Dizasta Vina a.k.a Maradona

Dizasta Vina a.k.a Maradona

Labda nimefilisika kimawazo ila wasanii wa hip-hop wa kizazi hiki hua wahanikoshi kabisa coz ngoma nzima unakuta hakuna mistari ambayo inakuacha na tafakuri nzito tofauti na wale niliokua nawakubali zamani...
Mfano nikikiliza ngoma za Fid q jamaa Alikua anaandikia ngoma flani yenye misemo ambayo inakugusa kinyama.. we kasilikze tu Mwanza mwanza, ielewe mitaa, sumu, fid Q dot com Rudi Hadi Ni hayo tu au propaganda... Wasanii wa sikuhizi hawana ile mistari Ila Ni Visa vingi tu....
Mchukilie mtu Kama Langa jamaa walikua wanaandika Sana yaani anatoa neno linalobamba tz nzima mfano "matawi ya juu" au msikilize Langa kwenye ngoma ya HIP-HOP utampenda. Sikuhizi hip-hop imekua Kama taarabu...
Kiukweli hawanibambi...
Dizasta Ni msimuliaji mzuri lakini Kuna kitu anapungukiwa uandishi wake bado sana compare to malegend wa hip-hop...
Angalau kwenye ngoma ya kanisa alijitahidi
I'm so sorry Ni mtazamo wangu naomba uheshimiwe
Umeheshimiwa.

Sent from my CPH1989 using JamiiForums mobile app
 
Nimesikiliza Hatia III jamaa anaenda off beat yaan hata Azma anamfunika mnamuover rate sana ndio maana hatoboi, wapi Kontawa? Hadi wamama wa kitaa wanaiimba Champion, mwambieni aendelee kukaza alafu anate na beat sio anatokatoka nje ya beat

Tafuta wimbo wa NF - STORY ingia YouTube ucheck utanielewa nazungumzia nini
Orthodox flow, and unorthodox flow
 
Labda nimefilisika kimawazo ila wasanii wa hip-hop wa kizazi hiki hua wahanikoshi kabisa coz ngoma nzima unakuta hakuna mistari ambayo inakuacha na tafakuri nzito tofauti na wale niliokua nawakubali zamani...
Mfano nikikiliza ngoma za Fid q jamaa Alikua anaandikia ngoma flani yenye misemo ambayo inakugusa kinyama.. we kasilikze tu Mwanza mwanza, ielewe mitaa, sumu, fid Q dot com Rudi Hadi Ni hayo tu au propaganda... Wasanii wa sikuhizi hawana ile mistari Ila Ni Visa vingi tu....
Mchukilie mtu Kama Langa jamaa walikua wanaandika Sana yaani anatoa neno linalobamba tz nzima mfano "matawi ya juu" au msikilize Langa kwenye ngoma ya HIP-HOP utampenda. Sikuhizi hip-hop imekua Kama taarabu...
Kiukweli hawanibambi...
Dizasta Ni msimuliaji mzuri lakini Kuna kitu anapungukiwa uandishi wake bado sana compare to malegend wa hip-hop...
Angalau kwenye ngoma ya kanisa alijitahidi
I'm so sorry Ni mtazamo wangu naomba uheshimiwe
Inategemeana u aposema Hip Hop ya siku hizi unakusudia wasanii gani

Kama ni hawa mainstream basi uko sahihi ila ukija underground hivyo vyote ulivyovitaja vipo

Kama umeisikiliza The Verteller ya Dizasta utaona lines fikirishi zimeanza kwenye ngoma ya kwanza ile intro mpaka unaifikia tatuu ya asili kote huko ame spit tungo tata

Achana na hizo

Kamsikilize Kinya Mistari, Nala Mzalendo, na dogo Boshoo japo siku hizi ameanza mitindo ya kina Lunya ila decent songs ziko vyema.
 
Labda nimefilisika kimawazo ila wasanii wa hip-hop wa kizazi hiki hua wahanikoshi kabisa coz ngoma nzima unakuta hakuna mistari ambayo inakuacha na tafakuri nzito tofauti na wale niliokua nawakubali zamani...
Mfano nikikiliza ngoma za Fid q jamaa Alikua anaandikia ngoma flani yenye misemo ambayo inakugusa kinyama.. we kasilikze tu Mwanza mwanza, ielewe mitaa, sumu, fid Q dot com Rudi Hadi Ni hayo tu au propaganda... Wasanii wa sikuhizi hawana ile mistari Ila Ni Visa vingi tu....
Mchukilie mtu Kama Langa jamaa walikua wanaandika Sana yaani anatoa neno linalobamba tz nzima mfano "matawi ya juu" au msikilize Langa kwenye ngoma ya HIP-HOP utampenda. Sikuhizi hip-hop imekua Kama taarabu...
Kiukweli hawanibambi...
Dizasta Ni msimuliaji mzuri lakini Kuna kitu anapungukiwa uandishi wake bado sana compare to malegend wa hip-hop...
Angalau kwenye ngoma ya kanisa alijitahidi
I'm so sorry Ni mtazamo wangu naomba uheshimiwe
Kwenye punchlines za kufikirisha hata hao malegend hawamfikii Dizasta. Ukimsikiliza kama hautoshi huwezi kumuelewa. Sema tu inatupasa kuwaheshimu kwa ulegend wao.
 
Dizasta ameua mende kwa bunduki

Rapcha hamuwezi chochote vina
Uandishi, rhymes, flows, vina, punchlines

Hii best friend labda ipambanishe na futi 6 ya mawenge
 
Nmekwambia Azma akiwekwa na Disasta mimi nampa Azma, sasa rapper mkali unaendaje off beat?

Pigo hizo kuna madogo walifukuzwa kwenye radio wanajifanya marapper wanapewa beat wanapuyanga, sikiliza hio Hatia III utanielewa nazungumzia nini yupo off beat kabisa alafu nyinyi ndio mnaoharibu wasanii kusifia hata visivyostahiri kusifiwa
Mkuu katika maisha huwezi kupendwa na kila mtu hilo linajulikana vizuri kabisa kwahiyo hatuwezi kushangaa unavokuja na cheap reasons ili kushusha uwezo wa Dizasta vina

Katika sanaa yoyote ile kuna kitu kinaitwa ushabiki, mtu anaweza akawa na uwezo mkubwa sana ila tu wewe asikuvutie kuwa shabiki wake na wala sio dhambi ila at least heshimu uwezo wake

Zababu za kusema kuwa Dizasta vina anashindwa kunata na beat ni ujinga wa kiwango cha Lami, umeskliza nature ya hiyo beat? Umeskliza mtindo alioamua kuutumia katika hiyo beat? Au ilimradi tu nawewe umekuja kuandika ili tujue waga unaskilizaga hip-hop

Dizasta vina ndie msanii wa hip hop ambae anatumia beat ngumu kuliko msanii yoyote yule bongo, kaskilize beat zote za Hatia kuanzia 1-5 ndio utajua na hizo beat hakuna msanii wa ajabu ajabu anaweza kupita nazo lazima azitwist

Dizasta vina ndio msanii peke ambae yupo Underground stream mwenye nyimbo nyingi kuliko wasanii wote wa underground stream akiwemo Azma, Dizasta ndio msanii pekee ambae yupo Underground stream lakini ana nyimbo nyingi kuliko almost wasanii wote wa hip hop walio Mainstream

Na hiyo yote kwa sababu jamaa kuandika kwake halijawahi kuwa tatizo ata siku moja kama ilivo kwa MCs wengine wengi, kaskilize Album ya the verteller ndio utajua kwanini Dizasta vina anakuwa high rated kama msanii Bora

With all due respect to Azma, ila Dizasta ni maji marefu sana kwa mshkaji, labda tu nikuulize Umewahi kuona Uzi ambao unamuongelea Azma? Kama hapana unahisi ni kwa sababu gani? Na je umeona nyuzi ngapi humu zinaongelea uwezo wa Dizasta vina kama jibu ni ndio je unahisi kwanini?

