Diwani huyu anatudhoofishia malengo yetu

kamatembo

JF-Expert Member
Sep 25, 2011
854
583
Diwani wa kata ya sinza C CHADEMA mr Simple anaidhoofisha CHADEMA kwa usharobaro wake na si ajabu tukaitema hii kata uchaguzi ujao.
Uchaguzi uliopita hata lingesimamishwa jiwe na mgombea wa magamba mzee Mwaking'inda(former katibu mwenezi magamba) lingeshinda tu
kwa vile madudu alioyafanya huyu fisadi kupe ya kuziuza kwa watu na kujiuzia yeye mwenyewe open spaces za sinza hakuna ambae hakuchoka nayo.

Hii nayo ni sababu kubwa ya mgombea wa CDM kuibuka kidedea,kinachoniuma na kuninyong'onyeza asilimia kubwa ya wakazi wa sinza wanaona ni heri ya mwendawazimu wa zamani kuliko huyu mpya.Jamaa 24/7 yuko bar zile ahadi zote za kero za utaratibu wa uzoaji takataka kazipa kisogo anakwepa vikao na wapiga kura wake,mwambie mademu tu na sasa hv tangu awe diwani kaanzisha mtindo wa kukodisha tax kwasiku anailipa elfu40 imzururishe kwenye bar zote za sinza na kwa madem..

.Imagine jamaa amehamia sinza less than 5yrs na amepanga chumba kimoja tu cha uani plus ni jobless na inasemekana kuandika japo barua kwake ni mgogoro....

SIPENDI,SIWAZI NA WALA SITAKI KUFIKIRIA KUIONA TENA KATA YETU HII YA SINZA C IKIONGOZWA NA DIWANI KUTOKA CCM LKN KWA MWENDO WA KIJANA MWENZETU HUYU NAWAOMBA CHONDE CHONDE VIONGOZI WA CDM TAIFA MUMKANYE HUYU KIJANA AMA SIVYO ATATUPA KIBARUA KIGUMU MNO UCHAGUZI UJAO,MAMAZETU WASHAANZA KUTUSUTA KWAJINSI TULIVYOMPAMBA NA ANAYOYAFANYA.
 
Sina la kusema!!!anatakiwa awajibishwe kwa matendo yake na kuwasahau wapiga kura wake!!!siyo desturi ya chadema!!sijui watakuwa wamemwokotea wapi huyo jamaa
 
Hivi hakuna uwezekano wa CDM kumpiga chini afu ukaitishwa uchaguzi na tukaweka jembe la kazi, maana hawa madiwani wasiofanya kazi wanaharibu sifa ya CDM. Hata diwani wetu wa mbezi luisi (CDM) hatumuoni huku, yaaani hawajibiki!
 
Yani inaudhi sana,mnyika umeskia?unatudanganya na matamko ya maandamano nchi nzima wakati kata tu imekushinda,simamia hyo mijamaa inatuaribia....nimekutaja ww koz km mbunge,diwani yupo ndani ya uwezo wako.. Chukua hatua kabla hatujawapeleka kanisani wakaombewe.
 
Huyu ndiye yule mwanamuzi wa Bong flava au?
mimi nawashangaa sana wana chadema; badala ya kushughulikia mambo muhimu katika kuimarisha chama chao, wao wameng'ang'ania hoja za dowans na ugonjwa wa mwakiembe! huku maeneo wanayoshikilia kiuongozi yakiwa na matatizo makubwa, wananchi wana lalamika huku uongozi wa chadema ukionesha kutokuwajibika: hii ni dalili tosha kwamba viti vya ubunge na udiwani walivyoazimwa na ccm 2010 watavirudisha kwa wenyewe 2015!
 
mimi nawashangaa sana wana chadema; badala ya kushughulikia mambo muhimu katika kuimarisha chama chao, wao wameng'ang'ania hoja za dowans na ugonjwa wa mwakiembe! huku maeneo wanayoshikilia kiuongozi yakiwa na matatizo makubwa, wananchi wana lalamika huku uongozi wa chadema ukionesha kutokuwajibika: hii ni dalili tosha kwamba viti vya ubunge na udiwani walivyoazimwa na ccm 2010 watavirudisha kwa wenyewe 2015!

Unataka kuniambia historia ya NCCR Mageuzi ya mwaka 1995 na 2000 itajirudia kwa CDM mwaka 2010 na 2015? Kilio cha wana Sinza C ni kilio cha wengi! Kimara pia kuna Diwani wa CDM na watu wanalia tu. Huyu Diwani wa Kimara kazi yake ni vurugu na kupanda juu ya meza wakati wa vikao vya Council huku Kimara ikipata utapiamlo wa maendeleo.
 
mimi nawashangaa sana wana chadema; badala ya kushughulikia mambo muhimu katika kuimarisha chama chao, wao wameng'ang'ania hoja za dowans na ugonjwa wa mwakiembe! huku maeneo wanayoshikilia kiuongozi yakiwa na matatizo makubwa, wananchi wana lalamika huku uongozi wa chadema ukionesha kutokuwajibika: hii ni dalili tosha kwamba viti vya ubunge na udiwani walivyoazimwa na ccm 2010 watavirudisha kwa wenyewe 2015!

endelea kuwaza hivyo hivyo! si ajabu nguvu ya mabadiliko itakupita pembeni na bado utaendelea kushangaaa.
 
Mnyika mbezi luisi unakuja lini tukuelezd matatizo ya diwani wetu? Usijisahau sana, bunge si limeisha? Usijisahau sana mheshimiwa
 
Taarifa ifike kwa Mbunge wake kama ni wa Chadema kama ni CCM basi pelekeni malalamiko kwenye Chama itasaidia maana JF si ya Chadema wala si ofisi ya Chadema jamani .Tufuate taratibu hii ni serious issue na Chadema wanatakiwa kuitolea uamuzi mgumu itakapo bidi .
 
Hoja ngumu zije jf,kabla ya kulileta suala hilo jf uliwasilisha malalamiko yako kwake?au je mbunge husika umemjuza?achan lawama za kizushi,lengo n kujenga chama kwa uwajibikaj ulo bora.Ushaur mwandikie barua mhusika nakala kwa viongoz wa chama sehemu hiyo,mbunge na katibu mkuu wa chama.Ukiona hamna la maana lete jf juhud zako zote wana jf wazijadili na ikiwezekana tutalifanyia kazi.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Tunashukuru kwa taarifa Mkuu, suala hili tungeomba lishughulikiwe ndani ya vikao vya CDM, katika muda muafaka kabula jua halijazama.
 
Dr Slaa,Mbowe,Zito huyo jamaa aanze kuchunguzwa mchana huu na hatua zichukuliwe mapema sana anatuharibia kauli mbiu zetu na sera zetu hivyo kukirudisha chama nyuma,Ikishindikana nguvu ya umma itatumika.This is funny.
 
ya kweli haya??? ni kama wiki mbili sasa kuna mbwa mwitu wenye ngozi ya Kondoo humu JF. wanajifanya ni CDM kumbe wapo kwenye payroll ya AIBU ya Magamba. Kama amekuwa akimuona sehemu zote anazozunguka je ameongea naye? au wanagombea Mademu anaowasema!
mambo ya chumba kimoja cha Uani yanakuhusu nini au yanauhusiano gani na utendaji? kama ana uwezo wa kulipa taxi 40,000 per day na hafanyi kazi anawezaje kumudu gharama hizo? umeenda mbali kwa kusema hawezi kuandika barua jambo ambalo mi naona haliwezekani kwa CDM.
 
vikao vya mara kwa mara na wapiga kura ni muhimu sana kama chadema inataka madiwani na wabunge wake waaminike kwa wapiga kura.

Madiwani na wabunge wa chadema saa nyingine wanaJidanganya kuwa kwa kuwa wao hawana serikali basi si wajibu wao kuleta maendeleo ili kazi yao ni kuibana tu serikali.

Wakumbuke kuwa wananchi wanahitaji mtu wa kuwaunganisha ili kutatua baadhi ya kero ambazo hata hawahitaji budget ya serikali maana wako tayari hata kujichangisha wenyewe. Kwa mfano issue ya usafi kwenye maeneo yao watu wako tayari kuunganishwa na kiongozi wao ili kufanya usafi kwa kuchagia uzoaji wa takataka.

Inasikitisha Mazingira ni machafu halafu mbunge na madiwani wanasubiria budget ya serikali ya ccm ambayo kwa makusudi haitolewi.

Chadema lazima wajuwe kuwa ccm na serikali yake haitakubali kuboresha maeneo ya wapinzani. Ni lazima cdm wawape wananchi wao feedback ya kinachoendelea kwa kila tatitizo hata kama serikali imegoma kufanya wao waishitaki kwa wananchi wao halafu wao waamue wanaiwajibisha vipi serikali.

Wabunge na madiwani wa chadema lazima waonekene tofauti. Wananchi wanataka kuwa na mawasiliano ya mara kwa mara juu ya kero zao. Mambo ya kujifanya wewe ni mbunge wa taifa huku matatizo ya jimbo lako umeyageuzia kisogo haitakusaidia m kwenye uchaguzi wa 2015. Watu wanaamini mbunge/diwani ndiyo watawaletea maendeleo na siyo serikali. Kumbuka ccm watatumia hii sababu kuwaambia wananchi ya kwamba Mbunge wa cdm amewafanyia nini watu wa jimbo hili?

Japo wabunge wa chadema wananfanya vizuri kwenye national issues lakini wakumbuke ubunge wao umepatikana na kura za majimboni. Msije mkashangaa mbunge kma Halima mdee anashindwa jimboni kiasa hajatumia muda wake kukaA na wananchi na kushirikiana nao kutatua matatizo yao. Hatakama serikali haitaki basi yeye kazi yake ni kuwajulisha wananchi wake kuwa serikali haitaki ili wasije wakatumia hii loop kwenye uchaguzi wa 2015.Wabunge na madiwani wa chadema angalieni mlipo simama msije mkaanguka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom