Dk. Salim, Prof. Shivji wawaamsha wasomi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Wameshaombwa mara nyingi na wasomi ndani na nje ya nchi wakutane nao uso kwa uso lakini huingia mitini au kujibu maswali kibabe na kudai muda hauwaruhusu wa kujibu maswali kwa muda mrefu.

Dk. Salim, Prof. Shivji wawaamsha wasomi

na Ratifa Baranyikwa
Tanzania Daima

KATIBU Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Dk. Salim Ahmed Salim, amewataka wasomi kuwaita na kuwahoji viongozi wanaodaiwa kusaini mikataba yenye utata.
Amesema wasomi wana haki ya kuwauliza viongozi na kuwataka watoe maelezo kuhusu mikataba kama ule wa Richmond na Buzwagi inayodaiwa kusainiwa kinyume cha taratibu.

Dk. Salim alitoa kauli hiyo jana wakati akijibu hoja za wasomi waliohudhuria maadhimisho ya kumkumbuka marehemu Kanyama Chiume (78), ambaye ni mmoja wa waasisi waliopigania kuundwa kwa Umoja wa Afrika, aliyefariki dunia mwezi uliopita, New York, Marekani.

" Waiteni, viongozi wa serikali muwahoji, ninyi mliopata fursa ya kusoma mna haki ya kuuliza pale panapokwenda kombo….waiteni muulize mambo ya Richmond, Buzwagi watoe maelezo, labda kuna vitu hamvijui.

"Haya mambo hayatokei ghafla tu, nchi za Afrika zina matatizo mengi, mengine tumeyarithi, haiwezekani leo hii wanafunzi msijihusishe na maendeleo na matatizo ya nchi," alisema Dk. Salim.

Alisema sambamba na kuwaita, wasomi wanayo nafasi ya kuitisha mjadala wa kitaifa utakaosaidia kuondoa hali ya shaka iliyopo sasa kuhusu kusainiwa kwa mikataba yote inayotiliwa shaka na makundi mbalimbali ya kijamii.

Dk. Salim, mmoja wa viongozi wanaoheshimika katika Bara la Afrika, pia aliwaonya wasomi kuwa macho na ajenda za wakubwa zinazotishia kusambaratisha mataifa ya Afrika, kwa sababu dunia ya sasa ni tofauti na dunia ya zamani, ambapo nchi za Afrika zilikuwa zikiweka agenda bila kuingiliwa na mataifa kutoka nje ya Bara la Afrika.

Alisema jeuri lililokuwa nayo Bara la Afrika zamani ilitokana na mataifa yanayounda bara hili kutokuwa tegemezi kwa mataifa makubwa.

"Zamani tulikuwa na ubavu, kwa sababu tulikuwa hatutegemei sana kutoka nje, lakini bado tuna uwezo kama bara letu tutalirejesha kuwa kama lililovyokuwa zamani," alisema.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji, aliwaeleza wasomi waliohudhuria kumbukumbu hiyo kuwa uzalendo wa kinchi katika siku za karibuni umeshindwa na kusambaratika kwa vile katika kipindi cha miaka 46 ya uhuru, maamuzi yanafanywa na watu kutoka nje, tofauti na zamani ambapo Watanzania walikuwa wakijiamulia mambo yao wenyewe.

"Uzalendo umesambaratika, msishangae uwanja wa ndege wametoa jina la Mwalimu, eti kwa sababu watalii wameshindwa kutamka jina la Mwalimu, nyaraka nyingi zinaandikwa kwa Kiingereza, lakini Azimio la Arusha liliandikwa kwa Kiswahili!" alisema kwa mshangao Prof. Shivji.

Aliwaonya vijana kuwa makini na mwenendo wa sasa wa uchumi wa ulimwengu ambao umebadili hali ya unyanyasaji kutoka ile ya kufanyishwa kazi kama watumwa hadi uporaji wa rasilimali zetu.

Mmoja wa wasomi waliotoa maoni yao katika kumbukumbu hiyo, alisema Tanzania imekuwa nchi ya mstari wa mbele kupigania uhuru wake na wa nchi nyingine barani Afrika, lakini sasa inaongoza kwa maovu, ufisadi, mikataba mibovu kama Richmond na Buzwagi.

Alisema viongozi wengi hapa nchini hawajali masilahi ya taifa wala kujadili mambo muhimu kama mabadiliko ya katiba, na badala yake wameweka kipaumbele katika kuangalia masilahi yao binafsi.

Kwamba hilo linathibitishwa na safari nyingi za nje zinazofanywa na viongozi wakuu wa taifa kwa madai ya kutafuta marafiki na wahisani kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya nchi yetu, kinyume chake marafiki hao wamekuwa mstari wa mbele katika kuvuna rasilimali zetu.