Katafute msanii yoyote mkubwa wa hip-hop bongo muulize wasanii wake 5-10 Bora wa hip-hop Kwa sasa Bongo asipomtaja Dizasta vina njoo na uthibitisho nikupe 50k

Kwahiyo hawa wote hapa chini wao hawajui muziki ila wewe ndio fundi au sio?
IMG_20230110_102747.jpg
Screenshot_2023-01-10-10-27-17-331_com.instagram.android.jpg
IMG_20230110_085700.jpg
IMG_20230110_085633.jpg
IMG_20230110_085558.jpg
 
umeskliza nature ya hiyo beat? Umeskliza mtindo alioamua kuutumia katika hiyo beat?
Beat nmesikiliza ambapo hata mimi naweza kutembea nayo bila kutokatoka nje ya beat ndio maana nikasema akipewa Azma anamtosha kumkalisha kutembea na hio beat bila kutoka nje ya beat namaanisha kunata na beat sio beat inaenda kushoto wewe unaenda kulia, hapo sijamtaja Moko wa Miujiza, PMawenge, Stereo, NikiMbishi, FidQ, Songa, Zaiid, CJaMoka, Conboi, Raptcha, Wakazi, Troubado Joji, Maalim Nash Mc

Mwambie atembee na beat km Bruno Mars mbon Msaga Sumu na Shoro Mwamba wananata na beat za Singeli, hio Hatia III angejua angefungia tu ndani kazidiwa hadi na Dulla Makabila, atembee na beat km anavyofanya Kontawa yaan anashindwa kujifunza kwa Mwana FA & AY, mwambie aende kwa Prof J ampe Darasa na Bill Nass

Yaan huyo rapper wenu hata Magazijuto hamfikii
 
Kwahiyo hawa wote hapa chini wao hawajui muziki ila wewe ndio fundi au sio?
Mzee nikwambie kitu kuhusu music industry nobody wants to disappoint anybody sababu watu wanaongea pale wanaponyimwa support kwa hio kuweka appreciation kwenye Insta yangu kua Disasta anafanya vyema simaanishi anafanya vyema kwenye kila kazi anayoitoa, elewa point nimesema jamaa kazi ya Hatia III kaiharibu ilibidi atembee na beat sijasema kwamba hana kazi nzuri alizowahi kuzitoa Ila hio Hatia III kaharibu simjui producer alietengeneza beat na kuproduce huo wimbo na kufanya mastering & mix Ila verse alipoingiza kabolonga yupo Off beat

Ukiona mtu anakukosoa means ameona uwezo wako ni kiasi gan na unaweza kufanya nini na kufika wapi na anataka u-Push zaidi ili ung'ae sio unasifiwa kijingajinga na wewe ulivyo mjinga unalewa sifa wakati kazi zingine unatoa mbovu, ukitaka msanii uwake na uwike make sure haya makando kando ya kazi mbovu unayaacha ndani usitoe ngoma mbovu narudia tena usitowe kazi mbovu hata moja huku street watu wanaujua mziki kuliko unavyoujua wewe, sio unaimbaimba tu unaishia kuimbia wanao wa mtaani kwenu nyumba mbili tatu basi umenasa hapo,

Street people need content za maana na zenye kujenga unaimba na kucheza na unahifadhi ujumbe they need something new sio unatuimbiaimbia unaenda off beat alafu tunakuchekea kuna madogo wanakimbiza vibaya Ila hawana majina alafu wewe unatuimbiaimbia off beat, hivi mfano ukisikiliza wimbo Nash Mc - Kaka Suma unajisikiaje anaenda off beat?

Hio Hatia III imeniuma sababu producer katengeneza beat nzuri sana na yeye mistari ameandika mizuri Ila jamaa kwenye kuingiza vocal kaenda Off beat yaan beat inaenda huku na yeye anaenda huku, so sad
 
Okay brother...!
 
Mzee nikwambie kitu kuhusu music industry nobody wants to disappoint anybody sababu watu wanaongea pale wanaponyimwa support kwa hio kuweka appreciation kwenye Insta yangu kua Disasta anafanya vyema simaanishi anafanya vyema kwenye kila kazi anayoitoa, elewa point nimesema jamaa kazi ya Hatia III kaiharibu ilibidi atembee na beat sijasema kwamba hana kazi nzuri alizowahi kuzitoa Ila hio Hatia III kaharibu simjui producer alietengeneza beat na kuproduce huo wimbo na kufanya mastering & mix Ila verse alipoingiza kabolonga yupo Off beat

