Dk Kitima aitabiria mabaya CCM mbele ya Wassira

Dk Kitima aitabiria mabaya CCM mbele ya Wassira

Ccm ni chama pendwa hapa tanzania...kitaongoza nchi hadi miaka mingi ijayo
 
Kitima na watembea na sumu wenzake wapanga ugaidi watakufa wao huku ccm ikiendelea kuwaletea wananchi maendeleo
 
Ccm ni chama cha watanzania wanyonge na maskini na lengo lake ni kuwakomboa na umaskini
 
Huyo kitima hajielewi na anaropoka bila kupanga maneno tatizo anaongoza chuo cha vilaza

"kidumu chama tawala"
 
Kiwiliwili kinapokosa mawasiliano na kichwa kinakuwaje!
?kuwa na akili ya kiwendawazimu si lazima kuokota makopo! Matendo
Kitima na watembea na sumu wenzake wapanga ugaidi watakufa wao huku ccm ikiendelea kuwaletea wananchi maendeleo
 
Humu kuna maamuma wengi kweili ...!!! hivi kushabikia mafisadi ndio ujanja eh! Kwa nini mzarau maneno ya KITIMA...?
 
Ni dunia ipi anayizungumzia kitima ambayo hakuna wawekezaji au anatokwa povu la kijinga tu
 
Kiwiliwili kinapokosa mawasiliano na kichwa kinakuwaje!
?kuwa na akili ya kiwendawazimu si lazima kuokota makopo! Matendo

dawa imekuingia, tulia isambae vzr mwilini...una sumu hapo mfukoni?
 
Ndg yangu fisadi ni fisadi tu wanawalipa hela ili kuwatetea waovu wa ccm
Humu kuna maamuma wengi kweili ...!!! hivi kushabikia mafisadi ndio ujanja eh! Kwa nini mzarau maneno ya KITIMA...?
 
Msomi anapotumia kigezo cha uwekezaji kujitafutia cheap popularity anatia aibu mbele za jamii
 
Umeshaoga kweli wewe na kupiga mswaki? Naona bado unaota yale madude uliyopewa usiku!
Msomi anapotumia kigezo cha uwekezaji kujitafutia cheap popularity anatia aibu mbele za jamii
 
