BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,148
Wameshaombwa mara nyingi na wasomi ndani na nje ya nchi wakutane nao uso kwa uso lakini huingia mitini au kujibu maswali kibabe na kudai muda hauwaruhusu wa kujibu maswali kwa muda mrefu.
Dk. Salim, Prof. Shivji wawaamsha wasomi
na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima
KATIBU Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Dk. Salim Ahmed Salim, amewataka wasomi kuwaita na kuwahoji viongozi wanaodaiwa kusaini mikataba yenye utata.
Amesema wasomi wana haki ya kuwauliza viongozi na kuwataka watoe maelezo kuhusu mikataba kama ule wa Richmond na Buzwagi inayodaiwa kusainiwa kinyume cha taratibu.
Dk. Salim alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu hoja za wasomi waliohudhuria maadhimisho ya kumkumbuka marehemu Kanyama Chiume (78), ambaye ni mmoja wa waasisi waliopigania kuundwa kwa Umoja wa Afrika, aliyefariki dunia mwezi uliopita, New York, Marekani.
" Waiteni, viongozi wa serikali muwahoji, ninyi mliopata fursa ya kusoma mna haki ya kuuliza pale panapokwenda kombo….waiteni muulize mambo ya Richmond, Buzwagi watoe maelezo, labda kuna vitu hamvijui.
"Haya mambo hayatokei ghafla tu, nchi za Afrika zina matatizo mengi, mengine tumeyarithi, haiwezekani leo hii wanafunzi msijihusishe na maendeleo na matatizo ya nchi," alisema Dk. Salim.
Alisema sambamba na kuwaita, wasomi wanayo nafasi ya kuitisha mjadala wa kitaifa utakaosaidia kuondoa hali ya shaka iliyopo sasa kuhusu kusainiwa kwa mikataba yote inayotiliwa shaka na makundi mbalimbali ya kijamii.
Dk. Salim, mmoja wa viongozi wanaoheshimika katika Bara la Afrika, pia aliwaonya wasomi kuwa macho na ajenda za wakubwa zinazotishia kusambaratisha mataifa ya Afrika, kwa sababu dunia ya sasa ni tofauti na dunia ya zamani, ambapo nchi za Afrika zilikuwa zikiweka agenda bila kuingiliwa na mataifa kutoka nje ya Bara la Afrika.
Alisema jeuri lililokuwa nayo Bara la Afrika zamani ilitokana na mataifa yanayounda bara hili kutokuwa tegemezi kwa mataifa makubwa.
"Zamani tulikuwa na ubavu, kwa sababu tulikuwa hatutegemei sana kutoka nje, lakini bado tuna uwezo kama bara letu tutalirejesha kuwa kama lililovyokuwa zamani," alisema.
Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji, aliwaeleza wasomi waliohudhuria kumbukumbu hiyo kuwa uzalendo wa kinchi katika siku za karibuni umeshindwa na kusambaratika kwa vile katika kipindi cha miaka 46 ya uhuru, maamuzi yanafanywa na watu kutoka nje, tofauti na zamani ambapo Watanzania walikuwa wakijiamulia mambo yao wenyewe.
"Uzalendo umesambaratika, msishangae uwanja wa ndege wametoa jina la Mwalimu, eti kwa sababu watalii wameshindwa kutamka jina la Mwalimu, nyaraka nyingi zinaandikwa kwa Kiingereza, lakini Azimio la Arusha liliandikwa kwa Kiswahili!" alisema kwa mshangao Prof. Shivji.
Aliwaonya vijana kuwa makini na mwenendo wa sasa wa uchumi wa ulimwengu ambao umebadili hali ya unyanyasaji kutoka ile ya kufanyishwa kazi kama watumwa hadi uporaji wa rasilimali zetu.
Mmoja wa wasomi waliotoa maoni yao katika kumbukumbu hiyo, alisema Tanzania imekuwa nchi ya mstari wa mbele kupigania uhuru wake na wa nchi nyingine barani Afrika, lakini sasa inaongoza kwa maovu, ufisadi, mikataba mibovu kama Richmond na Buzwagi.
Alisema viongozi wengi hapa nchini hawajali masilahi ya taifa wala kujadili mambo muhimu kama mabadiliko ya katiba, na badala yake wameweka kipaumbele katika kuangalia masilahi yao binafsi.
Kwamba hilo linathibitishwa na safari nyingi za nje zinazofanywa na viongozi wakuu wa taifa kwa madai ya kutafuta marafiki na wahisani kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya nchi yetu, kinyume chake marafiki hao wamekuwa mstari wa mbele katika kuvuna rasilimali zetu.
Akizungumza katika kumbukumbu hiyo, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, Absalom Kibanda, alionya kuhusu hatari ya nchi za Afrika kuendelea kuzalisha viongozi aina ya kina Kamuzu Banda, mtawala za zamani wa Malawi katika chaguzi.
Alisema hatari ya tatizo hili kutokea katika Afrika inagusa pia Tanzania kama yanavyoguswa mataifa mengine ya Afrika, na aliwataka Watanzania kujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na waasisi wa mataifa ya Afrika, wakiwamo kina Julius Nyerere, Kanyama Chiume na Kwame Nkrumah, ambao walihadaika na kudhani mtu kama Banda alikuwa mtetezi wa vuguvugu la Umoja wa Afrika, lakini kumbe alikuwa pandikizi la mataifa ya Magharibi.
Baadhi ya wanafunzi na watu mbalimbali waliozungumza katika kumbukumbu hiyo, waliwalaumu viongozi wa nchi za Afrika kwa kukumbatia udikteta na kuwafananisha na mtawala wa zamani wa Malawi, Kamuzu Banda, ambaye mawaziri wake walikuwa wakimpigia magoti kila wanapowasiliana naye au kujibu maswali aliyowauliza.
Kumbukumbu hiyo pia ilihudhuriwa na watoto wa Chiume, ambao walieleza kufarijika kwao na heshima aliyopewa baba yao na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa kuandaa kumbukumbu hiyo.
Watoto hao; Nathan, Jessie na Sonia Chiume, walimwelezea marehemu baba yao kuwa alikuwa mpigania uhuru hodari, aliyepigania kuundwa kwa umoja wa Afrika na mpinzani mkubwa wa ukabila na udikteta.
Marehemu Chiume, mzaliwa wa Malawi, enzi za uhai wake aliwahi kusoma nchini na baadaye katika harakati za kupigania uhuru nchini mwake, alilazimika kuishi uhamishoni hapa nchini tangu mwaka 1964 hadi 1994.