Ukiona mtu anakukosoa means ameona uwezo wako ni kiasi gan na unaweza kufanya nini na kufika wapi na anataka u-Push zaidi ili ung'ae sio unasifiwa kijingajinga na wewe ulivyo mjinga unalewa sifa wakati kazi zingine unatoa mbovu, ukitaka msanii uwake na uwike make sure haya makando kando ya kazi mbovu unayaacha ndani usitoe ngoma mbovu narudia tena usitowe kazi mbovu hata moja huku street watu wanaujua mziki kuliko unavyoujua wewe, sio unaimbaimba tu unaishia kuimbia wanao wa mtaani kwenu nyumba mbili tatu basi umenasa hapo,

Street people need content za maana na zenye kujenga unaimba na kucheza na unahifadhi ujumbe they need something new sio unatuimbiaimbia unaenda off beat alafu tunakuchekea kuna madogo wanakimbiza vibaya Ila hawana majina alafu wewe unatuimbiaimbia off beat, hivi mfano ukisikiliza wimbo Nash Mc - Kaka Suma unajisikiaje anaenda off beat?

Hio Hatia III imeniuma sababu producer katengeneza beat nzuri sana na yeye mistari ameandika mizuri Ila jamaa kwenye kuingiza vocal kaenda Off beat yaan beat inaenda huku na yeye anaenda huku, so sad
Okay brother...!
 
Mkuu katika maisha huwezi kupendwa na kila mtu hilo linajulikana vizuri kabisa kwahiyo hatuwezi kushangaa unavokuja na cheap reasons ili kushusha uwezo wa Dizasta vina

Katika sanaa yoyote ile kuna kitu kinaitwa ushabiki, mtu anaweza akawa na uwezo mkubwa sana ila tu wewe asikuvutie kuwa shabiki wake na wala sio dhambi ila at least heshimu uwezo wake

Zababu za kusema kuwa Dizasta vina anashindwa kunata na beat ni ujinga wa kiwango cha Lami, umeskliza nature ya hiyo beat? Umeskliza mtindo alioamua kuutumia katika hiyo beat? Au ilimradi tu nawewe umekuja kuandika ili tujue waga unaskilizaga hip-hop

Dizasta vina ndie msanii wa hip hop ambae anatumia beat ngumu kuliko msanii yoyote yule bongo, kaskilize beat zote za Hatia kuanzia 1-5 ndio utajua na hizo beat hakuna msanii wa ajabu ajabu anaweza kupita nazo lazima azitwist

Dizasta vina ndio msanii peke ambae yupo Underground stream mwenye nyimbo nyingi kuliko wasanii wote wa underground stream akiwemo Azma, Dizasta ndio msanii pekee ambae yupo Underground stream lakini ana nyimbo nyingi kuliko almost wasanii wote wa hip hop walio Mainstream

Na hiyo yote kwa sababu jamaa kuandika kwake halijawahi kuwa tatizo ata siku moja kama ilivo kwa MCs wengine wengi, kaskilize Album ya the verteller ndio utajua kwanini Dizasta vina anakuwa high rated kama msanii Bora

With all due respect to Azma, ila Dizasta ni maji marefu sana kwa mshkaji, labda tu nikuulize Umewahi kuona Uzi ambao unamuongelea Azma? Kama hapana unahisi ni kwa sababu gani? Na je umeona nyuzi ngapi humu zinaongelea uwezo wa Dizasta vina kama jibu ni ndio je unahisi kwanini?

Katafute msanii yoyote mkubwa wa hip-hop bongo muulize wasanii wake 5-10 Bora wa hip-hop Kwa sasa Bongo asipomtaja Dizasta vina njoo na uthibitisho nikupe 50k

Kwahiyo hawa wote hapa chini wao hawajui muziki ila wewe ndio fundi au sio?View attachment 2476038View attachment 2476040View attachment 2476041View attachment 2476042View attachment 2476043

Umeandika Vizuri sanaaaaaa

Naomba niquote haya maneno kwa herufi kubwa

“MSANII ANAWEZA KUWA MKALI LKN USIWE SHABIKI YAKE….HAINA MAANA UBEZE UWEZO WAKE”

Wakati naanzisha hii thread nlitaman sana watokee watu angalau wawili wanaifatilia hiphop na kumjua dizasta

Ili tu appreciate kitu alicho nacho jamaa

I got respect for you
Maelezo yamenyooka sana
Beat anazopita nazo Dizasta ni ngumu sana kwa msanii mwingine kupita.kwangu beat ambazo ni nyepesi labda
-siku mbaya
-mwanajua
-Baunsa
-mlemavu

