Dk. Mwakyembe aitahadharisha CCM

hongera kwa posti nzuri,mwakyembe ni mkweli,na wanao sema mnafiki ni wale walikula unga wa ndele kwa bahasha za fisadi,ametimiza ahadi zake

mwakyembe ni mkweli? ngoja niangalie tena kwenye dictionary yangu maana ya neno "kweli".

bahasha ya fisadi - si mwakyembe tu bali sisi wa-tz wote ni victims wa hizi bahasha, one of the most prominent ikiwa ile iliyotolewa kwa mtu ambaye alitoa taarifa nusu ya richmond. taarifa nusu iliyofichwa iko kwenye bahasha obviously!
 
hapa hajaongelea sumu, anaongelea uhai wa chama katika mazingira ya makundi ndani ya mfumo wa vyama vingi. Na katika kuthibitisha kuwa anasema kweli tazama matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni!
wanamagamba ni vigeugeu sana!!!!!!!!.hamfai na kwa taarifa yenu wananchi hawana imani na nyie hivi jiulize wmenywe tutawaamini kwa lipi sasa,ccm mnaigizahamfai hata kidogo matapeli wakubwa nyie.mwakyembe ni kigeugeu haeleweki hata kidogo ....................ccm 2015 itakuwa ni historia kwa uso wa dunia hii.
 
Mkweli kwa kudai kuna baadhi ya mambo kwenye ripoti ya richmond aliyaficha?
Mkweli kwa kupingana na kauli zake mara anaongea jambo kuashiria kuna mikono ya watu flani juu ya tatizo la afya yake halafu hataki weka ukweli hadharani?
Huyu mnafiki tu kama magamba wengine yani gamba ni gamba tu kumbe.
Kama wewe waona mwakyembe ni mkweli labda mimi neno ukweli nalielewa vibaya litakuwa na maana tofauti nijuayo mimi

uzalendo wa kweli wa mtanzania hujionyesha katika mtazamo. Sidhani kama nyie mnaochangia hapa dhidi ya Dr. ni watanzania wa kweli. Inasikitisha kwamba leo hii kuna mtu mzima na ndevu zake nne, anadiriki kumkejeli Dr. Mwakyembe. Kweli nchi hii imetekwa na watu wanalio na ndoto ya kwamba Lowassa atakuwa rais 2015. Mtatumika sana kama condom.
 
Wape ukweli mkuu magamba wenzako, ila ungetoka huko ungekuwa uko juu sana!!!!! big up
 

Dk. Mwakyembe aliweka msimamo kuwa atakapoamua kupumzika ubunge atakayembadili atakuwa mtu mwenye viwango na kasi ile ile, mwenye sifa ya ubunge kwa kutokuwa muoga ambaye akifika bungeni atakuwa hajikombi kwa kubeba mabegi ya mawaziri kwani huo ndio mwanzo wa kudharauliwa.

“Ndugu zangu usipokuwa na msimamo kwenye siasa za kitaifa, watakudharau, mara unasema unajua wazee eeeeh twendeni tukapate supu watakuambia sawa,” alisema na kuongeza:

“Hapana tunataka mbunge makini anayemwambia waziri chukua begi lako tukutane jioni tuongelee masuala ya maendeleo ya Kyela, nao watakuheshimu kuwa huyu jamaa ana kamsimamo.”

Dk. Mwakyembe alisema miradi yote aliyoiahidi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2010 atahakikisha inatekelezwa ikiwemo ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kyela kwenda Matema.



CHANZO: NIPASHE

MMMM, hapa ana mbipu mzee mzima Mwakalinga ha ha ha ha
 
Ujumbe wa Dr. ni mzuri sana, nawashangaa wanaombeza. Tujikumbushe tu kwamba hata Yesu alibondwa mawe. Uzuri wa mtu hujulikana akifa?

Namtakia afya njema Dr. Mwakyembe na pia asaidie kumpata mbunge wa jimbo la Kyela mwenye masilahi na wanakyela na si vinginevyo.
 
Mnafiki mkubwa huyu, kila siku mafisadi, mafisadi si awataje sasa.
Sijui kwa nini ili polonium ilishindwa kumpeleka afterlife, ili tuondokana na kichefu chefu chake.
 
anyamaze...........ukurutu umeisha?

Hakyamungu!!!! Hivi nyie Chadema mnataka nini lakini?? mbona hata hoja za msingi hivi mnazipotezea? Yani ningekuwa na mamlaka ningekifutilia mbali hiki chama. CCM imewalea mpaka hapo mlipofika, sasa hivi mnajidai kusahau fadhila?? kweli ubinadamu kazi
 
Mwakyembe na Kiwira wapi na wapi, inaonyesha ni jinsi gani mamluki mlivyojazana humu kuchafua watu, subirini kushikishwa kuta na hao wafadhili wenu.

kama ni ukuta wataanza na magamba wote maana nanyi mmezidi kuomba omba pamoja na baba riz wenu.
 
Anasubiri nini pande hizo?
Anafurahia kuwa na gamba gumu kama la kobe?
 
it sound like the dead fears death! toka alivyo classify ile document ya richmond nikampotezea kabisa huyu mchizi.
 
Mimi binafsi namuheshimu sana Mwakyembe, tatizo langu linakuja pale anapojisahau kwamba yupo kwenye CABINET-maswala mengine siya kuongea adhalani, unadhalilisha Baraza la Mawaziri na chama chako kwenye kadamunasi-wewe time yoyote unaweza kwenda kwa JK bila kipingamizi; kama una nia nzuri kwa nini usitenge muda wa kuonana na Jakaya in confidence ukumueleza duku duku lako, mbona namuonaga ni mtu msikivu sana. Msikilize atakujibu nini au ana maoni yepi au kama atatoa mapendekezo kwamba hili swala lifikishwe kwenya Baraza la Mawaziri au NEC hili lipatiwe ufumbuzi bila ya kukimbilia kwenye publicity STUNT.

Binafsi nimesikitishwa na kauri zako sijuhi ulikuwa unataka kutuma ujumbe gani kwa wananchi, lakini si Kikwete huyu huyu aliyekuteua kwenye nafasi ya Unaibu wa Waziri againist all ODDS - kama kweli angekuwa anavisikiliza vikundi vyenye nia ya kukigawa chama au kufitinisha watu-ebu tuwe wakweli kama angekuwa hana msimamo ungeteuliwa kweli kuwa naibu WAZIRI?

Kuhusu mambo ya VICOBA, mimi binafsi ni mmoja wa watu ambao hatukuwa comfortable na zoezi hilo; it never sank in my system to be frank - kweli walikuwa wana wasaidia wakina mama-lakini uki-play back kilichokuwa kinafanyika wakati wa kutoa misaada hiyo mtu mwenye akili za ku-analyse mambo unakuwa a bit concerned, maanake ilikuwa inageuzwa kama jukwaa la siasa especially kuzungumzia mambo ya ufisadi - kila raia nchi hii anachukia ufisadi, lakini watuhumiwa si wanashughulikiwa? Kulikuwa na faida gani ya kurudi rudia mambo hayo kila saa hasa hasa unapotoa misaada. Mbona mtu kama BAKHRESA anatoaga misaada chungu nzima kimya kimya, sijawahi kuona anaitisha wahandishi wa habari kutagazia dunia kwamba katoa hiki mara kile - tuwe wagarifu jamani, watu wenye long term plan wana njia nyingi za kufakinikisha malengo yao.

Mwisho niseme, ni kweli kuna baadhi ya watu/viongozi ni wazushi na wafitini au kuaribia sifa wenzao hasa wakiwaona ni tishio kwao; lakini mimi nina imani JK anaweza ku-deal na watu wa sampuli kama hiyo fasta, si mifano hipo-kama angekuwa ana-entertain vitu kama hivyo asingemteua Mwakyembe kwenye nafasi ya Unahibu wa Uwaziri. Niliyosema humu ni kwa nia ya kujenga si kwa nia mbaya, Nakutakia afya njema Mh.Mwakyembe (MB). ASANTENI.
 
Mbunge wa Kyela (CCM), Dk.Harrison Mwakyembe, amekirushia kombora Chama cha Mapinduzi kwamba kama kitaendelea na mivutano ya ndani, kuna uwezekano mkubwa wa kubwagwaa katika chaguzi zijazo na vyama vya upinzani.

Alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na mamia ya wananchi wa mji wa Kyela uliofanyika katika viwanja vya John Mwakangale wakati wa ziara yake ya siku tatu baada ya kutokuwepo jimboni mwake kwa zaidi ya miezi saba kutokana na kuugua na kulazwa nchini India.“Chochoko ndani ya CCM haziishi, kuna watu utafikili wamechanjiwa kwa ajili ya chokochoko, Katibu sitanii tupo kwenye ushindani mkubwa wa kisiasa, vyama vya upinzani siyo vya kuchezewa tena vina nguvu kubwa, na CCM tukiendelea na hizi ngumi za ndani tutabwagwa,” alisema Dk. Mwakyembe huku akishangiliwa na wananchi.

Dk.Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alisema baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge aliingia na hamasa kubwa na kuwa mtu wa pili kitaifa kuanzisha vikundi vya ushirika Vicoba ambavyo viliibuka kwa kasi na kuwa na mtaji Sh. bilioni tatu benki.

Alisema baada ya mafanikio hao kupatikana siasa ikaingia na kuanza kupiga fitina hali iliyopelekea mfadhili aliyekuwa ameahidi kutoa Sh. milioni 100 kusitisha mpango huo baada ya kuandikiwa barua na baadhi ya viongozi ndani ya chama kwamba yeye (mfadhili) anaendesha upinzani ndani ya CCM.

Aliongeza kuwa baadaye ilibainika kuwa waliokuwa wakipiga vita Vicoba walikuwa ni mafisadi ambao wameiba fedha za chama na serikali hivyo wanataka wao ndio watawale kwa jeuri ya pesa zao na kutotaka wananchi wapate msaada kutoka kwa watu wengine.

Dk. Mwakyembe aliweka msimamo kuwa atakapoamua kupumzika ubunge atakayembadili atakuwa mtu mwenye viwango na kasi ile ile, mwenye sifa ya ubunge kwa kutokuwa muoga ambaye akifika bungeni atakuwa hajikombi kwa kubeba mabegi ya mawaziri kwani huo ndio mwanzo wa kudharauliwa.

“Ndugu zangu usipokuwa na msimamo kwenye siasa za kitaifa, watakudharau, mara unasema unajua wazee eeeeh twendeni tukapate supu watakuambia sawa,” alisema na kuongeza:

“Hapana tunataka mbunge makini anayemwambia waziri chukua begi lako tukutane jioni tuongelee masuala ya maendeleo ya Kyela, nao watakuheshimu kuwa huyu jamaa ana kamsimamo.”

Dk. Mwakyembe alisema miradi yote aliyoiahidi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2010 atahakikisha inatekelezwa ikiwemo ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kyela kwenda Matema.



CHANZO: NIPASHE

Duh!kumbe mwakyembe ndiyo mwasisisi wa vikoba?gud 2 know!Mwakyembe kuna ushauri ulishatolewa usipigane vita ambayo una uhakika wa kushinda.
 
Huyu naye mnafiki mwingine mtu wa kutafta umaarufu na public sympath, yeye na mwenzake Sitta hawana jipya kazi kuropoka.

Hebu fikiria Mwakyembe na kauli zake tata; Mara kuna mambo hakuyasema kwenye report ya richmond. Kwanini mpaka leo hajayasema? Kama si unafiki ni nini? Mara kalishwa sumu lakini hataki weka mambo wazi mwisho wa siku kaibuka tuaachie vyombo vya usalama vifanye kazi yake tusijadili afya yake wakati mwanzo alisema hana imani na polisi.

Huyu mropokaji tu anatafta umashuhuri mimi alishanichosha japo mwanzo nilikuwa namkubali.

Magamba wanavutana acha wazikane

unatumiwa na mafisadi kama wewe siyo fisadi
 
huyu mwakyembe ni kama choo cha kuku,ambacho kinakuwa na rangi mbili au tatu na zaidi.

yeye ni waziri wa serikali ya ccm,anaporopoka hayo maneno anamwambia nani wakati yeye yumo humo ndani,asituzingue aendelee na matibabu kwanza

Tatizo lenu nyie wafuasi wa mafisadi ni kwamba mnasoma juujuu tu, ebu kuwa mstaarabu katika mambo yanayo husu nchi yako. Mwakyembe alikuwa anakitahadharisha chama chake na sio kulopoka. Subirini mshikishwe kuta tu.
 
Jamaa wamechakachua pesa za wana Vicoba kwa kuwachangisha kila kikoba laki tatu na kwamba Mengi atawaongezea milioni 100. Mpaka leo hakuna kitu zaidi ya porojo za majukwaani.

Pesa za maskini zinaliwa na wenye nacho.
 
Back
Top Bottom