Dk. Joyce Ndalichako atosha wizara ya elimu

Dk. Joyce Ndalichako atosha wizara ya elimu

Yaani Joycee Ndalichakooo ni Buldozaaaaaa!!safii sanaaa Jpm
 
Hivi ameolewa kweli? Kama bado nifanye mchakato wa kuvuta chombo, mwenyewe taarifa tafadhali
 
Ushauri kwa mh Rais Dk JPM. Huyu mama anafaa kabisa nafasi hiyo uliyoiacha kiporo na kutafuta mtu wa uhakika.

Huyu mama ni mama wa shoka kwa kasi yako hiyo ya hapa kazi tu yeye ndiye mtu sahihi kabisa. Naomba uliangalie hili kabla ya kuanua matanga ya mazishi ya elimu.

Nawasilisha kwako Mhe JPM.

Mkuu umetisha, ushauri wako umekubalika
 
Kwendeni zenu nyinyi wajahidina wakubwa hamuwezi kutufanya sisi wote tukawaogopa nyinyi. Yule naye mtu amekosea na amekili dini gani hiyo yabkishetani haisamei watu. NDALICHAKO ANAFAA KUWA WAZIRI WA ELIMU KWA HAPA TULIPO.
Mitihani unafanya kwa namba wala jina halijulikani, kama umeperform vibaya huwezi bebwa kisa eti dini au kubalansi, hiyo hakunaga!!
Elimu yetu ikiwa chini, au fake hatutaweza kushindana kwenye soko la ajira duniani!!
Huyo Dr Joyce ni the wright person wa kufufua standard yetu ya Elimu iwe ya kimataifa!!
Big up Mhs JPM kutupa jembe lililo sahaulika!!
 
BAKWATA Yataka Dk Joyce
Ndalichako Ajiuzulu:
Kisa Ukinyonga Katika Katokeo ya
Mitihani Form VI
BARAZA la Waislamu Tanzania
(Bakwata) limemtaka Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk
Joyce Ndalichako kujiuzulu wadhifa
huo akimtuhumu kuwafelisha mitihani
ya dini ya Kiislamu wanafunzi wa
kidato cha sita wa dini hiyo.
Kauli hiyo ya Bakwata imetolewa na
Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin
Shaaban Simba katika mkutano wake
na waandishi wa habari jijini Tanga jana
kuelezea msimamo wa Waislamu
nchini kuhusu matokeo ya kidato cha
sita, hujuma inayoandaliwa kufanyika
katika zoezi la sensa pamoja na
vurugu zilizotokea Zanzibar.
Kuhusu hujuma ya mtihani, Mufti
Simba alisema kuwa matokeo ya
mtihani ya dini hiyo ya Kidato cha Sita
yaliyotangazwa Mei Mosi 2012,
yaliwashtua wanafunzi Waislamu
waliofanya mtihani wa elimu ya dini ya
kiislamu (Islamic Knowledge), ambayo
yalionyesha kuwa asilimia 70 walifeli
kwa kupata daraja F.
Alisema matokeo hayo yalionyesha
kuwa ni asilimia 30 ndiyo waliofaulu
kwa kupata daraja D, ambapo
waliopata alama za juu kabisa nchi
nzima ni wanafunzi saba
pekee.?Matokeo haya yaliwashtua
wanafunzi na wazazi, taasisi
mbalimbali za kiislamu zilimua kukata
rufaa kuonyesha kutokubaliana na
matokeo hayo, hatimaye baraza hilo
likabaini kuwa lilikosea na likaidhinisha
kutolewa matokeo
mapya,? alisema Mufti Simba.
Tayari Ndalichako ametoa ufafanuzi
kuwa kosa lililotokea akisema si
hujuma bali ni la kiufundi lililotokana na
kubadili utaratibu wa kufanya mitihani
mitatu ya somo hilo kuwa miwili, lakini
mfumo wa ujumlishaji maksi
ulisahaulika kubadilishwa.
Ndalichako alilieleza gazeti dada la
Mwananchi, The Citizen, kuwa awali
matokeo ya mitihani mitatu yalikuwa
yanajumlishwa na kugawanywa kwa
tatu kwa kutumia mfumo wa kompyuta,
ili kupata alama rasmi za mtahiniwa,
lakini safari hii zilipojumlishwa alama
za mitihani miwili ya somo hilo
ziliendelea kugawanywa kwa tatu
badala ya mbili kimakosa.
Habari zilizopatikana kutoka Necta
zimesema kuwa baada ya kupata
malalamiko ya wanafunzi hao,
uchunguzi ulifanyika na kubaini kasoro
hiyo ambapo ilirekebishwa.Mei 30,
mwaka huu Necta ilikutana na Baraza
la Wakuu wa Shule za Kiisilamu na
kufafanua suala hilo, ambapo
ilionekana tatizo hilo si hujuma bali
kosa la kiufundi.
Mwenyekiti wa Islamic Education
Panel, Pilly H.H alimwandikia barua
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi na nakala kwa
Katibu Mtendaji wa Necta, Amir,
Jumuia na Taasisi za Kiislamu
Tanzania akishukuru wizara kwa hatua
zilizochukuliwa.
?Tunashukuru kwa jinsi Wizara ya
Elimu na mafunzo ya ufundi ilivyopokea
suala hili kwa uzito unaostahiki?Tun
atoa shukurani za pekee kwa katibu
mtendaji wa baraza la mitihani kwa
hatua alizochukua ndani ya muda
mfupi sana, nashukuru kwa
ushirikiano,? ilisema barua hiyo
iliyoandikwa na Mwenyekiti wa Baraza
la Wakuu wa Shule za Kiislamu.
Hata hivyo, akisistiza hoja yake Mufti
Simba alisema kuwa matokeo
yaliyotolewa upya yalionyesha
kwamba wanafunzi zaidi ya asilimia 70
ya wanafunzi walifaulu, jambo ambalo
Waislamu wanaamni kwamba ni
hujuma inayolenga kupunguza idadi ya
wanafunzi wa Kiislamu wa kujiunga na
vyuo vikuu.
Mufti huyo alisema jambo
lililomshangaza yeye pia pamoja na
Waislamu wote nchini ni tamko
lililotolewa na Ndalichako kupitia
vyombo vya habari Jumanne iliyopita
aliposema kuwa Baraza la Mitihani
halikukosea kutoa matokeo hayo kwa
kuwa waliosahihisha ni walimu wenye
sifa.
?Bakwata inamshangaa Katibu Mtendaji
wa Baraza la Mitihani, Ndalichako kwa
kauli yake aliyoitoa kupitia vyombo vya
habari juzi 5/6/2012 akisema hakuna
hujuma na mitihani inasahihishwa na
walimu wenye sifa na wanachaguliwa
na wakuu wa shule zao,?alisema Mufti
Simba.
Alisema hoja iliyotolewa na Ndalichako
kwamba wanaosahihisha ni wenye
uzoefu haina mashiko kwa sababu
Waisalmu wanacholalamikia ni mfumo
mzima wa ?Conveyor Belt?, aliodai
umewekwa kuwahujumu wanafunzi
Waislamu.
Alisema matokeo hayo ya mtihani wa
somo la kiislamu umeonyesha kuwa
upo wasiwasi kwamba kilichofanyika
huko ndicho wanachofanyiwa
wanafunzi wa kiislamu katika masomo
mengine kuanzia darasa la saba,
kidato cha nne na hata vyuo vikuu kwa
lengo la kupunguza idadi ya wasomi
waislamu.
?Waislamu tunaamini kwamba hila
kama hii inafanyika pia kwenye
masomo mengine, kwa maana hiyo
tunataka Ndalichako na watendaji
wengine wajiuzulu ili kuondoa kashfa
hii kwa Serikali, pia kuleta imani ya
Waislamu kwa Serikali yao, ?alisema
Mufti Simba.
Alifafanua kuwa baada ya kujiuzulu,
Serikali iunde tume ya kuchunguza
hujuma zilizotendeka katika baraza
hilo dhidi ya Waislamu kwa kipindi cha
miaka 10 iliyopita akieleza kuwa
Waislamu wanaamini kwamba
wanafunzi wengi
wamefelishwa kwa kusudi maalumu la
kuzorotesha kizazi chao.
SUALA LA SENSA YA WATU NA
MAKAZI.
Kuhusu Sensa, Mufti Simba alisema
kuwa kalenda iliyotolewa na Ofisi ya
Waziri Mkuu, takwimu zinaoonyesha
kuwa idadi ya Watanzania ni 43 milioni
ambapo Wakristo ni asilimia 52,
Waislamu asilimia 32 na dini nyingine ni
asilimia 16 akieleza kuwa takwimu hizo
si sahihi.
Alisema kuwa Bakwata inalaani kitendo
hicho alichosema kinapotosha
wananchi kwa kuwa sensa iliyofanyika
mwaka 2002 kipingele kinachobainisha
dini za Watanzania kiliondolewa.
MGOGORO WA ZANZIBAR
Akizungumzia matukio yauvunjifu wa
amani vilivyotokea visiwani Zanzibara
hivi karibuni Mufti Simba alisema
Bakwata inalaani kitendo inalaani
kitendo hicho ikiamini kwamba
waliofanya vurugu hizo siyo Waislamu
bali ni
wahuni.
Alishauri kuundwa kamati ya pamoja
kati ya Serikali na kikundi cha
Waislamu cha Uamsho ili kuchunguza
waliohusika na vurugu hizo na
waliohusika kuchukuliwa hatua.
Bakwata yataka Dk Ndalichako ajiuzulu
mwananchi.co.tz
June 7, 2012 at 4:59am ? Public
 
