Dk. Hamis Kigwangalla aikana kampuni ya Qnet

Dk. Hamis Kigwangalla aikana kampuni ya Qnet

Huyu jamaa ni kielelezo tosha cha aina ya mawaziri mizigo walioko CCM..

Sasa kama yeye mwenyewe alishakana mpaka jina lake ,siwezi kumshangaa kuikana hii kampuni ya kitapeli..
 
Huyu waziri siku zote mkurupukaji.waziri Husein Mwinyi hutamkuta katika upuuzi puuzi kama huu
 
Ktk pic wazir kingwa alivyoshikilia mkasi......Teh Teh

Ova
 
Hivi TISS kazi zao si pamoja na kuwapasha hawa mabwana wakubwa yanayojiri ili wasijeingizwa choo cha kike ama?
 
Hiyo Kampuni wana ka ' branch ' kao kamoja hivi kapo Sinza jirani na Hostels za UDSM ukienda hapo hata kama ni Saa Saba ( 7 ) mchana utasalimiwa kwa kuambiwa ' Good Morning ' na baada ya hapo utaanza ' Kuhubiriwa ' Kitapeli na Wanawake tofauti tofauti ambao huzungumza haraka haraka utadhani wamebanwa na Haja Kubwa na wanataka kuwahi Kujisaidia.

Ha ha ha ha ha kuna kaofisi kengine kapo hapo Mikocheni kwa Warioba alinipeleka jamaa yangu mmoja ilikuwa jioni nikaamkiwa Goodmorning!mahubiri yakaendeleaaa nikaambiwa ninunue saa sh milioni 5! Halafu nimlete nimlete mtu naye anunue ndo nianze kupata pesa!nikamtizama yule jamaa alonipeleka nikamuuliza wewe ushaweka?kanambia ndio nikamwambia la kuambiwa changanya Na zako!
 
Sasa mtu kama yeye anapeteza muda kwenye kitu ambacho hakijui itakuaje kwa watu wakawaida.
 
Tumeongea sana hapa kuhusu utapeli wa Qnet lakini hatukueleweka,sasa Dada yenu Mange kaja na kombora hiliView attachment 696289
Hapa alikuwa anamshutumu Kigwangalla kwa kukubali kutumika na matapeli Wakati alipokubali kuwa mgeni rasmi na kufungua ofisi ya Qnet.
Kigwangalla naye alipoona Post ya Mange akaja na hiiView attachment 696294

Kwa Ufupi ni Kwamba Kigwangalla ameshawaruka viunzi....jiongezeni akili vijana hakuna shortcut kwenye maisha......labda kwa vile kasema dada yenu Mange mnaweza mkaelewa mana sisi tumeimba sana hapa hamkutuelewa!!!
Duh what a shame Eti Mimi simo majibu ya kitoto
 
Waziri/naibu waziri unashiriki uzinduzi au shughuli ambayo hujui inajishughulisha na nini achilia mbali uhalali wake hata kama walikuokota baa siku hiyo Kigwa,hapana.



Magu utatumbua mpaka vidole viote vigimbi.
 
Mimi nilichoka maana nilikuwa nafanyiwa presentation na mrembo fulani hivi ,ananitajia mambo kibao ila sasa aliniboa maana puani kulikuwa na ukoko wa makamasi unachungulia basi nikamdharau sana. Yaani kidogo nimwambie atoe ule ukoko ila nikaona nitampotezea network nikamuacha.
nikisomaga hiz comments zinazohusiana na haya mambo ya Networking huwa nacheka sana dah
 
Hawa ndio mawaziri wanaosani mikataba bila hata kuiona....aibu yako Kigwangalla.

Ingekuwa enzi za Mwalimu huyu waziri angeandika barua ya kujiuzuru mwenyeweee. Ikifika mezani kwa Julius angeteua mwingine bila hata kujibu hiyo barua! Principal ya mke wa Kaizari is applicable !
 
Waziri/naibu waziri unashiriki uzinduzi au shughuli ambayo hujui inajishughulisha na nini achilia mbali uhalali wake hata kama walikuokota baa siku hiyo Kigwa,hapana.



Magu utatumbua mpaka vidole viote vigimbi.
eti vigimbi
 
Mara paaap... MAGU ametengeua uteuzi wa kigwangala
 
Comments za wadau zimeniacha hoi

Screenshot_2018-02-16-19-16-15.png
 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Instagram amekana kuwafahamu wamiliki waendeshaji wa biashara ya QNET

> Soma nukuu niliyoiweka hapa chini!


Nimeona nitoe ufafanuzi kwenye hili jambo. Maana kila mjadala juu ya hii kampuni ya QNet unapoibuka, jina langu linakuja, na mara nyingine picha yangu inawekwa.

Ukweli ni kwamba, nilialikwa kwenye shughuli ya uzinduzi wake kama mgeni wa heshima; mgeni rasmi alikuwa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa wakati huo, Dr. Adelhelm Meru.

Niliamini kwa heshima ya kuzinduliwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ambao ndiyo wenye dhamana ya usajili wa biashara zote nchini, ni lazima ni watu halali na bado ninaamini kama kuna shida mamlaka husika zitachunguza na kuchukua hatua stahiki na kama hakuna shida basi ni vema mamlaka husika zikatoa mwongozo utakaowaondoa hofu wananchi wenzetu wenye ‘interest’ ya kushiriki kwenye biashara hii.

Baada ya kufika eneo la tukio, kiitifaki ikaonekana nami lazima nishiriki zoezi, nikashindwa kukataa.

Nadhani inafahamika kwamba nimekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kwa vitendo jitihada nyingi mbalimbali za wajasiriamali vijana ambao wameamua kutoka [HASHTAG]#NjeYaBox[/HASHTAG]. Hata hawa nilishindwa kuwakatalia.

Ukweli ni kuwa, siwajui wao binafsi ‘at personal’ level na wala biashara yao, umiliki wake na muundo wake siujui zaidi ya kuelewa kwa juu juu kuwa ni ‘network marketing’.

Ifahamike hapa kuwa sina maslahi yoyote yale kwenye biashara hii na wala sikushiriki uzinduzi wake kwa malengo ya kutoa ushawishi ili watu wajiunge, na natoa rai kwamba wanaotaka kujiunga ama kuacha kujiunga wasitumie picha za ushiriki wangu siku ya uzinduzi, kwa namna yoyote ile, kujenga uhalali wa aina yoyote ile, bali watumie vipimo vyao vingine kufanya uamuzi na siyo picha zangu.

Sintohusika na matokeo yoyote yale, chanya ama hasi, ya ushiriki wa mtu yeyote yule ama taasisi yoyote ile, kwenye shughuli za kampuni hii.

Naomba pia izingatiwe kwamba, jina langu ama picha yangu haijaruhusiwa kutumika kama bango la matangazo ya biashara ya mtu au taasisi yoyote ile, na hivyo kufanya hivyo ni kosa kisheria na ikibainika nitachukua hatua kali za kisheria.

H.K
e30a0fb9578554825d0f4ff9218764f9.jpg



View attachment 696346

Hapa ni Waziri wa Utalii Kigwangalla wakati akiwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia, Wazee na Watoto, (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la Qnet uliofanyika Dar es Salaam, wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Qnet, David Sharma, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dk. Adelhelm Meru na Wakala wa Qnet Tanzania, Benjamini Mariki.


JamiiForums kuliletwa thread ya Malalamiko
Qnet Company "biashara mtandao" ni utapeli unaoenea kwa kasi Tanzania. Serikali mko wapi?
QNET acheni utapeli, rudisheni pesa ya mke wangu na shemeji shilingi milioni 8
Qnet naomba pesa yangu milioni 5, nimenunua saa mpaka sasa najuta kuwafahamu..
Kigwangala asikimbie hii hoja alikuwa anawasifia sana hawa Qnet siku ya uzinduzi na aliwaelezea kama watu anaowajua sasa leo anakimbia nini?
 
Pale unapokata utepe wakati si mgeni rasmi.....🙁🙁
 
Back
Top Bottom