Ila nyingi zilizobaki unahitaji pumzi/flow nzuri
 
Labda nimefilisika kimawazo ila wasanii wa hip-hop wa kizazi hiki hua wahanikoshi kabisa coz ngoma nzima unakuta hakuna mistari ambayo inakuacha na tafakuri nzito tofauti na wale niliokua nawakubali zamani...
Mfano nikikiliza ngoma za Fid q jamaa Alikua anaandikia ngoma flani yenye misemo ambayo inakugusa kinyama.. we kasilikze tu Mwanza mwanza, ielewe mitaa, sumu, fid Q dot com Rudi Hadi Ni hayo tu au propaganda... Wasanii wa sikuhizi hawana ile mistari Ila Ni Visa vingi tu....
Mchukilie mtu Kama Langa jamaa walikua wanaandika Sana yaani anatoa neno linalobamba tz nzima mfano "matawi ya juu" au msikilize Langa kwenye ngoma ya HIP-HOP utampenda. Sikuhizi hip-hop imekua Kama taarabu...
Kiukweli hawanibambi...
Dizasta Ni msimuliaji mzuri lakini Kuna kitu anapungukiwa uandishi wake bado sana compare to malegend wa hip-hop...
Angalau kwenye ngoma ya kanisa alijitahidi
I'm so sorry Ni mtazamo wangu naomba uheshimiwe

Sawa nazani kabla ya dizasta nliwasikiza sana akina
-fid q
-nikki mbishi
-one incredible
-stereo
-nash emcee
-p mawenge
-stamina

Lakini toka nmeanza kumsikiza dizasta pale tamaduni
Jamaa amekuja na kitu tofauti kuliko wote apo juu

Aina ya uandishi,story zake na flow!

Kwasasa watu ambao nawafatilia sana ni
1.Dizasta
2.young killer
3.G.H.A.F.L.A
4.Boshoo
5.Nacha
6.Toxic

Hawa marapper wengne akina Lunya,Rapcha ni vibes na flow tu hakuna.nachopata nkisiza ngoma zao
 
Nataka siku moja nione diss tracks kati ya P na Dizasta

Aisee itakuwa ni burudani sana

Weusi wangekuwa na contents walikuwa ni kundi lenye kuleta ushindani mkubwa sana kwa Kikosi Kazi.

Mi nilipenda sana ule msimu wa ma diss yani game linachangamka mizuka mingi mpaka unafurahi
Dizasta atatia huruma, ujue P kachangamka alafu hachagui chagui maneno ili aonekane yupo deep/concious kama anavyofanya Dizasta.
 
Kwa PMawenge bwana Disasta bado hamfikii, nyimbo za story alizoandika P zinaelimisha, zinafunza na zina ujumbe mwingi, ukitaka kunielewa vizuri sikiliza PMawenge - Mama Mjane utanielewa namaanisha nini

Alafu pia nilimfuatilia kuna kipindi fulani cha TV alikua anaruka kipindi kikiwa kinaisha sasa hivi hakiruki tena hewani kilikua kinaonyeshwa Star Tv I think alikua anachana story yenye mpangilio wa beti na vina tu mwanzo mwisho sijakumbuka ni kipindi kipi, oi emu acheni kutumix

Mwambieni dogo Disasta akaze sana kwenye gemu msimleweshe misifa mnamuaribu,

Baba ukitaka mwanao apate 100% km akipata 99% mtie makonzi na mabanzi sana mwambie wewe ni mjinga wa mwisho umeshindaje kupata 100%? Next time dogo atakuja na 100%
 
Dizasta atatia huruma, ujue P kachangamka alafu hachagui chagui maneno ili aonekane yupo deep/concious kama anavyofanya Dizasta.
Wote nawakubali kwa lyrical ila P kwenye diss ni mtu mwingine kabisa

Angalia kwenye ile "Kazini" alivyowapitia Weusi, njoo kwenye "Future Wife" na "Mmalizaji Luku"

Hapo sijaihesabia 6ft

Yani ni kama diss ndio eneo lake huyu jmaa
 
Kwa PMawenge bwana Disasta bado hamfikii, nyimbo za story alizoandika P zinaelimisha, zinafunza na zina ujumbe mwingi, ukitaka kunielewa vizuri sikiliza P The Mc - Mama Mjane utanielewa namaanisha nini