Aksante sana mtoa mada kwa kupendekeza jina La Ndalichako kumbe Tanzania wazalendo bado wapo pia Tunamshukuru sana Rais walau hata kupata wazo la kuchukua maoni yetu humu JF nakuyafanyia kazi na vyombo vyake Kwakweli safari hii tumelamba dume,Tunamuombea maisha marefu Mungu ambariki.
 
Sasa watu watumie hii forum kuweka mawazo mazuri...kufichua wezi na wazembe serikalini. Maana serikali yetu tukufu inatazama na kusikiza. Tusilete majungu tu. Na wale wanaccm waliozea siasa za kipuuzi wabadilike. Tanzania ni kubwa kuliko CCM.
 
Nguvu, umefeli kirahisi sana, Feza Schools ni Islamic Seminaries?

Vv

Kama vitu hujui nyamaza! Ulishawahi kuona feza schools wakitoa ofa ya kusoma bure kwa wanafunzi waliofaulu vizuri nafasi hiyo akipewa mkristo? Jiulize kwanini
 
Ndugu wanajamvi, baada ya rais Magufuli kutangaza baraza la mawaziri. Kuna members humu walikuja na pendekezo kwa rais amteue Dr. Ndalichako kuwa mbunge na amkabidhi wizara ya Elimu. Nina Imani pamoja na maono yake rais pia alichukua ya hapa JF.
Baada ya kusema hayo naomba jukwaa hili tupaze sauti kwa rais amrudishe Justice Warioba kazini ili akamilishe kazi ya kupata Katiba Mpya. Wote tu mashahidi kwamba rasmu iliyopo ilichakachuliwa sana.

Maulid Mubarak
Merry Christmas and Happy Holidays
 
Mitihani unafanya kwa namba wala jina halijulikani, kama umeperform vibaya huwezi bebwa kisa eti dini au kubalansi, hiyo hakunaga!!
Elimu yetu ikiwa chini, au fake hatutaweza kushindana kwenye soko la ajira duniani!!
Huyo Dr Joyce ni the wright person wa kufufua standard yetu ya Elimu iwe ya kimataifa!!
Big up Mhs JPM kutupa jembe lililo sahaulika!!
Msome boing mbowe hapo kwenye post yake ndio utaelewa,
 
Prof Njozi ni mzuri kuliko huyo mama yenu mwenye dhulma zidi ya wengine
 
Back
Top Bottom