Dira ya Rais Magufuli kwa watanzania ni ipi? (What vision Magufuli has for Tanzanians?)

Hivi niwaulize Wadanganyika toka imeanza serikali ya awamu ya tano tumeshapata dira ya maendeleo ya Taifa?. Je wananchi tunafahamu tunaelekea wapi kiuchumi, kimaendeleo, kisiasa, kijamii, kiutamaduni? au kiongozi anakurupuka na chochote kilichopo mbele yake. Binafsi naona kama tunazidi kupoteza mwelekeo, wataalam tusaidieni. Mara sukari ipo ya kutosha!!!, mwezi mmoja baadaye sukari imeadimika!!, wiki mbili sukari imefichwa!! tani ngapi tani 5, mara 165 n,k lakini ukiangalia ni sukari kidogo sana imeonekana kwenye maghala ya watu. Maana yake aliyesema Sukari ipo ya kutosha kadanganya ni jipu-litumbuliwe, aliyeagiza sukari isiingizwe kutoka nje bila kufanya utafiti/maandalizi ya kutosha na yeye ni jipu-litumbuliwe. Binafsi bado sijamwelewa Raisi wetu na sioni mwelekeo wa kumwelewa, shida zimeongezeka, hduma za afya zimeshuka sana, watendaji hawaajiamini tena kila kiongozi anafanya kazi kama vile kesho anafukuzwa. Rushwa sasa hivi Polisi hawapokei Tshs 2000 wanataka 30,000 hadi 100,000 wakidai ni bora apate za kutosha ili akitumbuliwa kafaidi. Mhh yangu macho
 
Huku mteule Naiba Spika akitekeleza wajibu wake aliotumwa na wakubwa zake wa kudidimiza demokrasia, ngoja tujikumbushe tuliyojadili hapo kabla.
 
Orodha ya kupapasa papasa bila ya direction inaongezeka. Ni mwendo wa nyuma geuka, kushoto geuka, kulia geuka, mara Dodoma, yaani ni giza nene.

Kuna ambao wanasema oo kuna dira ya viwanda, iko wapi? Nani atajenga viwanda wakati Magufuli anaua sekta binafsi ambayo inatakiwa iendelezwe ili ipate uwezo wa ku-reinvest kwenye maeneo mengine ikiwemo viwanda, Serikali haiwezi kujenga viwanda. Magufuli sasa amebaki kutukana wananchi wake mara vilazaa, mara sijaribiwi, mara msitangulize watoto mbele. Hakuna mwelekeo, nchi ipoipo tu.
 
Back
Top Bottom