Dk Kitima aitabiria mabaya CCM mbele ya Wassira

Dk Kitima aitabiria mabaya CCM mbele ya Wassira

CCM ina wenyewe wewe , ukiona tunajaa kwenye kwenye mikutano ya cdm ujuwe tunaenda kusikiliza santuri za uongo na matusi na cyo mnajidanganya kuwa tunayataka mnayaongea hapo.upinzani tukitaka utakufa wenyewe kwanza kabla ya ccm maana ccm ndio iliyozaa huo ipinzani na.inaendelea kuulea itakavyo.
Huna jipya wewe,ccm ina wenyewe kwenye kuiba.Mnakwenda kwenye mikutano ya CDM kuchukua sera,mfano mchakato wa katiba mpya ni wazo la CDM,nyie kazi yenu ni kukopi na kupaste.Mtakufa bila kujua,kaeni mkijifariji na liccm lenu
 
Ni dunia ipi anayizungumzia kitima ambayo hakuna wawekezaji au anatokwa povu la kijinga tu

dawa imekuingia, tulia isambae vzr mwilini...una sumu hapo mfukoni?

pole sana dada angu, endelea kulalamika hapo kwa dawa hii unayopata

Tanzania haitakaa iongozwe na walisha watu sumu..katu!

Msomi anapotumia kigezo cha uwekezaji kujitafutia cheap popularity anatia aibu mbele za jamii

Mkuu jitambue pangilia comments zako sio kupost ili kujaza ukurasa kama huwezi kuwa msomaji kama wengine unaharibu jukwaa, kwanza hoja zako ni hafifu unapaswa uwepo kwenye jukwaa la jokes na MMU ndio kunako kufaa
 
Maswaswa unatutafutia BAN asubuh.... Yaan unapost kila baada ya sek 20, halaf ujinga tu. Jibu hoja ni kwa namna gani hamtakufa
 
Makamu mkuu wa chuo cha mtakatifu Augustino SAUT,tawi la Mwanza,dk Charles Kitima amesema kutokana na mambo ya hovyohovyo yanayofanywa na serikali dhaifu ya CCM ni lazima itaondoka madarakani 2015 hata kama wataandaa mbinu zote za kuiba kura. Huku akishangiliwa kwa nguvu na wanachuo, Kitima anasema serikali haiwezi kudumu wakati wananchi wamepigika.

Wabunge wake wakipitisha bujeti mbovu na isiyo na maslahi,pia dk Kitima alianza kwa kuuponda upinzani wa Tz huku akimtaja mnadhimu wa kambi rasmi ya upinzani na mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu kwa kudai hajafanya jambo lolote jimboni mwake,na akitoboa siri kwamba hyo ndo sababu kubwa iliyomfanya asimruhusu kipindi flani asitoe mhadhara.

Itakumbukwa kuwa mwaka juzi Tundu Lissu alizuiwa asitoe mhadhara chuoni hapa kwa madai amepigiwa simu na usalama wataifa wakimtaka asimruhusu Tundu kutoa mada.,dk Kitima yupo mda huu anazungumza kama mchangiaji wa mada ya'AMANI NA MAENDELEO YA TANZANIA,'ambapo mgeni rasmi ni waziri wa mahusiano ndugu Steveni Wassira ,na mgeni mwalikwa mbunge wa Talime Nyambali Nyagwine.

Katika uwasilishwaji wa mada hii unaofanyika chuoni hapa,Wassira alianza kwa kutamba kwamba serikali kwa mda wa miaka yote 50 tangu uhuru imefanikiwa kudumisha Amani na Utulivu nchini,huku akisema kitu ambacho wapinzani hawawezi.

Nae mbunge Nyangwine amewataka wapinzani kuacha kulalamika kwani wanaweza kuliambukiza taifa na kuwa taifa la walalamikaji,huu ni mfululizo mwingne wa viongozi wa CCM na serikali kukitembelea chuo hiki ambacho ni maarufu kwa siasa za CHADEMA.

Wassira amekuja akitanguliwa na mawaziri wengne kama profesa Muhongo,Nyalandu na Sitta na wote wamekuwa wakipewa ukumbi ndani ya chuo na kuongea mambo tofauti na mada husika,wakijikita ,kinyume na ibara ya 53 na 54 za sheria ya vyuo vikuu inayokataza siasa vyuoni.

Niwapi Taarifa hii Imemtaja Tundu Lisu
[TABLE="class: MsoNormalTable, width: 759"]
[TR]
[TD] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"] CCM inakufa
• Wasira adai uzalendo umepungua Na Sitta Tumma, Mwanza.

na Sitta Tumma, Mwanza
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"] [TABLE="class: MsoNormalTable, width: 449"]
[TR]
[TD="bgcolor: transparent"] MAKAMU Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustine (SAUT) kilichoko mkoani Mwanza, Dk. Charles Kitima, ameitaka serikali ya CCM ijiandae kuondoka madarakani kwa aibu hata ikiiba kura.
Dk. Kitima alitoa kauli hiyo jana mkoani hapa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Masatu Wasira, ambapo alisema CCM imeonyesha idhaifu mkubwa katika kusimamia baadhi ya mambo.
Wasira na Dk. Kitima walikuwa kwenye mjadala wa Dira ya Maendeleo ya Serikali, uliofanyika mbele ya wanafunzi wa chuo hicho cha SAUT Nyegezi, jijini Mwanza.
Dk. Kitima alisema licha ya Wasira kutokuwa fisadi na ni mwanafunzi mzuri wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alimtaka awaambie wenzake wajiandae kuondoka kwa aibu.
“Mfano mzuri, Singapore wao walianza kusimamia utalii, lakini serikali yetu ilikosea sana kutokutekeleza mambo ya uzalishaji. Na msipotekeleza hili, CCM mtaondoka madarakani.
“Ulaji mkubwa wa fedha umeingia sekta ya elimu, hamtekelezi kwa vitendo sera na dira za taifa. Nasema msipobadilika serikali ya CCM itaondoka na hata mkiiba kura, lazima mtaondoka tu, tunawaandalia wapinzani,” alisema Dk. Kitima kisha ukumbi mzima ukamshangilia kwa nguvu.
Dk. Kitima ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisema Rais Jakaya Kikwete anao mawaziri watatu tu ambao wana mrengo chanya wa kuikomboa nchi.
Alibainisha kuwa kitendo cha serikali kuruhusu wawekezaji kuingia nchini na kudharau wazawa na mali zao hilo litakiangusha chama tawala.
Alisema kwa sasa katika vikao vya Bunge, hoja za msingi zinapingwa huku mtoa hoja akizomewa, lakini mambo ya kipuuzi ndiyo yanayoshabikiwa na wabunge wengi.
Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Masatu Wasira, amewashukia watumishi wote wanaojihusisha na ubadhirifu wa mali za nchi na kusema lazima watu hao wahenyeshwe kwa kuchukuliwa hatua bila kuonewa aibu.
Wasira ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, alianza kwa kusema: “Mimi nachukizwa sana na wanaoiba mali za nchi. Sipendi wizi na siwezi kuiba wala simung’unyi maneno kusema hili.”
Alisema wapo baadhi ya watumishi wanapoingia kwenye ajira kazi yao ni kuanza kuiba badala ya kujenga taifa, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya nchi, na kwamba fedha za EPA zilizorudishwa na wezi na zimetumika kuinua kilimo.
Waziri Wasira alisema kupungua kwa uadilifu hapa nchini ni tatizo kubwa, na linaweza kuleta mgogoro mkubwa na kudidimiza zaidi uchumi wa nchi, hivyo lazima kila Mtanzania awe muumini mzuri wa uzalendo.
“Rasilimali zote za nchi lazima zitumike kuwanufaisha Watanzania wote. Na bila hivyo hakuna nchi.
“Kupungua kwa uzalendo na uadilifu ni tatizo kubwa sana kwa nchi. Lazima tuenzi amani na upendo...ukishindwa kulinda na kuiheshimu Tanzania wakati na wewe ni Mtanzania hufai,” alisema Wasira.
Alisema rasilimali zote yakiwemo madini, maziwa, utalii na nyinginezo nyingi ni vema zikageuzwa kuwa mali zinazonufaisha na kuleta maendeleo kwa wananchi na kwamba dira ya maendeleo ya taifa ni kuboresha fursa nyingi za kiuchumi.
Alisema ili kufikia malengo halisi, mpango wa serikali uliopo sasa ni kuboresha huduma za viwanda, reli, viwanja vya ndege, kilimo bora, bandari, maliasili, miundombinu na nishati.
Kuhusu udini, Wasira alisema wamemeishi miaka 50 kwa amani, upendo na utulivu lakini sasa kuna chokochoko za baadhi ya watu ambao hawataki kuiona nchi ikitulia.
Aliwataka wasomi, waandishi wa habari, wanasiasa, viongozi na waumini wa dini zote na makundi ya kijamii, kuhakikisha wanapigania kuendelea kumea zaidi uharibifu wa amani ya nchi, maana lazima kila Mtanzania aihurumie nchi.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
CCM ina wenyewe wewe , ukiona tunajaa kwenye kwenye mikutano ya cdm ujuwe tunaenda kusikiliza santuri za uongo na matusi na cyo mnajidanganya kuwa tunayataka mnayaongea hapo.upinzani tukitaka utakufa wenyewe kwanza kabla ya ccm maana ccm ndio iliyozaa huo ipinzani na.inaendelea kuulea itakavyo.

