Dk slaa amechakachua barua


Kama serikali hii ina huruma sana, hiyo huruma ingeonekana:

1. Kwa Watanzania kwa kupunguza matumizi ya anasa serikalini na kuboresha huduma za jamii.
2. Kwa wazee wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuwalipa mafao yao kulingana na 'dollar value' kwa vile umepita muda mrefu sana walau zaidi ya miaka 30.
3. Kufanya juu-chini raslimali za nchi zinalindwa kwa udi na uvumba ili ziwanufaishe Watanzania na siyo matajiri wachache.
4. Udanganyifu unapungua ili watu wachague viongozi wao kwa haki na uhuru na pia wanaofaulu mitihani au kupata ajira wawe wale wenye 'merit' na siyo rushwa (uchakachuaji).
5. Ukuaji wa uchumi tunaousoma kwenye vyombo vya habari ungeendana na ubora wa huduma za jamii ili wananchi waondokane na umaskini unaowanyemelea kila siku.
6. Jiji la Dar es Salaam lisingekuwa linanuka kinyesi usiku na mchana kwani si salama kwa afya za wakazi na wageni wanakuja jijini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…