Dk. Mwakyembe aitahadharisha CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Mwakyembe aitahadharisha CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Apr 3, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa Kyela (CCM), Dk.Harrison Mwakyembe, amekirushia kombora Chama cha Mapinduzi kwamba kama kitaendelea na mivutano ya ndani, kuna uwezekano mkubwa wa kubwagwaa katika chaguzi zijazo na vyama vya upinzani.

  Alisema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na mamia ya wananchi wa mji wa Kyela uliofanyika katika viwanja vya John Mwakangale wakati wa ziara yake ya siku tatu baada ya kutokuwepo jimboni mwake kwa zaidi ya miezi saba kutokana na kuugua na kulazwa nchini India."Chochoko ndani ya CCM haziishi, kuna watu utafikili wamechanjiwa kwa ajili ya chokochoko, Katibu sitanii tupo kwenye ushindani mkubwa wa kisiasa, vyama vya upinzani siyo vya kuchezewa tena vina nguvu kubwa, na CCM tukiendelea na hizi ngumi za ndani tutabwagwa," alisema Dk. Mwakyembe huku akishangiliwa na wananchi.

  Dk.Mwakyembe ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, alisema baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge aliingia na hamasa kubwa na kuwa mtu wa pili kitaifa kuanzisha vikundi vya ushirika Vicoba ambavyo viliibuka kwa kasi na kuwa na mtaji Sh. bilioni tatu benki.

  Alisema baada ya mafanikio hao kupatikana siasa ikaingia na kuanza kupiga fitina hali iliyopelekea mfadhili aliyekuwa ameahidi kutoa Sh. milioni 100 kusitisha mpango huo baada ya kuandikiwa barua na baadhi ya viongozi ndani ya chama kwamba yeye (mfadhili) anaendesha upinzani ndani ya CCM.

  Aliongeza kuwa baadaye ilibainika kuwa waliokuwa wakipiga vita Vicoba walikuwa ni mafisadi ambao wameiba fedha za chama na serikali hivyo wanataka wao ndio watawale kwa jeuri ya pesa zao na kutotaka wananchi wapate msaada kutoka kwa watu wengine.

  Dk. Mwakyembe aliweka msimamo kuwa atakapoamua kupumzika ubunge atakayembadili atakuwa mtu mwenye viwango na kasi ile ile, mwenye sifa ya ubunge kwa kutokuwa muoga ambaye akifika bungeni atakuwa hajikombi kwa kubeba mabegi ya mawaziri kwani huo ndio mwanzo wa kudharauliwa.

  "Ndugu zangu usipokuwa na msimamo kwenye siasa za kitaifa, watakudharau, mara unasema unajua wazee eeeeh twendeni tukapate supu watakuambia sawa," alisema na kuongeza:

  "Hapana tunataka mbunge makini anayemwambia waziri chukua begi lako tukutane jioni tuongelee masuala ya maendeleo ya Kyela, nao watakuheshimu kuwa huyu jamaa ana kamsimamo."

  Dk. Mwakyembe alisema miradi yote aliyoiahidi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2010 atahakikisha inatekelezwa ikiwemo ujenzi wa barabara ya lami kutoka Kyela kwenda Matema.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  anyamaze...........ukurutu umeisha?
   
 3. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,457
  Trophy Points: 280
  Huyu naye mnafiki mwingine mtu wa kutafta umaarufu na public sympath, yeye na mwenzake Sitta hawana jipya kazi kuropoka.

  Hebu fikiria Mwakyembe na kauli zake tata; Mara kuna mambo hakuyasema kwenye report ya richmond. Kwanini mpaka leo hajayasema? Kama si unafiki ni nini? Mara kalishwa sumu lakini hataki weka mambo wazi mwisho wa siku kaibuka tuaachie vyombo vya usalama vifanye kazi yake tusijadili afya yake wakati mwanzo alisema hana imani na polisi.

  Huyu mropokaji tu anatafta umashuhuri mimi alishanichosha japo mwanzo nilikuwa namkubali.

