Dk. Hamis Kigwangalla aikana kampuni ya Qnet

Dk. Hamis Kigwangalla aikana kampuni ya Qnet

Hiyo Kampuni wana ka ' branch ' kao kamoja hivi kapo Sinza jirani na Hostels za UDSM ukienda hapo hata kama ni Saa Saba ( 7 ) mchana utasalimiwa kwa kuambiwa ' Good Morning ' na baada ya hapo utaanza ' Kuhubiriwa ' Kitapeli na Wanawake tofauti tofauti ambao huzungumza haraka haraka utadhani wamebanwa na Haja Kubwa na wanataka kuwahi Kujisaidia.
Ha ha ha eti "Good morning " Saa saba mchana
 
Mange Kimbambi anamadhara zaidi ya jamii forum, Mange anavistor wengi zaidi ya jamii forum, Mange anaeffect kwenye jamii ya mtanzani zaidi ya anywebsite

Na hii ni kwasababu ya Mamoderator wa jamii forum...............................Najua hii itafutwa lakini jamii forum lazimu mujitathimi, Otherwise in two year inaenda kufa
 
Kwanza wakikuita kwenye ofisi zao hawakwambii unaenda kufanya nn utasikia "njoo rafiki kuna opportunity nzuri" ukienda unaweza juta poteza mda wako.
Kuna rafiki wa mchumba wangu alimualika pale Sinza, aliponieleza nikamkubalia.
Picha linaanza alipofika kituoni akampigia simu then akajamchukua, chakushangaza baada ya kuingia kwenye ofisi zao tu shosti yake akamgeukia akamwambia "good morning madam" alishangaa sana inakuaje jioni hii shosti ananiambia good morning? tangulini ananiita madam?

Baada ya semina ya siku tatu"udwanzi wa kiwango cha lami" akaja nieleza yote pamoja na kiingilio, kwakua hesabu hazijanipiga chenga tukaanza kunyumbulishaa.

Alitakiwa kutoa kiingilio cha 4m then atafute watu wawili watakao jiunga kupitia yeye, na kila mmoja atoe 4m, ukijumlisha wote watatu itakuwa 12m then yeye ndio anaanza pokea mgao ambao hauzidi laki 4.

Pia anatakiwa awasimamia hao wawili nao waingize watu wawili wawili yani wapatikane wapya 4 na kila mmoja atoe 4m jumla 16m, ili yeye mgao wake uendelee kupanda kufikia around 1.2m na asipofanya hivyo basi hautapanda. Jumla mpenzi wangu na tawi lake lote atatakia kufikisha 12+16= 28m ili mgao wake ufikia around 1.2m

Nikamwambia siwezi kuruhusu uzwazwa wa kiwangu hiko.
Good morning ndio uchawi wao labda
 
Hahaha kuna mchizi ananiambia yeye ni injinia wa bandari ameamua kuacha kaz maana qnet inalipa balaa alaf nikimchek mchizi amechoka kidizain kuliko mimi mwingine alikua muhandis barric ameacha mwingine tbl yaan utapeli flan ivi wakitoto

Mimi nilichoka maana nilikuwa nafanyiwa presentation na mrembo fulani hivi ,ananitajia mambo kibao ila sasa aliniboa maana puani kulikuwa na ukoko wa makamasi unachungulia basi nikamdharau sana. Yaani kidogo nimwambie atoe ule ukoko ila nikaona nitampotezea network nikamuacha.
 
Hii Serikali kanyaboya imeshindwa kutekeleza ahadi walizowaadi watz ktk campaign zao kujenga viwanda ikiwemo, sasa wameamua kutuletea matapeli.
 
We GENTA mtani umeanza eeh...by the way vipi matokeo ya jana kule Shy? (off the book).
teh teh umeniwahi! hapa katolea hasira zake kidogo kwa kweli jana simba walifanya vizuri walipata matokeo yaliyopunguza makunyazi yetu! ikitokea wakapoteza mechi mbili mfululizo itakuwa poa sana!
 
Hiyo Kampuni wana ka ' branch ' kao kamoja hivi kapo Sinza jirani na Hostels za UDSM ukienda hapo hata kama ni Saa Saba ( 7 ) mchana utasalimiwa kwa kuambiwa ' Good Morning ' na baada ya hapo utaanza ' Kuhubiriwa ' Kitapeli na Wanawake tofauti tofauti ambao huzungumza haraka haraka utadhani wamebanwa na Haja Kubwa na wanataka kuwahi Kujisaidia.
Nyingine ipo mikocheni, kuna siku rafiki yangu aliniita kuna ishu ya biashara tukaongee, duuh nimefika ilikuwa mida ya saa 9 mchana, nasalimiwa good morning, nikiwa bado kwenye mshangao maana nnawajua hao wadada kiingereza hakiwapigi chenga, anaingia mama mmoja mweupe mtu mzima nae kashusha good morning duuh nikajisemea hii ishakua balaa ngoja nisikilize nisepe nilijilaumu sana kupoteza mda wangu na sikuelewa yule demu aliniona mimi mpori pori ama nini
 
Ni hatari kufanya jambo ambalo haulijui.
Kwa kweli hapa nimemuona NUNDA mmoja matata sana.
Na usomi wake hakufanya hata research na kufanya reference na kina DECI na forever living na kuwa ma doubts??
 
Nyingine ipo mikocheni, kuna siku rafiki yangu aliniita kuna ishu ya biashara tukaongee, duuh nimefika ilikuwa mida ya saa 9 mchana, nasalimiwa good morning, nikiwa bado kwenye mshangao maana nnawajua hao wadada kiingereza hakiwapigi chenga, anaingia mama mmoja mweupe mtu mzima nae kashusha good morning duuh nikajisemea hii ishakua balaa ngoja nisikilize nisepe nilijilaumu sana kupoteza mda wangu na sikuelewa yule demu aliniona mimi mpori pori ama nini

Qnet Qgwangala!
 
Haya mnaomwita Mange mwongo sijui kichaa, na hili si aliwajulisheni yeye !? Oneni sasa waziri wenu anajitapisha ujinga, kweli MTU mzima, waziri bila aibu unashiriki kuzindua kitu usichokijua ?? Sasa jaribu kuwaza kama alitakiwa kutoa speech angeongea nini ??
we waache kuna siku watamuelewa. na kama sio Mange kumlipua wale asingeongea kabisa. afu mleta mada ungeandika kabisa nini kimetokea had ikabidi ajieleze.
 
Matapeli wakiwatumia na baadhi ya viongozi wa serikali kuwa hadaa Watz ili wawapige hela zao....
Baadhi ya mitz imezidi umbwege kukubali kuingizwa kingi lkn yote ni kutaka usrahisi,hakuna hela za ubweteubwete

Ova
 
InashangazA waziri mzima kufanya jambo bila background check , how is this possible ? It’s amazing
 
Kuna jamaa wanafanya ishu za Rifaro eti unanunua vocha baadae unalipwa kwa idadi ya vocha unazouza na kununua sijui!..Nikashangaa nawekwa hadi group lao whatsapp nikajitoa nikamtumia naemjua sms akinirudisha namblock na asinijue tena!..
 
Mange Kimbambi anamadhara zaidi ya jamii forum, Mange anavistor wengi zaidi ya jamii forum, Mange anaeffect kwenye jamii ya mtanzani zaidi ya anywebsite

Na hii ni kwasababu ya Mamoderator wa jamii forum...............................Najua hii itafutwa lakini jamii forum lazimu mujitathimi, Otherwise in two year inaenda kufa
WaTz wengi wanapenda udaku ndio maana mange ana visitors wengi. Huku JF kuna mada fikirishi wapenda udaku huku hapawafai ndio maana watumiaji wa JF unaweza kujikuta mko watatu tu mtaa mzima
 
Nyingine ipo mikocheni, kuna siku rafiki yangu aliniita kuna ishu ya biashara tukaongee, duuh nimefika ilikuwa mida ya saa 9 mchana, nasalimiwa good morning, nikiwa bado kwenye mshangao maana nnawajua hao wadada kiingereza hakiwapigi chenga, anaingia mama mmoja mweupe mtu mzima nae kashusha good morning duuh nikajisemea hii ishakua balaa ngoja nisikilize nisepe nilijilaumu sana kupoteza mda wangu na sikuelewa yule demu aliniona mimi mpori pori ama nini
hahahah..hhahaha..haaaaaaaaaaa...walah! dah
 
Back
Top Bottom