ras jeff kapita
JF-Expert Member
- Jan 4, 2015
- 22,729
- 34,830
Si angekuja mlimani city tu kiroho safi....ama aliogopa kukutana
na konda
na konda
Hakupata bili 50,aliwekewa kwenye akaunti 2b alivyoenda kuchota akakuta milioni 2!akauliza why akaambiwa aliyeweka 2b anasema alikosea sifuri 3,Dr. alilia sana lakini tayari alishajiuzuru.chezea sisiyem
Kwa maisha ya Canada hiyo nayo ni pesa?The average salary for a Sales Manager/Officer is $60,063 kwa mwaka in Canada ambayo ni dola elfu 5 kwa mwezi
Kama milioni 11 na ushee kwa mwezi....
Endeleeni kusema kafulia
Umeshawahi kuishi canada? Embu labda tupe muongozo na maisha kwa ujumla na ulikua unaishi mji gani canadaKwa maisha ya Canada hiyo nayo ni pesa?
u must be joking
Jamaa hana ubunifu kabisa huyu.....angetuongoza vipiDoctorate yake ya Theology imeshindwa Kumkomboa na Yeye ameshindwa kuitumia kweli mpaka aende kufanya Kazi za Kiwango cha chini kabisa cha Hadhi yake?
Nilikua Toronto kwa miakaa kabla vyuma havijakaza nikahamia Calgary. Mkuu gharama za maisha huku ni ghali. Lazma ufanyekaz kw masaa. Rent, cable, steam, gas, transport, msosi bado wkend ukitaka kupata balimi ningumu.Umeshawahi kuishi canada? Embu labda tupe muongozo na maisha kwa ujumla na ulikua unaishi mji gani canada
Wonders shall never endHahahah, tena kaajiriwa
OntarioUmeshawahi kuishi canada? Embu labda tupe muongozo na maisha kwa ujumla na ulikua unaishi mji gani canada
Unataka debateKwa hiyo anafanya kazi 24 hours? Yaani halali,hapumziki!!!!
Average Working hours ni 8 ingawa inaweza kuzidi kidogo.
Na pia kazi sio 30 days,kuna weekend,kuna jumapili n.k
Ama kweli dah ...Watu wengi wanapiga kelele tu, lakini hawajui hata COSTCO ni mdudu gani. Hivi kweli kwa wanaoifahamu COSTCO wanaweza ilinganisha na NAKUMAT, Imalaseko na viduka vya kibongo kweli? Unaposema COSTCO unazungumzia the largest American membership-only warehouse club. It is the second largest retailer in the world after Walmart. Yaani kama ingekuwa ijengwe pale Mlimani City, inakusanya kale kajengo kote na eneo lote linakuwa na duka moja - hapa nazungumzia mpaka vile vibanda/nyumba zilizopangishwa. Si kwamba wanauza bidhaa za nyumbani tu, huu ni udhalilisha kama si upotoshaji usio na maana, wanauza mpaka mafuta ya magari - Petrol Filling Stations, matairi ya magari na vifaa mbalimbali vikiwemo vya ujenzi, huduma za upimaji wa macho na miwani pia huduma za masikio - audiology dept. Kuna wafanyibiashara wengi yakiwemo mahoteli yanajiendesha kwa kutegemea bidhaa zinazouzwa COSTCO. Kifupi wanakwenda COSTCO kufunga mzigo wa kuuza kwenye maduka na mahoteli yao.
Kuhusu mishahara, wanalipa vizuri kuliko supermarkets zozote unazozijua humu duniani. Hii ni policy yao uliza mfanyakazi yeyote aliye kwenye Retail or Wholesale industry atakwambia juu ya COSTCO iwe ni USA, CANADA, UK na hata Japan. Kwa hiyo kwa Dr Slaa kufanya kazi huko, si kwamba ka-lost, hapana ni maamuzi yake kuamua kuishi kwa namna hiyo. Nina uhakika kwa ngazi aliyopo Sales Advisor, atakuwa analipwa hela nzuri kwa fortnightly - kila wiki mbili kuliko hata Full-time lecturer wa Tanzania. Na kwa usawa huu wa Magufuli, wabongo wengi tunaisoma namba. Pia pamoja na mapungufu yake ya kisiasa, nina uhakika huko aliko atakuwa anakula good times kuliko wabongo wengi na viongozi wa kisiasa waliobaki Bongo. Job security nzuri, social services za uhakika, hakuna mizingwe ya mshahara, na bado usafiri na mazagi zagi mengine ya kumwaga. Mwacheni Mzee wa watu amalizie siku zake kwa amani huko aliko!
