagunduliwa bado yanavyotishia umoja wa taifa letu na muungano wetu na jinsi gani viongozi wetu wanashindwa kutatua matatizo madogo ya mjadala wa mafuta ambayo hayapo na kubakia wanapigana mikwara na kutunishiana misuri. Itakuwaje basi siku itakapotajwa kuwa hatimaye mafuta yamegundulika Zanzibar? Itakuwaje siku ambapo itakuja kuonekana kuwa Tanzania ina mafuta kupita Nigeria, Angola, Uganda na nchi nyingine za Afrika?

  Tutakuwa na uwezo kweli wa kuzuia makampuni makubwa ya mamluki na yale ya uchotaji raslimali kuingia nchini kwa mikataba mingine ya kiujima kama tulivyofanya kwenye sekta ya madini? Hivyo, kwa kuangalia ripoti hii tunaweza kuona pasipo shaka yoyote ile kuwa ni utajiri wetu ndio unatusababishia umaskini wetu!
   
 18. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,811
  Likes Received: 2,753
  Trophy Points: 280
  Hili zimwi litujualo, kwa mwendo huu, tukilipa mitano mingine tumekwisha! Tuwe wajanja!
   
 19. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2010
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Duuu.........this is soo scary........yaani hawana hata huruma japo kidogo. Na bado wanataka tuwaongezee ulaji kwenye masahani yao yaliyosheheni kila aina ya mapochopocho.

  MUNGU TUSAIDIE:disapointed:
   
 20. j

  jaffery hassan Member

  #20
  Oct 4, 2010
  Joined: Dec 9, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  :blah:eek:h time wil tell you think you are living in heaven but you are living in hell,ni hayo tu wanamtandao wapi mpo tunahitaji kujua hiyo stimulus package wapi imeenda?je kuprint posters,t shirt,kanga,kulipia ndege ya mama,you name it,:
   
Loading...