Dk slaa amechakachua barua

Unajua Makame maneno mengi hayawezi kumaanisha kuwa unasema ukweli. Barua unayoisema ilinandikwa na nani? je huyo mwandishi wa barua ameikana barua hiyo? Tuseme Kabwe akakiri kuwa ni kweli barua aliiandika wewe utasema nini? Pole. Naoma umeweka jitihada zako mahali pasipostahili. Hiyo haitasaidia mzee. Wakati wa EPA wenzio walisema kuwa nyaraka za Dr. Slaa ni fake lakini sasa EPA ni kitu cha ukweli. Hivi wewe unatumia akili au...
 
Weka Hoja Ndugu yangu, usikurupuke.

Mimi siongei siasa, naongelea reality; kwanza Dkt WPS alitaka kwenda Ikulu awape Watanzania First Lady wa Kuchakachuliwa! SAD STORY
Tatizo letu kubwa ni moja WATANZANIA, Tukishakuwa na MAPENZI basi ukweli unakaa KUSHOTO, barua imechakachuliwa HAWATAKI, DKT anadanganywa hilo WANALIKATAA, imefikia hatua sasa watu WAMEMPA DOKTA SIFA YA UUNGU. Siwaelewi watanzania haswaa wanachokitaka ni kipi? Imekuwa kama ibra ya kipofu aliejaaliwa kuona punda sasa...

HIVI KWANINI HOJA HAZIJIBIWI KWA HOJA???:A S angry: Makame kaleta hoja ijibuni kwa ufasaha sio....
 
Makame toa ushaidi uonyesha BARUA HIYO imechakachuliwa
 

Kama amechakachuwa kwa nini hajachuliwa hatua?
 

Matokeo ya kura yamechakachuliwa na hilo hawalitaki pia!
 
kwakweli sielewi hii ya slaa kuchakachua barua, kwani najua kwamba si yeye aliyeileta kwenye public, anyway, kwa ccm kila kitu kinawezekana kwani uwezo wao wa kufikiri ni mfupi mno hata wakiambiwa ila ya chadema kaandika slaa na ya ccm kaandika jk watakubali

myopia
 

hivi kwa akili zako za kawaida mkuu unadhani ile barua ni genuine? hivi kweli maagizo ya kuiba kura yanaandikiwa na ushaidi wa barua enzi hizi? hivi kikao cha kuiba kura kinachomuhusisha rais( anayemteua mwenyekiti wa tume) maagizo yake yanakwenda moja kwa moja kwa msimamizi wa jimbo( wapi itifaki). kubalini kuwa labda mlidanganywa na ninyi hamkushughulisha akili zenu au slaa kaichakachua ku explain defeat kwa waliomchangia.
 
Hivi anayedaiwa kuandika na kusaini barua hiyo (M. W. Kabwe) amekanusha? Nilitegemea awe mtu wa mwanzo kabisa kuikanusha na hata kushitaki mahakamani.
 

Kuandika kwa ufasaha namna hii si lazima uandike ukweli! Swali: kama ni ya uwongo kwa nini serikali yetu inayoimbwa kuwa ya utawala bora (wa sheria) haijachukua hatua dhidi ya mtu anayeitumia kuwa ni kweli? Hebu tumia lugha lugha nzuri pia kuelezea hili.
 
Baada ya ushindi wa wizi sasa mnataka kuhalalisha matokeo?kama unataka kujua garama ya uchakachuaji muulize mkurugenzi wa shinyanga aliyekimbia mji wake baada ya kutii amri ya vigogo wa CCM.Kiama yenu inakuja wala sio siku nyingi wapo kina moi wa hapo jirani walijiita majogoo wa siasa sasa wako wapi,yuko aliyejiita tingatinga ameondolewa jimboni na baiskel ya mbao wala sio tingatinga,2015 wala sio siku nyingi utakapohitaji mtuonyeshe international airport kigoma,barabara za juu na chini Dar,meli kuanzia ziwa tanganyika,victoria,nyasa na kwingineko.
 
Aalivyoanza kutangaza wizi wa EPA mkasema haiwanyimi usingizi lakini siku chache baadae likawa ni suala la kuwanyima usingizi mkaanza kukamatana uchawi,hatushangai kukanusha hili jambo maana ni kawaida yenu mlisema document alizonazo za EPA ni feki lakini hakuna aliyemfikisha kortin mapapa wakasema watamshtaki wakaanza kushtakiwa wenyewe,kwa hiyo tumewazoea wala msitumie jukwaa hili kujisafisha mmeshachafuka kwa kufanya wizi na hilo kila mtu anajua,
 