Akizungumza katika kumbukumbu hiyo, Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Free Media, Absalom Kibanda, alionya kuhusu hatari ya nchi za Afrika kuendelea kuzalisha viongozi aina ya kina Kamuzu Banda, mtawala za zamani wa Malawi katika chaguzi.

Alisema hatari ya tatizo hili kutokea katika Afrika inagusa pia Tanzania kama yanavyoguswa mataifa mengine ya Afrika, na aliwataka Watanzania kujifunza kutokana na makosa yaliyofanywa na waasisi wa mataifa ya Afrika, wakiwamo kina Julius Nyerere, Kanyama Chiume na Kwame Nkrumah, ambao walihadaika na kudhani mtu kama Banda alikuwa mtetezi wa vuguvugu la Umoja wa Afrika, lakini kumbe alikuwa pandikizi la mataifa ya Magharibi.

Baadhi ya wanafunzi na watu mbalimbali waliozungumza katika kumbukumbu hiyo, waliwalaumu viongozi wa nchi za Afrika kwa kukumbatia udikteta na kuwafananisha na mtawala wa zamani wa Malawi, Kamuzu Banda, ambaye mawaziri wake walikuwa wakimpigia magoti kila wanapowasiliana naye au kujibu maswali aliyowauliza.

Kumbukumbu hiyo pia ilihudhuriwa na watoto wa Chiume, ambao walieleza kufarijika kwao na heshima aliyopewa baba yao na wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa kuandaa kumbukumbu hiyo.

Watoto hao; Nathan, Jessie na Sonia Chiume, walimwelezea marehemu baba yao kuwa alikuwa mpigania uhuru hodari, aliyepigania kuundwa kwa umoja wa Afrika na mpinzani mkubwa wa ukabila na udikteta.

Marehemu Chiume, mzaliwa wa Malawi, enzi za uhai wake aliwahi kusoma nchini na baadaye katika harakati za kupigania uhuru nchini mwake, alilazimika kuishi uhamishoni hapa nchini tangu mwaka 1964 hadi 1994.

...................wasomi kuwaita na kuwahoji viongozi wanaodaiwa kusaini mikataba yenye utata.
Amesema wasomi wana haki ya kuwauliza viongozi na kuwataka watoe maelezo kuhusu mikataba kama ule wa Richmond na Buzwagi inayodaiwa kusainiwa kinyume cha taratibu.
....................................................................................................................................
" Waiteni, viongozi wa serikali muwahoji, ninyi mliopata fursa ya kusoma mna haki ya kuuliza pale panapokwenda kombo….waiteni muulize mambo ya Richmond, Buzwagi watoe maelezo, labda kuna vitu hamvijui.

"Haya mambo hayatokei ghafla tu, nchi za Afrika zina matatizo mengi, mengine tumeyarithi, haiwezekani leo hii wanafunzi msijihusishe na maendeleo na matatizo ya nchi," alisema Dk. Salim.

...................................................................................................................................................................................
Alisema jeuri lililokuwa nayo Bara la Afrika zamani ilitokana na mataifa yanayounda bara hili kutokuwa tegemezi kwa mataifa makubwa.

"Zamani tulikuwa na ubavu, kwa sababu tulikuwa hatutegemei sana kutoka nje, lakini bado tuna uwezo kama bara letu tutalirejesha kuwa kama lililovyokuwa zamani," alisema.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Issa Shivji, aliwaeleza wasomi waliohudhuria kumbukumbu hiyo kuwa uzalendo wa kinchi katika siku za karibuni umeshindwa na kusambaratika kwa vile katika kipindi cha miaka 46 ya uhuru, maamuzi yanafanywa na watu kutoka nje, tofauti na zamani ambapo Watanzania walikuwa wakijiamulia mambo yao wenyewe.

Viongozi wa serikali wanaposoma habari kama hizi wanatetema na kutaka kwenda kujisaidia kwani maneno hayo yanawaingia kama msumari.
 
je viongozi hao watakubali hiyo mialiko wakijua kwamba wanakwenda wekwa "kati"?

ni njia gani yaweza tumika kuwalazimisha viongozi kuitikia mialiko kama hiyo iliyotajwa na salim na shivji?
 
bado haitoshi, wasomi lazima wawe wa kwanza kukataa siyo tu kuhoji na kupewa majibu, bali wawe wa kwanza kukataa majibu ya kitoto na yasiyo na mantiki. Haitoshi kuhoji tu kuhusu Buzwagi, Richmond na vingine, ni lazima wasomi wetu waongoze katika kukataa hoja dhaifu, majibu yasiyo na maana na maelezo ya kitoto. HIvi ni wasomi wangapi wamekataa maelezo ya Khatibu kuhusu REDET?
 
Wewe si ndo mmoja wa hao wasomi? Umekubali/ umekataa maelezo ya Khatibu au unasubiri wasomi wengine watoe msimamo wao?
 
