Diwani na M/Kiti wa Kijiji (CCM) Mbigiri-Kilosa wanapora na kuuza mashamba ya wananchi. Serikali iingilie kati suala hili

mbikagani

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
3,107
1,782
Hiki ni Kijiji cha Mbigiri kata ya Mbigiri wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro ambacho kinaoongozwa na diwani anayefahamika kwa jina la Watende Rashidi na mw/kiti wa kijiji anaitwa Jalala.

Viongozi hawa kwa pamoja wanashirikiana KUPORA na KUUZA mashamba ya wananchi katika kata hiyo.

Wanachokifanya bila woga ni kupora wananchi mashamba yao kwa kisingizio cha kuyarudisha hayo mashamba kwenye miliki ya kijiji na kisha wao kama watu binafsi kufanya mpango wa kuyauza kwa watu wanaotoka nje ya kata hiyo, na pesa zinazopatikana wanagawana wenyewe.

mpunga.jpg
mpunga.jpg
mpunga.jpg


Watu wengi walioporwa mashamba yao na mashamba yao kuuzwa, wamejaribu bila mafanikio kudai mashamba yao kwenye vyombo vya sheria.

Mtandao wao hawa viongozi ni mkubwa wakishirikiana na viongozi akiwemo mw/kiti wa CCM wa wilaya ya kilosa ndg Ameir.

Wengi miongoni mwa walioporwa mashamba yao wamejawa na hofu, kwani viongozi hao wanatumia vitisho.

Dhuruma ya viongozi hao inafahamika na mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa, lakini kwa vile mtandao wao unaongozwa na mw/kiti wa CCM wa wilaya, viongozi hao wa wilaya na mkoa wanashindwa kuwawajibisha viongozi wa kata na kijiji.

Kuna baadhi ya wananchi walioporwa mashamba yao wamefanikiwa fika ofisi ya raisi Dodoma na wamefanikiwa kurejeshewa mashamba yao. Mmoja kati ya hao ni mtu anayejulikana kwa jina la mzee Ndovu, amerejeshewa ekari zake 30 zilizoporwa na kuuzwa.

Mtandao huo wa kifisadi umediriki hata kupora shamba la ushirika wa miwa (AMCOS). Ushirika uliosajiliwa kisheria ambao unamilki ekari 499 za miwa.

Ushirika huo umekopa benki ya AZANIA kiasi cha pesa zaidi ya Tshs 580milioni na kuwekeza hapo shambani kwa kuchimba visima vya kisasa na kuotesha eneo kubwa la miwa.

Lakini kwa bahati mbaya sana mw/kiti wa CCM wilaya ya Kilosa kwa kuwatumia diwani na mw/kiti wa kijiji cha Mbigiri, wamevamia shamba hilo, kupora na kuchoma moto miwa hiyo na kuleta uharibifu mkubwa.

Na hata bwana shamba alipopelekwa kufanya tathmini ya miwa iliyochomwa, akasema miwa hiyo haina thamani yoyote. Kila mtu anamuhofia mw/kiti wa CCM wa wilaya.

Shamba hilo la ushirika lina thamani ya Tshs 900milioni, lakini mw/kiti wa CCM wa wilaya ndg Ameir kwa kushirikiana na diwani na mw/kiti wa kijiji cha Mbigiri amefanikiwa kulipata kwa Tshs 300milioni tu.

Na kwa vile huyu mw/kiti wa CCM wilaya ni mzoefu wa kupora mashamba ya wananchi (ikumbukwe waziri mkuu Majaliwa alishawai mnyang’anya shamba huyu na kuwarudishia wananchi hapa Kilosa), badala ya kutumia jina lake kwenye hilo shamba, katumia jina la ndg Tarick Suleimani.

Viongozi hawa wa kijiji, kata na hata wilaya wanamuogopa sana huyu Mw/kiti. Msaada pekee uliobaki ni kwa mkuu wa mkoa ambaye amepelekewa suala hilo na kikundi hicho cha ushirika(AMCOS) na maamuzi yanasubiriwa kutoka kwake.

Nawashauri katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru, katibu muenezi ndg Polepole na Mw.kiti wa taifa wa CCM Dr Magufuli ambao wanajinasibu kuwasaidia wananchi wa chini, wamulike macho yao kwenye wilaya hii ya Kilosa hasa kata ya Mbigiri kuna madudu ya kutisha.
 
Kijiji hicho nakikumbuka tulipoanzisha mashamba yetu kama marasta suala litafanyiwa kazi kama halina chembe chembe za chuki baada ya kunyimwa mgao!
 
Kwani hao si viongozi kupitia CCM? Kama wamepitia CCM, usiwe na shaka. Hao lazima ni wazalendo. Wewe utakuwa hujaelewa tu.

Unga mkono serikali kuanzia kitongoji mpaka Taifa, ni serikali ya kizalendo ya CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujifunze uandishi wenye staha kuchafua majina ya watu sio hekima,walau anza na neno tetesi,ama anza na nukuu chombo cha habari ama taasis iliyotoa habari.
 
Walipora uchaguzi na wananchi wakakaa kimya, yale yalikuwa maandalizi ya huu uporaji unaoendelea. Na yote haya ni malengo ya mwenyekiti wa ccm kuua mfumo wa vyama vingi, ili wananchi watawaliwe kibabe na Makada wa chama cha Mapinduzi.
 
Tujifunze uandishi wenye staha kuchafua majina ya watu sio hekima,walau anza na neno tetesi,ama anza na nukuu chombo cha habari ama taasis iliyotoa habari.

Uandishi wenye staha au uandishi wa uoga ili kuendelea kutawaliwa kibabe?
 
Tujifunze uandishi wenye staha kuchafua majina ya watu sio hekima,walau anza na neno tetesi,ama anza na nukuu chombo cha habari ama taasis iliyotoa habari.
Tetesi wakati watu wana nyaraka mkononi!
 
Hao ni wanaCCM wanaendeleza porapora,maana ni kawaida yao,walishapora kura,wakapora rambirambi na sasa ni kuporwa ardhi
 
Hapa kazi tu. Naona baada ya kuona eneo linafaa kwa kilimo chan miwa sasa wanasiasa wameanza kupora haki za watu waziwazi
 
Back
Top Bottom