Diwani amcharukia Magufuli: Hakuna Mwananchi atakayefyeka bangi kwenye kata yangu

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,500
2,000
hivi umesoma ukaelewa kweli?ni wapi alipotetea bangi?ni mkuu wa nchi gani Tanzania aliye juu ya sheria?
Hakuna sheria inayomkataza mwananchi kuhoji na kukosoa mamlaka,hakuna,zaidi sana sheria nyingi mantiki yake ni mamlaka kuheshimu wananchi waliowaweka madarakani.
Diwani amekosoa agizo la rais kwa kutumia sheria,akitetea wananchi wake,na wewe mkosoe diwani kwa sheria.
Akimpinga diwani kwa hoja na vifungu vya sheria bila blah blah na mahaba yake kwa rais nitag mkuu
 

sagaciR

JF-Expert Member
Jun 17, 2017
647
1,000
Huyu Diwani ni Kipepe tu kama siyo Ndumilakuwili. Diwani ni mwakilishi wa wananchi (kwenye kata inayoundwa na vijiji - vitatu/vinne) katika Halmshauri (wilaya/mji/manispaa/jiji) hana eneo la utawala, na hivyo, kutokuwa na mandate ya juu ya political management ya serikali za vijiji vilivyomo kwenye kata anayoiwasilisha. Kwa hiyo, kama si mchehche au political insanity, wala hakustahili kujibu chochote kuhusu agizo la Rais wa JMT. Ananukuu piecemeal za vifungu vya sheria badala ya comprehensive notion ya agizo la Rais ambaye ni Mkuu wa Nchi na Serikali ya JMT. Bado diwani msomi (wa sheria) hajui kuwa katika muundo wa sasa wa serikali, uwakilishi wake (yeye binafsi) unapata mamlaka kupitia PORLARG/OR-TAMISEMI. Pengine kwa wanaomjua muulize iwapo software pekee inaweza kufanyakazi nje ya hardware! Pengine watani zake watasema, tatizo lake linatokana na kuwa Mha.
Kwa kuwa una_element za kikabila je wewe ni kabila gan??

Pia wewe unaamini mzazi ndo hutenda mema tu (hakosei) kuliko mtoto/watoto wake??
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,128
2,000
JPM nae amezidi kukurupuka na kujitamkia lolote. PhD holders hawabehave namna hiyo.
 

Tzr786

Member
Jan 17, 2018
87
125
Nilichoelewa mimi ni kwamba kuna mijitu humu jf inawaigi seat tu, comments zao hazina mashiko....kijiji kina watoto,wazee, wanawake wajawazito , vilema na wachungaji so unaposema wote wakamatwe inamanisha hajaangalia mazingira ya watu hawa. Diwani yupo sawa na mheshimiwa kateleza angei elaborate kauli yake ili raia waielewe vizuri
 

morenja

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
4,363
2,000
Maana ya kauli ni kuwakumbusha nyinyi madiwani na wenyeviti wa mtaa majukumu yenu yani mnakaa na watu wanalima bange mnawajua alafu mamlaka mnayo ya kuwazuia mnaogopa kisa waliwaweka hapo sasa polisi hapigiwi kura ngoja afanye kazi yake kuharibu mihadarati
Angeagiza serikali ya kijiji kuchukua wajibu huo wakisaidiana na vyombo vya ulinzi .na maana angetoa agizo kukumbushia jukumu hilo kutekelezwa na serikali za vijiji .na sio kuagiza Polisi kuamrisha serikali ya kijiji .kisheria serikali ya kijiji ina mamlaka kamili.ndio maana polisi wakitaka kukagua nyumba ya mwanakijiji au kata lazima awepo mwakilishi wa serikali kijiji au kata
 

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,189
2,000
Amezungumza mambo ya msingi sana kiasi kwamba ameonesha ni kiasi gani phd zingine ni za hovyo. Unamkamata mtu na kumpa adhabu kwa kosa la mtu mwingine kivipi? Na gongo ikikamatwa watawalazimisha wanakijiji wote wainywe? Hiyo mihadarati mingine kama cokein na heroin wanapoikamata kwanini wasikamate na wananchi wote kwenda kuiteketeza badala yake wanabeba na kuipeleka kusikojulikana
 

bhokesa

Senior Member
Feb 23, 2018
138
250
Insubordination.Hawezi kumjibu mkuu wa nchi hivyo hasa anapoagiza vyombo vyake vifanye kazi. Ni kutokuelewa tu kile anachopaswa kukifanya. Wajibu wake ni kutoa ushirikiano na vyombo hivyo. Yeye asipokubali yupo Mkuu wa Wilaya atatekeleza hilo na yeye kuwekwa pembeni. Bangi lazima ifyekwe ikipatikana. Nani atakayefeka ni kitu kingine. Huwezi ukaitetea bangi na ukaeleweka vizuri.
Hujitambui rais ni taasisi hakuna ruksa kuvunja sheria kisa rais. Ataambiwa tu. Huyo si john magufuri wa chato au akiwa rais anakuwa mungu acheni ujuha
 

Theunknown

JF-Expert Member
Dec 30, 2017
290
500
Thst was a political statement rather than a political decree. Diwani amekurupuka kujibu a political statement kwa vifungu vya sheria. Nyie wote mnajua any political statement lazima iwe enacted na Bunge kuwa sheria kabla ya utekelezaji. Hakuna agizo pale bali a political statement. Tumeona akifanya hivi na akisema kwa mambo kadhaa muhimu kuwa Serikali itapeleka mswada bungeni kutunga sheria. Hili la juzi ni just a political statement na sio presidential decree. Akitaks anaweza kuagiza sheria husika itungwe pale ilipo na haja ya kisheria.
Mkuu kwa ushahidi,Mkuu amekuwa akitoa maagizo yanayokinzana na sheria na yakatekelezwa,mfano.mahakama ilitoa zuio la watu wa kimara kuvunjiwa nyumba zao zikavunjwa!!
Aliagiza machinga wauze barabarani pasipo kubugudhiwa,japo kuna sheria zinazoongoza mambo hayo,mwisho wa siku machinga wakajaa mpaka ikawa kero!(rejea Mwanza,Morogoro na kariakoo)
Na hii unaitetea kwamba ni jambo la kisiasa haliwezi kutekelezeka,tusubiri!!!
 

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,500
2,000
Tusiishie kwenye bange tu,tuwajibishane kwenye aina zote za maovu,haiwezekani watu wagawane mabilioni ya wizara ya ujenzi kisha waziri husika asijuwe wakati ubadhirifu huo umefanyika katika "eneo lake la utendaji".

Kwa mujibu wa ripoti ya CAG ya 2015/2016,zaidi ya bilioni 320 zililiwa kifisadi katika wizara ya ujenzi iliyokuwa chini ya JPM,yeye kama kiongozi wa wizara(eneo lake la utawala),tunaomba awaswage wenzake wazirudishe hela zetu!

Tukitumia falsafa ya kuwajibishana kila penye uovu tutadhibiti mianya yote ya Wizi na ubadhirifu,tendo lolote la ufisadi likitokea kwenye eneo la utawala la kiongozi,kiongozi husika aswagwe.Ni wakati wa kumswaga aliyeleta kivuko kibovu ambacho hata wanaonunua vyuma chakavu hawawezi kukinunua,ni muda muafaka kumswaga aliyevunja kimakosa mkataba wa ujenzi wa barabara ambao leo tumelipa mabilioni ya shillings kama fidia baada ya wadai wetu kuzishikilia ndege na bado aliyesababisha hayo anawakejeli wanaohoji aliyevunja mkataba huo ambao ndiyo chanzo cha ndege kushikiliwa!

Anawashangaa wanaohoji Taifa kuingizwa hasara ya kulipa mabilioni badala ya kumlaani aliyetuletea kadhia hiyo? Huo ni uhayawani wa kiwango cha PhD ya maganda ya korosho iliyokataliwa kutambuliwa na wasomi kiasi cha kumfanya mwenye nayo aanze kulazimisha itambuliwe!

Kwa kutumia falsafa ya wanakijiji kuwajibishwa kwa kosa la bange kulimwa kijijini kwao,tuanze kuwawajibisha viongozi wote ambao katika maeneo yao ya utawala kulitokea ufisadi wa Escrow,EPA,Richmond,Meli ya samaki,Kivuko kibovu,Radar,mikataba ya uchimbaji madini,mauwaji,utekaji na utesaji,Nyumba za serikali kuhongwa vidosho,Kusafirishwa kwa wanyama hai na uozo wote.

Mabilioni ya Escrow yalipelekwa hadi ikulu na mnikulu Shaaban Gurumo,lakini ikulu hadi leo imepiga kimya!Mabilioni ya EPA(kagoda agricultural)jeshi lilisingiziwa kuyatumia kwa matumizi nyeti,kauli hiyo ilitolewa na Bi Zakia Meghj aliyekuwa waziri wa fedha,baada ya kuthibitika kagoda ni kampuni la kitapeli na halihusiani na jeshi letu,jeshi limekaa kimya na halijawahi kuwachukulia hatua waliolichafua.

Juzijuzi mtu katumia mabilioni kununua skrepa,kaenda kuificha jeshini na jeshi limeipokea skrepa hiyo,badala ya kuhoji jeshi limegeuzwa kichaka cha kufichia ufisadi wa mkuu.

