Siamini kama Dr. Kitima aliyasema hayo kuhusu Tundu Lissu. kama kweli kasema hayo, nadhani amepotoka kwani atakuwa amezungumza kama mwanakijiji wa kawaida. Dr. Kitima asome katiba ya nchi ambayo imeainisha kazi za mbunge na kwa uchache ni kutunga sheria, kuisimamia serikali na kuiwajibisha. Sidhani katika hizo kazi za mbunge kama kuna eneo ambalo Tundu aliwahi kuwa mzembe hata mara moja.
Dr. Kitima aainishe ni aina gani ya maendeleo na kwamba Tundu Lissu angewaletea watu wa Singida kwa namna gani? Inawezekana kwa namna moja au nyingine anaweza akawa na kasoro lakini kwa vinawango vya kumrejea kama mbunge ambaye hafanyi chochote basi Dr. ktima analo lake jambo. Ufanisi wa mtu katika kutekeleza majukumu yake hupimwa kwa malengo yaliyowekwa kuendana na majukumu yake, hapo Dr. Kitiama alikuwa anarejea nini anaposema kuwa Mh. Tundu Lissu ameshindwa?
Dr. Kitima nakuambia kuwa ukigombea ubunge huko Singida huwezi kufikia hata 5% ya kazi alizofanya Tundu Lissu. Kama amemkosoa, tunakubali lakini sikubaliani na hoja za ukosoaji. Nakumbuka siku moja Tundu Lissu aliibana serikali bungeni siku moja, akiikosoa Halmashauri moja huko Singida kurejesha wizarani fedha za maendeleo ya elimu huku wananchi wakichangisha fedha kwa ajili ya maendeleo ya elimu. Nilivyoona Tundu Lissu alikuwa sahihi kwa sababu huwezi kufanya mchezo wa kitoto namna hiyo.