Dk. Slaa aajiriwa supermarket

Dk. Slaa aajiriwa supermarket

Duh uache mshahara karibu M7,nyumba,gari na marupu rupu yakutosha hatari,nje sio kuzuri kama bongo hilu uishi lazima upige kazi aswa.
 
Waswahili tuna msemo wetu wa..'kazi ni kazi, ilimradi mkono uende kinywani'; yaani haitakiwi mtu kuchagua kazi, kikubwa kazi husika iwe halali na iwe inakulipa.

Kama kichwa habari kinavyosema kuwa, Dk. Wilbroad Slaa aliyewahi kuwa katibu mkuu wa CHADEMA amepewa ajira ya afisa mauzo wa supermarket huko Canada, je, hii tuite kupanda na kuangakuka kisiasa kwa Dk. Slaa?

Itakumbukwa pia, Dk. Slaa aliwahi kuwa Rais wa bodi ya hospitali ya CCBRT, ya jijini Dar Es Salaam.

=======

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, ameajiriwa katika duka kubwa la bidhaa za majumbani (Supermarket) la Costco lililopo Oakville, Toronto nchini Canada, imebainika.

Dk. Slaa, kwa sasa anaishi nchini Canada alikokwenda kwa masomo, tangu alipotangaza kuachana na siasa Septemba 1, mwaka 2105.

Kwa muda wa wiki kadhaa, ziliibuka taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa zamani wa Karatu, amemaliza masomo yake na sasa anafanya kazi katika moja ya maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali nchini humo – Supermarket.

Supermarket ya Costco anayofanya kazi Dk. Slaa akihudumu kama Mshauri wa Mauzo (Sales Advisor), akilipwa Dola za Marekani 10 (zaidi ya Sh 20,000) kwa saa, ina hadhi kama Nakumat, Shopers, Imalaseko, Game na maduka mengine makubwa nchini.

Akizungumza na MTANZANIA jana kwa simu katika mahojiano maalumu, Dk. Slaa alisema kuwa kwa sasa anaishi kwa kazi ya mikono yake kwani ili aweze kuishi anahitaji kufanya kazi zaidi ya mbili hadi nne kwa siku.

“Niko, ninafuatilia matukio Mutukula (ziara ya Rais Dk. John Magufuli jana). Siku zote nimesema ninaishi kwa jasho na kazi ya mikono yangu. Canada ili uishi vizuri, unahitaji kazi zaidi ya mbili au tatu mpaka nne. Hayo nimeweka wazi, sijui jambo jipya kama mtu alikuwa hafuatilii.

“Mimi ninafanya kazi PWD/CDS/COSTCO kama Sales Advisor, baada ya kumaliza masomo yangu hasa Interpersonal Communication. Costco ninakofanya kazi ina members (wanachama) 10,000. Kwa siku wanaofika Warehouse ni kati ya 5,000 hadi 7,000,” alisema Dk. Slaa.

Mbali na hilo, alisema kuwa pia anafanya kazi nyingine ikiwa ni pamoja na ushauri (Consultancy).

Alisema kila mara amekuwa akiwataka Watanzania na vijana wafanye kazi kwani fedha haziji kwa kukesha kwenye mtandao wala propaganda.

“Canada ni kazi, Profesa wa Chuo Kikuu anafanya kazi ya Uber. Sijui kama Uber inafahamika Tanzania, ni dereva Taxi kwa kutumia gari lake binafsi. Ofisa wa Serikali usiku anaosha vyombo hotelini.

“Ndiyo maana familia ina magari mawili au zaidi, TV, nyumba ya kisasa, chakula cha kisasa. Wanatekeleza sera ya ‘Hapa Kazi Tu’ kwa matendo. Nadhani nimekupa taarifa za kutosha ikiwa ni pamoja na kujibu propaganda kuwa nilihongwa mabilioni.

“Niwahakikishie tena, wakati wa kusoma nilikuwa na scholarship, tangu nianze kazi ninaishi kwa jasho la mikono yangu. Mke wangu yeye ameingia Chuo Kikuu cha York baada ya Diploma yake na bado anapata scholarship.

“Ndiyo maana tuna uwezo wa kuwa na magari mawili aina ya Jeep na Dodge, ukifanya kazi utaishi vizuri. Hii ni pamoja na kugharamiwa bima ya afya (Health Insurance), watoto kusomeshwa na Serikali ya Canada,” alisema Dk. Slaa.

Mei mwaka huu, Dk. Slaa, alisema hana mpango wa kurudi nchini kwa sasa na kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii hazina ukweli wowote.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu wakati huo, alisema pamoja na kumaliza masomo yake, anatafakari uamuzi wa kurudi nchini ama la.

Hata hivyo, Dk. Slaa ambaye alipata kuwa Mbunge wa Karatu kwa vipindi vitatu mfululizo, hakuweza kuainisha mazingira yaliyomfanya aondoke nchini na kwenda kuishi ughaibuni.

Septemba, 2015 wakati wa Uchaguzi Mkuu, Dk. Slaa alijiweka kando na siasa, kwa kile alichokieleza kutofautiana na viongozi wenzake ndani ya chama chake juu ya masharti ya kumpokea aliyekuwa mgombea urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa.

“Sina tabia ya kuyumbishwaa, sina chuki na mtu yeyote, sipendi siasa za udanganyifu na propaganda. Nimeachana na siasa tangu Julai 28, 2015, baada ya kuona misingi ya chama nilichoshiriki kukijenga imepotoshwa,” alisema Dk. Slaa siku alipotangaza kuachana na siasa.

Alisema sharti la kwanza ambalo alitaka Chadema izingatie, ni kiongozi huyo wa zamani ndani ya Serikali ya CCM, kujisafisha dhidi ya tuhuma ya kashfa ya sakata la Kampuni ya Kufua Umeme ya Richmond aliyohusishwa nayo akiwa Waziri Mkuu.

Chanzo: Mtanzania
Chadema si walisema amehongwa. Sasa imekuaje. Na walisema amepewa hela nyingi. Muda ni kipimo kizuri huumbua watu. Hata MZEE lowasa walimsema sana muda ukawa kipimo kizuri sana
 
Dr Slaa sio tapeli ni tofauti na hawa wengine ndio maana kapata ajira,hawa wengine ni matajiri bila hata kufanya biashara
 
Acha ale mafao yake....amepumzika kwa pesa ya kuuza utu wake....sasa pesa zimepungua lazima ale kwa jasho.....!! Mnafiki San huyo babu...acha tu ameuza utu wake kw pesa
Mkuu unajibebesha dhambi ya kutuhumu mambo mazito usiyoyajua. Usipende kutumia maneno makali kwa binadamu mwenzako kwa issue ambayo nina uhakika huijui vizuri. Fake ID haikuondoi kwenye hii dhambi. Bora utuhumu ukiweka akiba ya maneno maana siasa zetu zimebeba mengi mno.....acha kumtukana mzee wa watu ambaye kwa umri wake tu unastahili kuweka staha... chuki za kisiasa zisitupofushe ...
 
Kwa kila SAA 20000

Kwa siku 20000×24=480,000

Kwa mwezi 480,000×30=14,400,000

Sijajua tax and rant kwa huko Canada ikoje
Kwa hiyo anafanya kazi 24 hours? Yaani halali,hapumziki!!!!

Average Working hours ni 8 ingawa inaweza kuzidi kidogo.

Na pia kazi sio 30 days,kuna weekend,kuna jumapili n.k
 
Muonekano wa nje Supermarket anayofanyia kazi Dk. Slaa....

CostcoSM.png
 
Nafikir umeongea bila kufikir mkuu....kwa haraka haraka tu labda nikwambie km lisaa anakula dola 10 ambayo kwa kuaproximate ni km buku 25 kwa 24 hrs inakua ni laki 6 ambayo kwa mwez ni mil 18....na ukumbuke ulaya wengii wanafanya kazii chini ya masaa 12 ila apo nimepgia masaa 24....kwhyo km kwa mwez anakula mil 18 wapi watu wengi bongo wanao okota zaidi ya iyo milion 18 kwa mwez kama mshahara...fanya utaft vzr
Unafanyaje kazi masaa 24? Kwamba hulali,hupumziki???

Hizo calculations zako ni Uchwara.
 
Prof. Lipumba bado anaishi Buguruni ofisini?
 
Chadema si walisema amehongwa. Sasa imekuaje. Na walisema amepewa hela nyingi. Muda ni kipimo kizuri huumbua watu. Hata MZEE lowasa walimsema sana muda ukawa kipimo kizuri sana
aliambiwa kaingiziwa bilioni 2 kwenye akaunti kwenda kuchungulia kakuta milioni 2 hiyo ndio ccm
 
50bil ishakata? Angebaki hapa halafu akajenga kiwanda cha hizo bidhaa za majumbani si angefanya exportation mpaka huko Canada kwenye hiyo min supermarket? 50bil si haba hasa kwa MTU wa rika lile.
Maswali haya huwezi jibu, una uhakika gani alipewa bil50, je ameajiriwa supermarket au mini supermarket kama ulivyoandika.
 
Wabongo ni wanafiki sana na vijicho vitatupeleka kubaya. Mbona anaonekana kuwa na kazi nyingine na hamzisemi? Na mnataka akae kule afanyaje ama labda hamuelewi kule ziko kazi mpaka za ajabu hatari watu wanafanya na wanaishi? Mlioko hapa bongo ni bora mkae hapa make kule kwanza ni kazi, ni aina gani ya kazi mtabaki kufanya umbea huko fb
Hivi hata wewe leo usikie Kikwete anauza duka la spare parts pale Chicago mkuu hautashangaa? tuwe wawazi tuache unafiki.ingawa kazi ni kazi kweli.
 
Unafanyaje kazi masaa 24? Kwamba hulali,hupumziki???

Hizo calculations zako ni Uchwara.

soma vizuri mkuuu....nimeongea kbsa apo kua wengi wanafanya kaz chini ya masaa 12....apo nmepgia maximum range incase km labda kun ela ya chakula anapokea au la
 
Naona bawacha wanamshambulia Dr Slaa eti kaishiwa hivi mtu anayemiliki hizi ndinga
images
images

Unajilinganisha nae wakati wewe hata wheel cover mbovu ya swift huna?
acha uzushi wewe tuletee karatasi za umiliki au hata picha tu ya Dr.akiendesha moja ya hizi gari.
 
Back
Top Bottom