Diwani mwingine (CCM Mwanza) ahamia CHADEMA

ulitaka niongozwe na serikali ya chama ambacho, kiongozi wake amefungua danguro, ameuza dawa za kulevya na katibu wake ameasi dini? kuliko hayo, tutaingia porini na tutaanza na wao maana watu wa kuondoka nao wako tayari, msione kobe ameinamisha kichwa.

Fisadi utamjua tu, tumia japo hekima kidogo kama unayo!
 
Breaking News,
Jinamizi la Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kuhamia CHADEMA sasa limehamia Mwanza.
Diwani wa Kata ya Nyampulukano, Jimbo la Sengerema Mjini amehamia Chadema leo hii, Arusha Mambo itakatisha kwa muda matangazo yake kutoka Dodoma na kuwaletea mahojiano ya moja kwa moja na Diwani huyo kutoka Mwanza.

Kama huyo diwani hana jina, weka hata la baba yake.......
 
nimeichapa hii kwa faida ya wanaotumia simu na wale ambao hawataweza kusoma maandishi vizuri ya barua ya kujiuzuruu

YAH: KUJIUZURU NAFASI YA UDIWANI KATIKA KATA YA NYAMPULUKANO SENGEREMA MJINI (W) SENGEREMA


Somo taja hapo juu lahusika nimeamua kujiuzuru nafasi ya udiwani niliyoipata kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi na nafasi zote katika chama.

Hii inatokana na kushindwa kuafikiana na mambo yanayogusa masilahi ya wananchi katika halmashauri ya (W) Sengerema mafisadi maadui wameliteka baraza. Sababu zilinifanya nijiuzuru nafasi hii ya utenaji wa halmashauri ni


  1. Kupitia madiwani wasio wazalendo kuhamisha mnada wa ng’ombe toka eneo uliopangwa kujengwa katika eneo la Ibondo Nyampulukano kuhamishia kata ya sima km 13 toka sengerema mjini
  2. Ucheleweshaji wa maksudi kuunda halmashauri ya mji wa sengerema kuanzia mwaka 1990
  3. Kuipunguzia eneo la mipaka ya mji mdogo wa sengerema bila kikao
  4. Kushindwa kuwachukulia hatua wezi waliotajwa na CAG, PPRA pamoja na maelekezo ya hatua za kisheria wachuliwe wahusika mpaka leo halijafanyika
 
Ngoma ivumayo sana ...

Ndiyo idumuyo.......

Barubaru mbona sijasikia habari ya viongozi wa vyama vingine wakihamia cuf, bali tunashuhudia wkiikimbia cuf!?

Najua hii movement 4 change itawapukutisha wengi bila kujali ni wa chama gani, iwe ccm, cuf ama adc.
 
Naamini kuna watu hawajapata usingizi kwa siku kadhaa mpaka leo, CDM ongeza Music tuwashike............M4C nouma.
 
Hadi ufike mwaka 2015 tutaona na kusikia mengi sana. Poleni CCM kwa kumpoteza kondoo, hongera Chadema kwa kuongeza kondoo.

Ila kwamtazamo wangu na jinsi hali ilivyo ccm watapoteza wanachama wengi sana hadi ifikapo 2015
 
Wadau, kwakuwa yeye ni Diwani inamaana ni kiongozi wa kata, sasa inapotokea kuwa amehama chama kimoja kwenda kingine, je nilazima ufanyike uchaguzi mwingine tena kushirikisha vyama vya siasa ?
 
mnada wanapeleka sima kwa nini kote huko?...ibondo pale panafaa sana
 
Hapa sasa nayakumbuka maneno ya MUNGU "Mavuno ni mengi wavunaji ni wachache"shime wana CDM kwa pamoja njooni shambani tuwavune toka ccm tuwaachie magugu tu
 
Tokeni kwake enyi watu wangu msishiriki dhambi zake (sikijui vizuri kifungu hiki) CCM ya sasa ni sawa na BABELI wa kwenye bible.
 
kipugala

Walikuwa wanajidanganya kuwa ni kaskazini tu,watakapoamini watakuwa wamechelewa.Wa Tanzania sasa tumeamka si mliona na Wanamagamba wengine jana bungeni walivyocharuka kazi kwao,na kazi inaendelea hadi kieleweke.
 
Yote yanawezekana katika yeye atupaye nguvu.Baadhi ya wanaccm wameanza kuponywa na kufikia 2014 ccm itakuwa chali
 
wakati wan-ccm wakihamia chadema, chadema kwenyewe kuna vurugu za chini kwa chini, kwa mfano huu;

mbunge wa viti maalum lucy owenya kwa kushirikiana na baba yake ndesamburo, walimnunua anthony komu ili agombee ubunge wa afrika mashariki kwa sharti komu amuachie lucy kugombea jimbo la moshi vijijini, sasa komu kapigwa chini, milioni 100 walizotumia zimeenda chini sasa hofu ni kwamba kama komu ataendelea kugombea moshi vijijini ni mvutano mkubwa. Hiki ni chama kinachotarajiwa kuwakomboa watanzania. Tafakari.

Mbowe aliingilia kati kijanja ili wagomee uchaguzi ili kumkomoa mzee ndesamburo kwa vile hawaivi lakini ikashindikana baada ya komu kulazimisha kuendelea na mchakato huo, kisa? Shilingi milioni 100 za ndesamburo famili.

Wooooooooooooooooooo huyooooooooooooooo muongo zomeeeeno huyoooooooooooooooo:)
 
Back
Top Bottom