Diwani amcharukia Magufuli: Hakuna Mwananchi atakayefyeka bangi kwenye kata yangu

Nina wasiwasi na uraia wako mkuu. Labda kama ni viongozi wa vijiji na kata za huko kwenu Kajiado na Kericho. Haiwezekani shamba la bangi ekari kumi lilimwe,lipaliliwe bila mwanakijiji kujua na kutoa ripoti. Nia ya mheshimiwa Rais ni uwajibikaji wa kila mmoja wetu ktk kulinda jamii hii na madawa ya kulevya na uhalifu mwingine.
Ni Sheria tu ifatwe, hakuna jingine..!!!
 
Insubordination.Hawezi kumjibu mkuu wa nchi hivyo hasa anapoagiza vyombo vyake vifanye kazi. Ni kutokuelewa tu kile anachopaswa kukifanya. Wajibu wake ni kutoa ushirikiano na vyombo hivyo. Yeye asipokubali yupo Mkuu wa Wilaya atatekeleza hilo na yeye kuwekwa pembeni. Bangi lazima ifyekwe ikipatikana. Nani atakayefeka ni kitu kingine. Huwezi ukaitetea bangi na ukaeleweka vizuri.
Aisee! Hivi kuna sehemu huyo Diwani katetea bhangi?? Kuna watu sijui hata niseme nini!
 
Wananchi kufyeka bangi eti si kazi yao, kwani polisi ni kazi yao? Rais kasema polisi wamtafute mlimaji wa hiyo bangi kama wananchi wakimficha wakafyeke wao ili siku nyingine wakimjua mlima bangi watoe taarifa mapema kuwaepusha wa kufyeka bangi.
CC Nondo.
Mzee kwanza kuteketeza mihadarati ni kazi ya polisi kwa mujibu wa katiba.

Pili, likigundulika shamba la bangi alieresponsible kutoa Maelezo juu ya mmiliki wa hilo shamba ni serikali ya mtaa,

Hapo wanakijiji hawahusiki kabisa, labda wanawezatoa ushirikiano kwa polis na viongoz wa mtaa ili kufanikisha kumpata mmiliki. Ila kazi ya kufyeka ni polisi na wanalipwa kwa kazi kama hizo,

Ukisema wafyeke wananchi bas polisi tuwapnguzie mshahara, maana hwezniachisha kazi zangu(mf. Nifunge duka langu) nkafyeke bangi porini, theni bado nikulipe, kwa uzuri gani ulionao? Kwa utakatifu gani ulionao?

Waliotunga hizi sheriawalikua na busara sana, ila kizibo mmoja anajikuta yeye mbabe sana anataka aipindue sheria anavotaka! Very stupid
 
Apimwe mkojo,Haiwezekani amjibu Amiri Jeshi kama anajibizana na hawara ake.Shubamiiiiit!
 
Mbona unakuwa mgumu kuelewa
hajakata ufyekaji wa bangi ila kakataa kulazimisha wananchi wote wanaohusika na wasiohusika kushirik ufyekaji.

halafu mtambue sheria za nchi hii hazitokan na matamko ya mtu binafsi.

Nimejibu ya kuwa ile ya Rais ilikuwa political statement na sio presidential decree. Diwani alienda maili mbili mbele. Yaliyo ya kisheria mheshimiwa kama mnavyofahamu amekuwa akiagiza miswada iletwe bungeni kupitisha sheria anayoilenga. Ile ilikuwa ni political statement na sio agizo ka kisheria na siyo presidential decree. Mmepata cha kumsema kipenzi cha watanzania wenye kuipenda nchi hii.
 
Mimi nilimuelewa Rais hataki mkatekate na kuchoma bangi hovyo haswa police
Nimpongeze mh Raisi kwa hili dunia haitaki uteketezaji wa mimea hovyo tutunze mimea na mazingira
 
Magu akisoma hii atajuta kua rais wa nchi inayotakiwa kuongozwa kwa mujibu wa sheria.

Jamaa kachambua vizuri, kaeleza kwanini hataki na vifungu vya sheria kaweka

Rais wetu anatamani kusingekua na sheria ili atuburuze atakavyo.
 
Aisee! Hivi kuna sehemu huyo Diwani katetea bhangi?? Kuna watu sijui hata niseme nini!
Kilichomponza msemaji huyo ni kutoa tamko kwa jambo ambalo wengi wasingependa kujihusisha nalo. Wapo wanasheria ambao hata kesi za jinsi hiyo hawazitaki. Mnaona hata kule majuu wanasheria wanajitoa kutetea baadhi ya mambo ambayo kiongozi mmoja anatuhumiwa. It is very unfortunate kwa diwani huyo kutoa comment kama hiyo. Wenye busara husema "No comnent!"
 
kama wamemtuma ataenda kuwasimulia vzr wenzake ...tamko la rais ni sheria haiwezekani watu walime bangi halafu jirani zake msijue ile ni bangi ya nani ndicho alichomaanisha mh rais vinginevyo mkimlinda mtuhumiwa ndipo hapo mkaifyeke hiyo bangi
Elimika ww tamko la rais kwa sasa ni maoni yake tu hayo. Kabla ya katiba kauli ya rais ndo ilikuwa sheria lakini kwa sasa tunafata katiba 2 ambayo yeye mwenyewe aliapa kuilinda
 
kama wamemtuma ataenda kuwasimulia vzr wenzake ...tamko la rais ni sheria haiwezekani watu walime bangi halafu jirani zake msijue ile ni bangi ya nani ndicho alichomaanisha mh rais vinginevyo mkimlinda mtuhumiwa ndipo hapo mkaifyeke hiyo bangi
tamko LA raisi halifuati sheria, Mimi na umri wangu 40+ years sijui mmea waa bangi ukoje, ikitokea Sikh hiyo Niko kijijini kwangu, kwa hiyo nihukumiwe kwa kosa lisilonihusu
 
Diwani wa kata ya Gwarama wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Bw.Elia Michael amepinga vikali agizo la Rais JPM la kuwataka polisi kukamata wananchi wa kijiji kizima kwenda kufyeka bangi ikiwa kijiji chao kitabainika kuwa na shamba la bangi.

Diwani huyo amewaeleza wananchi wake kuwa agizo hilo ni batili na ni kinyume na sheria mbalimbali na katiba ya nchi, ikiwemo sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (Criminal Procedure Act, Cap 20) na sheria ya polisi (Police Force and Auxiliary Services Act, Cap.322) zinazozuia polisi kukamata mtu asiye mtuhumiwa wa kosa lolote, na kusisitiza kuwa ni kosa kuadhibiwa kwa kosa la mtu mwingine.

Ameeleza pia agizo hilo ni kinyume na utaratibu wa utendaji wa serikali za mitaa, kwani serikali ya kijiji haiwajibiki kwa jeshi la polisi, bali jeshi la polisi linawajibika kwa serikali ikiwemo ya kijiji. "Polisi haina mamlaka ya kuiagiza serikali ya kijiji, ila serikali ya kijiji ina mamlaka ya kuwaagiza polisi" amesema na kuwataka washauri wa JPM kusoma sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 1982.

"Kila kijiji kina serikali yake, inayofanya kazi kwa mujibu wa sheria. Haiwajibiki polisi. Lazima serikali hizo ziheshimiwe. Kama kutatokea shamba la bangi kijijini, serikali ya kijiji ichukue hatua. Ikiwa mtuhumiwa atashindwa kubainika, viongozi wa kijiji husika wawajibike, lakini sio kukamata kila mtu hadi viongozi wa dini kwa jambo ambalo hawahusiki nalo." Amesema Elia.

"Kama kwenye vijiji vya kata yangu ya Gwarama, ikaonekana shamba la bangi wananchi hawatafyeka bangi hiyo. Mark my words HAKUNA MWANANCHI ATAKAYEKAMATWA KWENDA KUFYEKA BANGI KWENYE KATA YANGU" amesisitiza Elia.

"Ni jukumu la vyombo vya usalama kuteketeza mihadarati. Mbona wakikamata aina nyingine ya dawa za kulevya kama cocaine hawaiti wananchi wakateketeze, ila bangi wanalazimisha wananchi wote washiriki kuteketeza? Hii si sawa. Ikitokea bangi kwenye kata yangu polisi ndio watafyeka bangi hiyo. Hakuna atakayeweza kuwalazimisha wananchi wakafyeke." Amesema diwani huyo mwenye umri mdogo kuliko madiwani wote nchini, ambaye pia ni mhitimu wa chuo kikuu UDSM.!

My Take
We diwani mwenyewe wa Kigoma,tutakurudisha kwenu Burundi......Jumatatu tukukute Uhamiaji
Ukumbuke Amri ya Rais ni kubwa kuliko kanuni za jeshi. TPDF, POLICE, MAGEREZA nk........ usidangaje watu
 
Hu

Huo ndio Uhuru wa kutoa mawazo anaosema umebanwa.
 
Ila kule kigoma ni mpakani ngoja tusubiri maana njia iliyobaki ni uraia tu kwa sasa
 
Insubordination.Hawezi kumjibu mkuu wa nchi hivyo hasa anapoagiza vyombo vyake vifanye kazi. Ni kutokuelewa tu kile anachopaswa kukifanya. Wajibu wake ni kutoa ushirikiano na vyombo hivyo. Yeye asipokubali yupo Mkuu wa Wilaya atatekeleza hilo na yeye kuwekwa pembeni. Bangi lazima ifyekwe ikipatikana. Nani atakayefeka ni kitu kingine. Huwezi ukaitetea bangi na ukaeleweka vizuri.
Nakiri kuamini kuwa kijana amekurupuka kutamka na alichopaswa kufanya ni kungojea utekelezaji wa maelekezo ya rais yafike kwenye kata yake. Hata hivyo, hoja yake ni makini ila haukuwa wakati muafaka kuitoa. Kijana hakuwa anatetea bangi na wa kumuelewa tumemuelewa ila anaweza kuwa victimized kama mkulu ataumizwa na kauli hiyo!
 
Hu

Huo ndio Uhuru wa kutoa mawazo anaosema umebanwa.
Ni mjinga pekee asiyejua kama Uhuru unebanwa isipokuwa kwa kulazimisha. Na sote tunajua wanaotoa maoni tofauti wanafanywa nini. Siku sio nyingi diwani atatiwa nguvuni halafu utasema nini
 
Insubordination.Hawezi kumjibu mkuu wa nchi hivyo hasa anapoagiza vyombo vyake vifanye kazi. Ni kutokuelewa tu kile anachopaswa kukifanya. Wajibu wake ni kutoa ushirikiano na vyombo hivyo. Yeye asipokubali yupo Mkuu wa Wilaya atatekeleza hilo na yeye kuwekwa pembeni. Bangi lazima ifyekwe ikipatikana. Nani atakayefeka ni kitu kingine. Huwezi ukaitetea bangi na ukaeleweka vizuri.

kwhyo kama uyo rais kavunja sheria hasikosolewe?
 
Back
Top Bottom