Division 2 Wa PCB: Je kuna ambao hawajapata selection?

Division 2 Wa PCB: Je kuna ambao hawajapata selection?

Ushauri wangu vijana wasibague vyuo na fani mtu unakuta anabagua chuo cha dodoma (eti cha kata) matokeo yake wanakuwa wengi sehemu moja mwishowe wanakosa wengi.
Hii ndo inawakabili vijana wengi kubagua vyuo bila kuangalia ufaulu wao. Haishangazi 33000 wamekosa round ya kwanza. TCU wasinge fungua round ya pili ina maana hao wote ni vilio vitupu. Na bado mwanga sio mkubwa wa kutosha dirisha linafungwa 10.10.2017 na ndo siku ya mwisho kwa vyuo vingi kwa wale wenye multple selections kureport. Sijui kama vyuo vinaonyesha nafasi ambazo hazija jazwa au tunaomba bila kujua nafasi ziko wapi. Wakati wa CAS round ya pii unaona kabisa nafasi zipi zimebakia.
Safari hii hata UDOM inaelekea imetema watu!
 
Hata UDOM kama hauna divisio 1 huwezi kupata MD wala nursing

TCU wamefanya kitu mbaya mwaka huu upande wa afya (MD, DDentistry, BPharm) si tu uwe na point 8 ( Div 2:10) lakini ukidhi kigezo cha kila somo PCB (DCC respectively), ikipungua moja tu kwaheri na kama haitoshi total slots kwa Tanzania nzima zimepungua (kuzuiwa vyuo visidahili).

Nashangaa mwaka wangu nakumbuka alieongoza alikuwa na C ya physics huyo PCM! PCB wengi tulikuwa na two na one za kuning'inia. Ndalichako Mungu anakuona maana ulitukazia balaaaaa
 
PCB mwaka huu hawajafaulu sana tatizo ni vyuo vingi vilivyokuwa vinawachukua vimefungiwa

UDSM hawajachukua MD mwaka huu
KCMC Kimefungiwa
Ifakara Kimefungiwa
Be nawashaur waombe nje ya nchi vyuo vimejaaa vinauwezo wakuchukua wanafunz weng kama kenya south Africa kwa wenye uwezo wasio weza Wamtumain Mungu mwakakesho watapata kama kuna chance ya kuomba pia waombe tena kw wale wanaoitaji kwenda nje ya nchi wafuate Global inducation link pale sabsaba kila kitu kinsenda barida
 
Enzi zetu pcb ukiwa na three wewe ni kichwa na unatafuwa cjui siku hzi kuna nini naona pcb wanakosa vyuo while wamefaulu vzur tu..aiseeee
 
ACSEE 2013 .. T.O alikuwa na ^C^ ya physics noma sana. tuliumia wengi...
Hahahahahaha yani we achaaaa ule mwaka tulipita kimungu Mungu huwa nikiangalia cheti changu naona sina F huwa namshukuru sana Mungu. Physics acha kabisa siku izi sijui mambo yakoje
 
Enzi zetu pcb ukiwa na three wewe ni kichwa na unatafuwa cjui siku hzi kuna nini naona pcb wanakosa vyuo while wamefaulu vzur tu..aiseeee
Tusipo angalia PCB itakuwa combi ya kukimbia kama ukoma hasa kama una angalia course za MD, DDentistry na B.Pharmacy. Itabidi ujiulize mara 3 kabla ya kwenda huko. Na ukikosa ukiamua kwenda Diploma za Afya matokeo yako ya F6 unatupilia mbali unatumia cheti cha F4. Sielewi kabisa.
 
Enzi zetu pcb ukiwa na three wewe ni kichwa na unatafuwa cjui siku hzi kuna nini naona pcb wanakosa vyuo while wamefaulu vzur tu..aiseeee
Kweli nakumbuka mwaka waliotutangulia kuna waliopata division three ya points kumi na sita enzi kabla hawajabadilisha badilisha grading lakini wale mabro walipata vyuo na washamaliza kuna waliosoma computer engineering nk.
 
Kweli nakumbuka mwaka waliotutangulia kuna waliopata division three ya points kumi na sita enzi kabla hawajabadilisha badilisha grading lakini wale mabro walipata vyuo na washamaliza kuna waliosoma computer engineering nk.
Yaahh it was before grading and before g.p.a system shule ilikua tait sana na div three walipata nafas za kusoma vyuo
 
PCB mwaka huu hawajafaulu sana tatizo ni vyuo vingi vilivyokuwa vinawachukua vimefungiwa

UDSM hawajachukua MD mwaka huu
KCMC Kimefungiwa
Ifakara Kimefungiwa
Wewe kijana bravo. Kweli PCB huwa ufaulu ni mdogo miaka yote. Ni combination ngumu. Vyuo vingi vya medicine vimefungiwa including Ifakara, songea, etc kama ulivyotaja. On top of that, idadi ya wanafunzi imepunguzwa, mfano Bugando wamedahili 87 badala ya 170 ya miaka yote. Hii imebikumba vyuo vingine pia.
 
Yaani PCB imekua rahisi hivi.....nyie madogo wa sikuhizi inaelekea necta mnaulizwa Define biology?, how many legs does insect have.....
madogo wamekula mabanda (A) mpaka najiuliza hivi sisi ndio tulikuwa vilaza miaka hiyo.....
 
Sehemu kubwa ya waliochaguliwa muhas, wamechaguliwa pia cuhas na udom, na kwa kiasi kikubwa watamua kuconfirm Muhas kutokana na IMANI kuwa hicho ndo bora. Kwa hiyo ombeni tena cuhas na udom na st.John's. Naamini wengi mtapata. Vinginevyo plan B ni kutumia matokeo ya form 4 na kusoma diploma husika na kuhakikisha GPA unayopata haishuki chini ya 3.8 ili kujihskikishia nafasi ya kusoma digrii mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom