Dira ya Rais Magufuli kwa watanzania ni ipi? (What vision Magufuli has for Tanzanians?)

Stabilaiza

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
1,843
1,143
Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.
 
Kwa nini hukumuweka Ikulu huyo unayedhani aliyejiandaa kuongoza nchi yako?

Kulitetea gazeti la Mawio lazima uwe mjinga au ujivike ujinga na upumbavu.

Kama ungekuwa umesikiliza hotuba ya Rais Magufuli wakati wa ufunguzi wa Bunge la 11 nadhani usingeweza kujenga hoja za kijinga!

Kabla hujaanza kubwabwaja ujinga ungepitia kwanza hapa;

In coming to terms with this challenge the people of Tanzania, led by their Government, recognised the need to prepare a New National Development Vision which will guide economic and social development efforts up to the year 2025. The objective of this Development Vision is to awaken, co-ordinate and direct the people's efforts, minds and our national resources towards those core sectors that will enable us attain our development goals and withstand the expected intensive economic competition ahead of us.

It is necessary, therefore, that this Development Vision is shared and supported by all Tanzanians. That is why we sought the views and consensus of a wide cross-section of our society during the formulation process. The draft Development Vision was discussed by various societal groups including Honourable Members of Parliament, all political parties, leaders of various religious denominations, women and youth organisations, chambers of commerce and industry, farmers, professional associations, renowned personalities in our nation's history and ordinary Tanzanians. A Development Vision formulated through such a process is an important pillar in building that level of national unity and cohesion needed to ensure economic development in an environment of peace, security and patriotism.

Ujinga pia ni kipaji!
 
huyu jamaa mwanzoni nilifikiri ni mtu wa ku " take orders" kutoka kwa mkubwa wa nchi tu na kwenda kuzitekeleza, lakini kadri siku zinavyoenda nazidi ku realize nilimu-underestimate, huyu jamaa ni mbunifu wa sera na ni very strategic aisee, subiri time will prove all that
 
1.kubomoa waliojenga holela
Unafikiri ni sahihi kwa watu kujenga bila kuzingatia sheria za nchi!?
2.kufukuza watumishi wazembe na wasio na maadili
Kama ungekuwa rais unafikiri ni njia gani ingefaa kutatua hili tatizo?
Yes obama alitarget elimu na science,lakini raisi wetu aliposema hapa kazi tu we hujafikiria kwamba ametarget nini!?hii yaweza kuwa ndio dira yake,kimsingi kila mamlaka na pia watu binafsi tukifanya kazi kwa manufaa ya nchi kila kitu kitakuwa sawa.
 
Ina maana hukumsikiliza ktk hotuba yake ya kufungua bunge?? Alisema dira yake na sasa anajenga A CONCRETE FOUNDATION.
 
Watanzania bwana.
Yule alyetoka dira yake ilkua ipi na ameitekeleza vp.
Mimi hata sitaki kujua dira ya huyu wa sasa coz nnayoyaona na kuyaskia yananpa faraja zaidi...
We are about to see the light at the end of the turnel...
 
Mtu kuwa na uhuru wa kuji express haimaanishi utumie haki yako hiyo ya msingi kutoa opinions za hovyo hovyo. Obama mwenyewe kachemsha sana kule US nchi ni kama imemshinda afu kwani mfano wa uongozi bora lazima iwe marekani na Obama!?!? Kuna watu kama akina Senkara walifanya makubwa. Magufuri anaanza upya kuisuka nchi na kuendeleza yale mazuri aloyakuta. Ushauri tu don't let emotions cloud your judgement. ' Follow your heart but take your brain with you.'... Chillax sheikh mwache jamaa afanye kazi yake.
 
Inaonyesha wazi, hauko Tanzania ya leo!!
Wizi wa pesa zote hizo na kuzirejesha kwa watanzania huoni dira?
Wazembe na wazinzi kutumbuliwa kama Jipu huoni dira?
Elimu bure sasa huoni dira?
Heshima kila ofisi ya serikali huoni dira?
Basi yawezekana wewe ni MEMBE Era.
Poleni sana utaiona dira baadaye.
Hapo ni kazi tu.
 
w
Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.
wewe ngojea kutumbuliwa tu. vision gani unataka kuelezwa zaidi ya hotuba aliyotoa bungeni kuelezea muelekeo wa serikalu yake.
 
Kwani hao watangulizi wake walokuja na dira zenye mbwembwe na bashasha waliifikisha wapi nchi yetu zaidi ya kutuibia na kutufanya tuwe hapa tulipo? Tulia uone game linavyokwenda ndugu, unataka dira ndani ya miezi miwili?
Dira ni kama zifuatazo;
-kila mtanzania kupata huduma bora za afya ikiwa ni pamoja na madawa na tiba
-kuwa na tanzania ambayo itakuwa bora kwa kukomesha wizi wa mali za umma nk
-nk
MWACHE RAIS WETU AFANYE KAZI YAKE
 
Dira yake ni ilani ya ccm.

Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom