Dira ya Rais Magufuli kwa watanzania ni ipi? (What vision Magufuli has for Tanzanians?)

Hiyo vision ameitamkia wapi na lini. Hiyo vision inafikiwa kwa kipaumbele cha kuvunja nyumba na kudidimiza demokrasia. Vision hiyo inafikiwa kwa kuwaaminisha watumishi wa umma kama mashetani na kuaminisha wanasiasa hasa wa CCM kama malaika wakati ufisadi unaanzishwa na kusimamiwa na wanasiasa na hasa wa CCM.

You see what you want to see, hata kioo kitakuonyesha unachotaka kuona, ukitaka kujiona ulivyo baunsa basi utajiona umejaa, na ukitaka kujiona ulivyokonda utaona ukondefu wako. Toka Gerezani ulikojifunga uishi katika ulimwengu wa uhalisia!!
 
kufanya kazi kwa wanachi kunahusiana nini na utawala bora

Wananchi wakifanya kazi na kuzalisha hawatakuwa mzigo kwa serikali na pia watalipa kodi ambayo itaiwezesha serikali kutimiza wajibu wake wa kulinda usalama wa watu na mali zao; jamii inayozalisha na kujitosheleza ni jamii inayoweza kujitegemea na kuwa na uhuru wa kiuchumi na kimawazo, hivi vyote vinachangia kuwepo na utawala bora!!
 
Kwani wapi wananchi ni mzigo wa serikali? unadhani serikali ipo kwa sababu gani. sio unaweka upuuzi hapa kisa kuna uhuru wa kujieleza.
 
Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.

Hapa hakuna kitu ulichosema:

1.Most of the civil servants ni wazembe, wezi, na hawana moral ya kazi..... hatatua hizi anazochukua raisi ni sahiihi kabisa
2. Watu waliojenga mabondeni wameshaonywa mara nyingi lakini wanakaidi inabidi kufika wakati hatua zichukuliwe
3. Gazeti hili kama limekiuka masharti ya registration yake no way ... sheria ni msumeno
 
Hiyo (Capitalist Mixed Economy) siyo vision bali ni mfumo wa uchumi.

Ndugu: kwani, falsafa za kitaifa kama vile 'Capitalist Mixed Economy,' 'Ujamaa,' 'Harambee,' etc hazina dira ndani yake?
Huna 'competency' katika jambo hili.
For you to learn, you better stay a spectator.
 
kwa kikwte alipo tuachia ilitakiwa aje raisi wakuwarudihisa imani na tumaini jipya kwa wananchi, ilitakiwa aje raisi mwenye busara,hekima,huruma na mchapakazi,yaani na maanisha kiongozi sio manager kama ulivyotanguia kusema,lakini leo unapokuwa na raisi ambaye jambo dongo tu anashindwa kulihandle anakimbilia kwenye media nakuanza kutoa maneno ya ukali na kufukuza fukuza hovyo watu,
mfano mzuri kwa watumishi wa umma wengi wanamatatizo mengi hasa kada za chini,nilijua raisi atakuja na mkakati kuwasaidia hawa walipa kodi kujua kiini cha matatizo yao kabla yakukimbilia kuwatuhumu ni wavivu na wabadhilifu,jambo dogo lingine fikiria tu issue ya watu wamabondeni kabla kuwaadhili watu wewe kama kiongozi wao waandalie mazingira ya kujihifadhi na yenye sura ya ubinadamu....!!!
ningependa wajue ccm inaongoza taifa la idadi kubwa ya watu waliokata tamaa
 
Hapa hakuna kitu ulichosema:

1.Most of the civil servants ni wazembe, wezi, na hawana moral ya kazi..... hatatua hizi anazochukua raisi ni sahiihi kabisa
2. Watu waliojenga mabondeni wameshaonywa mara nyingi lakini wanakaidi inabidi kufika wakati hatua zichukuliwe
3. Gazeti hili kama limekiuka masharti ya registration yake no way ... sheria ni msumeno