  Magamba wanavutana acha wazikane
   
 4. J

  Juma Hamis Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hongera kwa posti nzuri,mwakyembe ni mkweli,na wanao sema mnafiki ni wale walikula unga wa ndele kwa bahasha za fisadi,ametimiza ahadi zake
   
 5. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hizi ndizo siasa za maji taka zisemwazo, siamini tena kile kinachozungumzwa na Dr. huyu toka awe mtu wa kujichangaya na kauli zake toka Richmond mpaka kwenye afya yake. Wadanganyika tushituke.
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Magamba bana!1 Wana rangi nyingi nyingi tu!!!
   
 7. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  Hata kama wewe umesema hivi,
  kumbe ni wengi tumemchoka huyo msomi kigeugeu.

   
 8. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,340
  Trophy Points: 280
  Nimefurahi sana jinsi wananchi wa Kiwira walivyo mpuuza huyu mnafiki Mwakyembe na kuipa CHADEMA udiwani wa Kiwira. Mwakyembe naye ni CCM tu kama CCM wengine hana jipya.
   
 9. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwacheni ubongo wake umeshakuwa affected na pollonium 310. Anahitaji counciling.
   
 10. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,457
  Trophy Points: 280
  Mkweli kwa kudai kuna baadhi ya mambo kwenye ripoti ya richmond aliyaficha?
  Mkweli kwa kupingana na kauli zake mara anaongea jambo kuashiria kuna mikono ya watu flani juu ya tatizo la afya yake halafu hataki weka ukweli hadharani?
  Huyu mnafiki tu kama magamba wengine yani gamba ni gamba tu kumbe.
  Kama wewe waona mwakyembe ni mkweli labda mimi neno ukweli nalielewa vibaya litakuwa na maana tofauti nijuayo mimi
   
 11. N

  Nsesi JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 374
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe na Kiwira wapi na wapi, inaonyesha ni jinsi gani mamluki mlivyojazana humu kuchafua watu, subirini kushikishwa kuta na hao wafadhili wenu.
   
 12. Omonto wa-hene

  Omonto wa-hene Senior Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Shame onto you CCM adherants!!!
   
 13. PENDING'ULA

  PENDING'ULA JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 269
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa hajaongelea sumu, anaongelea uhai wa chama katika mazingira ya makundi ndani ya mfumo wa vyama vingi. Na katika kuthibitisha kuwa anasema kweli tazama matokeo ya chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni!
   
 14. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 330
  Trophy Points: 180
  "Mwakyembe ni mjinga na mpumbavu",
  ELIAH KAMWELA anaweza kuripoti hivyo kwa uhakika!
  Hii ni ukizingatia tangu role yake kwenye rich monduli kwa kuficha ukweli,madai yao na 6 juu ya sumu,na baada ya muda mfupi kuyakana wenyewe!
  Shame on you,MWAKYEMBE!
   
 15. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mwakyembeeeeeeeeeeeee!!!!! unataka mafisadi wapigwe chini achukuliwe sitta? ufisadi=unafiki..... what is the difference?
   
 16. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,457
  Trophy Points: 280
  Nmeongelea hayo kufanya reference juu ya unafiki wake kama mwenzake sitta. Hayo angeyasema kabla ya kupigwa kura na kama kweli yeye ni bora basi ajitoe ccm
   
 17. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #17
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mwakyembe mnafiki sana!kumbuka tulivyo mfanyia maombiachaneni nae akafie mbele ya safh
   
 18. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #18
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ukurutu wa akili ugonjwa mbaya sana
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,530
  Likes Received: 10,442
  Trophy Points: 280
  ajitahadharishe yeye mwenyewe maana walitaka afe hajafa...kuihangaikia ccm ni kuhangaikia kifo chake.
   
 20. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #20
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  huyu mwakyembe ni kama choo cha kuku,ambacho kinakuwa na rangi mbili au tatu na zaidi.

  yeye ni waziri wa serikali ya ccm,anaporopoka hayo maneno anamwambia nani wakati yeye yumo humo ndani,asituzingue aendelee na matibabu kwanza
   
Loading...