Alafu pia nilimfuatilia kuna kipindi fulani cha TV alikua anaruka kipindi kikiwa kinaisha sasa hivi hakiruki tena hewani kilikua kinaonyeshwa Star Tv I think alikua anachana story yenye mpangilio wa beti na vina tu mwanzo mwisho sijakumbuka ni kipindi kipi, oi emu acheni kutumix

Mwambieni dogo Disasta akaze sana kwenye gemu msimleweshe misifa mnamuaribu,

Baba ukitaka mwanao apate 100% km akipata 99% mtie makonzi na mabanzi sana mwambie wewe ni mjinga wa mwisho umeshindaje kupata 100%? Next time dogo atakuja na 100%
P alisign na kile kipindi cha daladla kilichokuwa kinaendeshwa na kiroboto

Ulivyokuja utawala wa Magu ulikuja kuondoa kile kipindi kutokana na ukosoaji wa wadau kuhusu serikali

P alikuwa kila wiki anaachia ngoma fupi ya 8 bars ikizidi basi 16 bars inayo dedicate mada itayojadiliwa siku hiyo.
 
Yes mkuu kipindi kilikua kimetulia sana nilipenda ile arrangement ya kipindi na segment ya P ndio nilikua naingojea sana kila nikicheck kipindi
 
Kwenye punchlines za kufikirisha hata hao malegend hawamfikii Dizasta. Ukimsikiliza kama hautoshi huwezi kumuelewa. Sema tu inatupasa kuwaheshimu kwa ulegend wao.
Punchline Dizasta anazo chache sana huwezi kompare na hao niliowataja hata kidogo hawezi kabisa....

Ukipata muda chagua ngoma yake moja tu unayoikubali halafu compare na ngoma yoyote ya Fid kwenye albamu ya "VINA MWANZO KATI NA MWISHO" ilikua na haya Mapini....
1. August 13 ft. Juma nature
2. Kadi na Ua Rose ft. Jay see
3. Chagua moja ft. TID Langa & black rhino
4. Mwanangu ft Banana Zoro
5. Utaua bendi ft magazijuto
6. Vina mwanzo Kati na mwisho
7. Dunia nzima
8. Ni hayo tu ft. Langa & professor Jay
9. Unanijua unanisikia
10. Mwanza mwanza
11. Goodnite ft lady Jay dee

Kama ulikua tayari umeanza kusikiliza muziki hapo hamna ngoma hata moja ambayo haikuwa hit zote zilisumbua Sana top ten na pia ngoma ya "Ni hayo tu" pamoja na "mwanza mwanza" zilishinda Tuzo enzi zile kili music awards zikitamba.

Njoo album ya PROPAGANDA humo Kuna mawe si masikhara na zote zilitamba Sana kila pembe na Zina punchlines za kutisha..
Hebu pitia hii list iliyomo kwenye hiyo album ndo utaelewa nachomaanisha Nini maana ya mistari...
1.Propaganda
2.Wananiita king ft Nylon
3. Juhudi za wasio jiweza ft bi kidude
4. Utaua game ft juma nature
5. Kila siku ft Q Jay
6. Hey Lord ft Mzungu kichaa
7. Temanoleji ( Natamani kwanza wasanii wa hip-hop wangesikiliza hii ngoma kabla ya kwenda studio)
8. Mwanamalundi
9. Shimo limetema ft. AY & Ncha Kali
10. Mama ft Banana Zoro
11. Nyota ya mchezo ft Doreen
12. Usinikubali haraka ft matonya
13. Ripoti za mtaani ft Zahiri Zoro
14. Nilipotoka
15. Danger

Kiukweli Mimi Ni shabiki wa Dizasta Tena nina ngoma zake kwenye simu na hua namsikiliza Ila Kuna vitu vingi sana anamiss sahivi naona anadisiana na kina maarifa...
Kiukweli bado ana safari sana... ukiacha track ya SHAHIDI, Ngoma ya KANISA aliandika akiwa ametuliza Sana akili walau angekua kwenye hiyo class kwenye ngoma zingine Kama tano ningemshindanisha na Nikki mbishi lakini bado ajipange
 
Back
Top Bottom