1.kwanini watu mishi wauma niwazembe wezi n.k??ulisha jiuliza hilo swali kima chachini pale masjala jiji analipwa shingapi tazama hata mazingira yake yakazi,tazama maisha yake nje ya ofisi,rudi kwa maaskari polisi nenda kwa maafisa ugani,thaminisha kipato na kazi ya mtendaji wa mtaa.
2.Eti watu wanajenga mabondeni na wameonywa sasa huduma za kijamii unapelekaje mahala pasipo stahili kati ya wewe ulibatilisha matumizi ya maeneo hayo na waliojenga nani mwenye akili timamu..!!!
3.huo msumeno unakuwa na makali pale unapowakata walio wanyonge ukigeukia kwenu walaa!!mkosahihi watendaji wa serikali wapelekwa sero na mkuu wa wilaya kisa wamechelewa kwa kifungu kipi cha sheria katika sheria za utumishi wa umma??
 
Nakubaliana na wewe kuwa hiyo ndio VISION YAKE. Hii slogan ya HAPA NI KAZI TU inaweza kutafsiliwa kuwa ni kuhimiza wananchi wafanye kazi ili WAJITEGEMEE; Kama watafanya kazi ni wazi watawajibika[ ACCOUNTABLE}; na kama watawajibila ni dhahili kazi yao itaonekana [ TRANSPARENT} na mambo yote haya nido yanayoleta UTAWALA BORA!!! Mahala popote penye utawala bora wa kweli rushwa haina nafasi!!
kwa kuwarudisha wenye tuhuma mbalimbali kukaa madarakani!! hapa ndio nawakubali wana ccm kwa unafiki
 
Hotuba ya Mhe Rais wakati wa ufunguzi wa Bunge ilionyesha dira na muono wake juu ya Tanzania anayoitarajia / anayoitaka.
 
Dira ya Magufuli mbona iko wazi tunaona inatekelezwa?

Tatizo mnayo macho hamtaki kuona, mnayo masikio hamtaki kusikia.

Mnataka mambo yabaki yaleyale muendelee kunufaika na mfumo wa kipuuzi.

Magufuli dira yake ni kuona rasilimali za nchi hii zinanufaisha watanzania wote na sio watu wachache. Majipu yanayotumbuliwa sasa ni yale ambayo hayataki kubadilika kufuata dira ya rais. Kama na wewe ni mmojawapo pole sana...
kwakukubali kuwarudishia madaraka walio tuhumiwa kuliibia taifa katika sekta hizo nyeti
 
Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa.

Raisi Magufuli anatekeleza dira ya sera na dira ya CCM.

1. Ni pamoja na kuboresha hali za wananchi hasa wale wa kipato cha chini -hii ni kupitia mpango wa elimu ya bure na unafuu wa kulipa kodi. Hii ni pamoja na elimu bure kuanzia darasa la kwanza.

2. Kuwa na serikali isiyo tegemezi kwa fedha za misaada kutoka mataifa tajiri na kugemea kutumia fedha hizo kuendesha serikali. Hii inathibitishwa na ongezeko la ukusanyaji kodi kutoka TRA.

Pia kumbuka fedha hizi (za wafadhii) sehemu kubwa ndio ziliishia kununua tiketi za ndege za kuzunguka dunia kusambaza mabakuli ya kuombea fedha ingine.

3. Kuondoa vitendo vya RUSHWA na UFISADI ambavyo ziliota mizizi na sasa tumeona yalotokea Bandarini, TRA, Uhamiaji na NIDA ambapotumeona jinsi fedha za umma zilivyokosekana kutokana na watu kutolipa kodi na pia zilivyoibiwa.

4. Kuboresha mazingira ya AJIRA na waajiriwa kwa kuondoa wageni ambao wanafanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania na kuwatengenezeawafanyabiasha na wenye viwanda mazingira mazuri ya kustawisha biashara zao na ajira kwa watanzania.

5. Kufufua viwanda na kuviboresha vingine kama viwanda vya ngua na vile vya kusindika samaki.

6.Maboresho ya katiba - kumbuka aliemtangulia hakuweza kushughulikia suala la katiba kikamilifu kwa miaka 10 ilopita.

7. Suala la Zanzibar tulivu- kuhakikisha kisiwa hiki kina uongozi makini na wananchi wenye Amani.- Hii nafahamu utasema kitu.

