figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,698
- 59,208
Nchi hii haiishi Vituko,
Baada ya Kampuni ya Qnet kuanza kukalalamikiwa na Wananchi kwamba inawatapeli hela zao, Waziri wa Utalii Kigwangalla ameibuka na kusema
Ukweli ni kuwa, siwajui wao binafsi ‘at personal’ level na wala biashara yao, umiliki wake na muundo wake siujui zaidi ya kuelewa kwa juu juu kuwa ni ‘network marketing’.
Waziri Kigwangalla akiwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk. Adelhem Meru Mshauri wa bodi ya QNET David Sharma, meneja mkuu wa QNET-Tanzania Benjamin Mariki wakisoma gazeti lenye bidhaa za kampuni hiyo mara baada ya Ufunguzi wa ofisi ya shirika hilo nchini Tanzaniza..
Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Instagram amekana kuwafahamu wamiliki waendeshaji wa biashara ya QNET
> Soma nukuu niliyoiweka hapa chini!
''Nimeona nitoe ufafanuzi kwenye hili jambo. Maana kila mjadala juu ya hii kampuni ya QNet unapoibuka, jina langu linakuja, na mara nyingine picha yangu inawekwa.
Ukweli ni kwamba, nilialikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wake kama mgeni wa heshima; mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa wakati huo, Dr. Adelhelm Meru.
Niliamini kwa heshima ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ambao ndiyo wenye dhamana ya usajili wa biashara zote nchini, ni lazima ni watu halali na bado ninaamini kama kuna shida mamlaka husika zitachunguza na kuchukua hatua stahiki na kama hakuna shida basi ni vema mamlaka husika zikatoa mwongozo utakaowaondoa hofu wananchi wenzetu wenye ‘interest’ ya kushiriki kwenye biashara hii.
Baada ya kufika eneo la tukio, kiitifaki ikaonekana nami lazima nishiriki zoezi, nikashindwa kukataa. Nadhani inafahamika kwamba nimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kwa vitendo jitihada nyingi mbalimbali za wajasiriamali vijana ambao wameamua kutoka [HASHTAG]#NjeYaBox[/HASHTAG].
Hata hawa nilishindwa kuwakatalia. Ukweli ni kuwa, siwajui wao binafsi ‘at personal’ level na wala biashara yao, umiliki wake na muundo wake siujui zaidi ya kuelewa kwa juu juu kuwa ni ‘network marketing’.
Ifahamike hapa kuwa sina maslahi yoyote yale kwenye biashara hii na wala sikushiriki uzinduzi wake kwa malengo ya kutoa ushawishi ili watu wajiunge, na natoa rai kwamba wanaotaka kujiunga ama kuacha kujiunga wasitumie picha za ushiriki wangu siku ya uzinduzi, kwa namna yoyote ile, kujenga uhalali wa aina yoyote ile, bali watumie vipimo vyao vingine kufanya uamuzi na siyo picha zangu.
Sintohusika na matokeo yoyote yale, chanya ama hasi, ya ushiriki wa mtu yeyote yule ama taasisi yoyote ile, kwenye shughuli za kampuni hii.
Naomba pia izingatiwe kwamba, jina langu ama picha yangu haijaruhusiwa kutumika kama bango la matangazo ya biashara ya mtu au taasisi yoyote ile, na hivyo kufanya hivyo ni kosa kisheria na ikibainika nitachukua hatua kali za kisheria''
#HK
=====
Hapa ni Waziri wa Utalii Kigwangalla wakati akiwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto, (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Qnet uliofanyika Dar es Salaam, wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Qnet, David Sharma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk. Adelhelm Meru na Wakala wa Qnet Tanzania, Benjamini Mariki.
JamiiForums kuliletwa thread ya Malalamiko nikawa nashangaa kwanini hawachukuliwi hatua? Nini kinafanya wasishughulikiwe kama wengine? Qnet Company "biashara mtandao" ni utapeli unaoenea kwa kasi Tanzania. Serikali mko wapi?
=====
My Take:
Hapo mimi ndo nashangaa, anakataa vipi wakati yeye ndo alizindua Ofisi? Alikuwa hajapewa maelezo wanajihusisha na nini?
Bora angekaa kimya sababu wakati anazindua alifanya hivyo hadharani.
Haikwepeki kwamba ana maelezo ya kutosha kuhusu hii Kampuni.