Wasomi wengi wameingia siasa na wengine kuondoka nchini. Na tuliobaki TZ wengi wetu tumekuwa waoga kuhoji kwa kuogopa "kushughulikiwa".
 
Wasomi wengi wameingia siasa na wengine kuondoka nchini. Na tuliobaki TZ wengi wetu tumekuwa waoga kuhoji kwa kuogopa "kushughulikiwa".

Kumbe na wewe ni msomi? Hofu yako ni hewa tu....hakuna atakayekushughulikia ukihoji na kukataa hoja za kitoto. Kuwa jasiri ndugu yangu.
 
bado haitoshi, wasomi lazima wawe wa kwanza kukataa siyo tu kuhoji na kupewa majibu, bali wawe wa kwanza kukataa majibu ya kitoto na yasiyo na mantiki. Haitoshi kuhoji tu kuhusu Buzwagi, Richmond na vingine, ni lazima wasomi wetu waongoze katika kukataa hoja dhaifu, majibu yasiyo na maana na maelezo ya kitoto. HIvi ni wasomi wangapi wamekataa maelezo ya Khatibu kuhusu REDET?

Wasomi wanafanya hivyo, na pale wanapopewa majibu yaliyojaa uongo au yasiyokuwa na kichwa wala miguu huyakataa majibu hayo, ndio maana Muungwana anaanza kuonyesha dalili za kuwakwepa Watanzania wanaoishi nje ambao asilimia kubwa ni wasomi na wana maswali mengi kuhusu mambo mbali mbali kuhusiana na maamuzi ya viongozi.
 
Ukweli ni kwamba wasomi wa Tz wameshindwa kupambana kwa hiyo wameamua kujiunga "nao", as the saying goes "if you can't fight them, join them!". Ushahidi ni msururu mrefu wa wasomi wanaomiminika na kukimbilia kwenye siasa, ambako ndiko kunakoonekana kuna "maisha bora". Wale wasomi waliobaki nje ya siasa wamebaki walalamishi tu wa chinichini, wasio na nguvu ya kuhamasisha uungwaji mkono wa hoja zao, na hata walalahoi wengine tukisikia malalamiko ya hawa wasomi tunaona ni kwa vile tu wako nje ya "karamu ya bwana", kwani wanapoalikwa humo wote huufyata, hadi tunajiuliza hivi zile hoja zao ziliishia wapi vile? Na ushahidi wa hili pia upo. Kwa hiyo wasomi wameshashindwa, tunahitaji suluhisho litoke kwa kundi lingine la wanamapinduzi ambao nguvu na ushawishi wao ni zaidi ya shahada za vyuo vikuu! Sijui Simon Bolivar na Ernesto che Guevara walikuwa na shahada ngapi za vyuo vikuu, lakini impact yao ipo hadi leo. Pengine tunahitaji watu wa aina hii leo.
 
Wewe si ndo mmoja wa hao wasomi? Umekubali/ umekataa maelezo ya Khatibu au unasubiri wasomi wengine watoe msimamo wao?

hapana miye si msomi. Mimi ni mwana fikara tu. Na kutokana na fikara zangu nakataa ninavyoona mimi na majibu ya Khatib yatapatiwa majibu jumatano. I'm all giddy here!
 
Aaaah we na wewe sasa myeyusho. Hebu nipe definisheni ya usomi maana siku zingine unakuwa una-act kaa msomi flani hivi halafu tukikuita msomi unakataa
 
Kithuku,
maneno yako kweli tupu hasa pale waswahili tunapokuwa na tafsiri zetu wenyewe...
Navyofahamu mimi ni kwamba kama tumeshindwa kuwahoji hawa viongozi wetu nje ya siasa itabidi sisi tuingie ktk siasa ili mapambano yawe ktk uwanja huru badala ya kukaa nje na kupiga makelele ambayo hayawazuii kulala lakini ktk maajabu ya firaun, wasomi wetu wanajiunga na CCM ambako juhudi zao zote huzimwa kama taa...

Kitu kimoja tu ambacho kimenichosha na mawazo ya hawa wazee wetu waliposema wasomi wana haki ya kuhoji hii mikataba kwani wao wapo fungu gani? kwa nini wao wasiwe mstari wa mbele kuongoza mapambano haya ama ndio wameshavua majukumu haya. Hivi kweli Salim na Shivji wakisimama na kuanzisha vagi kuna mtu ataweza kusimama kupinga hoja zao?....
 
Aaaah we na wewe sasa myeyusho. Hebu nipe definisheni ya usomi maana siku zingine unakuwa una-act kaa msomi flani hivi halafu tukikuita msomi unakataa

msomi ni mtu ambaye amebobea katika fani fulani au taaluma fulani na kubobea huko kunamfanya atambulike na wanataaluma wenzake na taasisi mbalimbali kuwa yeye ni gwiji.

Kwangu miye siye kila aliye na digrii moja au mbili anastahili kuitwa msomi. Na wale wenye udaktari na shahada nyingine ni wasomi pale tu wanapothibitika kuwa wamebobea katika taaluma au fani zao.

Sasa siamini mtu wa darasa la saba anaweza kuwa msomi kwa maana hiyo.
 
Mmhhh haya bana....ila wakati mwingine uwe unaacha kujifanya msomi...maana kila kitu we unajua...iwe sheria...sayansi....medicine....ngonjera....ngono....eeeehhhh....
 
Mmhhh haya bana....ila wakati mwingine uwe unaacha kujifanya msomi...maana kila kitu we unajua...iwe sheria...sayansi....medicine....ngonjera....ngono....eeeehhhh....

Kweli bana umenikumbusha, hivi ile mikasa ya Mwanakijiji na Dada Chiku huwa ya kweli au ni sehemu ya usanii? Na kama ni usanii tutaaminije kama mengine anayotuwekea hapa si mwendelezo wa huo usanii?
 
mzee kujua mambo mengi siyo sawa na usomi. Na kuna watu wengine wanajua mambo mengi kwa sababu ya udadisi na vipaji vyao tu. Sasa kama unajua hili na lile na wengine wanajua hili na jingine ndio maisha yalivyo. Sasa ndugu yangu ukiamua mawazoni mwako kuwa "mwanakijiji anajifanya msomi" mimi nitaweza vipi kukuzuia.Hakuna mahali hata pamojaambapo nimedai kuwa mimi ni msomi kwani kwenye jukwaa la wasomi mimi sistahili hata kupitisha ungo wa karanga!

Nyinyi wasomi mfanye mnayofanya na mnayopaswa kufanya sisi wengine ni wapiga domo tu...
 
KATIBU Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Dk. Salim Ahmed Salim, amewataka wasomi kuwaita na kuwahoji viongozi wanaodaiwa kusaini mikataba yenye utata. Amesema wasomi wana haki ya kuwauliza viongozi na kuwataka watoe maelezo kuhusu mikataba kama ule wa Richmond na Buzwagi inayodaiwa kusainiwa kinyume cha taratibu. " Waiteni, viongozi wa serikali muwahoji, ninyi mliopata fursa ya kusoma mna haki ya kuuliza pale panapokwenda kombo….waiteni muulize mambo ya Richmond, Buzwagi watoe maelezo, labda kuna vitu hamvijui.

Lovely!, huu sio ukinyonga mkuu anaishi nje ya nchi, the first opportunity ameweka mambo hadharani, saaafi sana,

However, the ishu hapa sio kuwasukumia wasomi kuwa ndio chanzo cha matatizo yetu bongo, ya bongo ni matatizo yetu wote wananchi wa Tanzania na yeye pia Salim, akiwa mmojawapo, lawama ni yetu wote tusianze kutafutana uchawi, mbele ya Mungu we are all guilty kwa sababu ni sisi wenyewe tunaowachagua viongozi wetu kuanzia upinzani na CCM, they are all responsible for this national misery of ours, na ni sisi wananchi ndio tunaowachagua, na Salim included, FULL STOP!

Yeye Salim, pia ni msomi sasa kwa nini asiwaulize alipokuwa kwenye kikao cha CCM, majuzi Dodoma?
 
msomi ni mtu ambaye amebobea katika fani fulani au taaluma fulani na kubobea huko kunamfanya atambulike na wanataaluma wenzake na taasisi mbalimbali kuwa yeye ni gwiji.

Kwangu miye siye kila aliye na digrii moja au mbili anastahili kuitwa msomi. Na wale wenye udaktari na shahada nyingine ni wasomi pale tu wanapothibitika kuwa wamebobea katika taaluma au fani zao.

Sasa siamini mtu wa darasa la saba anaweza kuwa msomi kwa maana hiyo.

Kwa maana nyembamba ya 'usomi' kama hii, ina maana hata hao waliobobea katika fani fulani ya taaluma, kama kwa mfano wa biochemistry, watakuwa sio wasomi panapozungumziwa mambo yanayohusu, kwa mfano mambo ya genetic engineering, au msomi aliyebobea katika uhasibu wa mambo ya mashirika ya kimataifa atakuwa sio msomi wakati mahesabu ya biashara za machinga zinapohusika! n.k.
 
Hivi kuna mtu dunia hii anayejiita yeye msomi? Maana hata hao wasomi wenyewe ukiwaita wasomi wanakataa katakata kuwa hawastahili kuwekwa kwenye jukwaa moja na wasomi. So I wonder who is msomi?
 
Back
Top Bottom