Haya ni machache tu mengine huwa raisi anawea kuja nayo kadiri muda unavyozidi kujongea.

Hivyo basi kwa kifupi DIRA ni katika maeneo haya:

SERIKALI KUJITEGEEA KWA KUTUMIA KODI INAYOKUSANYA NA KUBANA MATUMIZI
ELIMU
RUSHWA NA UFISADI
AJIRA
VIWANDA
KATIBA

NA MENGINE Afya na Zaidi na Zaidi.

HITIMISHO

Mkuu, kama wewe ni Mbunge basi timiza wajibu wako wa kujadili matatizo na kero za wananchi kwa kutumia uhuru ulopewa haki au "mandate" na wananchi wako ya kufanya hivyo, bila kungoja kwanza Live Broadcasting ya TBC.

Serikali ikiishajiweka sawa matangazo yatakuja yenyewe, isipokuwa hakuna nchi yoyote duniani ambayo inaweka matangazo yake ya Bunge Live siku nzima bali kwa majadiliano maalum ambayo huwa hayazidi hata saa moja.

Angalia SKY NEWS, BBC, CNN au hata KBC wa jirani kama wanafanya live parliament broadcasting all day huo ni ujinga.

Ila kama wewe ni mwananchi basi subiri recorded programmes ambazo hutayarishwa ili kuonyesha sehemu muhimu za majadiliano Bungeni, si unafanya kazi mkuu?

Fuatilia tena kama KBC na nchi jirani kama wanafanya hivyo, halafu nda nchi zilizoendelea kama UIngereza na wengine kama hawaweki recorded sessions maana Mbunge akienda jimboni si atatoa taarifa ya kazi yake Bungeni?

Kuhusu UHURU wa vyombo ya habari kuna mwanachama amekujibu vizuri kuhusu hilo hapo juu.

Hata nchi zilizoendelea kama Marekani na hasa Uingereza sasa hivi wamepitisha kitu kinaitwa Royal Charter, hii ni kuvibana vyombo vya habari ambayo vinaandika habari za uongo, zile ambazo zimepata kwa njia ya kuingilia mawasiliano ambapo ni kuvunja sheria.

Kwahio tusipende kurudisha nyuma jitihada za serikali ya awamu ya tano bila sababu za msingi au zile za kitoto.

Tanzania Oyeeeeee!

MUNGU Ibariki Tanzania
 
Ukitaka kuijua vision ya Magufuli jitahidi upate maoni ya watu waliompigia kura. Ni jambo la maana sana kwa mleta mada kuhamisha akili yake kutoka awamu ya nne ili ihamie katika awamu ya tano. Anaonekana kuwa ni wale wale wakazi wa Dar waliopigia kura UKAWA wakasahau kuwa kanda yote ya ziwa umempigia kura Ngosha. Bomoa bomoa ni zoezi lililochelewa kufanyika kwa sababu ya siasa za awamu zilizopita. Na sio kweli kuwa watumishi wa umma wanachukuliwa kama mashetani, Magufuli anataka watu wafanye kazi wakiwatanguliza wananchi na sio kutanguliza akili za ubinafsi na dharau. Nilishawahi kushuhudia mfanyakazi wa wizara ya ardhi makao makuu akimtukana bibi anayeweza kumzaa mama yake, tena bila hata ya kumtazama usoni kwa sababu yule bibi alikuwa kasimama pembeni ya foleni kwani hana nguvu ya kupanga foleni, alisema miguu inamuuma, sasa mfanyakazi kama huyo wa wizara ya ardhi ni lazima akumbane na moto wa Magufuli. Ngosha apewe muda, na tunapompima utendani wake tuondoe vichwani mwetu yale mazoea ya maisha ya awamu ya nne.
 