hapo ndo tunaposhindwa kuelewana na nyie vibaraka wa hao mafisadi... mnaforce mambo ambayo mtu mzima hawezi kukubali kuendeshwa kwa staili izo...umeanza ameghushi then unasema hajaudhuria kuapishwa.....mnakwepa hoja, kama mnaona ameghushi si mmshitaki...kwani kughushi ni kosa la jinai....PRESS CONFERENCE sio adhabu ya mtu anaeghushi....
kimsingi Dr. Slaa ni mtu makini kuliko hao wa miungu watu mnao waabudu.......na mmemdhulumu haki,sio yeye tu, bali watanzania wote wapenda mabadiliko..
KAMA ULIKUWA MPANGO WA MUNGU MTAFANIKIWA, ILA KAMA HAUKUWA MPANGO WA MUNGU NAJUA TUTASIKIA MENGINE KMA ILIVYOKUWA KWA LOWASA NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI:yield:
 
Kuna watu wengine kwenye ukumbi huu wanaibisha JF,they are not GREAT THINKERS!

Hivi barua kama hii unaweza kuitilia shaka yoyote kuwa ni fake kama wewe ni Great thinker? Hii barua inaonekana imekuwa-scanned kama ilivyo.


Vitu ambavyo ni vya msingi kabisa kwenye barua yoyote ni pamoja na:
  1. Nembo(Logo) ya mwandishi au mwenye barua. Ipo inasomeka vizuri kuwa ni ya JIJI LA MWANZA.
  2. Anuani/e-mail/Namba za Simu.Namba za simu zipo na zinasomeka vizuri.
  3. Sahihi ya Mwandishi. Ipo na amesaini. Kumbuka Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwanza Mjini Bw. Kabwe ambaye kwa wadhifa ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza alipoonyeshwa barua hii alikiri kuwa SAHIHI NI YA KWAKE LAKINI MANENO SI YAKE!!!!!Another Longolongo za CCM!
  4. Maelekezo kwenye barua ile ndiyo yalivyotekelezwa. Hilo kila mtu analijua. Rejea ucheleweshaji wa kutangaza matokeo ya kura na vurugu zilizofuata kwa watu kupigwa mabomu Nyamagana na Ilemera.
  5. Mhuri wa JIJI haupo. Siyo lazima kulingana na unyeti wa barua yenyewe.
  6. Namba za rejea(Ref.number)hazipo. Siyo lazima kwasababu kama ya bullet number 5.
Hapa HAKUNA UCHAKACHUAJI. Kwa hiyo acha ubishi wa kipuuzi usio na msingi.Try to be a Great Thinker not a Great Sink!
 
sio rahisi kwa watu kuagiza kimaandishi mambo kinyume na sheria za utawala bora.

Hayo mambo yashapitwa na wakati.

Sasa kama CHADEMA bought it wholly, maanake ni kwamba wamekuwa discredited kwa kukubali such a letter. It is vividly clear kwamba it is not authentic


 
Barua yenye content ya aina hiyo haiwezi kuandikwa; hata kama kuna nia ya kucheza rafu. Watu wakiweka mambo kimaandishi huwa kunabaki na permanent record and it can go against them.

Hivyo< kitendo cha kuamini tu kama hiyo ni authentic kunanilazimisha nijiulize more questions


 
Magobe

haya mambo yanafanyika. Sio lazima yaishe kwa kasi unayotaaka


 
WATU WANACHAKACHUA MENGI IKIWEMO

1. Mafuta
2. Leseni
3. Vyeti
4. Ndoa
5. Vibali

Na huchakachua kwa kutumia NEMBO, MIHURI, SIGN na vyengine

Unashangaa hilo

Au wewe ndio unakuwa Mbishi?

Au unakuwa GREAT SINK?

 
Hiyo Press Conference ni Ya Idara ya Usalama wa Taifa; ambayo iliona UMUHIMU KUJIBU TUHUMA NZITO DHIDI YAKE.

Wengine pia wamejibu

1. Rostam
2. Lowasa
3. Ridhwani
4. Kinana
5. NEC

Serikali hii inahuruma Sana; kwa kuwa wanailea Democracy; hawataki kuonekana wanamuonea Slaa kwa kumshtaki. Ila wakiamua, wanamshtaki. SEMA ATAANZA KUTAKA UJIKO, ETI ANAONEWA; wakati ameshiriki kuchakachua barua kwa lengo zima la kuitukanisha serikali wa Wananchi na kutafuta CHEAP POPULARITY


 
SWALA LA EPA Liko Mahakamani; sitoliongelea

Fuatilia vizuri chimbuko lake kabla hujampa SLAA credit ya watu wengine.

 
wewe makame ni bogasi,hiyo ccm imekusaidia nini?mtu mwenyewe ni masikini wa kutupa,pole sana.chademe oyeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…