Mimi binafsi namuheshimu sana Mwakyembe, tatizo langu linakuja pale anapojisahau kwamba yupo kwenye CABINET-maswala mengine siya kuongea adhalani, unadhalilisha Baraza la Mawaziri na chama chako kwenye kadamunasi-wewe time yoyote unaweza kwenda kwa JK bila kipingamizi; kama una nia nzuri kwa nini usitenge muda wa kuonana na Jakaya in confidence ukumueleza duku duku lako, mbona namuonaga ni mtu msikivu sana. Msikilize atakujibu nini au ana maoni yepi au kama atatoa mapendekezo kwamba hili swala lifikishwe kwenya Baraza la Mawaziri au NEC hili lipatiwe ufumbuzi bila ya kukimbilia kwenye publicity STUNT.
Binafsi nimesikitishwa na kauri zako sijuhi ulikuwa unataka kutuma ujumbe gani kwa wananchi, lakini si Kikwete huyu huyu aliyekuteua kwenye nafasi ya Unaibu wa Waziri againist all ODDS - kama kweli angekuwa anavisikiliza vikundi vyenye nia ya kukigawa chama au kufitinisha watu-ebu tuwe wakweli kama angekuwa hana msimamo ungeteuliwa kweli kuwa naibu WAZIRI?
Kuhusu mambo ya VICOBA, mimi binafsi ni mmoja wa watu ambao hatukuwa comfortable na zoezi hilo; it never sank in my system to be frank - kweli walikuwa wana wasaidia wakina mama-lakini uki-play back kilichokuwa kinafanyika wakati wa kutoa misaada hiyo mtu mwenye akili za ku-analyse mambo unakuwa a bit concerned, maanake ilikuwa inageuzwa kama jukwaa la siasa especially kuzungumzia mambo ya ufisadi - kila raia nchi hii anachukia ufisadi, lakini watuhumiwa si wanashughulikiwa? Kulikuwa na faida gani ya kurudi rudia mambo hayo kila saa hasa hasa unapotoa misaada. Mbona mtu kama BAKHRESA anatoaga misaada chungu nzima kimya kimya, sijawahi kuona anaitisha wahandishi wa habari kutagazia dunia kwamba katoa hiki mara kile - tuwe wagarifu jamani, watu wenye long term plan wana njia nyingi za kufakinikisha malengo yao.
Mwisho niseme, ni kweli kuna baadhi ya watu/viongozi ni wazushi na wafitini au kuaribia sifa wenzao hasa wakiwaona ni tishio kwao; lakini mimi nina imani JK anaweza ku-deal na watu wa sampuli kama hiyo fasta, si mifano hipo-kama angekuwa ana-entertain vitu kama hivyo asingemteua Mwakyembe kwenye nafasi ya Unahibu wa Uwaziri. Niliyosema humu ni kwa nia ya kujenga si kwa nia mbaya, Nakutakia afya njema Mh.Mwakyembe (MB). ASANTENI.