Wananchi wakifanya kazi na kuzalisha hawatakuwa mzigo kwa serikali na pia watalipa kodi ambayo itaiwezesha serikali kutimiza wajibu wake wa kulinda usalama wa watu na mali zao; jamii inayozalisha na kujitosheleza ni jamii inayoweza kujitegemea na kuwa na uhuru wa kiuchumi na kimawazo, hivi vyote vinachangia kuwepo na utawala bora!!
watu wakafanye wapi kazi,....
kma serikali haijaweka vyanzo vya ajira?????
na watu hawana mitaki ya kujiajili,..
hayo mambo unayozungumzia zungumziakma kuna sources za ajira,...
 
watu wakafanye wapi kazi,....
kma serikali haijaweka vyanzo vya ajira?????
na watu hawana mitaki ya kujiajili,..
hayo mambo unayozungumzia zungumziakma kuna sources za ajira

Kazi kubwa ambayo jamii yetu inatakiwa kufanya ni kufuta hii mentality ya kutegemea kuwa serikali ndio itatengeneza ajira za watu wake!!! Serikali kweli ina wajibu wa kuweka mazingira rafiki ya kuwezesha wananchi wafanye shuhuri za kuweza kujiajili wenyewe; lakini sisi wananchi wenyewe ndio tunatakiwa kuwa na dhamira ya kufanya shuhuri zetu kwa kujitegemea wenyewe.
 
shuhuri zetu kwa kujitegemea wenyewe
shughuli gani sasa mkuu mbna huna facts,...
mamantiliee????
wanafukuzwa na police,mgambo wakichukua sifuria dk5 mbele zinarejeshwa tupu,..
shughuli gani mkuu????
serikali haiwezi kukwepa dhana ya kuandaa mazingira rafiki ya upatikanaji wa ajira,..
 
Mpaka sasa ni miezi mitatu tangu Magufuli awe Rais lakini ni vigumu kujua dira yake kama Rais ni ipi hasa. Naomba niseme awali kabisa kwamba uhuru wa kuongea na kutoa maoni ni haki ya msingi anayozaliwa nayo binadamu siyo hisani ya mtu. Ndiyo maana mtoto akizaliwa hulia kama ishara ya uhuru huo wa asili. Ndiyo maana katiba ya nchi yetu imezingatia asili ya mtu ya kuwa na uhuru wa kutoa na kutafuta habari. Angalizo la awali ni kuwa habari siyo za kupamba tu, hata za kuuliza au kukosoa nazo ni habari na zinaenda sambamba na uhuru huo wa asili. Asije mtu akasema hapa kwamba ni makosa kuacha kumsifia Rais bali ni halali kumsifia Rais.

Nikirejea Obama, japo si rais wa Tanzania, lakini ilikuwa ni rahisi kwa mtu kutambua kuwa dira ya Obama katika uongozi wake ni pamoja na kuona kuwa Marekani inaongoza katika Nyanja ya Sayansi na Elimu. Hivyo akafanya jitihada za kuchangia kufikia dira hiyo ya uongozi wa marekani. Cha kushangaza katika nchi yetu tunashuhudia mambo mchanganyiko ambayo hata haijulikani yanachangia dira gani ya Magufuli kama rais. Sababu zifuatazo zinachangia mkanganyiko wa kutojua dira ya Rais.

1. Kuvunja nyumba za watu bila msaada wowote
Sifahamu kuvunja nyumba za raia wan chi yetu kunachangia katika dira gani ya rais. Ninachoelewa ni kuwa wananchi wakikosa makazi na huduma zingine za jamii, hakuna maendeleo.

2. Kuaminisha umma kuwa wafanyakazi wa umma ni mashetani (Demonizing Public Servants)
Mpaka sasa kumekuwa na fukuzafukuza ya wafanyakazi wa umma. Pia kumekuwa na maamuzi mbalimbali ya kudhibiti wafanyakazi wa umma, hata pale wanapotafuta maarifa zaidi. Sababu mbalimbali za kufukuza na kudhibiti zinatolewa. Fukuzafukuza na kudhibiti wafanyakazi vyote vinatoapicha kuwa wafanyakazi wa umma ni wabaya kabisa kushinda watu wote katika nchi hii.

Lakini katika nchi yetu ni mfanyakazi gani mwenye uwezo wa kumdhibiti mwanasiasa? Ninachoamini ni kuwa watendaji wa umma wanazidiwa nguvu na wanasiasa na ndiyo maana wanalazimishwa kuingizwa katika maamuzi yasiyofaa ya ufisadi. Tujiulize ni wanasiasa wangapi ambao waliokuwa kwenye serikali iliyopita ambao wamewajibishwa kwa kuwalazimisha wafanyakazi wa umma kufanya kinyume na matakwa yao? Hii fukuzafukuza inawafanya wanasiasa kuzudi kuwa na nguvu ya kufanya chochote wanachojisikia kufanya kwa waajiriwa wa umma. Hivi, wanasiasa ndiyo wako sahihi siku zote na kwamba wafanyakazi wa umma ndiyo mashetani siku zote? Ni vigumu kuamini hii hali na serikali inatakuwa kubadili mwelekeo huu. Wafanyakazi wa umma wanastahili kuheshimiwa na siyo kuonekana kama hawafai kabisa, na kwamba wanaofaa ni wanasiasa pekee. Kwa kuonyesha wafanyakazi wa umma kuwa ni mashetani na wanasiasa na hasa wa kutoka CCM ni malaika kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

3. Kudidimia kwa demokrasia nchini
Tumeshukudia mamluki wakiletwa na CCM kutoka Zanzibar ili wachague Meya wa Ilala na Kinondoni kabla ya UKAWA kuja juu kupinga ukiukwaji wa sheria wa waziwazi. Kama hiyo haitoshi, Kilombelo nako Mbunge amedhalilishwa kwa kukatazwa kupiga kura ya kuchagua Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji. Pia tumesikia watu wakikatazwa kuwa ni mwiko kumkosoa Rais, kwamba kumkosoa Rais kunatakiwa kufanywa kwenye siri. Gazeti la MAWIO limefutwa. Kitu cha kujiuliza, kudidimizwa huku kwa demokrasia kunachangia dira gani ya Magufuli kama Rais?

Hitimisho

Inaonekana kuwa Rais Magufuli hakujiandaa kuongoza nchi yetu na hajui afanye kitu gani hasa. Kwa ufupi ni kama Rais hana dira kwa nchi yetu. Magufuli anaonekana kama Meneja siyo kiongozi wa kuonyesha njia (dira). Yeye ni mtu wa kudhibiti, tena wakati mwingine udhibiti ambao unafifisha demokrasia na asili ya mwanadamu kuwaza na kutenda kwa uhuru ili kufikia maendeleo. Sasa wanasiasa wanatamba wanavyopenda, hivi sheria inawapa heshima wanasiasa pekee na inawanyima heshima wafanyakazi wa umma? Rais anatakiwa afahamu kuwa hakuna maendeleo bila demokrasia na uhuru wa kuwaza na kuwasiliana.

Question?

Can one have a vision for Tanzanians?
 
shughuli gani sasa mkuu mbna huna facts,...
mamantiliee????
wanafukuzwa na police,mgambo wakichukua sifuria dk5 mbele zinarejeshwa tupu,..
shughuli gani mkuu????
serikali haiwezi kukwepa dhana ya kuandaa mazingira rafiki ya upatikanaji wa ajira,

Tatizo linalowapata wakina mama ntilie ni sababu ya kuwa na uongozi mbovu kwenye halmashauri na manispaa zetu; wakina mama ntilie wanatakiwa watengewe sehemu mahususi ambapo watafanya kazi zao bila bugudha , lakini kwa vile hawatengewe sehemu za kufanyia kazi zao ndio maana wana zagaazagaa sehemu wasizostahili kuwepo.

Serikali pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwa hairuhusu wageni kutoka nchi za nje kuja kufanya kazi hapa nchini ambazo zinaweza kufanywa na vijana wetu; mfano hivi sasa kuna vyuo vya VETA vinafundisha vijana wetu stadi mbali mbali lakini wakisha hitimu hawapati ajira kwa sababu serikali imeachia wazi watu kutoka nje wakiwemo wachina kufanya kazi hizo. Idara ya uhamiaji kama ingefanya kazi yake vizuri vijana wetu wangekuwa wanafanya kazi ambazo wachina hawa wanazifanya sasa!
 
Back
Top Bottom