Ni kweli Upinzani umetokana na CCM ..... ajabu mwenzetu unaamini eti kwenye mikutano ya CDM wanaCCM hua manaenda kusikiliza matusi ... sioni busara uliotumia kutufikishia uongo huu... wanaCCM mnajaa kusikiliza matusi?
 
Huyu kitima amestaafu na leo ndio anaagwa, aende zake mtaani akachili huko ameshindwa kazi ya kuongoza taasisi nyeti ya elimu matokeo yake amekuwa mhubiri wa chadema amemuweka mungu pembeni
 
Mkuu jitambue pangilia comments zako sio kupost ili kujaza ukurasa kama huwezi kuwa msomaji kama wengine unaharibu jukwaa, kwanza hoja zako ni hafifu unapaswa uwepo kwenye jukwaa la jokes na MMU ndio kunako kufaa

mda wa kula huu umeshatumika vya kutosha..mia mbili per post zimekutosha kwa leo...lazima uone hizi comment ni chungu kwa sababu zinasema ukweli
 
Ktk habari itv jana kuna shule ya msingi kule muheza inawanafunzi 300 lakini waalimu wawili kwa miaka kumi sasa
 
Dr Kitima ni namba nyingine, hapendi kuzunguka kama watanzania tulivyozoea yeye ni mtu wa fact na hawezi kujipendekeza kwa mtu! Mh Wassira alijikuta anaanzisha propaganda za next time.......sasa mimi najiuliza CCM wamekuwa wapi mpaka aseme next time Serikali ya CCM itakuwa kali sana.....Aagh! CCM mi hata nilishashindwa kuwaelewa kabisa. Mh Nyambari anapoongelea wapinzani kuwa walalamishi alikuwa anamsema bosi wake au alimaanisha nini? Mwenyekiti wa chama chake ndo kiongozi wa ulalamishi hapa Tanzania, mheshiwa Nyambari anausingizia upinzania. Na CCM wasiposhtuka toka huu usingizi wa pono wanaolala basi 2015 hata kama wataiba kura kweli hawatapata kitu.
 
Kitima na watembea na sumu wenzake wapanga ugaidi watakufa wao huku ccm ikiendelea kuwaletea wananchi maendeleo

Wanaokufa kwa Ugaidi Tz ni Wakristo wanaoingia makanisani siyo wewe. Hakuma ugaidi wa maandamanoni pengine ndio linalopangwa na "wasanii"..... manake hawachoki kuja na toleo jipya la usalama
 
Bavicha ni janga la Taifa.

Hata mpangilio wa uandishi ni kizungumkuti achilia mbali kujenga hoja kimantiki.

Hiki ulichokiandika ndiyo nini?. Pay attention kwanza kwenye elimu ili uelimike.
Kitu gani ambacho wewe hujakielewa kwenye hii post????
Nini Mantik ya kuchangia Post ambayo hujaielewa???
Hii inadhihirisha how Zero Brain are Vijana wa Lumumba...
 
Definition ya bavicha inapatikana kwenye mantiki iliyoko kwenye hilo bandiko hapo juu. Utakacho kipata kwenye hilo bandiko ndiyo bavicha UNLESS na wewe ni bavicha kwa maana kuwa, hutaelewa mantiki iliyotumika katika bandiko hilo.

Ww unalipwa buku saba kudefend lichama lililooza tena umesoma kwa kodi za wtz huku ukiendelea kuwasaliti ole wenu siku mkitokea live mikononi mwa wtz tutawanyonyoa.shame on you.
 
Kasema kweli. Sasa kwa ujinga wa viongozi wa CCM badala ya kuuona ukweli utawasikia wakisema huyo ni CHADEMA na kuwa anaongoza chuo cha wakristo na hivyo wakristo wote ni CHADEMA. Subirini Nape atakapofungua mdomo na mahubiri yake ya ukabila na udini!
 
