Dira ya Rais Magufuli kwa watanzania ni ipi? (What vision Magufuli has for Tanzanians?)

CCM mbele kwa mbele ... wacha waisome number ... Magufuli ni Chaguo la Mungu.... New Sokoine, New Mrema ...
 
2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?
ndugu yani watz sisi ni shida,...
wanasiasa ndo wanaonekana safi kuliko watumishi wengine,....
nahuu msingi umejrngwa na wanasiasa ili kujiandalia mazingira ya upigaji dili,..
hii leo ukijulikana upo b.o.t2 mtaani ni shida,..
na kma umechukua kamkopo kako bas taarifa zinaenea mtaa mzima flani ni mwizi,...
inabididi hizi dhana zibadilishe,.na kubadilisha kwake ni kuingoa FISIEM
 
Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.
Dira ni kumkamata fisadi Lowasa,

Hatua kwa hatua atafikiwa
 
3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?
hapa napata picha1,..
hivi kama rais ni mwema na anafanya kaz za waTZ kwanini asikosolewe,..,,,
na kinachoogopwa ninini kukosolewa kwake,,,..
alafu hizi sheria zipo kwa watu maskini akina sie,...
mbna watu wazito wanakosoa serikali bila tatizooo...,...
hii nchi ni yetu na marais tunawachagua kufanya kaz za wanachi,..sasa kma wanakosea tatizo ni nini
kuwakosoa wajirekebishe,....shida ni nini,...
hii nchi tangu jp awe rais naona harufu ya udictator inakuja,,....
lazima ujiulize kwanini asikosolewe??????anakosolewa obama rais mwenye kauli duniani sembuse jm
aaaaahhhhh TZ ni nchi yetu,...
tunaibiwa mali na rasilimali zetu,..na huku nako tusiongeeee???
 
mnauliza vision wakati mshampa ikulu? na mmesahau urais wa Tz ni ufalme mdogo. tulieni jahazi liende kwa upepo likigota 2020 ndo tutaulizana vision
ni watu wachache wasiojielewa ndo walimpitisha,...
uki+ na wizi,..
but majority hawakumpisha,..
 
Nakubaliana na wewe kuwa hiyo ndio VISION YAKE. Hii slogan ya HAPA NI KAZI TU inaweza kutafsiliwa kuwa ni kuhimiza wananchi wafanye kazi ili WAJITEGEMEE; Kama watafanya kazi ni wazi watawajibika[ ACCOUNTABLE}; na kama watawajibila ni dhahili kazi yao itaonekana [ TRANSPARENT} na mambo yote haya nido yanayoleta UTAWALA BORA!!! Mahala popote penye utawala bora wa kweli rushwa haina nafasi!!
kufanya kazi kwa wanachi kunahusiana nini na utawala bora??????
a
 
DIRA YA NINI? KWANZA ANA KAZI KUBWA YA KUREKEBISHA MADUDU YALIYOFANYWA. TUMPE USHIRIKIANO KWANZA BAADAE TUTAJUA DIRA YAKE!
 
DIRA YA NINI? KWANZA ANA KAZI KUBWA YA KUREKEBISHA MADUDU YALIYOFANYWA. TUMPE USHIRIKIANO KWANZA BAADAE TUTAJUA DIRA YAKE!
madudu yalifanywa na rais wa chama gani??
na je alipokuwa akifanya hayo madudu wananchi mlikuwa wapi???
na pia mlichukua hatua gani????
na kama mlishindwa kujua hayo madudu yaliyopita kwa sababu zenu
je mtawezaje kujua madudu ya ssa hivi????
na huyu akifanya madudu tufanyaje????wakati zama zake zitakuwa zimepita,.....
na je kwanini tusimkosoe sasahivi asifanye na ajiepushe na hayo madudu??????
tz tusisubiri muda wa kiongozi upite ndo tuanze kublame,...
mda ni ssa wa kujudge
 
Huyu mtoa post amebeba nafsi yake wala ajafanya utafiti wowote.mi nataka tu aniambie miez 2 kama yeye angekuwa rais WA tz iliyokuwa imeoza angeifanyia nini.au ulikuwa hujawai kwenda kupata Huduma kwenye ofisi yeyote za serikali?. Maana ungeona utofaut kidogo na sasa.na hapo ni miez 2 nizam imeanza kukaa sawa.na swala la nizam kazn ndo Lamsing kuliko kitu chochote.ulitaka wala rushwa waendelee kula rushwa?.au ulitaka nini.wakati mwingne tuwe tunashukuru hata kwa hich kidogo magufuli alichotufanyia.watoto wetu wanasoma bule.tumpe miaka 5 hii ndo uje ulalamike.we mwenyewe maendeleo ya familia yako hukuyafanya kwa miez miwili.
 
... Gazeti la MAWIO limefutwa... Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo....

Ukitaka kujua dira ya Magufuli sikiliza hotuba yake kwa viongozi wa chama cha wafanyabiashara hivi karibuni. Kama unajua maana ya dira itaiona dira yake. Anaongelea "Capitalist Mixed Economy." Tafuta kwenye google ujielimishe zaidi kuhusu falsafa hii na dira yake.

