Diva'loveneslove' hajui kupika

Mkare_wenu

JF-Expert Member
Mar 11, 2011
1,714
442
Nilikuwa nasikiliza kipindi chake cha 'ALA ZA ROHO' kinachoruka hewani kuanzia saa 4-6 usiku(clouds fm) ambapo alikuwa anasherehekea birthday yake na aliwaalika watu kadhaa studio.Katika porojo za hapa na 'waalikwa' alinishangaza pale aliposema HAJUI KUPIKA,nikajiuliza inakuwaje msichana wa kitanzania umri kama wake asijue kupika,au ndio uzungu?!

NAWASILISHA.....!!!
 
We unatakaje? Wanaosomea mapishi hawana wazazi?
Acha kumpa umaarufu asio stahili.
Yaani tuache kujadili hatma ya nchi tumjadili mtu asiyejua kupika?
 
We unatakaje? Wanaosomea mapishi hawana wazazi?
Acha kumpa umaarufu asio stahili.
Yaani tuache kujadili hatma ya nchi tumjadili mtu asiyejua kupika?
hatima ya nchi! Unaingia jukwaa hili, si ungeenda jukwaa la siasa.
 
Kuna pattern hapa JF ya kuiandama sana Clouds Media group na personalities wake. Najiuliza kwa nini iwe hivyo? Mara mishahara ya watangazaji, mara Kibonde, mara sijui Adam Mchomvu na Fetty wamefanya nini, mara Diva Loveness Love (I like her by the way. She is sassy and classy and perfect for her job) hajui kupika. Kama hajui kupika wewe inakuhusu nini hasa?
 
Hawana uzalendo na Tanganyika
 
huyu mtoto ni limbukeni, sidhani ka kutokujua kupika kwa mtoto wa kike ni sifa njema, na hapa anaeonekana na makosa si yeye bali ni wazazi wake alilewaje? hata watoto wa huko mbefele ambao anajaribu kuimitate lifestyle yao wengi tu wanajua kupika na ka hawajufundishwa utotoni anajifunza kwa kusoma au kuangalia aache ulimbukeni hizo ni sifa za kijinga badae atasema hajui kufua, then hajui kuoga. Chores ni kuonyesha ustaarabu wako na sio ushamba hebu mwambieni huyo kinda aache udunya
Pukudu@ Ilkiding'a, Arusha

Pale kuna ajira gani? upande mwingine wa shillingi ndo umewaajiri kufunika kikombe

Sasa unataka kusema wafanyakazi wa pale wanafanya kazi ya kanisa? Hebu acheni kuwa na roho za kutu bana. Clouds wametokea mbali sana na jitihada na juhudi zao yatupasa kuzithamini. Wanachangia kwenye uchumi wa taifa na kuna watu familia zao zinategemea hizo kazi watoazo Clouds.
 
wanapewa mshahara na posho kama kawa angalia upande wa pili nani kawaweka hapo?

kuchangia uchumi wa taifa? with what sense? kodi ya jengo na paye? kama ni kuchangia wanachangia matumbo ya watu
 
wanapewa mshahara na posho kama kawa angalia upande wa pili nani kawaweka hapo?

kuchangia uchumi wa taifa? with what sense? kodi ya jengo na paye? kama ni kuchangia wanachangia matumbo ya watu

Kila mjasiriamali anayelipa kodi anachangia uchumi wa taifa. Na kila mfanyakazi anayelipa kodi ya mapato anachangia uchumi wa taifa. Hii ni nadharia nyepesi sana.

Kuhusu ya nani kawaweka hapo hiyo sijui na hainihusu. Navyojua mimi ajira ni hiari. Kama mwenye kampuni anaona biashara haina faida na haki na ni hiari yake kuiacha hiyo biashara. Kama mfanyakazi haipendi hiyo kazi yake naye ana haki ya kuiacha hiyo kazi ili mradi tu taratibu zote zinafuatwa.
 
kila mjasiriamali anayelipa kodi anachangia uchumi wa taifa. Na kila mfanyakazi anayelipa kodi ya mapato anachangia uchumi wa taifa. Hii ni nadharia nyepesi sana.

Kuhusu ya nani kawaweka hapo hiyo sijui na hainihusu. Navyojua mimi ajira ni hiari. Kama mwenye kampuni anaona biashara haina faida na haki na ni hiari yake kuiacha hiyo biashara. Kama mfanyakazi haipendi hiyo kazi yake naye ana haki ya kuiacha hiyo kazi ili mradi tu taratibu zote
zinafuatwa.

:a s 103::a s 103:
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom