Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 3,579
- 2,906
==
Kuelekea 2030 upatikanaji wa huduma za afya kuwa zero kilometa kutoka kilometa 5 ya sasa ambazo zimefikiwa chini ya Uongozi wa Rais Samia.
Kufikia mwaka 2050 Dira ya maendeleo ya Taifa inatarajia kuwa na jamii yenye afya ambapo kila mtu anapata huduma za afya kwa usawa na kwa gharama nafuu. Rais Samia ametengeneza msingi wa kufanikisha matarajio haya kwa kuongeza vituo vya kutolea huduma za afya (Health facilities) kutoka 8,783 mwaka 2020, na kufikia 12,846 Mwaka 2025, sawa na ongezeko la vituo 4,063 ikiwa ni 46.26% Ongezeko hilo limesogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi ambapo sasa 75%ya wananchi wanapata huduma za afya ndani ya kilomita 5 ya maeneo wanayoishi.Rasilimali watu ni muhimu katika maendeleo kiuchumi na ndiyo maana Rais Samia ameongeza vituo na ni msingi wa kufikia matarajio haya ya Dira ya maendeleo ya 2025-2050.
Dira mpya ya maendeleo inatarajia kuwa ifikapo mwaka 2050, Tanzania inakua ni taifa ambalo hakuna mwanamke anayepoteza maisha wakati wa kujifungua na kila mtoto anayezaliwa anaishi na kustawi. Rais Samia ameongeza mara 18 ya idadi ya hospitali zinazotoa huduma ya magonjwa ya dharura (EMD) kutoka hospitali saba (7) mwaka 2020 hadi 125 mwaka 2024. Vilevile, vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma za upasuaji wa dharura wa kumtoa mtoto tumboni vimeongezeka kutoka 340 mwaka 2020, hadi 577. ambapo vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka vifo 556 kwa kila vizazihai 100,000 mwaka 2015 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi mwaka 2022 ambapo ni tofauti ya vifo 452 ambayo ni zaidi ya mara tano ya vile vilivyokuwepo mwaka 2020 sawa na asilimia 435.
==