Dk. Slaa Ajibu Mapigo ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa Ajibu Mapigo ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dudus, Mar 6, 2011.

 1. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,764
  Likes Received: 6,075
  Trophy Points: 280
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa amejibu mapigo ya Chama cha Mapinduzi(CCM) na kusema kuwa Chama chake hakitasitisha maandamano yanayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini na kwamba yupo tayari kwa lolote.

  ........

  Kwa msisitizo akasema kuwa yeye na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe wako tayari kwa lolote hata kama ni kukamatwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya Watanzania.

  .......

  Hata hivyo, Dk. Slaa alisema CCM ndio inasababisha vitendo vya uvunjifu wa amani nchini kutokana na Serikali yake kutowajali wananchi maskini, hivyo lawama hizo hazipaswi kwenda kwa viongozi wa Chadema waliojitolea kufa kwa ajili kupiga kelele kwa kukataa ukandamizwaji huo.

  "Mimi sina hofu na kauli wanazozitoa CCM, waache wapige kelele kwani inaonyesha ni jinsi gani serikali ilivyoshindwa kuongoza na sasa wanahitaji huruma za wananchi ambao kwa miaka mingi wamenyimwa haki zao," alisema Dk. Slaa.

  Aliendelea kusema "Nchi ni sawa na tunda la amani, lilokuwa juu ya mti unaoitwa haki, nashangaa sana CCM inavyopaza sauti juu ya amani pekee ikiwa inakakataa kutoa haki, tunachohitaji ni haki ifanyike."

  Hata hivyo, alisema kabla ya kwenda kushtaki kwa wananchi kwa njia ya maandamano katika mikoa mbalimbali, walitumia wabunge kuilalamikia Serikali ndani ya Bunge juu ya malipo ya Dowans, Kagoda na Meremeta, lakini serikali ilikataa kutoa majibu. Alisema, kama Serikali inaona maandamano wanayoyafanya yanavunja sheria ya nchi hakuna haja ya kukiadhibu Chadema, bali yeye na Mwenyekiti wake Mbowe wakamatwe.

  Alimtaka Kapteni Chiligati kujifunza sheria na kusoma Katiba ya nchi kwanza kabla ya kuanza kutoa vitisho ambavyo vinaweza kuipeleka nchi katika sehemu mbaya.

  "Naomba waache kukiadhibu chama, naomba wanitafute mimi na Mbowe watukamate tupo tayari kukamatwa kwa ajili ya kutetea wananchi, kinyume cha hapo moto huu hautazimika hadi kieleweke," aliongeza kusema.


  Full Story: Home

  SOURCE: NIPASHE, Jumapili, 06th March 2011.
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa amejibu mapigo ya Chama cha Mapinduzi(CCM) na kusema kuwa Chama chake hakitasitisha maandamano yanayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini na kwamba yupo tayari kwa lolote.
  Akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kutoka Mkoa wa Kagera jana, Katibu huyo aliitaka CCM iache kutapatapa baada ya kuona umma wa Watanzania wameamka na kuona jinsi serikali isivyopatia ufumbuzi kero zinazolalamikiwa na wananchi.
  Kwa msisitizo akasema kuwa yeye na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe wako tayari kwa lolote hata kama ni kukamatwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya Watanzania.
  Dk. Slaa alikuwa akijibu kauli ya Kamati Kuu ya CCM iliyotolewa juzi ambapo mbali na mambo mengine, imekilaumu Chadema kufanya maandamano katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuchochea uasi na machafuko nchini.
  Akitoa tamko hilo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Kapteni mstaafu John Chiligati, alisema kufanya maandamano ni haki kikatiba, lakini kitendo cha viongozi wa Chadema kuhamasisha uasi na kuchochea chuki dhidi ya serikali iliyowekwa madarakani na wananchi ni kitendo kinachoweza kuvunja amani nchini.
  Hata hivyo, Dk. Slaa alisema CCM ndio inasababisha vitendo vya uvunjifu wa amani nchini kutokana na Serikali yake kutowajali wananchi maskini, hivyo lawama hizo hazipaswi kwenda kwa viongozi wa Chadema waliojitolea kufa kwa ajili kupiga kelele kwa kukataa ukandamizwaji huo.
  "Mimi sina hofu na kauli wanazozitoa CCM, waache wapige kelele kwani inaonyesha ni jinsi gani serikali ilivyoshindwa kuongoza na sasa wanahitaji huruma za wananchi ambao kwa miaka mingi wamenyimwa haki zao," alisema Dk. Slaa.
  Aliendelea kusema "Nchi ni sawa na tunda la amani, lilokuwa juu ya mti unaoitwa haki, nashangaa sana CCM inavyopaza sauti juu ya amani pekee ikiwa inakakataa kutoa haki, tunachohitaji ni haki ifanyike."
  Hata hivyo, alisema kabla ya kwenda kushtaki kwa wananchi kwa njia ya maandamano katika mikoa mbalimbali, walitumia wabunge kuilalamikia Serikali ndani ya Bunge juu ya malipo ya Dowans, Kagoda na Meremeta, lakini serikali ilikataa kutoa majibu.
  Alisema, kama Serikali inaona maandamano wanayoyafanya yanavunja sheria ya nchi hakuna haja ya kukiadhibu Chadema, bali yeye na Mwenyekiti wake Mbowe wakamatwe.
  Alimtaka Kapteni Chiligati kujifunza sheria na kusoma Katiba ya nchi kwanza kabla ya kuanza kutoa vitisho ambavyo vinaweza kuipeleka nchi katika sehemu mbaya.
  "Naomba waache kukiadhibu chama, naomba wanitafute mimi na Mbowe watukamate tupo tayari kukamatwa kwa ajili ya kutetea wananchi, kinyume cha hapo moto huu hautazimika hadi kieleweke," aliongeza kusema.
  Alisema wao kama chama cha upinzani wapo kama kioo cha kueleza mabaya yanayofanywa na serikali na kamwe hakuna vyama vya upinzani vinavyofanya kazi kuipigia debe Serikali kama wanavyotaka CCM.
  Mapigo haya ya Dk. Slaa yanakuja siku moja baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa(Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Kapteni John Chiligati kukutana na waandishi wa habari na kusema kuwa nyendo za Chadema zina agenda ya siri ya kuing’oa kwa nguvu serikali iliyoko madarakani kinyume cha Katiba, hivyo akaitaka serikali pamoja na vyombo vyake vya dola kuchukua hatua za kisheria haraka.
  Kapteni Chiligati alisema Kamati Kuu inaungana na hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa mwishoni mwa Mwezi wa Februari, mwaka huu kukemea kauli za uchochezi ili kuinusuru nchi katika machafuko na pia zinavunja sheria za kikatiba za nchi.
  “CCM inaviomba vyombo vya dola viwe imara kuchukua hatua za kisheria…wanachofanya Chadema ni kutuchonganisha na wananchi, kutoa kauli hatari za kujaribu kugilibu akili za watu ili kuchochea machafuko, umwagaji wa damu na uasi”, alisema Chiligati.
  Alisema, hatua za Dk. Slaa kuendeleza malumbano na uchochezi kupitia maandamano ya wafuasi wake kunaonyesha kuwa hajakubaliana na matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwishoni mwa mwaka jana na kumfananisha na Jonas Savimbi aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Unita cha nchini Angola.
  Hata hivyo, kumeibuka kauli mbalimbali kutoka kwa viongozi wa vyama na taasisi binafsi wakikemea kitendo cha Chadema kuhamasisha uasi na chuki dhidi ya serikali iliyopo madarakani.
  Miongoni mwa waliopaza sauti zao kukemea ni pamoja na Waziri wa Nchi ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu, Steven Wasira ambaye alikitaka chama hicho kisije kikajilaumu pale Serikali itakapokosa uvumilivu na kutumia dola kudhibiti hali hiyo.
  Wasira alisema Chadema hakina haki ya kufikiria kuiondoa Serikali madarakani ikiwa imechaguliwa na wananchi walio wengi kwa kura halali.
  Waziri huyo alisema, kama hali ngumu ambayo Chadema inasema ndio chanzo cha wao kuandamana, ni jambo ambalo linatokana na mlolongo mrefu kutokana na dunia kukabiliana na matatizo ikiwemo kupanda kwa bei ya mafuta.
  Naye Anne Kilango,Mbunge wa Same Mashariki (CCM), alinukuliwa akisema maandamano ya Chadema hayalengi kupinga malipo ya Dowans na badala yake yanafanywa ili kuhamasisha wananchi kufanya vurugu.
  Kilango alisema kama kweli Chadema kinataka Dowans isilipwe kingeongeza nguvu za wanasheria ili kuhakikisha kesi iliyofunguliwa mahakamani na wanaharakati inafanikiwa na sio kuzunguka nchi mzima kumtaka Rais ajiuzulu.
  "Najua ndugu zangu wa Chadema hawataki kusemeshwa lakini mimi kama kiongozi lazima niwaambie ukweli, kauli ya kumtaka Rais ajiuzulu hazifanani na lengo la kuishinikiza Serikali isilipe Dowans." alisema Kilango.
  Naye Mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema alisema kitendo cha kuiondoa madarakani Serikali bila kufuata taratibu za kikatiba kunaweza kuzalisha matatizo makubwa na kuliangamiza Taifa.
  Mrema ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), alisema ufisadi na matatizo mbalimbali yanayoikumba Taifa sasa hayawezi kutatuliwa kwa maandamano na kwamba njia sahihi za kuleta ufumbuzi kwa wadau wote kuangalia njia bora isiyohatarisha uvunjifu wa amani ya nchi.
  Naye Risasi Mwaulanga ambaye ni balozi wa Amani kutoka taasisi ya Unirvesal Peace Federation ametaka viongozi wa Chadema kukamatwa mara moja kwa kile alichokisema wanavunja amani ya nchi.
  Akasema kuwa maandamano yanayoongozwa na Mwenyekiti wa Chadema ni ubunifu wa kutaka kukiangusha chama tawala kwa kupandikiza chuki baina ya wananchi na serikali kwa yale wanayoyaongea hadharani kuwa serikali imesababisha maisha magumu kwa wananchi.
  ”Hakika huu ni uhaini wa wazi ambao Chadema inaufanya, kwani unapokasirika umma na kupata hamasa mbaya matokeo yake ni kuzigomea sera na kukataa kushirikiana na serikali katika kazi za maendeleo." alisisitiza.


  Source: :: IPPMEDIA  My take:
  Ni kwa nini Dr Slaa na Mbowe wasikamatwe ikiwa tayari kuna ushahidi wa UHAINI wanaotaka kuufanya. Pia ikiwa rais kupitia hotuba yake anakiri mambo wanayofanya CDM si halali ni nini kinachomshinda kuwachukulia hatua! Hapa inatutulisha mashaka kama kiongozi wa nchi kutambua ukweli wa kile kinachoelezwa lakini anatafuta njia mbadala ya kuwaziba mdomo.


  Kilango ana chuki sana na CDM kwa kuwa jimbo alipata upinzani mkali ambao hakuutegemea hivyo ni kama anapunguza sumu yake, upiganaji wote umekwisha anachokiona saizi ni CDM pekee.


  Mrema yeye anatafuta kujijenga upya simshangai.
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Aluta continua haki kieleweke. Tusubiri Dar
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Tatizo viongozi wetu wa CCM wanafanyakazi kwa mambo ya Mtabiri Yahya; CDM wanafanyakazi yao Kikatiba na Kisheria, CCM waondoke wenyewe kwa amani kama hawataki machafuko.
   
 5. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,832
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Safi sana!nilikuwa nasubiri kauli ya hawa makamanda dhidi ya upupu wa ccm na serikali yake.Wao wanadhani CDM huwa wanakurupuka tu ktk mikakati yao!
   
 6. a

  asakuta same JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 15,065
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 0
  viva la revolusion! mpaka haki ipatikane makamanda wa ukombozi.
   
 7. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  dr phd ya ukweli unatupa ujasiri mimi nishaandaa wosia tayari kwani nipo tayari kusimama mstari wa mbele kupigania haki zetu watanzania fa ni matokeo tuu kwani ni aibu kufa kwa maralia au kipindupindu magonjwa yanayotibika lkn serikali mbovu ya ccm imhina kupambana nayo,ni heri kufa ukidai haki kwani historia haitafutika milele
   
 8. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Rula umevua magwanda lini? Kuna thread kama hii humu ndani mna-miss use distribution!!
   
 9. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CCM , mwaka huu lazima mchanganyikiweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 10. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  uvunjifu wa amani unaofanya na ccm ni kama walivyofanya mubarak na ben ali wa misri na tunisia. We huwapi wananchi huduma muhimu then unataka wakae kimya. Kama mnajiuliza mfanyeje nendeni mkapate uzoefu wa misukosuko kwa ben ali na mubarak sio kuwatishia mbowe na dkt slaa. Ushauri kwa ccm timizeni mahitaji muhimu kwa wananchi na kujibu tuhuma zote zinazo wahusu (jambo ambalo najua hamuwezi coz nyie ndio wahusika wakuu wa wizi na ujambazi wa mali za watanzania).
   
 11. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  kuna mtu amekamatwa Karagwe eti an mabango aliyoandaa kumwonyesha pinda. polisi wamekataa na yeye wamemwamulu asiseme kitu maana watampoteza. Binafsi namfahamu na amenipa habari usiku wa saa nane. mabango yake yalisema
  1.'TUPE CHAKULA KABLA YA KULIPA DOWNS MAANA MIGOMBA IMENYAUKA"
  2. 'MBUNGEWA KARAGWE NI NANI'
  3. KWA NINI MAGANDA YA KAHAWA YANAUZWA UGANDA WAKATI ZILIZOKOBOLEWA NI KAHAWA ZETU NA SISI TUNAYATAKA."
  4. WANAOCHIMBA TINI KYERWA NA MURONGO MBONA WANAUWAWA NA POLISI"
  5. JE MBUNGE WA KYERWA ANESEMA UKWELI ETI NGUZO ZA UMEME WETU ZIMETEKWA KWENYE MELI SOMALIA'.
  Wenye uwezo wa kufatilia wafanye hivyo, na nasikia wote waliogombea chadema wanafatiliwa mpaka mkuu atakapoondoka
   
 12. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  imekaa vizuri
   
 13. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Aluta continua dkt wa ukweli na mapambano ndio yanaanza, huo ni mwanzo tu hadi tufike 2015 ccm watakuwa hoi na dkt slaa anakuwa raisi kiulaini bila ubishi. Kama mnabisha muulizen jk alivyohaha kuiba kura za dkt kwa msaada wa usalama wa taifa na nec.
   
 14. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Ukimya wetu watanzania kwa muda mrefu serikali ya CCM imekuwa ikiutafsiri kama uoga na udhaifu.sasa wakirusha bomu litakutana na bomu.
   
 15. n

  nyamagaro JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Hata Fredrick Sumaye amekiambia ccm kujibu hoja siyo kutoa vitisho vya uvunjifu wa amani
   
 16. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hakili ni nywele kila mtu anazake! kwa kuwa wapambe wapo Dr slaa atavimba kichwa na kujiona shujaa,haya mshangilieni.
   
 17. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  CDM kanyaaaaga tweeeeeeeeeende............................
   
 18. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo mwaka huu....Safari sana Dr tuko pamoja
   
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  DR SLAA na MBOWE tupo nyuma yenu waacheni ccm iwakamate sisi wananchi tutakuja kuwachukua kwa nguvu ya PEOPLES POWEEEER. ccm wanatapatapa huyu chiligati nadhani hajui nguvu ya umma.
   
 20. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Uko sawa kabisa Kanyasu.
  Watu badala ya kuwashangilia mashujaa kama Chiligati, Makamba, Wasira au Pinda wanamshangilia Slaa.

  Tanzania zaidi ya uijuavyo!!!
   
Loading...