Naomba kuingilia kati mjadala huu kwa sababu naona, kwa kiasi fulani, unanihusu. Na nataka niweke maelezo ya upande wangu ili angalau kumbu kumbu ziwe sawa. Mwanzoni mwa mwaka jana nikiwa Mwanza kwa ajili ya kesi ya uchaguzi yabMbunge wa Ilemela, Mh. Highness Kiwia, Nilialikwa na jumuiya ya wanafunzi wa SAUT Mwanza kutoa mhadhara wa wazi kuhusu masuala ya kikatiba na ya kisiasa ya nchi yetu. Niliwauliza vijana hao Kama mamlaka ya Chuo chao imeridhia mwaliko huo na wakanihakikishia kwamba VC Kitima mwenyewe alikuwa nyuma ya mwaliko huo. Jioni ya siku hiyo hiyo VC Kitima mwenyewe alinialika chuoni kwa ajili ya chakula cha jioni. Nilikwenda na tulikula nae chakula cha jioni pamoja na watu wengine akiwemo Mkuu wa Kitivo cha Sheria Esterlatus (kama sikosei) Kilangi. Tukiwa tunakula, Dr. Kitima alimwelekeza Kilangi kuhakikisha wanaandaa ukumbi mkubwa wa mihadhara hapo chuoni kesho yake kwa sababu kulikuwa na matazamio ya mahudhurio makubwa kwenye mhadhara huo. Siku iliyofuata, yaani siku ya mhadhara wenyewe, nikiwa naelekea chuoni (in fact nilikuwa getini) nilipigiwa simu na Dean Kilangi na kuambiwa kwamba mamlaka ya Chuo, yaani VC Kitima, alikuwa ame-cancel hiyo public lecture. Kwa vile nilikwishafika chuoni, nilikwenda kumwona Dean Kilangi ili anipatie maelezo ya mabadiliko hayo ya ghafla. Dean Kilangi alinieleza kwamba walielekezwa na Usalama wa Taifa kwamba siwezi kutoa mhadhara bila kuwepo upande wa pili, yaani maCCM! Na kwa vile hakukuwa na uwezekano wa kupata liCCM lolote kwa muda mfupi kama huo, waliona ni busara wasitishe mhadhara huo! Nilijaribu kuongea na VC Kitima mwenyewe. Yeye aliniambia some bishop was uneasy about mhadhara wangu na reaction ya watawala juu ya nitakayosema hapo chuoni! Of course, wanafunzi wengi waliokuwa wamekuja kunisikiliza walikuwa disappointed sana na wakanilazimisha kwenda kuzungumza nao nje ya ofisi yao ya CHADEMA nje kidogo ya Chuo. Nilifanya hivyo na nakumbuka nilisema, among many other things, kwamba vyuo vikuu vya Tanzania vilikuwa hatarini kugeuzwa kuwa VETA kwa sababu ya hofu ya watawala wa vyuo hivyo kuwaudhi watawala wenzao wa nchi kwa kukaribisha mawazo tofauti vyuoni. A university that proscribes certain ideas and criminalizes free debate on the major issues of the day facing the nation forfeits its right to call itself a university! Kwa hiyo kilichosababisha ninyimwe fursa ya kuhutubia jumuiya ya SAUT Mwanza sio habari ya kutofanya lolote jimboni kwangu, itself a major talking point! Ni hofu ya Dr. Kitima na wasomi wenzake juu ya msimamo wangu wa kisiasa. Kwa ushahidi zaidi, mwezi Machi huu huu nilialikwa na Chama cha Wanafunzi wa Uchumi chuoni kwenda kushiriki kwenye mjadala wa wazi juu ya masuala yanayohusu uchimbaji gesi Tanzania. Kwa bahati nzuri au mbaya sikuweza kuonana na Dr. Kitima au Dean Kilangi, au pengine hawakuwepo, vinginevyo ningefukuzwa kwenye mjadala huo kwa sababu sijafanya chochote jimboni kwangu! One final point: kuna watu wengi wanaongea kwa ukali sana juu ya matendo maovu ya watawala huku wakishirikiana na hao hao wanaowasema. Ni vema kuchukua tahadhari: not everyone who roars is a lion!!!!

Tundu














Kuna kitu bado sijaelewa hapo kuhusu Tundu Lissu na Upinzani.

Huenda mleta mada katuchanganya au Dr.Kitima kapotoka!!

Kusema kuwa Dr.Kitima alimkataza Tundu Lissu asifanye Mhadhara hapo chuoni kisa hajafanya maendeleo jimboni kwake, hicho ni kichekesho kikubwa kwa sababu:

1/Anadai hiyo ilikuwa mwaka juzi(2011) na Tundu Lissu ameingia bungeni mwishoni mwa 2010, alitegemea maendeleo gani kwa muda huo kutoka kwa mbunge mpya tena kutoka upinzani?

2/Je, ni sera ya chuo chake kumwita mwanasiasa kama mbunge ili kutoa muhadhara SAUT kwa kigezo cha maendeleo aliyoleta jimboni mwake?

3/Je, hao wanasiasa wabunge wa CCM wamefanya nini kikubwa cha maendeleo majimboni mwao mpaka wapewe nafasi?

4/Paul Makonda sio mbunge wala kiongozi wa nchi bali ni kada wa CCM, naye siku chache zilizopita alikuja SAUT akiwa na Samweli Sitta nk na kupewa nafasi ya kuongea, ni maendeleo yapi amefanya katika nchi yetu mpaka apewe nafasi hiyo?
 
Atakufa yy na watembea na sumu wenzake wanaomdanganya akiiacha ccm ikiwatumikia watanzania
 
Back
Top Bottom