Dira ya Rais Magufuli kwa watanzania ni ipi? (What vision Magufuli has for Tanzanians?)

Dira ya Magufuli mbona iko wazi tunaona inatekelezwa?

Tatizo mnayo macho hamtaki kuona, mnayo masikio hamtaki kusikia.

Mnataka mambo yabaki yaleyale muendelee kunufaika na mfumo wa kipuuzi.

Magufuli dira yake ni kuona rasilimali za nchi hii zinanufaisha watanzania wote na sio watu wachache. Majipu yanayotumbuliwa sasa ni yale ambayo hayataki kubadilika kufuata dira ya rais. Kama na wewe ni mmojawapo pole sana...
 
He have a concrete foundation with our country coz nch yetu Ina msng mbovu yote anayoyafanya ni dira pekee kuonyesha matumain kwa watanzania weng
 
Ni Rais mwenye rangi 2, tujiulize hizi vurugu zinazoendelea kwenye chaguzi za mwenyeviti wa halmashauri, manispaa na majiji hazioni? Hivi wakurugenzi sio waajiriwa wa serikali? Kosa la kuvuruga uchaguzi pasipo sababu za msingi zinatofauti gani na wale wanaotimuliwa?

"Hakuna mwananchi wa Dar aliyemwambia Magufuli wakati wa kampeni kuwa tatizo/kero kuu ya Dar ni watu kujenga mabondeni, kufa kwa mafuliko au Matajiri wa Dar wanapata shida kuishi na masikini"
 
mnauliza vision wakati mshampa ikulu? na mmesahau urais wa Tz ni ufalme mdogo. tulieni jahazi liende kwa upepo likigota 2020 ndo tutaulizana vision
 
VISION 2025 na ilani ya CCM

Queen Esther

Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.
 
Vision;
A corrupt free nation and economically independent, functioning government and responsible citizens:

Nakubaliana na wewe kuwa hiyo ndio VISION YAKE. Hii slogan ya HAPA NI KAZI TU inaweza kutafsiliwa kuwa ni kuhimiza wananchi wafanye kazi ili WAJITEGEMEE; Kama watafanya kazi ni wazi watawajibika[ ACCOUNTABLE}; na kama watawajibila ni dhahili kazi yao itaonekana [ TRANSPARENT} na mambo yote haya nido yanayoleta UTAWALA BORA!!! Mahala popote penye utawala bora wa kweli rushwa haina nafasi!!
 
Halafu nadhani ww unatizama sana CNN, Obama kati ya yote aliyoahidi ni mangapi katimiza????
 
Tutaheshimiana mwaka huu. Eti Rais hana dira. Mtoa hoja akajipange. Whoever ulietoa hoja ukitudi uanze na kusema na ni lipi ambalo JPM kakosea mpaka sasa.
 
Halafu nadhani ww unatizama sana CNN, Obama kati ya yote aliyoahidi ni mangapi katimiza????
Huyo Obama misingi mingi imetengenezwa kabla hata hajazaliwa yeye kafanya kuchagua afanye kipi!sidhani kama mfano huo utatufaa pana mtu katoa mfano wa Thomas sankara naungana nae.Nchi hii leo yanafanyika mambo yanaonekana mapya waqt ni utaratibu wa kawaida kwenye serikali so tumpe muda na support than time will tell.
 
Mimi kuwa tu na confidance kuwa lolote la uzembe likitokea nikashitaki yupo mtu wakunipa haki yangu inatosha kabisa..... Ilifika wakati wengi tulikuwa hatujui tukimbilie wapi maana kulikuwa na raia daraja la kwanza la pili na la tatu.... Sasa hivi ninajisikia kuwa raia ambaye nina Rais anayejali haki zangu za kiraia!
 
Halafu nadhani ww unatizama sana CNN, Obama kati ya yote aliyoahidi ni mangapi katimiza????
Katimiza almost yote..... affordable care act, kurudisha majeshi kutoka Irak & Afganistan, kuzungumza na Russia na kupunguza nuclear arsenal, kutengeneza ajira zaidi ya 18 mill., climate agreement, kusimamisha mradi wa keystone pipeline, kuzungumza na Iran & Cuba, haki za wasenge, kuchimba na kujitegemea kwa mafuta, excecutive order za uhamiaji, nk. Kabakiza moja tu la kufunga Guantanamo Bay detention camp ambalo anahakikisha atalifunga mwaka huu.
 
Vision inaendana na wakati.

Vision ya sasa ni kuondoa mabaki yote ya Lowasa kwenye serikali yake.
 
Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.
Kimsingi, unataka kuaminisha wasomaji wa hoja yako kwamba wewe ni mwelewa, and you are NOT. Vinginevyo, usingeanza kutuuliza dira ya serikali iliyo madarakani. Rais Baraka Obama wa US ni mwana chama wa Democratic party, na kwa hiyo anatekeleza dira na policies za chama chake. Rais JP Magufuli wa JMT ni mwana chama wa CCM. Kwa hiyo anatekelezo dira na policies za CCM. Katika kipindi chote cha campaign JPM amezunguka nchi nzima kutangaza vision na mission ya serikali yake. Kama hukupata kusikia alichosema tafuta angalao hotuba yake ya Bungeni miezi michache tu iliyopita. Then, naamini hutarudia tena kuja na hoja za kizushi na kinafiki.
 
Mie nafikiri kweli raisi wetu anajitahidi kufanya kazi...na ni dhahiri ana nia ya Dhati hata matendo yake anaonyesha. .. anania nzuri!! Lkn ukweli kuna makosa anafanya japo ni ya kiufundi, mf.watumishi wa Umma kama ilivyo kwa watumishi wa aina yeyote ile duniani ile waweze kufanya kazi lazima uwape motisha. Na motisha sio lazima iwe pesa tu la hasha, hata maneno wakati mwingine hutumika kama motisha. Sasa, Tanzania ya sasa watumishi wa Umma wanaishi kwa kutishwa tu, kila kiongozi anaeongea nao ni vitisho tu...vinatumika eti ili wafanye kazi na wa lete ufanisi kazini!! Vitisho kwa wakurugenzi, mawaziri, makatibu wakuu, maofisa, polisi, walimu , wauguzi , madaktari n.k.... vitisho, vitisho....ili lazima wafanye kazi! Kweli itasaidia????
 
Hivi utawezaje kufuata dira yako kabla ya kujisafishia njia yako iliyojaa miba na misitu mikubwa? utajiendea tu? labda huishi Tanzania, lkn kama unaishi Tanzania huwezi kushangaa anayoyafanya rais Magufuli.

Ni ukweli usiofichika kwamba wakati anaingia madarakani aliachiwa hazina ikiwa haina kitu huku serikali ikukabiliwa na viporo vya madeni kutoka kwa makundi mbalimbali nchini.

Ukata wa fedha umesababishwa na nini?imesababishwa na matumizi mabaya ya fedha za umma kulikofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali na watumishi wa umma..

Aidha imebainika kwamba serikali imekuwa ikikoseshwa mapato yake yatokanayo na kodi kutokana na wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi,yaani serikalini na ktk sekta ya umma kulijaa uchafu kupitiliza.

Rais yeyote makini angeanza na kusafisha huu uchafu kwanza ili kurejesha nidhamu ya uwajibikaji miongoni mwaka viongozi wa serikali na watumishi wa umma kwanza kabla ya kuanza kuifanyia kazi dira yake ya maendeleo,la sivyo atakuwa anajisumbua bure tu.

Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.
 
1.kubomoa waliojenga holela
Unafikiri ni sahihi kwa watu kujenga bila kuzingatia sheria za nchi!?
2.kufukuza watumishi wazembe na wasio na maadili
Kama ungekuwa rais unafikiri ni njia gani ingefaa kutatua hili tatizo?
Yes obama alitarget elimu na science,lakini raisi wetu aliposema hapa kazi tu we hujafikiria kwamba ametarget nini!?hii yaweza kuwa ndio dira yake,kimsingi kila mamlaka na pia watu binafsi tukifanya kazi kwa manufaa ya nchi kila kitu kitakuwa sawa.

Nakubaliana na wewe kuhusu kufuata sheria hasa hiyo case namba1.

Kiasia nakubaliana na mtoa mada mkuu kuhusu namba2, na pia nakubaliana na wewe kiasi kuhusu namba mbili pia.

Kwamba wanasiasa hujifanya hawakosei na wao siku zote wanajifanya wako sahihi. Hii siyo kweli kabisa. Maeneo mengi waweza kukuta ilikua ni collective responsibility, lakini mwisho wa Siku mtumishi ndiyo huchukuliwa hatua pekee, hii ni double standard. Ni vigumu kuamini kuwa Mabilion yanayotajwa kuliwa au kutumika vibaya ni watumishi wa Umma pekee ndiyo wanahusika bila ya viongozi wanasiasa kuhusika, akili ya kawaida inagoma kufikiri hivyo. Mwisho wa yote mtumishi wa Umma ataanikwa kuwa kafisadi nchi kumbe wakati mwingine maskini aliingizwa mkenge na mamlaka zilizo juu yake.

Lakini pia nikubaliane na wewe pia watumishi wa umma mafisadi lazima waburuzwe Kortini ili iwe fundisho na kwa hakika ili kuondoa ufisadi. Matumizi mabaya ya madaraka, manunuzi yasiyozingatia maslahi ya Taifa ni ya kupigwa vita sana. Kwa pamoja tumsaidie Mh Rais kuondoa makandokando ili tusonge mbele.

Kuhusu hilo la dira ya Rais kwa sasa nachelea kusema ni mapema mno kutoa hukumu, nchi ni kubwa na ina mambo mengi ya kuyatatua, ifike mahali tuvute subira kwanza.

Ama kuhusu kusifia na kukosoa, mimi naamini vyote viende kwa pamoja kwa kuwa hakuna BINADAM Perfect 100%!
 
Back
Top Bottom