Kuna kitu bado sijaelewa hapo kuhusu Tundu Lissu na Upinzani.

Huenda mleta mada katuchanganya au Dr.Kitima kapotoka!!

Kusema kuwa Dr.Kitima alimkataza Tundu Lissu asifanye Mhadhara hapo chuoni kisa hajafanya maendeleo jimboni kwake, hicho ni kichekesho kikubwa kwa sababu:

1/Anadai hiyo ilikuwa mwaka juzi(2011) na Tundu Lissu ameingia bungeni mwishoni mwa 2010, alitegemea maendeleo gani kwa muda huo kutoka kwa mbunge mpya tena kutoka upinzani?

2/Je, ni sera ya chuo chake kumwita mwanasiasa kama mbunge ili kutoa muhadhara SAUT kwa kigezo cha maendeleo aliyoleta jimboni mwake?

3/Je, hao wanasiasa wabunge wa CCM wamefanya nini kikubwa cha maendeleo majimboni mwao mpaka wapewe nafasi?

4/Paul Makonda sio mbunge wala kiongozi wa nchi bali ni kada wa CCM, naye siku chache zilizopita alikuja SAUT akiwa na Samweli Sitta nk na kupewa nafasi ya kuongea, ni maendeleo yapi amefanya katika nchi yetu mpaka apewe nafasi hiyo?
Kimsingi dk Kitima ambaye ameagwa jana rasmi akimaliza muda wake wa uongozi kama makamu mkuu wa chuo,alichokimaanisha hapa ni kwamba kwenye ujio wa Wassira chuoni hapa kama mtoa mada ,ulijadiliwa na kukubaliwa na uuongozi wa chuo na kitengo husika,so wakati wanajadili nani aje chuoni kutoa mada wajumbe wengi walimpendekeze mh Tundu Lissu,bt yeye kama makamu alikataa,so sijajua wana ugomvi gani wa kimaslahi,bt mwaka 2011 Lissu alapaswa atoe mhadhara na walikubaliana na Kitima bt kufika kesho yake dakika za mwisho alizuiwa kwa madai USALAMA WA TAIFA WAMETOA KATAZO HILO
 
POINT OF CORRECTION: Kamanda Tundu Lissu alitoa mhadhara kuhusiana na mikataba ya rasilimali asilia kama gesi na madini.Nakumbuka ilikuwa imeandaliwa na kitengo cha uchumi kwa kushirikiana na SAUTESA hivyo kudai Mhe.Lissu alizuiliwa ni upotoshaji mkubwa, ilikuwa ni March,2013 ndani ya ukumbi wa M13 na alipotoka kwenye mhadhara alitembelea ofisi ya CHADEMA-SAUT!

Mkuu Makala kada wa CDM SAUT,kumbuka mwaka 2011,jioni ile alipozuiwa kutoa mada eneola chuo na nyie makada wa CDM SAUT mkaampeleka ofisini kwenu.
A%20S%20576.gif
remember?
 
kumbuka me nilik8wemo ukumbini ,nami si mwandishi sijui lolote kuhusu maadili ya uandishi wala kufanya editing me nimenukuu na kuripoti bila kuongez wala kupungza kitu mkuu
 
oneblood; Nijuavyo mimi Dr.Kitima hana ugomvi wala chuki binafsi dhidi ya yeyote akiwemo Mhe.Tundu Lissu.Tarehe 16.03.2013 Kamanda Lissu alialikwa kutoa mhadhara wa uchumi na mikataba mbalimbali katika kuchangia maendeleo ya taifa hivyo kumwalika tena baada ya miezi miwili isingeleta mvuto sana ukizingatia kwamba mada zilikuwa zinaendana.Ninyi wenyewe mliona Mhe.Wassira alivyokuwa anajing'ata midomo lakini pia ilikuwa ni wiki moja tu baada ya Samwel Sitta kulikoroga na bila shaka sasa wanajua kwamba wakitembelea SAUT kitawakuta nini! Kilichotokea 2011, haukuwa mgogoro bali maelewano kwani Mhe.Lissu alizuiwa kuzungumza na wanachuo kwa kuwa haukuwa mhadhara but alitembelea tu na aliomba then kutokana na mvuto wake kuwa mkubwa sana ukijumlisha na mwamko wa wana-SAUT alikataliwa kwa kuwa haikuwepo kwenye ratiba na ndiyo maana aliandaliwa mhadhara mwingine march, 2013.A rose by any other name would smell the same, so get back to the topic!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom