Dk. Hamis Kigwangalla aikana kampuni ya Qnet

Mr Suprize

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
825
848
Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Instagram amekana kuwafahamu wamiliki waendeshaji wa biashara ya QNET

> Soma nukuu niliyoiweka hapa chini!

Nimeona nitoe ufafanuzi kwenye hili jambo. Maana kila mjadala juu ya hii kampuni ya QNet unapoibuka, jina langu linakuja, na mara nyingine picha yangu inawekwa.

Ukweli ni kwamba, nilialikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wake kama mgeni wa heshima; mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa wakati huo, Dr. Adelhelm Meru.

Niliamini kwa heshima ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ambao ndiyo wenye dhamana ya usajili wa biashara zote nchini, ni lazima ni watu halali na bado ninaamini kama kuna shida mamlaka husika zitachunguza na kuchukua hatua stahiki na kama hakuna shida basi ni vema mamlaka husika zikatoa mwongozo utakaowaondoa hofu wananchi wenzetu wenye ‘interest’ ya kushiriki kwenye biashara hii.

Baada ya kufika eneo la tukio, kiitifaki ikaonekana nami lazima nishiriki zoezi, nikashindwa kukataa.

Nadhani inafahamika kwamba nimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kwa vitendo jitihada nyingi mbalimbali za wajasiriamali vijana ambao wameamua kutoka [HASHTAG]#NjeYaBox[/HASHTAG]. Hata hawa nilishindwa kuwakatalia.

Ukweli ni kuwa, siwajui wao binafsi ‘at personal’ level na wala biashara yao, umiliki wake na muundo wake siujui zaidi ya kuelewa kwa juu juu kuwa ni ‘network marketing’.

Ifahamike hapa kuwa sina maslahi yoyote yale kwenye biashara hii na wala sikushiriki uzinduzi wake kwa malengo ya kutoa ushawishi ili watu wajiunge, na natoa rai kwamba wanaotaka kujiunga ama kuacha kujiunga wasitumie picha za ushiriki wangu siku ya uzinduzi, kwa namna yoyote ile, kujenga uhalali wa aina yoyote ile, bali watumie vipimo vyao vingine kufanya uamuzi na siyo picha zangu.

Sintohusika na matokeo yoyote yale, chanya ama hasi, ya ushiriki wa mtu yeyote yule ama taasisi yoyote ile, kwenye shughuli za kampuni hii.

Naomba pia izingatiwe kwamba, jina langu ama picha yangu haijaruhusiwa kutumika kama bango la matangazo ya biashara ya mtu au taasisi yoyote ile, na hivyo kufanya hivyo ni kosa kisheria na ikibainika nitachukua hatua kali za kisheria.

H.K
e30a0fb9578554825d0f4ff9218764f9.jpg

Screenshot from 2018-02-16 10-19-53.png

Hapa ni Waziri wa Utalii Kigwangalla wakati akiwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto, (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Qnet uliofanyika Dar es Salaam, wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Qnet, David Sharma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk. Adelhelm Meru na Wakala wa Qnet Tanzania, Benjamini Mariki.

JamiiForums kuliletwa thread ya Malalamiko
Qnet Company "biashara mtandao" ni utapeli unaoenea kwa kasi Tanzania. Serikali mko wapi?
QNET acheni utapeli, rudisheni pesa ya mke wangu na shemeji shilingi milioni 8
Qnet naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu..
 
Bila shaka naye kigwangala na fursa kwa upande flani kaliwa ama kabebwa ilia kujiaminisha kwamba wao sio matapeli.... Network marketing ni uchwara na uwizi mtupuu...

Cc forever living

Hide my id da mange watu wanatupia sana macho kwa mange kimambi
 
Yeye alikuwa mwalikwa tu ikawaje akakata utepe wakati Katibu Mkuu wa wizara ndo alikuwa mwalikwa?
Ni dharau kubwa sana anatuletea huyo mchumia tumbo na ndo wanachofundishwa huko chamani kuwa watz wote ni mazwazwa chochote atakacho waeleza wataafiki......picha inaonyesha anakata utepe kuashiria uzinduzi.T afadhalini sana wewe Na kundi lenu inatakiwa mjue kuwa tupo tunaoweza kufanya reasoning na hata Twaweza walikuonyesheni ktk tafiti zao
 
Nimeona nitoe ufafanuzi kwenye hili jambo. Maana kila mjadala juu ya hii kampuni ya QNet unapoibuka, jina langu linakuja, na mara nyingine picha yangu inawekwa.

Ukweli ni kwamba, nilialikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wake kama mgeni wa heshima; mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa wakati huo, Dr. Adelhelm Meru.

Niliamini kwa heshima ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ambao ndiyo wenye dhamana ya usajili wa biashara zote nchini, ni lazima ni watu halali na bado ninaamini kama kuna shida mamlaka husika zitachunguza na kuchukua hatua stahiki na kama hakuna shida basi ni vema mamlaka husika zikatoa mwongozo utakaowaondoa hofu wananchi wenzetu wenye ‘interest’ ya kushiriki kwenye biashara hii.

Baada ya kufika eneo la tukio, kiitifaki ikaonekana nami lazima nishiriki zoezi, nikashindwa kukataa.

Nadhani inafahamika kwamba nimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kwa vitendo jitihada nyingi mbalimbali za wajasiriamali vijana ambao wameamua kutoka [HASHTAG]#NjeYaBox[/HASHTAG]. Hata hawa nilishindwa kuwakatalia.

Ukweli ni kuwa, siwajui wao binafsi ‘at personal’ level na wala biashara yao, umiliki wake na muundo wake siujui zaidi ya kuelewa kwa juu juu kuwa ni ‘network marketing’.

Ifahamike hapa kuwa sina maslahi yoyote yale kwenye biashara hii na wala sikushiriki uzinduzi wake kwa malengo ya kutoa ushawishi ili watu wajiunge, na natoa rai kwamba wanaotaka kujiunga ama kuacha kujiunga wasitumie picha za ushiriki wangu siku ya uzinduzi, kwa namna yoyote ile, kujenga uhalali wa aina yoyote ile, bali watumie vipimo vyao vingine kufanya uamuzi na siyo picha zangu.

Sintohusika na matokeo yoyote yale, chanya ama hasi, ya ushiriki wa mtu yeyote yule ama taasisi yoyote ile, kwenye shughuli za kampuni hii.

Naomba pia izingatiwe kwamba, jina langu ama picha yangu haijaruhusiwa kutumika kama bango la matangazo ya biashara ya mtu au taasisi yoyote ile, na hivyo kufanya hivyo ni kosa kisheria na ikibainika nitachukua hatua kali za kisheria.

H.K
e30a0fb9578554825d0f4ff9218764f9.jpg
Haya mnaomwita Mange mwongo sijui kichaa, na hili si aliwajulisheni yeye !? Oneni sasa waziri wenu anajitapisha ujinga, kweli MTU mzima, waziri bila aibu unashiriki kuzindua kitu usichokijua ?? Sasa jaribu kuwaza kama alitakiwa kutoa speech angeongea nini ??
 
Tumeongea sana hapa kuhusu utapeli wa Qnet lakini hatukueleweka,sasa Dada yenu Mange kaja na kombora hili
IMG_20180216_072137 (1).jpg

Hapa alikuwa anamshutumu Kigwangalla kwa kukubali kutumika na matapeli Wakati alipokubali kuwa mgeni rasmi na kufungua ofisi ya Qnet.
Kigwangalla naye alipoona Post ya Mange akaja na hii
PhotoCollage_1532567181 (1).jpg

Kwa Ufupi ni Kwamba Kigwangalla ameshawaruka viunzi....jiongezeni akili vijana hakuna shortcut kwenye maisha......labda kwa vile kasema dada yenu Mange mnaweza mkaelewa mana sisi tumeimba sana hapa hamkutuelewa!!!
 
Attachments

  • IMG_20180216_072137.jpg
    IMG_20180216_072137.jpg
    76.2 KB · Views: 252
  • PhotoCollage_1532567181 (1).jpg
    PhotoCollage_1532567181 (1).jpg
    199.4 KB · Views: 227
Back
Top Bottom