Dizasta Vina a.k.a Maradona

Dizasta Vina a.k.a Maradona

Kwanza hao kina boshoo ndo hamna kila kitu. Uwezo wao ni hamna ni dhaifu Ila hamna namna ndo maana Nikki mbishi kwenye ngoma ya maji Ni uhai Kuna mstari anasema "naaumia kujua chin bees ndo Yule King Kong" yaani kina chin bees wanaonekana ndio warithi wa kina chid Benz.. kilasiku... Mistari Yao Ni Kama mfano wa kile kisichofaa kuandikwa/ sauti zao si za michano walipaswa wajiunge misifa...."
Mkuu boshoo sio msanii mbovu wakumuweka kwenye rank za kina lunya

Huyu ni zao la Tamaduni, tamaduni haijawahi toa kitu kibovu hata siku moja

Boshoo ni msanii mzuri na amefanya poa sana kwenye tracks zake za mwanzo na hizi za mwishoni mwishoni baadhi

Kinachokuja kumtofautisha na zamani ni jinsi anavyo fanya mziki kwa kuangalia soko la sasa linatakaje.

Dogo ni story teller mzuri kuna ngoma yake moja (nimeisahau jina nitaiweka hapa nikiikumbuka) kachana vizuri sana mle

"Walete" aliyomshirikisha na Dizasta umeisikia?

Baadhi ua lines kwenye ngoma yake ya "Nilipotoka"

Natoka kwenye kona za mateja kujidunga, wale walotoka jela kujifunza.../

Napotoka mimi shujaa ni mama muuza, anaye somesha watoto huku polisi wanambugudha.../
 
We ndo hujanisoma Kama unakumbuka zamani hip-hop ndo ilikua haipewi kabisa kipaumbele na ulikua unaonekana mziki wa kihuni.... Hadi pale genius Professor Jay alipokuja kutoa ngoma ya CHEMSHA BONGO enzi zile anajiita nigger Jay akiwa na kundi la hard blaster crew HBC.. hii ngoma sio Siri iliyafanya mapinduzi makubwa Sana ndo watu wakaanza kuitazama hip-hop kwa jicho lingine.. enzi zile muziki uliokua unabamba bongo Ni dansi kina mumini mwijuma na takeu za kina mr. Nice ndipo kina fid wakaibuka.

Kubali kataa Ni utunzi tu mzee mtu akiandika ngoma inayoigusa jamii lazima atapata airtime kubwa.

Dizasta nilianza kumfatilia alipotoa ngoma ya KANISA. lakini hakua na consistency ya vitu Kama hivo....

Young Lunya Ni msanii wa mchongo tukianza kuzungumzia hip-hop labda kategori nyingine kuvuma n Jambo la kawaida hata mandonga n superstar au hamorapa.... Lakini huwezi sema ni wasanii

Swala Ni moja tu wanahiphop wenyewe ndo wamekubali kutumika vibaya...

Mtu Kama Nash unakuta anauza albamu insta na hataki kuziweka kwenye platform zingine we unazani mtu ambaye hamjui Nash atamjuaje!? Sawa Ni swala la mapato je kwanini baada ya muda asiziachie? Mfano albamu ya diwani ya maaalim Hadi leo sijui Kama Kuna ngoma iliwahi kupigwa redioni... Hii sio nzuri kabisa msanii lazima uwe na brand... Sizani kama Tupac angejulikana angetumia hii njia... Nash mcee n msanii mkali lakini kwa staili hiyo n ngumu kuacha alama

Nmekuelewa mambo ni mengi muda hautoshi

Tumalize utata we unazani nani aachiwe kijiti cha hiphop
 
Ukipata muda chagua ngoma yake moja tu unayoikubali halafu compare na ngoma yoyote ya Fid kwenye albamu ya "VINA MWANZO KATI NA MWISHO" ilikua na haya Mapini....
1. August 13 ft. Juma nature
2. Kadi na Ua Rose ft. Jay see
3. Chagua moja ft. TID Langa & black rhino
4. Mwanangu ft Banana Zoro
5. Utaua bendi ft magazijuto
6. Vina mwanzo Kati na mwisho
7. Dunia nzima
8. Ni hayo tu ft. Langa & professor Jay
9. Unanijua unanisikia
10. Mwanza mwanza
11. Goodnite ft lady Jay dee
Hii ndio album yangu pendwa ya Fid Q,
 
Punchline Dizasta anazo chache sana huwezi kompare na hao niliowataja hata kidogo hawezi kabisa....

Ukipata muda chagua ngoma yake moja tu unayoikubali halafu compare na ngoma yoyote ya Fid kwenye albamu ya "VINA MWANZO KATI NA MWISHO" ilikua na haya Mapini....
1. August 13 ft. Juma nature
2. Kadi na Ua Rose ft. Jay see
3. Chagua moja ft. TID Langa & black rhino
4. Mwanangu ft Banana Zoro
5. Utaua bendi ft magazijuto
6. Vina mwanzo Kati na mwisho
7. Dunia nzima
8. Ni hayo tu ft. Langa & professor Jay
9. Unanijua unanisikia
10. Mwanza mwanza
11. Goodnite ft lady Jay dee

Kama ulikua tayari umeanza kusikiliza muziki hapo hamna ngoma hata moja ambayo haikuwa hit zote zilisumbua Sana top ten na pia ngoma ya "Ni hayo tu" pamoja na "mwanza mwanza" zilishinda Tuzo enzi zile kili music awards zikitamba.

Njoo album ya PROPAGANDA humo Kuna mawe si masikhara na zote zilitamba Sana kila pembe na Zina punchlines za kutisha..
Hebu pitia hii list iliyomo kwenye hiyo album ndo utaelewa nachomaanisha Nini maana ya mistari...
1.Propaganda
2.Wananiita king ft Nylon
3. Juhudi za wasio jiweza ft bi kidude
4. Utaua game ft juma nature
5. Kila siku ft Q Jay
6. Hey Lord ft Mzungu kichaa
7. Temanoleji ( Natamani kwanza wasanii wa hip-hop wangesikiliza hii ngoma kabla ya kwenda studio)
8. Mwanamalundi
9. Shimo limetema ft. AY & Ncha Kali
10. Mama ft Banana Zoro
11. Nyota ya mchezo ft Doreen
12. Usinikubali haraka ft matonya
13. Ripoti za mtaani ft Zahiri Zoro
14. Nilipotoka
15. Danger

Kiukweli Mimi Ni shabiki wa Dizasta Tena nina ngoma zake kwenye simu na hua namsikiliza Ila Kuna vitu vingi sana anamiss sahivi naona anadisiana na kina maarifa...
Kiukweli bado ana safari sana... ukiacha track ya SHAHIDI, Ngoma ya KANISA aliandika akiwa ametuliza Sana akili walau angekua kwenye hiyo class kwenye ngoma zingine Kama tano ningemshindanisha na Nikki mbishi lakini bado ajipange
Hatusemei ngoma zilizohit top ten na kusumbua. Tunazungumzia puchline yaani mistari ya akili. Ya kufikirisha. Ukiona ngoma imebamba sana, yaani imwhit jua kuna. Mashairi yake mepesi yanaeleweka kirahisi au yana beat la kuvibe. Dizasta Album zake zote mbili haziko hivyo, ndiyo maana hajahit kwenye hizo top ten.

Na kama nyimbo kali za Dizasta unaona ni Shahidi na Kanisa basi hujamsikiliza, umemsikiliza kimeinstream. Hizo ndizo wengi wanazizungumzia. Nyimbo za Dizasta zinatisha. Ile Ndoa ndoano huwezi sikiliza na mkeo. Hatia II huwezi sikiliza na manzi wako. Sikiliza Kikaoni anavyoomba kuuliwa. Sikiliza Yuleyule, sikiliza Harder. Siwezi elezea zote, kila wimbo wake unafikirisha.