View attachment 628021
COSTCO Gasoline station
View attachment 628018
View attachment 628019
Piga kazi mzee achana na story za wabongo wanaongea sana halafu kazi hawataki ila hela wanazitakaWaswahili tuna msemo wetu wa..'kazi ni kazi, ilimradi mkono uende kinywani'; yaani haitakiwi mtu kuchagua kazi, kikubwa kazi husika iwe halali na iwe inakulipa.
Kama kichwa habari kinavyosema kuwa, Dk. Wilbroad Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CHADEMA amepewa ajira ya afisa mauzo wa supermarket huko Canada, je, hii tuite kupanda na kuangakuka kisiasa kwa Dk. Slaa?
Itakumbukwa pia, Dk. Slaa aliwahi kuwa Rais wa bodi ya hospitali ya CCBRT, ya jijini Dar Es Salaam.
=======
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za majumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, imebainika.
Dk. Slaa, kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2105.
Kwa muda wa wiki kadhaa, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani wa Karatu, amemaliza masomo yake na sasa anafanya kazi katika moja ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini humo – Supermarket.
Supermarket ya Costco anayofanya kazi Dk. Slaa akihudumu kama Mshauri wa Mauzo (Sales Advisor), akilipwa Dola za Marekani 10 (zaidi ya Sh 20,000) kwa saa, ina hadhi kama Nakumat, Shopers, Imalaseko, Game na maduka mengine makubwa nchini.
Akizungumza na MTANZANIA jana kwa simu katika mahojiano maalumu, Dk. Slaa alisema kuwa kwa sasa anaishi kwa kazi ya mikono yake kwani ili aweze kuishi anahitaji kufanya kazi zaidi ya mbili hadi nne kwa siku.
“Niko, ninafuatilia matukio Mutukula (ziara ya Rais Dk. John Magufuli jana). Siku zote nimesema ninaishi kwa jasho na kazi ya mikono yangu. Canada ili uishi vizuri, unahitaji kazi zaidi ya mbili au tatu mpaka nne. Hayo nimeweka wazi, sijui jambo jipya kama mtu alikuwa hafuatilii.
“Mimi ninafanya kazi PWD/CDS/COSTCO kama Sales Advisor, baada ya kumaliza masomo yangu hasa Interpersonal Communication. Costco ninakofanya kazi ina members (wanachama) 10,000. Kwa siku wanaofika Warehouse ni kati ya 5,000 hadi 7,000,” alisema Dk. Slaa.
Mbali na hilo, alisema kuwa pia anafanya kazi nyingine ikiwa ni pamoja na ushauri (Consultancy).
Alisema kila mara amekuwa akiwataka Watanzania na vijana wafanye kazi kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mtandao wala propaganda.
“Canada ni kazi, Profesa wa Chuo Kikuu anafanya kazi ya Uber. Sijui kama Uber inafahamika Tanzania, ni dereva Taxi kwa kutumia gari lake binafsi. Ofisa wa Serikali usiku anaosha vyombo hotelini.
“Ndiyo maana familia ina magari mawili au zaidi, TV, nyumba ya kisasa, chakula cha kisasa. Wanatekeleza sera ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa matendo. Nadhani nimekupa taarifa za kutosha ikiwa ni pamoja na kujibu propaganda kuwa nilihongwa mabilioni.
“Niwahakikishie tena, wakati wa kusoma nilikuwa na scholarship, tangu nianze kazi ninaishi kwa jasho la mikono yangu. Mke wangu yeye ameingia Chuo Kikuu cha York baada ya Diploma yake na bado anapata scholarship.
“Ndiyo maana tuna uwezo wa kuwa na magari mawili aina ya Jeep na Dodge, ukifanya kazi utaishi vizuri. Hii ni pamoja na kugharamiwa bima ya afya (Health Insurance), watoto kusomeshwa na Serikali ya Canada,” alisema Dk. Slaa.
Mei mwaka huu, Dk. Slaa, alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu wakati huo, alisema pamoja na kumaliza masomo yake, anatafakari uamuzi wa kurudi nchini ama la.
Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.
Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.
“Sina tabia ya kuyumbishwaa, sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,” alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.
Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie, ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.
Chanzo: Mtanzania