Halafu, usichanganye mambo. Mawio wanayo makosa yao. Walistahili adhabu tangu siku zile wanaandika story za uwongo kama vile story ya "Maaskofu wapigwa." Hii ilikuwa story ya uwongo. Walishatoka nje ya mstari siku nyingi. Sio halali kwa gazeti kumsafisha Askofu aliyezaa watoto watatu nje ya ndoa, huku akiwa amezaa watoto hao na wanawake tofauti. DECEPTION ni kosa kubwa sana kwenye media industry. Na wahariri wa Mawio walikuwa wanasumbuliwa na upofu wa kimaadili.
 
Watanzania bwana.
Yule alyetoka dira yake ilkua ipi na ameitekeleza vp.
Mimi hata sitaki kujua dira ya huyu wa sasa coz nnayoyaona na kuyaskia yananpa faraja zaidi...
We are about to see the light at the end of the turnel...
Umeongea vema mkuu. Watu wanakosoa bila kutoa solution na kama tupo smart inabidi tufanye evaluation ya utawala uliopita ili tuone kama huyu wa sasa anaperform above or under. Mm sioni logic ya kukosoa timua timua wakati watu wanaotimuliwa wanaonesha kabisa udhaifu wa moja kwa moja. Mf ishu ya utoroshwaji wa makontena, ishu ya NIDA hakuna jinsi viongozi wa taasisi izo kubaki kazini wakati wanaharibu, wapo watu wengi wanaoweza kufanya kazi kwa ufanisi
 
Ukitaka kujua dira ya Magufuli sikiliza hotuba yake kwa viongozi wa chama cha wafanyabiashara hivi karibuni. Kama unajua maana ya dira itaiona dira yake. Anaongelea "Capitalist Mixed Economy." Tafuta kwenye google ujielimishe zaidi kuhusu falsafa hii na dira yake.

Halafu, usichanganye mambo. Mawio wanayo makosa yao. Walistahili adhabu tangu siku zile wanaandika story za uwongo kama vile story ya "Maaskofu wapigwa." Hii ilikuwa story ya uwongo. Walishatoka nje ya mstari siku nyingi. Sio halali kwa gazeti kumsafisha Askofu aliyezaa watoto watatu nje ya ndoa, huku akiwa amezaa watoto hao na wanawake tofauti. DECEPTION ni kosa kubwa sana kwenye media industry. Na wahariri wa Mawio walikuwa wanasumbuliwa na upofu wa kimaadili.
Hiyo siyo vision bali ni mfumo wa uchumi.
 
Tutaheshimiana mwaka huu. Eti Rais hana dira. Mtoa hoja akajipange. Whoever ulietoa hoja ukitudi uanze na kusema na ni lipi ambalo JPM kakosea mpaka sasa.
Niambie dira ya Magufuli ni ipi, kwani ni siri?
 
Vision;
A corrupt free nation and economically independent, functioning government and responsible citizens:
Hiyo vision ameitamkia wapi na lini. Hiyo vision inafikiwa kwa kipaumbele cha kuvunja nyumba na kudidimiza demokrasia. Vision hiyo inafikiwa kwa kuwaaminisha watumishi wa umma kama mashetani na kuaminisha wanasiasa hasa wa CCM kama malaika wakati ufisadi unaanzishwa na kusimamiwa na wanasiasa na hasa wa CCM.
 
Inaonyesha wazi, hauko Tanzania ya leo!!
Wizi wa pesa zote hizo na kuzirejesha kwa watanzania huoni dira?
Wazembe na wazinzi kutumbuliwa kama Jipu huoni dira?
Elimu bure sasa huoni dira?
Heshima kila ofisi ya serikali huoni dira?
Basi yawezekana wewe ni MEMBE Era.
Poleni sana utaiona dira baadaye.
Hapo ni kazi tu.
Maskni, kama hizi ndiyo dira basi nchi hii hatujui Magufuli anatupeleka wapi?
 
Kwa nini hukumuweka Ikulu huyo unayedhani aliyejiandaa kuongoza nchi yako?

Kulitetea gazeti la Mawio lazima uwe mjinga au ujivike ujinga na upumbavu.

Kama ungekuwa umesikiliza hotuba ya Rais Magufuli wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 nadhani usingeweza kujenga hoja za kijinga!

Kabla hujaanza kubwabwaja ujinga ungepitia kwanza hapa;

Ujinga pia ni kipaji!
Kwa hiyo wewe unaona kuwa vision ya Magufuli ni hiyo mpaka ukatafute kitabu ndiyo usome? Vision inakaa kwenye finger tips wala huhitaji kutafuta makabrasha
 
Dira yake ni BomoaBomoa na Fukuza Fukuza ndo maana anaitwa Tingatinga.
Hii yaweza kuwa ndiyo dira yake maana ndiyo inaonekana ni kipaumbele chake. Ila umesahau ana dira ya kudidimiza uhuru wa kutafuta na kupata habari. Ona yanayoendelea bungeni. Ni aibu tupu.
 
Back
Top Bottom