Tuanze kuwajibishana kila litokeapo jambo kwenye maeneo yetu ya utawala,tusiishie kwenye mashamba ya bange tu.
Hahahaha absolutely
 

Nyamtalakyono

JF-Expert Member
Dec 17, 2015
794
500
Akili za CCM ni za kupengea kamasi tu,hivi umeelewa hoja ya diwani?
Hata hivyo CHADEMA mmelalamikiwa muda mrefu hadi yakatolewa maoni mmpimwe maana mnatumia. Rais ana maana nzuri. Haiwezekani mtu alime bangi wananchi au wakazi wa eneo husika wasichujue. Kumbuka huyo mkulima wa Bangi ana majirani, Mwenyekiti wa Kitongoji na Mwenyekiti wa kijiji. Ifikie hatua tusitete maovu. Kila mwanamchi awe Mlinzi wa mwenzake. Pia unakushauri usifikiri kama taahira.
 

bhokesa

Senior Member
Feb 23, 2018
138
250
kama wamemtuma ataenda kuwasimulia vzr wenzake ...tamko la rais ni sheria haiwezekani watu walime bangi halafu jirani zake msijue ile ni bangi ya nani ndicho alichomaanisha mh rais vinginevyo mkimlinda mtuhumiwa ndipo hapo mkaifyeke hiyo bangi
Kwa sheria mmea hauwezi kuthibitika kuwa ni bangi mpaka athibitishe mkemia
 

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,500
2,000
Wapenda umaarufu kwenye utawala huu wataumia sana eti diwani na yeye anasema "mark my words" kupinga amri ya magufuri atapoteza kila kitu

Someni alama za nyakati umaarufu wa kisiasa kwenye huu utawala utawapoteza sasa jiandae kuulizwa uraia
Uelewa wenu ni mdogo sana kama huyo rais wenu, diwani kapinga kwa vifungi vya sheria vilivyo chini ya sheria mama ya nchi (Katiba) ambayo rais aliapa kuilinda na kuitetea kwa nguvu zote, sasa ninyi badala ya kuja na vifungu vya sheria kumpinga Mh diwani mnakuja na mihemko na mahaba yenu kwa rais....hovyo sana ninyi mbumbumbu
 

Konsciouz

JF-Expert Member
Aug 12, 2015
4,829
2,000
Inaonyesha dogo ni very smart upstairs...
Hofu yangu ni reaction ya mpokeaji wa huu ujumbe.
 

much know

JF-Expert Member
Oct 22, 2017
2,641
2,000
Uelewa wenu ni mdogo sana kama huyo rais wenu, diwani kapinga kwa vifungi vya sheria vilivyo chini ya sheria mama ya nchi (Katiba) ambayo rais aliapa kuilinda na kuitetea kwa nguvu zote, sasa ninyi badala ya kuja na vifungu vya sheria kumpinga Mh diwani mnakuja na mihemko na mahaba yenu kwa rais....hovyo sana ninyi mbumbumbu
Mimi sipingi lakini approach aliyotumia sio sahihi na itamugharimu
 

gemmanuel265

JF-Expert Member
Feb 16, 2016
8,500
2,000
Wapenda umaarufu kwenye utawala huu wataumia sana eti diwani na yeye anasema "mark my words" kupinga amri ya magufuri atapoteza kila kitu

Someni alama za nyakati umaarufu wa kisiasa kwenye huu utawala utawapoteza sasa jiandae kuulizwa uraia
Huwezi kuacha dhuluma itawala kwa kisingio cha kusoma alama za nyakati huo utakuwa uzuzu
 

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
4,194
2,000
Kwani cocaine huwa mnawapa mliowakamata nayo waiteketeze!? Maagizo ya kiendewazimu hayo.
Insubordination.Hawezi kumjibu mkuu wa nchi hivyo hasa anapoagiza vyombo vyake vifanye kazi. Ni kutokuelewa tu kile anachopaswa kukifanya. Wajibu wake ni kutoa ushirikiano na vyombo hivyo. Yeye asipokubali yupo Mkuu wa Wilaya atatekeleza hilo na yeye kuwekwa pembeni. Bangi lazima ifyekwe ikipatikana. Nani atakayefeka ni kitu kingine. Huwezi ukaitetea bangi na ukaeleweka vizuri.
 

Cicero

JF-Expert Member
Jan 20, 2016
2,925
2,000
Insubordination.Hawezi kumjibu mkuu wa nchi hivyo hasa anapoagiza vyombo vyake vifanye kazi. Ni kutokuelewa tu kile anachopaswa kukifanya. Wajibu wake ni kutoa ushirikiano na vyombo hivyo. Yeye asipokubali yupo Mkuu wa Wilaya atatekeleza hilo na yeye kuwekwa pembeni. Bangi lazima ifyekwe ikipatikana. Nani atakayefeka ni kitu kingine. Huwezi ukaitetea bangi na ukaeleweka vizuri.
Yeye ana backing ya sheria na ameziquote sheria hizo.
Agizo la JPM lina backing ya sheria?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom