Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.
Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.
1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.
2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.
Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?
3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?
Hitimisho
Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.