Na hajamdiss mtu. Kamuelekeza tu. Ukitaka kuona jamaa akichafukwa anakuwaje kasikilize No body is Safe 2. Fid q ni legend, lakini tunapokuja kwenye mistari ya kufikirisha, yaani mizito. Hamgusi Dizasta.
 
Hio ipo kwenye album ya Fid Q inaitwa VINA MWANZO KATI NA MWISHO niliweka nyimbo zake zote kichwani kila ngoma nilikua nachana hata ukiniwekea beat kavu na-flow na sitoki nje ya beat, enzi hizo album inatoka mahome tunatumia Radio Cassatte bro akanizawadia Tape kilichofuata ni hakuna kuruka nyimbo maana nyimbo zote kali
Hatari mwannagu mi nilikua napenda verse ya Langa japokua wote waliua Sana...
1. Fid Q "mi kujiita Rasta wenye chuki eti wanapinga.. wanashangaa nakula nyama hawajui nyota yangu Ni ya Simba"..
2. Professor Jay " nilichuna wakati wa kwenda Ila Sasa narudi nikanyage bahati mbaya nikulipue makusudi"

3. Kwa heshima ya Langa ntaandika verse nzima...
natumia akili ustaarabu na subira,
situmii nguvu jaziba na hasira,
mapinduzi daima msimamo ka Che Guevara,
usingizi ndugu yake kifo sipendi kulala,
nafata mipango yangu sifati mipango ya wengine Niko focused hata ilibidi vingine nijinyime,
wote tukiwa masikini Nani atamsaidia mwenzake,
acheni niwini majungu msinipake,
wanasema nime-change eti so Mimi wa zamani,
sionekani maskani kwa darubini Wala miwani,
lawama kibao utazani mahakamani,
mi nisipohangaika atakaenilisha Nani?
wanichekea usoni kisogoni wananisema,
wanatafuta mabaya wanajifanya wahaoni mema,
kisichoniua kitanikomaza kiaskari,
unavonichukia unadhihirisha mi mkali,
Sina haja ya kurudia Fid Alisha waambia,
u-superstar ! mzigo wa mwiba ukiubeba unaumia.." da noma
RIP Lyrical And Natural Gifted Artist LANGA
 
Noma sana hio ngoma mkuu,
 
Kwa PMawenge bwana Disasta bado hamfikii, nyimbo za story alizoandika P zinaelimisha, zinafunza na zina ujumbe mwingi, ukitaka kunielewa vizuri sikiliza PMawenge - Mama Mjane utanielewa namaanisha nini

Alafu pia nilimfuatilia kuna kipindi fulani cha TV alikua anaruka kipindi kikiwa kinaisha sasa hivi hakiruki tena hewani kilikua kinaonyeshwa Star Tv I think alikua anachana story yenye mpangilio wa beti na vina tu mwanzo mwisho sijakumbuka ni kipindi kipi, oi emu acheni kutumix

Mwambieni dogo Disasta akaze sana kwenye gemu msimleweshe misifa mnamuaribu,

Baba ukitaka mwanao apate 100% km akipata 99% mtie makonzi na mabanzi sana mwambie wewe ni mjinga wa mwisho umeshindaje kupata 100%? Next time dogo atakuja na 100%

P.mawenge best story telling songs kwangu ni
-mama mjane
-baba msaliti
-afande msela
-Huna jipya
-Binti

Kuna nyingine alimuimbia msela wake alifariki nmeisahau jina.Naheshimu sana uwezo wake pia🫡
 
Walau Lunduno members/Tamaduni music ndo wasanii wangu wa mwisho kabisa baada ya hapo sitaki kabisa kusikiliza kizazi kilichofata....

Msikilize Bando mc anakwambia eti "demu wako akilala na Dera jua Kuna mtu anaenda kuchambwa ndotoni" Sasa kweli huu Ni mstari????

Kwenye ngoma ya TEMANOLEJI ya Fid Kuna mstari anasema "nikisikiliza hip-hop ya bongo si-gain na-lose vitu/ mamc wote waongo na wananiiuzi kilasiku... Mistari Yao Ni Kama mfano wa kile kisichofaa kuandikwa/ sauti zao si za michano walipaswa wajiunge misifa...."

Jamani jamani hip-hop bongo imekosa watu kabisa Kama young Lunya anaonekana n msanii bora wa hip-hop si Ni aibu kwa taifa
Mkuu Dizasta, Kadgo, Ghetto, Boshoo, Kinya, Nala nk. yani hao wote niliokutajia wote ni products ya tamaduni

Tamaduni imezalisha wasanii wengi sana na wengine hata hawajulikani ila hakujawahi kuwa na msanii mbovu kwenye hilo kundi.

Bando Mc ni huyu ni msanii wa Stamina na sijawahi kumuelewa uchanaji wake

Huyu na Nacha mara nyingi nawaona ni watu ambao wanafanya plagiarism kwa kumuiga Songa aina yake ya uchanaji

Songa ana aina yake ya upekee ya uchanaji kwa kucheza na maneno ambayo yanafikirisha sana.

"Hii ndio new carrier, Songa ni mkubwa akisimama hakuna wa kuukalia

"Hakuna wa kusalia, duniani hakufai ndio maana ukizaliwa tu unalia"

Sasa kina Nacha wakiimba wanakosa ubunifu wa kuifanya verse ilete maana zaidi zaidi inaonekana ameifanya tu ili kutafuta vina

Halafu kingine ukisema Fid Q hata mimi binafsi nishabiki wake, ila Fid Q naye mkubali mimi kuanzia yule Fid Q aliyetoa ngoma ya Sumu kushuka miaka ya chini

Lakini huku kwa kina Christian Bella na Fresh aliyopiga na WCB pale nimemvua vyeo though he's my GOAT

Young Lunya mara nyingi namskia humu JF na mtaani kwenye saluni zenye kelele kelele

Huyu nilishawahi kusema ni mpayukaji hajui kuchana watu wakawa wanataka kumfananisha na P Mawenge kiuwezo

Nikawaambia kipimo kiwe ngoma ambayo kila mmoja amewahi kuifanya

Ambapo ni ile Yes Bana challenge ambayo P aliifanya na huyo Lunya naye aliifanya

Ukiisikilza yes bana ya P utaona hata Khali graph hakuitendea haki nyimbo yake

Ukimsikiza Lunya utaona ni msanii ambaye yupo tayati kuimba chochote ili mradi tu mwishoni amalize na kina ambacho alianza nacho

Na pamoja na hilo bado kuna verse hazikuwa na vina, lakini cheki za P kila angle ameua.
 
Ni kweli P.mawenge ni mada ya siku nyingne

Katika list yako hawa new generation product ya tamaduni bahati nzuuri nmefatilia wote from the scratch

Wote wana aina yao tofauti ya uchanajibna uandishi

Mfano Kadgo na boshoo naweza sema ndo wakali wa freestyle kwa sasa yaani man to man madogo wako vizuri

Lakini the black maradona anabaki kuwa Lyricist bora!
 
Mkuu Dizasta, Kadgo, Ghetto, Boshoo, Kinya, Nala nk. yani hao wote niliokutajia wote ni products ya tamaduni

Tamaduni imezalisha wasanii wengi sana na wengine hata hawajulikani ila hakujawahi kuwa na msanii mbovu kwenye hilo kundi.

Bando Mc ni huyu ni msanii wa Stamina na sijawahi kumuelewa uchanaji wake

Huyu na Nacha mara nyingi nawaona ni watu ambao wanafanya plagiarism kwa kumuiga Songa aina yake ya uchanaji

Songa ana aina yake ya upekee ya uchanaji kwa kucheza na maneno ambayo yanafikirisha sana.

"Hii ndio new carrier, Songa ni mkubwa akisimama hakuna wa kuukalia

"Hakuna wa kusalia, duniani hakufai ndio maana ukizaliwa tu unalia"

Sasa kina Nacha wakiimba wanakosa ubunifu wa kuifanya verse ilete maana zaidi zaidi inaonekana ameifanya tu ili kutafuta vina

Halafu kingine ukisema Fid Q hata mimi binafsi nishabiki wake, ila Fid Q naye mkubali mimi kuanzia yule Fid Q aliyetoa ngoma ya Sumu kushuka miaka ya chini

Lakini huku kwa kina Christian Bella na Fresh aliyopiga na WCB pale nimemvua vyeo though he's my GOAT

Young Lunya mara nyingi namskia humu JF na mtaani kwenye saluni zenye kelele kelele

Huyu nilishawahi kusema ni mpayukaji hajui kuchana watu wakawa wanataka kumfananisha na P Mawenge kiuwezo

Nikawaambia kipimo kiwe ngoma ambayo kila mmoja amewahi kuifanya

Ambapo ni ile Yes Bana challenge ambayo P aliifanya na huyo Lunya naye aliifanya

Ukiisikilza yes bana ya P utaona hata Khali graph hakuitendea haki nyimbo yake

Ukimsikiza Lunya utaona ni msanii ambaye yupo tayati kuimba chochote ili mradi tu mwishoni amalize na kina ambacho alianza nacho

Na pamoja na hilo bado kuna verse hazikuwa na vina, lakini cheki za P kila angle ameua.
Da mwamba Sina la kuongeza ndo maana nikasema baada ya Tamaduni hamna Tena wengine... Sema boshoo sizani Kama n mmoja wa Tamaduni labda Kama amekuja baadae maana enzi zile za kina getto ambassador... Boshoo sijui Kama Alikua kamaliza shule...
All in all umetisha Sana Fid wa sumu kurudi chini Alikua mnyama Sana sema hizi kina freshi Ni za kujitafutia tu mafao Ni Kama CR 7 kule saudia...

Yap duniani hakufai ndo maana ukizaliwa tu unalia....
Hii ndo ngoma ya Songa nayoipenda zaidi akiwa na Dado Hisia za moyoni......
 
Kwanza nimefurahi sana kuona kwa hili wazo lako la kumwanzishia Uzi huyu mwamba

Nilikuwa naomba Kama ikiwezekana updates zote za dizasta tuzikute hapaaa

Huyu jamaa ni genius, mchafu, hafai, anatisha, anafikilisha, anafurahisha, anaelimisha he's a full package

Mdogo wenu raptcha nadhani hata hajatoka matanga uko
 
P.mawenge best story telling songs kwangu ni
-mama mjane
-baba msaliti
-afande msela
-Huna jipya
-Binti

Kuna nyingine alimuimbia msela wake alifariki nmeisahau jina.Naheshimu sana uwezo wake pia🫡
Io ngoma aliyo muimbiaa mshikaji wake ukiikumbuka weka hapa, maana kuna goma lake nalitafuta sana sema sijui linaitwaje ila ina kisa cha namna io.

Sent from my CPH1989 using JamiiForums mobile app
 
Hatari mwannagu mi nilikua napenda verse ya Langa japokua wote waliua Sana...
1. Fid Q "mi kujiita Rasta wenye chuki eti wanapinga.. wanashangaa nakula nyama hawajui nyota yangu Ni ya Simba"..
2. Professor Jay " nilichuna wakati wa kwenda Ila Sasa narudi nikanyage bahati mbaya nikulipue makusudi"

3. Kwa heshima ya Langa ntaandika verse nzima...
natumia akili ustaarabu na subira,
situmii nguvu jaziba na hasira,
mapinduzi daima msimamo ka Che Guevara,
usingizi ndugu yake kifo sipendi kulala,
nafata mipango yangu sifati mipango ya wengine Niko focused hata ilibidi vingine nijinyime,
wote tukiwa masikini Nani atamsaidia mwenzake,
acheni niwini majungu msinipake,
wanasema nime-change eti so Mimi wa zamani,
sionekani maskani kwa darubini Wala miwani,
lawama kibao utazani mahakamani,
mi nisipohangaika atakaenilisha Nani?
wanichekea usoni kisogoni wananisema,
wanatafuta mabaya wanajifanya wahaoni mema,
kisichoniua kitanikomaza kiaskari,
unavonichukia unadhihirisha mi mkali,
Sina haja ya kurudia Fid Alisha waambia,
u-superstar ! mzigo wa mwiba ukiubeba unaumia.." da noma
RIP Lyrical And Natural Gifted Artist LANGA
Sawa Fid apewe heshima yake sema mahaba kwa mwamba yamezidi sana mpaka unaharibu.

1. Fid Q "mi kujiita Rasta wenye chuki eti wanapinga.. wanashangaa nakula nyama hawajui nyota yangu Ni ya Simba"

Sent from my CPH1989 using JamiiForums mobile app[/URL
 
Kwa PMawenge bwana Disasta bado hamfikii, nyimbo za story alizoandika P zinaelimisha, zinafunza na zina ujumbe mwingi, ukitaka kunielewa vizuri sikiliza PMawenge - Mama Mjane utanielewa namaanisha nini

Alafu pia nilimfuatilia kuna kipindi fulani cha TV alikua anaruka kipindi kikiwa kinaisha sasa hivi hakiruki tena hewani kilikua kinaonyeshwa Star Tv I think alikua anachana story yenye mpangilio wa beti na vina tu mwanzo mwisho sijakumbuka ni kipindi kipi, oi emu acheni kutumix

Mwambieni dogo Disasta akaze sana kwenye gemu msimleweshe misifa mnamuaribu,

Baba ukitaka mwanao apate 100% km akipata 99% mtie makonzi na mabanzi sana mwambie wewe ni mjinga wa mwisho umeshindaje kupata 100%? Next time dogo atakuja na 100%
nakubaliana na wewe, kifupi P anayo ladha ya kisanii. Ukiona unasikiliza nyimbo then hauwezi hata kunesa nesa jua hamna kitu hapo.

Sikiliza nyimbo kama Hunajipya ya P, japo ni storytelling ila uta nesa tu. Sasa Dizasta yeye anafanya mahubiri kama mziki haburudishi kabisa wakati lengo la kwanza la mziki ni kuburudisha.

Bado ana safari ndefu akitaka kufika mbali
 
IMG_0400.png

Mpaka leo jioni “Best friend”

Ilikwa No.2 top searched song BoomPlay

Numbers don’t lie
 
IMG_0403.png

Top Searched Artist No.10

“Mwanza na Dodoma Zinasikika singo napo-dribble mtaani wananiita black Maradona.

I am ready I was ready I've born ready men/

Choose beautiful start or choose scary end/

Ka' ulisikia mi sifai hii ni evidence/
Kibaha maili noja mi' ni eight miles Eminem”
 
View attachment 2476794

Salamu wana sio kwema nilikotoka,/

Ninatema ngumu mpaka sio vyema kuokota,/

Nikitema nawa...kosha,

Wanatamani niwe nabii sema suna wema wa kutosha,

Round kwenye jiji nasign madeal wima,

Matatizo kibao na bado still nina
Punchlines na flows ma-style ma-skill ting'a,

Sipo chimbo nipo period nableed vina..

Nobody is Safe 2
 
Back
Top Bottom