Dk. Slaa Aibua Mapya IPTL, asema ni bil 400 na si bil. 306 Zilizochotwa ESCROW!!!!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, amesema fedha zilizochotwa katika Akaunti ya Tegeta Escrow ni sh bilion 400 badala sh bilioni 306 kama ilivyokaririwa na vyombo vya habari kutoka bungeni.

Hayo aliyabainisha juzi na Katibu Mkuu huyo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika katika mtaa wa Mnazi mmoja Manzese, Tip top jijini Dar es Salaam.
Dk. Slaa alisema kutokana na tuhuma hizo, alifuatilia bunge hatua kwa hatua hadi likaisha kwa maridhiano, akiamini wezi wa fedha hizo watachukuliwa hatua lakini cha kushangaza hadi leo hawajachukuliwa hatua nab ado wanaendelea na kazi.
“Fedha alizochukua Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo ni ukweli uliowazi kuwa Rais Jakaya Kikwete anajua na ndio maana mawaziri hao wamekuwa na jeuri.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa.


“Suala la Escrow ni bichi kuliko mnavyofikiria, lugha ya Mwalimu Nyerere aliposema watu wanaokimbilia Ikulu tuwaogope kama ukoma, Ikulu ni mahali patakatifu mahali pa heshima kumbe wakubwa walijua kuna nini? Atoke Kikwete hadharani kama nasema uongo,” alisema.
Alisema hajawahi kuona Waziri dhaifu kama Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwani kama angekuwa makini, angeweza kuzuia wizi huo usitokee.
“Mfumo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mbovu kuanzia Kikwete mwenyewe na serikali za mitaa hata wabadilishwe viongozi katika chama hicho bado hakutakuwa na mabadiliko ya kimaendeleo nchini,” alisema Dk. Slaa.
Naye Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe alisema kuwa nguvu ya CHADEMA ya kusimamisha wagombea katika mitaa na vitongoji kwa asilimia 98 katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini imewatia hofu CCM.
Mbowe, alisema baada ya kubaini mbinu chafu za chama hicho, kuwawekea wagombea wa CHADEMA pingamizi huku wengine wakienguliwa kimizengwe ni dalili ya wazi kwamba chama hicho kinahofu ya kushindwa.
“Presha hiyo inawafanya wawaengue wagombea wetu kwa kuwajengea hoja zisizo na msingi mara utasikia jina limekosewa mara sijui jina la chama liko hivi ili mradi tu wakipunguze nguvu chama chetu.
“Nawaomba wakazi wa Vijibweni ikifika Desemba 14 siku ambayo itakuwa ya uchaguzi, mjitokeze kwa wingi kama mlivyojitokeza leo ili mkawapigie kura wagombea wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),” alisema Mbowe.
Mbowe, alisema CHADEMA haitaki ushindi wa dezo bali wanataka uchaguzi huru na wa haki ili mshindi atakayepatikana, ashinde kwa haki.
Aidha, CHADEMA imetahadharisha kuwa endapo vurugu za kuwaengua wagombea wake zitaendelea, chama hicho kitakwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi huo.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, Issaya Mwita, awali akitoa taarifa ya mchakato wa uchaguzi huo alisema katika Kata hiyo ya Vijibweni kuna mitaa sita.
Alisema katika mitaa hiyo, Chama Cha Wananchi (CUF), kimesimamisha wagombea wawili huku CHADEMA kikisimamisha wanne.
Chanzo: GPL



 
Lakini kwenye mada yako sijaona paliposema pesa ya ESCROW ni bil.400 na siyo bil.306. Hata kama ingesema, ushahidi ni muhimu. NAKUMBUKA waliokuwa wanapigia DEBE Escrow walikuwa wanasema serikali ya CCM inashindwa kuamini ripoti yavyombo vyake yaani CAG na PCCB. Leo SLAA anaibuka na bil.400, Ina maana Wapinzani nao hawana imani tena na hiyo ripoti?
 
Huyu Mzee naye Kaanza Kanchanganyikiwa.

CAG na PAC wanasema ni 306Bln, hizo 400Bln kazitoa wapi????.

Pia anapaswa kuelewa kuwa raisi kwasasa anaumwa, tumpe muda arejee ktk hali ..
 
Huyu Mzee naye Kaanza Kanchanganyikiwa.

CAG na PAC wanasema ni 306Bln, hizo 400Bln kazitoa wapi????.

Pia anapaswa kuelewa kuwa raisi kwasasa anaumwa, tumpe muda arejee ktk hali ..
Tena nakumnuka ZITTTO na kamati yake walikuwa wanailaumu serikali kwa kutokuwa na imani na CAG na PCCB ambao ni vyombo vyake, leo SLAA anataka kutuaminisha kuwa yuko tofauti na Mbowe, ZITTO na KAFULILA na wengine waliokuwa na imani na hivyo vyombo kwa 100%
 
Huyu mzee nasikia MSHUMBUSI akitishia tu kumuacha huwa anachanganyikiwa, tumsamehe bure
 
Kumbe huyu mzee bado yupo kwenye siasa? Long time sijaingia kwenye hili jukwaa....nashangaa kumuona bado yupo na anaendelea kutoa pumba kama zamani.
 
Kumbe huyu mzee bado yupo kwenye siasa? Long time sijaingia kwenye hili jukwaa....nashangaa kumuona bado yupo na anaendelea kutoa pumba kama zamani.

tena sasa pumba ndo zimeongezeka.
 
Kumbe huyu mzee bado yupo kwenye siasa? Long time sijaingia kwenye hili jukwaa....nashangaa kumuona bado yupo na anaendelea kutoa pumba kama zamani.
Pumba kama za Richmond zilizomng'oa Lowasa. Ebu mlinganishe na babako kidogo tuone babako kachangia hoja gani mpaka za Slaa uziite pumba.
 
CCM wanaweweseka sasa, mara wawajibishwe mara CAG mwongo mara sisi nani kazeeka wanaacha kujadilidi hoja za msingi. Muda wa CCM wa kutawala nchi hii unahesabika hata kama si 2015 lakini wajiandae. Wamejaribu kuisambaratisha CHADEMA kwa hali na mali lkn wameshindwa. Sasa sijui watakuja na hoja gani 2015, wao kwao kustaafisha viongozi imekuwa kama ndo njia ya kuwaonyesha wananchi wanafanya kazi.

Dalili za mtu kufa huongea hongea sana siku hiyo.
 
Pumba kama za Richmond zilizomng'oa Lowasa. Ebu mlinganishe na babako kidogo tuone babako kachangia hoja gani mpaka za Slaa uziite pumba.

Kwanza mzee wa kaya anamgwaya sana Slaa. alipoona kaitwa Dr. naye chapchap kajiita dr.
 
Back
Top Bottom