Hawa Ng'humbi unapoteza muda na fedha za serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa Ng'humbi unapoteza muda na fedha za serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mtoka Pabaya, Apr 22, 2012.

 1. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,746
  Likes Received: 8,006
  Trophy Points: 280
  Huu ni ujumbe wangu kwa aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo la Ubungo, Hawa Ng'humbi.

  Kwanza nikupe pole kwa kushindwa vibaya katika uchaguzi huo na pia nikupe pole nyingine kwa kushindwa kuuona ukweli. Najua kinachokusumbua ni fedha zako ulizozitumia kutoa rushwa kwenye mchakato wa kura za maoni jimbo zima ukihaha wewe na meneja kampeni wako Somebody Isabela (aliyekuwa mwenyekiti wa UWT kata ya Makuburi).

  Ni imani yangu kuwa, kinachokusukuma kuanza kutapatapa mahakamani ni madeni yanayotokana na matumizi makubwa ya fedha kuwahonga wajumbe wakupigie debe kwenye kura ya maoni ili umshinde Nape (ambaye hata hivyo naye angeshindwa tu) na ukafanikiwa kweli kumshinda baada ya kugawa fedha kwa wajumbe. (Rifaa tu zos mane yu ofad to zat kikundi of kinamama wajasiriamali kule Kajima karibu na nyaya kubwa za umeme), Mlingi Bar na Kwa Mlacha bar.

  Kwa msiomjua huyu mama, ni mwepesi kweli kweli. Alipokuwa kwenye mkutano wa kampeni Makoka Shuleni, Hawa Ng'humbi, bila aibu alisema kuwa amewachimbia kisima wakazi wa Kajima. Kwa kuwa watu wa Kajima ni wasomi na hawamkopeshi mtu, walimuomba wamgharamie usafiri akawaoneshe wapi amechimba kisima. Baada ya kuona maji yapo shingoni, alibadili maneno na kusema kuwa sio Kajima bali Kibangu. Watu wa Kibangu walimkaushia tu, lkn ukweli ni kwamba, kisima anchosema kimechimbwa bureee na SAS, yule mwarabu mwenye malori pale River Side na kimekuwepo kabla yeye hajafika Ubungo.

  Sasa hili la kupinga matokeo ni kioja na kutaka kujidhalilisha na kuiongezea CCM matatizo. Nafikiri impct ya kumfanyia mizengwe Godbless Lema (yule jasiri aliyeuambia umma wa Watanzania kuwa PM ni muongo na mpk leo SPIKA anaogopa kumpa nafasi kuthibitisha kauli yake) kufanyiwa mizengwe mahakamani. Kila mwenye akili za kesho anahamia CHADEMA na chama chenu kimebakiwa na watu wenye akili za Ki-Lusinde Lusinde. Sasa naona na wewe unataka kuhamishia balaa hili DAR.

  Nionavyo mimi, leo hii uchaguzi wa jimbo la Ubungo ukirudiwa, Dr.Slaa na timu yake ya "TOBO wa TOBO, TOBOA" watapiga kambi Ubungo na kwa taarifa yako Hawa Ng'humbi, hicho ni kiama kwa CCM. Hapa sizungumzii jimbo kurudi CHADEMA, bali nazungumzia MAVUNO ambayo CDM itafanya kwenye ghala lenu.

  Kwanza nikukumbushe kuwa kwenye kata ya Sinza ambapo ndio unatoka, ulianguka zaidi ya kata nyingine, hii ni dalili hata kushinda kwako kura ya maoni ni vile tu ulihonga.

  Ushauri wa bure kwa CCM. Muda huu uliobaki hadi kufikia uchaguzi mkuu ujao mngeutumia kuboresha magereza. Wekeni vitanda vya maana kule na masofa na TV sets zenye ving'amuzi vya ting kwani muda ukifika hayo yatakuwa makazi yenu kwa muda mrefu.

  Wasalaaam!
  Mwana Mtoka Pabaya.
  Mndengereko pekee nayeongea kihispaniola
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Nakugongea "Likes" kama tatu hivi fasta fasta!
   
 3. Endangered

  Endangered JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 929
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mkuu naunga hoja mkono. Hawa apumzike tu. Maana hata wafanyeje watu wanaona faida ya Mnyika, ambaye kimsingi hata 2005 alipokwa ushindi. Na bado tunasubiri ufisadi wote jimboni unavyofumuliwa. Sisi em wanachotaka ni kuficha madhambi yake - lakini kadri wanavyofanikiwa, ndivyo bomu linakolea zaidi!
   
 4. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #4
  Apr 22, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ushahidi umesimama lazima ashinde kesi mnyika aliiba kura
   
 5. sembo

  sembo JF-Expert Member

  #5
  Apr 22, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 3,350
  Likes Received: 1,202
  Trophy Points: 280
  Saaaaafi,
   
 6. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #6
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni ushauri mzuri sana kwa Mafisadi wa Magamba, hasa Kikwete sasa hivi anaouwezo wa kuzijenga vizuri hizo jela, huko ndio kutakapokuwa nyumbani kwake yeye na Mkapa pamoja na Mafisadi wengine. Kama Nape upo humu na umepitia post hii basi muambie Kikwete aweke mambo sawa huko Sogerea au Keko, asije kujijutia kuwa alisahau kujenga nyumba yake ya maisha.
   
 7. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #7
  Apr 22, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda hiyo ya ndengereko pekee anayeongea kihispaniola
   
 8. POLITIBURO

  POLITIBURO Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakuaminia Mndege wa kwa Manjenga! Pokea tano! Duh umepasha sasa mwenye masikio na asikie lile Mndengereko Mtoka Pabaya anayowaambia magamba!!!!!!!!!!!!!
   
 9. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Huyu s.h.a hawa alinisababishia ban majuzi tu. Naomba nikomee hapo maana ban nyingine inataka kunukia hapa!
   
 10. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Yupo mtu ndo anamdanganya mama Hawa. Wanataka Mnyika apgwe chn ksha Nape agombee kuptia ccm.
  Subirien mtaona
   
Loading...